Mungu yuko wapi?

Mungu yuko wapi?

Kabla ya kutaka kujua yupo wapi ufahamu kwanza ulimwengu na ramani yake ili ukipewa jibu uelewe hilo eneo.

Anza na sayari ya Mecury na mitaa yake kama dunia umeshaijua yote. Ulimwengu hatuujui ila tunataka tujue alipo aliyeuumba.

Babu kaona dagaa baharini akipita kamuhadithia baba yako, baba yako kaja kukuhadithia wewe halafu wewe unauliza watoto wenzako mtaani yule dagaa aliyemuona babu anaishi eneo gani baharini?
 
Wakiwa wanakujibu, wanajibu pia je hadithi ya mnara wa baberi ni kweli au si kweli. Maana ndio hadithi inayozungumzia chimbuko la lugha.

Je huo mnara ulikua na urefu gani hadi Mungu aone binadamu watamfikia?.. maana vyombo vya usafiri vinatoka hadi nje ya dunia
 
Mungu yupo Mkuu, unajua hii Dunia ukiitafakari Sana huenda usipate majibu ila Amini hivyo Mungu yupo na kwakulithibitisha hili hebu angalia jinsi tunavyopata usiku namchana.
kupata usiku na mchana haitoshi kumfanyatu Amin kuwa Mungu yupo maana sio sisi tu tupatao usiku na mchana ata sayari zingne nazo zina usiku na mchana.
 
Never got a place to post this 😄

Screenshot_20210529-115628.jpg
 
Wakiwa wanakujibu, wanajibu pia je hadithi ya mnara wa baberi ni kweli au si kweli. Maana ndio hadithi inayozungumzia chimbuko la lugha.

Je huo mnara ulikua na urefu gani hadi Mungu aone binadamu watamfikia?.. maana vyombo vya usafiri vinatoka hadi nje ya dunia
hapa ndipo lilipo jibu. Wenda haukuwa mnara wakawaida kama tunavyo aminisha.
Kuna kitu hapo uwa wanakifichwa
 
Salaam wanabodi,

Very simple. Swali linajieleza hapo juu. Je Mungu yuko wapi? Kabla ya Mungu kuumba ulimwengu/dunia na vitu vyoooote vilivyopo, yeye binafsi alikuwa wapi? Alikuwa kwenye nini? Aliketi au kusimama kwenye kitu gani? Je ni yeye aliyeumba sayari nyingine zaidi ya 9 zinazofahamika? Kwanini amemuweka mwanadamu kwenye sayari moja tu ya DUNIA?
Swali zuri japo ukishaelewa msingi linakuwa la kijinga sana. Kwa hiyo nitakusaidia kuuona msingi na kuona kwa nini ni swali lisilo na maana.

Kitu cha msingi hapa ni kuwa yote nitakayoongelea ni kwa mujibu wa Biblia na kwa sababu naamini, kwa sababu nzito tu, kuwa Biblia ni Neno la Mungu na kuwa Mungu aliyejifunua ndiye Mungu muumba mbingu na nchi. Kwa hiyo jibu ni very specific. Kama unataka majibu juu ya jumla sina na wala sitawajibika kujibia miungu.

Biblia inafungua na mstari huu:
"Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi" - Mwanzo 1:1

Hapo maneno ya msingi ni Mwanzo, Mbingu na Nchi. Mstari huu unatuonesha kuwa kuna kipindi kulikuwa na mwanzo yaani muda haukuwepo ziku zote ulianza katika "kipindi" fulani. Kabla ya mwanzo hakukuwa na muda.

Pili tunaona Mungu akiumba mbingu na nchi. Mbingu na nchi au ulimwengu (universe) kama unavyofahamika kisayansi ni nafasi. Tunajua kuwa Ulimwengu upo katika muda na nafasi. Muda unatuambia wakati kitu kimefanyika au kimekuwepo na nafasi inatuambia mahali tukio lilifanyika. Huwezi kuwa na muda bila nafasi, kwa sababi ili kitu kifanyike au kiwepo kwenye ulimwengu huu lazima kiwe katika nafasi fulani na huwezi kusema nafasi ni nafasi mpaka iwepo ndani ya muda.

Kwa sababu wakati-nafasi sio mada niishie hapa. Ila ili ulimwengu wetu uwepo ni lazima wakati na nafasi viwepo kwa wakati mmoja. Na hapa Biblia inatuambia Mungu aliumba wakati na nafasi.

Tunajuaje? Kwa sababu Biblia si tu inatuambia Mungu aliumba mbingu na nchi "hapo mwanzo", bali pia inatuambia kuwa huyu Mungu alikuwako tayari kabla ya huo mwanzo. Kwa lugha rahisi kabla ya huo mwanzo (muda) kuwepo, Mungu alikuwepo!

"Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika" Yohana 1:1-3

Na ndio maana jina lake anaitwa NIKO. Yaani baada ya muda Yeye yuko, "hapo mwanzo" Yeye yuko na kabla ya muda Yeye yuko!

"Musa akamwambia Mungu, Tazama, nitakapofika kwa wana wa Israeli, na kuwaambia, Mungu wa baba zenu amenituma kwenu; nao wakaniuliza, Jina lake n’nani? Niwaambie nini? Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO; akasema, Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli; MIMI NIKO amenituma kwenu" - Kutoka 3:13-14

Kwa hiyo msingi hapa ni kuwa
1. Ulimwengu na vyote vilivyomo, vinavyoonekana na visivyoonekana viliumbwa hapo mwanzo
2. Muda na Nafasi havikuwepo milele, kuna wakati hakukuwa na wakati wala nafasi.
3. Mungu Yehova Yeye Yuko, kabla ya wakati na wakati utakapokoma.


Tukirudi swali la msingi, ambalo lina sehemu mbili:


Mungu yuko wapi?
Kuuliza Mungu yupo wapi maana yake unadhania Mungu anafungwa na muda na nafasi. Maana ukisema yuko wapi unaongelea muda na nafasi. Mfano tukisema Mwanyuma yuko wapi, jibu litakuwa linaambatana na nafasi na muda. Kwa hiyo jibu la swali hili lina dhahania ndani yake kuwa "wapi" hiyo itakuwa ndani ya huu ulimwengu uliofungwa kwa muda na nafasi.

Basi Jibu lake ni kuwa Mungu yupo kila mahali, katika ulimwengu wetu huu. Lakini kwa sababu Mungu hafungwi na muda na nafasi, basi kuna jibu ambalo linapaswa kufafanuliwa hapa kwamba nje ya ulimwengu huu wa muda-nafasi Mungu Yuko! Kwa sababu nje ya huu ulimwengu hakuna kitu kinaitwa wapi, kwa sababu ili kuwe na wapi unahitaji uwe na muda na nafasi.

Kujibu swali lako kwa ukamilifu ni kuwa Mungu YUKO! iwe ni mahali popote, muda wowote au iwe nje ya muda, Yeye Yuko!

Kabla ya Mungu kuumba ulimwengu/dunia na vitu vyoooote vilivyopo, yeye binafsi alikuwa wapi?
Kabla ya kuumba vyote, hakukuwa na muda wala nafasi. Kwa hiyo kusema alikuwa wapi ni swali la kijinga kwa sababu hakukuwa na wapi bado. Au ukisema Mungu alianza lini ni swali la kipuuzi pia kwa sababu ukirudi nyuma kabla ya mwanzo hakuna muda na hivyo kuanza (muda) hakupo!

Kwa hiyo jibu rahisi ni kuwa kabla ya vyote kuumbwa Yeye alikuwepo. Siku zote Yehova Yuko na ndio maana jina lake ni MIMI NIKO!
 
Wakiwa wanakujibu, wanajibu pia je hadithi ya mnara wa baberi ni kweli au si kweli. Maana ndio hadithi inayozungumzia chimbuko la lugha.
Mnara wa Babeli ile sio hadithi bali historia na matukio yale yalitokea!
Je huo mnara ulikua na urefu gani hadi Mungu aone binadamu watamfikia?.. maana vyombo vya usafiri vinatoka hadi nje ya dunia
Historia yenyewe iko hivi:
"...Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote. BWANA akashuka ili auone mji na mnara waliokuwa wakiujenga wanadamu. BWANA akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya. Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao" Mwanzo 11:4-7

Hawa wanadamu wanasema wajenge mnara na mji, na huo mnara ufike mbinguni ili wajifanyie jina. Kumbuka amri ya Mungu ilikuwa "Mungu akambariki Nuhu na wanawe, akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi" - Mwanzo 9:1. Mungu anawaambia watawanyike wazaliane waijaze nchi wao wanasema hapana tujenge mji na mnara ili tusitawanyike. Wanapingana na amri ya Mungu moja kwa moja.

Lakini pia mnara huu sio mnara wa mlinzi, ni minara katika enzi hizo zilifahamika kama mahekalu ya ibada. Hawa watu walitaka kuanzisha serikali yao na dini yao ili wasitawanyike. Na mbingu isikuchanganye hapa. Neno mbingu linatumika katika Biblia kumaanisha aidha atmosphere, galaxy au realm/dimension ambako Mungu amepatengeneza kwa kusudi maalum. Hapa ni wazi walikusudia mnara huu ufike kwenye atmospheric heaven au kama walikuwa na teknolojia kubwa, galaxy. Ukisoma Muktadha lengo halikuwa kufikia "God's heaven" kama utaniruhusu nitumie neno hilo, lengo ni mnara mrefu uwe kwa ajili ya ibada.

Kuasi agizo la Mungu na kuamua kuanzisha serikali na dini yao ya waasi ndio sababu iliyomfanya Mungu aamue kuiharibu project yao!

Kwa sababu mada ni tofauti nisianzishe mada juu ya mada, itoshe kuishia hapa!

Hope itatoa mwanga kwako na Patra31
 
Ninavyojua Mimi uwezo wa Binaadamu kumfahamu Mungu mwenyezi ni mdogo na hatuwezi kudhibiti elimu hio ya kumjua kwasababu NI pana Sana, kwahio hatufahamu isipokuwa kwa uchache Sana.

Ukisema Mwenyezimungu yupo wapi jibu jepesi Mwenyezimungu yupo kila sehemu.

Kwasababu katika sifa zake kwa mujibu wa vitabu vitakatifu ni kwamba Yeye anasifa ya kuwepo kila sehemu.

Lakini kwa upande wa sayari kwa mujibu wa Wana sayansi wanatuambia kunakitu kinaitwa Gallax, ukubwa wa Gallax moja ni sawasawa na upana Solar System, na hii solar system yetu NI moja Kati ya hizo Gallax.

Sasa kwa mujibu wa Wana sayansi wanasema Gallax zilizogundulika MPAKA Sasa ni billioni 175, ambazo ktk hizo wamegungua sayari 1560 ambazo zinafanana na dunia kwa kila kitu.

Lakini Kuna moja inayoitwa Eath Twins iliogunduliwa 2006, wanasema ipo umbali wa Safari ya miaka 600 kwa mwendo wa kimondo.

Lakini wana sayansi wanadai ukubwa wa Universe unaweza ukawa Mara billioni kadhaa kwa upana wa upeo waliogundua mpaka Sasa.

Na Hilo lote NI eneo la Mungu, na kwa mujibu wa vitabu Hakuna Eneo ambalo sio lake.

Mi nafikiri tuendelee kula ugali wetu na Dagaa kuliko kufananisha mambo ya Mungu kwa akili zetu za kisayansi na kitechnolojia ingawa hakazwi mtu kuendeleza juhudi na utafiti.
🙏
 
Haya maswal hakunaga mwenye majibu sahihi maana hawa wote wanaokujibu wanalazimisha uamini bila kutumia akili.

Huyo Mungu kama alkuumba na akili bas alimaanisha uzitumie kufikir.

Biblia husema hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na ardhi, kumaanisha kuwa ardhi ni dunia na mbingu ni anga, lkn hakuna sehem biblia imeongelea uumbaji wa ufalme wake wa kiroho ambao unajumuisha Mbingu(heaven) yaan makao yake na malaika, pia hakuna sehem ktk biblia inaonesha ama kuongelea mwanzo wa viumbe wa kiroho kama shetan na malaika wengine, na hapa ndipo palitakiwa pawe sehem ya kufanyia judgement ya swali la mtoa post.

Hivyo basi biblia inakosa majibu sahihi ya kujibu kuwa Mungu alikuwa wapi kabla ya uumbaji wa mwanadamu na Mbingu maana mbingu iliyoongelewa ktk kitabu cha mwanzo haiimaanishi mbingu makazi ya roho bali Anga la juu ya dunia.

Kiufupi ni kuwa hizi dini na vitabu vyake tulipigwa pakubwa sana , kuna mengi washika dini hawayajui na kwa upumbavu wao wa ubishi watabak kuamn ujinga mpaka mwisho.

Ukiwa mtu wa kufuatilia mambo bila kuegemea upande wowote ule ktk mambo ya imani, utagundua kuwa Huyo wanaemuita Mungu ktk vitabu vya dini, hakuwai kuwepo kabla ya uumbaji bali nae amezikuta mbingu na dunia zikiwa tayari zmeumbwa na ndiomaana anauwezo wa kuingia ktk mbingu hizo na kutembelea makazi yaliyoumbwa na kusingizia ameyaumba yeye mwenyewe.

mfano utauona ktk vitabu vyenu pale Mungu wenu anaposhuka ktk vilindi vya maji kufanya uumbaji pia vitabu vyenu vyaonesha kuwa Mungu wenu anaish ktk Ulimwengu wa roho ambao kuna mahala panaitwa mbinguni, hivyo basi kama hizi zote ni sehemu kuna viumbe wanaishi je mjenzi wake anawezaje kuishi humo? Kabla ya ujenzi wa hizo sehemu aliishi wapi? na kwanini aondoke alipokuwa mwanzo na kuhamia ktk hizo sehemu?(mbingu)hamuoni kama mnapigwa hapa? Ama fikra zenu zipo tu kukubali kila kitu makanisan na misikitini kwa kuitikia aminaaaa.

Ukweli ni kwamba Kuna Nguvu kubwa ambayo ni zaidi ya Umungu ambayo ndyo ilifanya haya yote yatokee kutoka ktk upeo usioonekana mpaka uhalisia na Nguvu hiyo ndyo chanzo cha uhai na ndyo chanzo cha kila kitu ukionacho na usichokiona na nguvu hizo ndizo hubalance misingi ya Limwengu zote ikiwepo ulimwengu huu tulionao pia dunia hii tulio nayo, na Nguvu hizo ndzo ziliabudiwa na watu kabla ya ujio wa mafundisho ya uongo Kuhusu Nguvu hizo, mafundisho hayo ndyo yaliyotungwa na watu weupe kwa kuleta nadharia ya Umungu baada ya upeo wao wa kufikiri kufika mwsho kwa kuamua Kushindwa kuelewa Jinsi Nguvu hizo zlvyokuwa zikifanya kazi, na ndipo wakazilimit ili ziendane na upeo wa akili zao, lkn kiuhalisia hakuna kwel ktk mafundisho yao ndiomaana yamejawa mikanganyiko na kujipinga kwakuwa ni sehemu ya nadharia zilizotungwa na wanadamu wenye upeo mdogo na kuforce watu weusi mziamini.

Mungu wa dini zote ni Huyo huyo mnaemuita shetan ktk majina ya vificho
img_16_1617349787370.jpg
 
Salaam wanabodi,

Very simple. Swali linajieleza hapo juu. Je Mungu yuko wapi? Kabla ya Mungu kuumba ulimwengu/dunia na vitu vyoooote vilivyopo, yeye binafsi alikuwa wapi? Alikuwa kwenye nini? Aliketi au kusimama kwenye kitu gani? Je ni yeye aliyeumba sayari nyingine zaidi ya 9 zinazofahamika? Kwanini amemuweka mwanadamu kwenye sayari moja tu ya DUNIA?

Tusaidiane kujua majibu ya haya maswali muhimu kwenye historia ya ulimwengu.
Soma Biblia Yeremia 23:23-24.
 
Salaam wanabodi,

Very simple. Swali linajieleza hapo juu. Je Mungu yuko wapi? Kabla ya Mungu kuumba ulimwengu/dunia na vitu vyoooote vilivyopo, yeye binafsi alikuwa wapi? Alikuwa kwenye nini? Aliketi au kusimama kwenye kitu gani? Je ni yeye aliyeumba sayari nyingine zaidi ya 9 zinazofahamika? Kwanini amemuweka mwanadamu kwenye sayari moja tu ya DUNIA?

Tusaidiane kujua majibu ya haya maswali muhimu kwenye historia ya ulimwengu.
MUNGU NI ROHO YUPO KILA MAHALI.
 
Back
Top Bottom