Mungu yuko wapi?

Mungu yuko wapi?

Kabla ya uuambaji..Mungu alikuwepo katikati ya Giza Totoro na huko alitambulika kam "ELOHIM"
 
Nimeshakuambia na nairejea tena haya hayatakusaidia! Mimi sihimiliwi kwenye hoja kwa mfano wa unayoyafanya. Aliyesoma vitabu iwezo wake unakwenda sambamba na hoja anazozitoa uwiano wake upo kwa kiasi gani! Ukiwa uwiano ni mashariki na magharibi jawabu lipo wazi ya kuwa mhusika anajaribu kututumua misuli. Mimi sishindani na wala si kuonekana mjuzi Jf. Nitakusanya ninachokijua hatua hatua ushahidi kwa ushahidi pindi nitakapopata muda inshaallah ili kukupatia.
Nani amekwambia anashindana, wewe si ulisema hili jambo la kielimu ? Sasa tulijadili kielimu, usitafute udhuru. Kijana dini yetu haitaki ujanja ujanja, nikichokiona kwako huenda hata hivyo vitabu huna yaani hujasoma bali una copy mahali kisha unakuja kubwaga humu. Sasa unatakiwa usome haya mambo na usomeshwe.

Mimi nakupa muda wa kutosha nenda katafute, na nakupa kazi nyingine kayasome haya mapote Jahmiya, Ashaaira/Ashaariya, Muutazila, Kullabiya hawa ndiyo waliathiriwa na Falsafa na wakaingiza fikra za kikafiri katika itikadi ya Uislamu.
 
Naona Mzee unaleta ligi!

Anaitwa Nafii Ibn Mawla ambaye mwalimu wake ni ibnu Umar (Abdallah Ibn Umar).
Jalia ni Mawla siyo jina la mtu, Mawla kwa maana ya asili yake au mzazi au yeye alikuwa mjakazi, na si jina lake kwa maana ya jina.

Hapa hakuna ligi, shida ulianza na ujuaji mwingi katika hili jambo, hapo ndipo ulipo kosea. Sasa sisi hivi vitu wenzako tumeshomeshwa hatujaanza navyo mitandaoni. Siku nyingine ukiwa unakuja unakuja vizuri na usijitie mjuaji na hoja huna.
Ushahidi wa aya nitakupatia tu nitakupigia na picha na usikimbie humu. Kesho au kesho kutwa nitakupatia humu Inshaallah! Na Uzuri Imam Qurtubi ndivyo alivyotafsiri Aya!
Sasa nikimbie ili iweje wewe niletee maana ya aya kwa mujibu wa waja wema. Hizo fikra tunajua asil yake ni wapi, Wanazuoni wetu walishafanya kazi ya kutuwekea wazi fikra hizi na makundi haya yaliyo kuwa yanajinasibisha na Uislamu.

Kwa ufupi huwezi kupata ushahidi unao onyesha ya kuwa Allah hayupo juu. Zaidi ya hizo falsafa na mambo ya Logic.

Kisha kawasome Wanazuoni kama Abul Maali al Juweni naye alikuwa na fikra kama hizo za kutumia falsafa na Kalamu pasi na kurejea kwa waja wema, ila alikuja kurejea katika Haki kadhalika tafuta kitabu cha Imam Al Harawi kiitwacho "Dham al Kalam wa ahlihi" uone asili ya hiyo mitazamo.

Wewe utaleta na mimi nitakuwekea alicjokisema Imam Al-Qurtubiy katika Tafsiri Jamiul ahkaam al Qur'aan.
 
Kuwa na mipaka!

Mwenye elimu huwa anasema mimi kwangu haikunifikia, kama unaelimu nalo tupatie ushahidi.

Inshaallah nitakueletea ushahidi ila usikimbie humu! Tuwekane wazi kabisaaa usikimbie humu!
Ina maana unaposema sanadi hukuwa unamaanisha ? Maana ya Isnaad kwa umoja ni hiyo lazima turudi kwenye "Primary Source" kisha tunakuja kwa hawa walio wafata maswahaba na walio kuja baada yao.

Kijana naanzaje kukimbia ? Kwa lipi yaani ? Haya mambo yana wenyewe, mimi ile siku ya kwanza tu kunijibu nikajua weww mweupe katika hili jambo, nikawa nakusubiri uje. Yaani kuna vitu vingi ulionyesha kwamba hujui na hivyo vitabu huna wala huenda hujawahi kuviona.

Kuna mtu mwingine nikawa naona anakusifia sasa sijui ulikuwa unajisifia mwenyewe kwa ID yaki nyingine (hili siyo la msingi, ni mtazamo wangu) nikasema ujinga ni ugonjwa mbaya sana, yaani mjinga fulani anamsifia mjinga mwenzake, haya ndiyo aliyo yabashiri mtume.
 
Kwa kusema Imam Qurtubi ameegemea wapi(?) hili swali linaonyesha dhahiri tunahitaji kukaa chini kusoma. Quran tafsiri yake yote ni kauli thabiti haina kusema imeegemea wapi! Tafsiri za aya si rai/jitihada za wanawazuoni bali ni kama zilivyopokelewa na maswahaba kutoka kwa Mtume. Wanawazuoni wanasema aya 1 ya Quran kwa uchache ina maana zaidi ya 7 na kila moja ni tofauti na ipo deep. Imam Qurtubi kakusanya takribani zote na ndiyo maana kwa tafsiri za Quran huyu Imam yeye ndiye anayeitwa Beberu kwa Imam wote Mufassoruun basi yeye ndiye Beberu.
Hakuna haja ya kukaa chini sababu haya ni mambo mepesi na madogo sana, tena sisi Waislamu mizani tunayo.

Kukusanya zote siyo hoja, sababu elimu ilikuwa imesambaa zama zile na maswahaba walikuwa wamehama miji na wengine kufariki, kwahiyo huenda kuna mengi hakuyadiriki wakaja kuyadiriki walio kuja kabla yake. Hili lipo sana.

Hoja hapa ni kupatia.
 
Uwe najibu kwanza swali ulilo ulizwa kisha unauliza swali.
Umeleta ushahidi kila anapotajwa Allah yupo!

-Kisha akawa istawaa juu ya Arshi: Jawabu lako Mungu yupo juu ya Arshi.

Swali langu linakuja nahitaji msaada:

-Mtume anasema mmoja wenu akiswali asitupe mate mbele, kwani yupo Mungu.

-Hadithi ya Mtume inasema Mungu anamwambia mja: Mja wangu mimj nimeumwa hukuja kunitembelea! Mja akauliza Mola wangu kwani wewe huumwa? Mungu akajibu; lau ungeenda kunitembelea ungenipata kwake!

Sasa nisaidie Mungu yupo wapi?
-Yupo juu ya Arshi?
-Yupo mbele unaposwali?
-Yupo kwa wagonjwa?

Subiri kidogo pia!
-Hata Nabii Ibrahim alipoulizwa unaenda wapi? akajibu naenda(naelekea) kwa Mola wangu! Sikumbuki ni aya gani ila ukipata muda utaiweka mwenyewe sana!

Ila mwisho wa siku Nabii Ibrahim (kama kumbukumbu yangu ipo sawa) aliishia Palestina!

Mtumé kasema ukisujudu upo karibu na Mungu. Haya maeneo yote Mungu katajwa yupo! Sasa yupo wapi?

-Yupo juu ya Arsh?
-Yupo kwa wagonjwa?
-Yupo mbele unaposwali?
-Yupo Palestina?
-Yupo kwenye sijda?

Ikiwa kama kila eneo takapotajwa basi yupo tuambie Mungu yupo wapi? Ila ukumbuke tunaposwali ni ardhini!

Nisaidie yupo wapi?
 
Kabla ya kutaka kujua yupo wapi ufahamu kwanza ulimwengu na ramani yake ili ukipewa jibu uelewe hilo eneo.

Anza na sayari ya Mecury na mitaa yake kama dunia umeshaijua yote. Ulimwengu hatuujui ila tunataka tujue alipo aliyeuumba.

Babu kaona dagaa baharini akipita kamuhadithia baba yako, baba yako kaja kukuhadithia wewe halafu wewe unauliza watoto wenzako mtaani yule dagaa aliyemuona babu anaishi eneo gani baharini?
Hueleweki!
 
Mnara wa Babeli ile sio hadithi bali historia na matukio yale yalitokea!

Historia yenyewe iko hivi:
"...Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote. BWANA akashuka ili auone mji na mnara waliokuwa wakiujenga wanadamu. BWANA akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya. Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao" Mwanzo 11:4-7

Hawa wanadamu wanasema wajenge mnara na mji, na huo mnara ufike mbinguni ili wajifanyie jina. Kumbuka amri ya Mungu ilikuwa "Mungu akambariki Nuhu na wanawe, akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi" - Mwanzo 9:1. Mungu anawaambia watawanyike wazaliane waijaze nchi wao wanasema hapana tujenge mji na mnara ili tusitawanyike. Wanapingana na amri ya Mungu moja kwa moja.

Lakini pia mnara huu sio mnara wa mlinzi, ni minara katika enzi hizo zilifahamika kama mahekalu ya ibada. Hawa watu walitaka kuanzisha serikali yao na dini yao ili wasitawanyike. Na mbingu isikuchanganye hapa. Neno mbingu linatumika katika Biblia kumaanisha aidha atmosphere, galaxy au realm/dimension ambako Mungu amepatengeneza kwa kusudi maalum. Hapa ni wazi walikusudia mnara huu ufike kwenye atmospheric heaven au kama walikuwa na teknolojia kubwa, galaxy. Ukisoma Muktadha lengo halikuwa kufikia "God's heaven" kama utaniruhusu nitumie neno hilo, lengo ni mnara mrefu uwe kwa ajili ya ibada.

Kuasi agizo la Mungu na kuamua kuanzisha serikali na dini yao ya waasi ndio sababu iliyomfanya Mungu aamue kuiharibu project yao!

Kwa sababu mada ni tofauti nisianzishe mada juu ya mada, itoshe kuishia hapa!

Hope itatoa mwanga kwako na Patra31
Biblia imesema walitaka kujenga mnara kuelekea juu alipo Mungu, wewe unakuja na hekaya za siyo mnara wa kawaida ila ni mnara wa ibada!!!!!
 
Swali zuri japo ukishaelewa msingi linakuwa la kijinga sana. Kwa hiyo nitakusaidia kuuona msingi na kuona kwa nini ni swali lisilo na maana.

Kitu cha msingi hapa ni kuwa yote nitakayoongelea ni kwa mujibu wa Biblia na kwa sababu naamini, kwa sababu nzito tu, kuwa Biblia ni Neno la Mungu na kuwa Mungu aliyejifunua ndiye Mungu muumba mbingu na nchi. Kwa hiyo jibu ni very specific. Kama unataka majibu juu ya jumla sina na wala sitawajibika kujibia miungu.

Biblia inafungua na mstari huu:
"Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi" - Mwanzo 1:1

Hapo maneno ya msingi ni Mwanzo, Mbingu na Nchi. Mstari huu unatuonesha kuwa kuna kipindi kulikuwa na mwanzo yaani muda haukuwepo ziku zote ulianza katika "kipindi" fulani. Kabla ya mwanzo hakukuwa na muda.

Pili tunaona Mungu akiumba mbingu na nchi. Mbingu na nchi au ulimwengu (universe) kama unavyofahamika kisayansi ni nafasi. Tunajua kuwa Ulimwengu upo katika muda na nafasi. Muda unatuambia wakati kitu kimefanyika au kimekuwepo na nafasi inatuambia mahali tukio lilifanyika. Huwezi kuwa na muda bila nafasi, kwa sababi ili kitu kifanyike au kiwepo kwenye ulimwengu huu lazima kiwe katika nafasi fulani na huwezi kusema nafasi ni nafasi mpaka iwepo ndani ya muda.

Kwa sababu wakati-nafasi sio mada niishie hapa. Ila ili ulimwengu wetu uwepo ni lazima wakati na nafasi viwepo kwa wakati mmoja. Na hapa Biblia inatuambia Mungu aliumba wakati na nafasi.

Tunajuaje? Kwa sababu Biblia si tu inatuambia Mungu aliumba mbingu na nchi "hapo mwanzo", bali pia inatuambia kuwa huyu Mungu alikuwako tayari kabla ya huo mwanzo. Kwa lugha rahisi kabla ya huo mwanzo (muda) kuwepo, Mungu alikuwepo!

"Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika" Yohana 1:1-3

Na ndio maana jina lake anaitwa NIKO. Yaani baada ya muda Yeye yuko, "hapo mwanzo" Yeye yuko na kabla ya muda Yeye yuko!

"Musa akamwambia Mungu, Tazama, nitakapofika kwa wana wa Israeli, na kuwaambia, Mungu wa baba zenu amenituma kwenu; nao wakaniuliza, Jina lake n’nani? Niwaambie nini? Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO; akasema, Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli; MIMI NIKO amenituma kwenu" - Kutoka 3:13-14

Kwa hiyo msingi hapa ni kuwa
1. Ulimwengu na vyote vilivyomo, vinavyoonekana na visivyoonekana viliumbwa hapo mwanzo
2. Muda na Nafasi havikuwepo milele, kuna wakati hakukuwa na wakati wala nafasi.
3. Mungu Yehova Yeye Yuko, kabla ya wakati na wakati utakapokoma.


Tukirudi swali la msingi, ambalo lina sehemu mbili:



Kuuliza Mungu yupo wapi maana yake unadhania Mungu anafungwa na muda na nafasi. Maana ukisema yuko wapi unaongelea muda na nafasi. Mfano tukisema Mwanyuma yuko wapi, jibu litakuwa linaambatana na nafasi na muda. Kwa hiyo jibu la swali hili lina dhahania ndani yake kuwa "wapi" hiyo itakuwa ndani ya huu ulimwengu uliofungwa kwa muda na nafasi.

Basi Jibu lake ni kuwa Mungu yupo kila mahali, katika ulimwengu wetu huu. Lakini kwa sababu Mungu hafungwi na muda na nafasi, basi kuna jibu ambalo linapaswa kufafanuliwa hapa kwamba nje ya ulimwengu huu wa muda-nafasi Mungu Yuko! Kwa sababu nje ya huu ulimwengu hakuna kitu kinaitwa wapi, kwa sababu ili kuwe na wapi unahitaji uwe na muda na nafasi.

Kujibu swali lako kwa ukamilifu ni kuwa Mungu YUKO! iwe ni mahali popote, muda wowote au iwe nje ya muda, Yeye Yuko!


Kabla ya kuumba vyote, hakukuwa na muda wala nafasi. Kwa hiyo kusema alikuwa wapi ni swali la kijinga kwa sababu hakukuwa na wapi bado. Au ukisema Mungu alianza lini ni swali la kipuuzi pia kwa sababu ukirudi nyuma kabla ya mwanzo hakuna muda na hivyo kuanza (muda) hakupo!

Kwa hiyo jibu rahisi ni kuwa kabla ya vyote kuumbwa Yeye alikuwepo. Siku zote Yehova Yuko na ndio maana jina lake ni MIMI NIKO!
Wakristo huwa mnanichekesha sana mkiulizwa Mungo yuko wapi mnasema kuwa hamjui ,mara sijui mungu ni niko!!!

Si mumwambie kwa mujibu wa imani yenu kuwa Mungu wenu ni YESU!! Na ameshawahi kuonekana hapa duniani alikuwa akila,akinywa,akilala na kwenda msalani kujisaidia!! Mungu wenu alizaliwa na Mariam, infact Mungu wenu ana mama na amenyonya maziwa ya mama yake.


Kwa Mujibu wa dini yetu ya Kiislam ni kuwa MUNGU hajazaliwa wala hajazaa, yupo mmoja tu na yeye ndiye anayetegemewa na kila kitu na hakuna afananae nae hata mmoja.

Mungu ametufunulia majina yake matukufu 99 na ametufundisha kuwa pindi tunapokuwa na shida tumuombe kupitia majina hayo naye atajibu.

Miongoni mwa majina hayo matukufu ni.

Al-Awwal (MWANZO) - Mungu ndiye mwanzo kabla yake hakuna mwanzo kila jambo unaloliona lina anzia kwake, yeye ndie originator wa unavyovijua na vile usivyovijua.

Al-Akhir (MWISHO) - Mungu ndie wa mwisho yaani baada yake hakuna mwisho.

Haya ni majina yake mawili matukufu miongoni mwa majina yake 99 aliyotufunulia sisi wanaadamu kupitia kwa mtume wake Muhammad (sala na amani ziwe juu yake).

Mungu ndiye mmiliki wa muda (nyakati), Katika mkono wake amemiliki usiku na huu mchana na ameumba usiku na mchana kama alama mbili kuonesha kuwa yupo ila hizi alama mbili ni kwa ajili ya watu wenye akili bimaana kuna wengine ni mazezeta kila siku wanaona usiku na mchana vinapishana ila wanakwambia kuwa hakuna Mungu.

Pia muda ameuumba ili tu utusaidie sisi hapa duniani tujue majira, hesabu za siku,miezi na miaka. Katika ulimwengu ujao baada ya kufa na kufufuliwa kutakuwa hakuna usiku wala mchana. Na maisha yatakuwa ni ya milele hakuna tena kufa.
 
Salaam wanabodi,

Very simple. Swali linajieleza hapo juu. Je Mungu yuko wapi? Kabla ya Mungu kuumba ulimwengu/dunia na vitu vyoooote vilivyopo, yeye binafsi alikuwa wapi? Alikuwa kwenye nini? Aliketi au kusimama kwenye kitu gani? Je ni yeye aliyeumba sayari nyingine zaidi ya 9 zinazofahamika? Kwanini amemuweka mwanadamu kwenye sayari moja tu ya DUNIA?

Tusaidiane kujua majibu ya haya maswali muhimu kwenye historia ya ulimwengu.
Mungu yupo everywhere.
ndio maana anayetenda dhambi hapa Tz ama Marekani au Japan anawaona at the same time
 
Katika tumbo la mama kulikuwa na watoto wawili. Mmoja akamuuliza mwenzake: “Je, unaamini maisha baada ya kujifungua?” Yule mwingine akajibu, “Kwa nini, bila shaka. Lazima kuwe na kitu baada ya kujifungua. Labda tuko hapa kujitayarisha kwa kile tutakachokuwa baadaye.”

"Upuuzi," wa kwanza alisema. "Hakuna maisha baada ya kujifungua. Je, hayo yangekuwa maisha ya aina gani?” Wa pili akasema, "Sijui, lakini kutakuwa na mwanga zaidi kuliko hapa. Labda tutatembea kwa miguu yetu na kula kutoka kwa midomo yetu. Labda tutakuwa na hisia zingine ambazo hatuwezi kuelewa sasa.

Wa kwanza akajibu, “Huo ni upuuzi. Kutembea haiwezekani. Na kula kwa midomo yetu? Kichekesho! Kamba ya umbilical hutoa lishe na kila kitu tunachohitaji. Lakini kamba ya umbilical ni fupi sana. Maisha baada ya kujifungua yanapaswa kutengwa kimantiki.” Wa pili alisisitiza, "Nadhani kuna kitu na labda ni tofauti na ilivyo hapa. Labda hatutahitaji kamba hii ya mwili tena." Wa kwanza akajibu, “Upuuzi. Na zaidi ya hayo, ikiwa kuna uhai, basi kwa nini hakuna mtu aliyewahi kurudi kutoka huko? Kujifungua ni mwisho wa maisha, na katika baada ya kuzaa hakuna ila giza na ukimya na usahaulifu. Haitupeleki popote.” “Sawa, sijui,” akasema wa pili, “lakini hakika tutakutana na Mama naye atatutunza.

” Wa kwanza akajibu “Mama? Unamwamini Mama kweli? Hiyo inachekesha. Kama mama yupo, yuko wapi sasa hivi?" Wa pili akasema, “Anatuzunguka pande zote. Tumezungukwa naye. Sisi ni wake. Ni ndani Yake tunaishi. Bila Yeye, ulimwengu huu haungekuwepo na tusingekuwepo." Alisema wa kwanza:

"Kweli, simuoni, kwa hivyo ni sawa kwamba Yeye hayupo." Ambayo wa pili alijibu, "Wakati mwingine, unapokuwa kimya na ukizingatia na kusikiliza, unaweza kuona uwepo Wake, na unaweza kusikia sauti Yake ya upendo, ikiita kutoka juu." Labda hii ilikuwa moja ya maelezo bora ya dhana ya MUNGU.
Hakika huu ni mfano bora sana ila hawataelewa haya ila wenye akili!! Kuna wanaadamu wanavichwa ila akili hawana licha ya kuwa na vyeti vingi kuonesha wamehitimu elimu za juu!!,

leo hii ukimwambia kuwa kuna maisha ya kaburini hawezi kukuelewa ,atakuona umechanganyikiwa na ukimwambia kuwa mara baada ya mwili kusagika na kuwa mchanga ,Mungu atatufufua sote na kuturudisha ktk maumbile ya awali ,vilevile atakuona umechanganyikiwa na maisha.


Mwanadamu ameumbwa akiwa na asili ya ubishi, mwanadamu ni mtu wa kupinga vitu hata kama hana elimu au ujuzi navyo.
 
Hapa kidogo una shida, aya iko wazi sana, aya inasema kisha akastawi juu ya Arshi yake. Maana ya juu iko wazi sana. Sasa unapo taka tafsiri sijui unataka tafsiri gani zaidi ya hiyo ?

Je hakuwataja wanazuoni hao wa karne ya tatu ?

Hakuna aqida ya Uislamu inayosema hivi. Sababu hapo mnapingana na aya, maana yake kama Imamu Qurtubiy amesema haya amekosea, anakuwa amefanya "taawili" katika aya.

Tamko kustawi lina maana yake.

Hapa naona unataka kumsingizia Imam Abul Fida Ismail Imaad diin Ibn Kathiir, katika aya hii yeye anafata uelewa wa wema walio tangulia ambao ni Malik, Al-Awza`i, Ath-Thawri, Al-Layth bin Sa`d, Ash-Shafi`i, Ahmad, Ishaq bin Rahwayh na wengine kwa kuchukua maana ya wazi kama ilivyo kuja katika Qur'aan, na maana hiyo iko wazi na tamko "Istawa" liko wazi. Rejea katika tafsiri yake alipokuwa anafasiri aya hiyo.

Sasa swali langu kwako hiyo kauli yako inayokwenda sambamba na kauli ya Imam Ibn Kathir ni ipi ? Imam Ibn Kathir hana kauli hiyo, sasa kama hujasoma vitabu umekopi marejeo bila kusoma, nenda kasome tena.

Allab hayupo juu ya Arshi kwa ushahudi gani ? Maana huna ushahidi wowote unao utoa zaidi ya maoni ya hao Wanachuoni, huku ukimsingizia uongo Imam Ibn Kathir.

Haya si madhebeu ya wema walio tanguli, hili amelithibitisha Imam Ibn Kathir, kadhalika Imam Shafii hakuwa na itikadi hiyo.

Nikirudi nakuja kukuelezea wapi hii Itikadi waliitoa. Nilikuuliza unamjua Jahm Ibn Saf'wan ? Huyu ndiyo mwenye itikadi hii na hawa waliathirika na Wanafalsafa na Wakrsito.
Akhi unabishana na mtu anayejiita hammaz? Huyo jamaa anawasingizia wanazuoni tu wala haweki marejeo yao humu.Wapo watu wengi sana watakutajia majina lukuki na rejea nyingi za uongo za wanazuoni wengi waliotangulia . Aqidah ya ahlul sunna wal jamaa ipo wazi kabisa kuwa ALLAH yupo juu ya arshi..ipo hivyo na itaendelea kuwa hivyo.

Hao wanaosema kuwa ALLAH hayupo juu ya arshi yake wanaficha tu aqidah zao , mwisho wa siku atajifunua na kusema ALLAH yupo kila sehemu.

Hata mwanangu mdogo wa mwaka mmoja nikimuuliza suali kuwa ALLAH yupo wapi ,atanijibu kuwa ALLAH yupo juu!!
 
Si mumwambie kwa mujibu wa imani yenu kuwa Mungu wenu ni YESU!! Na maeshwahi kuonekana hapa duniani alikuwa akila,akinywa,akilala na kwenda msalani kujisaidia!! Mungu wenu alizaliwa na Mariam, infact Mungu wenu ana mama na amenyonya maziwa ya mama yake.
Kama umeamua kujivika mamlaka ya kujibia Wakristo basi acha longolongo, jibu Mungu yuko wapi? Huyohuyo Yesu uliyemkebehi hapo yuko wapi? Jibu swali acha taralila
 
Kwa Mujibu wa dini yetu ya Kiislam ni kuwa MUNGU hajazaliwa wala hajazaa, yupo mmoja tu na yeye ndiye anayetegemewa na kila kitu na hakuna afananae nae hata mmoja.
Kwa hiyo huyo mungu wa kiislam yupo wapi?
Maana umekimbilia kujibu swali ambalo hujaulizwa. Hujaulizwa kama huyo mungu wako kazaa au kazaliwa. Umeulizwa yuko wapi? Badala ya kujibu mungu wako mwenye mikono miwili na yote ni ya kulia na ana mguu mmoja yuko wapi umekurupuka na kuwa msemaji wa Mungu wa wakristo.

Jibu swali Allah yuko wapi?
 
Salaam wanabodi,

Very simple. Swali linajieleza hapo juu. Je Mungu yuko wapi? Kabla ya Mungu kuumba ulimwengu/dunia na vitu vyoooote vilivyopo, yeye binafsi alikuwa wapi? Alikuwa kwenye nini? Aliketi au kusimama kwenye kitu gani? Je ni yeye aliyeumba sayari nyingine zaidi ya 9 zinazofahamika? Kwanini amemuweka mwanadamu kwenye sayari moja tu ya DUNIA?

Tusaidiane kujua majibu ya haya maswali muhimu kwenye historia ya ulimwengu.
Soma maandiko, usituchoshe!!
 
Kwa hiyo huyo mungu wa kiislam yupo wapi?
Maana umekimbilia kujibu swali ambalo hujaulizwa. Hujaulizwa kama huyo mungu wako kazaa au kazaliwa. Umeulizwa yuko wapi? Badala ya kujibu mungu wako mwenye mikono miwili na yote ni ya kulia na ana mguu mmoja yuko wapi umekurupuka na kuwa msemaji wa Mungu wa wakristo.

Jibu swali Allah yuko wapi?
Quran 7:54

Hakika Mola Mlezi wenu ni Mwenyezi Mungu aliye ziumba mbingu na ardhi katika siku sita. Kisha akatawala juu ya Kiti cha Enzi. Huufunika usiku kwa mchana, ufuatao upesi upesi. Na jua, na mwezi, na nyota zinazo tumika kwa amri yake. Fahamuni! Kuumba na amri ni zake. Ametukuka kabisa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote.
 
Quran 7:54

Hakika Mola Mlezi wenu ni Mwenyezi Mungu aliye ziumba mbingu na ardhi katika siku sita. Kisha akatawala juu ya Kiti cha Enzi. Huufunika usiku kwa mchana, ufuatao upesi upesi. Na jua, na mwezi, na nyota zinazo tumika kwa amri yake. Fahamuni! Kuumba na amri ni zake. Ametukuka kabisa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote.
Allah yuko wapi? Kwani ni swali gumu sana hili? Mbona unazunguka? Kumbe ni rahisi kurukia kwenye kukashifu imani zingine ilhali ya kwako mwenyewe huna hata idea?

Allah yuko wapi, shaikh?
 
Back
Top Bottom