Mungu yuko wapi?

Mungu yuko wapi?

Hapa aje Kiranga
Katika tumbo la mama kulikuwa na watoto wawili. Mmoja akamuuliza mwenzake: “Je, unaamini maisha baada ya kujifungua?” Yule mwingine akajibu, “Kwa nini, bila shaka. Lazima kuwe na kitu baada ya kujifungua. Labda tuko hapa kujitayarisha kwa kile tutakachokuwa baadaye.”

"Upuuzi," wa kwanza alisema. "Hakuna maisha baada ya kujifungua. Je, hayo yangekuwa maisha ya aina gani?” Wa pili akasema, "Sijui, lakini kutakuwa na mwanga zaidi kuliko hapa. Labda tutatembea kwa miguu yetu na kula kutoka kwa midomo yetu. Labda tutakuwa na hisia zingine ambazo hatuwezi kuelewa sasa.

Wa kwanza akajibu, “Huo ni upuuzi. Kutembea haiwezekani. Na kula kwa midomo yetu? Kichekesho! Kamba ya umbilical hutoa lishe na kila kitu tunachohitaji. Lakini kamba ya umbilical ni fupi sana. Maisha baada ya kujifungua yanapaswa kutengwa kimantiki.” Wa pili alisisitiza, "Nadhani kuna kitu na labda ni tofauti na ilivyo hapa. Labda hatutahitaji kamba hii ya mwili tena." Wa kwanza akajibu, “Upuuzi. Na zaidi ya hayo, ikiwa kuna uhai, basi kwa nini hakuna mtu aliyewahi kurudi kutoka huko? Kujifungua ni mwisho wa maisha, na katika baada ya kuzaa hakuna ila giza na ukimya na usahaulifu. Haitupeleki popote.” “Sawa, sijui,” akasema wa pili, “lakini hakika tutakutana na Mama naye atatutunza.

” Wa kwanza akajibu “Mama? Unamwamini Mama kweli? Hiyo inachekesha. Kama mama yupo, yuko wapi sasa hivi?" Wa pili akasema, “Anatuzunguka pande zote. Tumezungukwa naye. Sisi ni wake. Ni ndani Yake tunaishi. Bila Yeye, ulimwengu huu haungekuwepo na tusingekuwepo." Alisema wa kwanza:

"Kweli, simuoni, kwa hivyo ni sawa kwamba Yeye hayupo." Ambayo wa pili alijibu, "Wakati mwingine, unapokuwa kimya na ukizingatia na kusikiliza, unaweza kuona uwepo Wake, na unaweza kusikia sauti Yake ya upendo, ikiita kutoka juu." Labda hii ilikuwa moja ya maelezo bora ya dhana ya MUNGU.
 
Hii ni tafsiri ya tarjama/subtitle lete tafsiri ya wafasiri wa Quran walivyotafsiri.
Hapa kidogo una shida, aya iko wazi sana, aya inasema kisha akastawi juu ya Arshi yake. Maana ya juu iko wazi sana. Sasa unapo taka tafsiri sijui unataka tafsiri gani zaidi ya hiyo ?
Tafsiri ya Imam Qurtubi imeelezea vyema maana ya hiyo aya na ameweka wazi kuwa wanawazuoni wa karne 3 bora msimamo wao ni kuwa Allah ameepukana na upande. Iwe juu, chini, mbele, nyuma, kulia ama kushoto hivyo vyote Allah ameepukana navyo. Kusema Allah yupo juu ya ni makosa. Kwa usahihi na uelewe zaidi na huu si msimamo wangu bali ni Aqida ndivyo inavyosema kwa maelezo ya kina na ya usahihi kaangalie tafsiri ya Imam Qurtubi Juz.7 ukurasa wa 196 ambao ndiyo kauli niliyokupatia.
Je hakuwataja wanazuoni hao wa karne ya tatu ?

Hakuna aqida ya Uislamu inayosema hivi. Sababu hapo mnapingana na aya, maana yake kama Imamu Qurtubiy amesema haya amekosea, anakuwa amefanya "taawili" katika aya.

Tamko kustawi lina maana yake.
Kauli yangu inakwenda sambamba na Imam Hafiz ibn Katheer (Tafseer ibn Katheer Juz. 2 ukurasa 220.
Hapa naona unataka kumsingizia Imam Abul Fida Ismail Imaad diin Ibn Kathiir, katika aya hii yeye anafata uelewa wa wema walio tangulia ambao ni Malik, Al-Awza`i, Ath-Thawri, Al-Layth bin Sa`d, Ash-Shafi`i, Ahmad, Ishaq bin Rahwayh na wengine kwa kuchukua maana ya wazi kama ilivyo kuja katika Qur'aan, na maana hiyo iko wazi na tamko "Istawa" liko wazi. Rejea katika tafsiri yake alipokuwa anafasiri aya hiyo.

Sasa swali langu kwako hiyo kauli yako inayokwenda sambamba na kauli ya Imam Ibn Kathir ni ipi ? Imam Ibn Kathir hana kauli hiyo, sasa kama hujasoma vitabu umekopi marejeo bila kusoma, nenda kasome tena.
-Mungu hayupo juu ya Arshi, na kama yupo juu ya Arshi jiulize kabla ya kuiumba hiyo Arshi alikuwa wapi?
Allab hayupo juu ya Arshi kwa ushahudi gani ? Maana huna ushahidi wowote unao utoa zaidi ya maoni ya hao Wanachuoni, huku ukimsingizia uongo Imam Ibn Kathir.
Wanawazuoni wa Sunnah wal Jamaa wanasema kuwa: Alikuwepo Mwenyezi Mungu bila ya sehemu (juu ya Arshi). Na kama alivyokuwepo bila ya sehemu basi yupo bila ya sehemu. Hii kauli utaipata kwenye kitabu cha Sheikh Mansoor Al Bakhdadi cha Al Farqu baynal Firaq. Ni mwanawazuoni mkubwa wa madhheb ya Imam Shafii. Na huo ndio msingi katika sheria ya Kiislamu kuwa Allah habadiliki.
Haya si madhebeu ya wema walio tanguli, hili amelithibitisha Imam Ibn Kathir, kadhalika Imam Shafii hakuwa na itikadi hiyo.

Nikirudi nakuja kukuelezea wapi hii Itikadi waliitoa. Nilikuuliza unamjua Jahm Ibn Saf'wan ? Huyu ndiyo mwenye itikadi hii na hawa waliathirika na Wanafalsafa na Wakrsito.
 
Hapa kidogo una shida, aya iko wazi sana, aya inasema kisha akastawi juu ya Arshi yake. Maana ya juu iko wazi sana. Sasa unapo taka tafsiri sijui unataka tafsiri gani zaidi ya hiyo ?

Je hakuwataja wanazuoni hao wa karne ya tatu ?

Hakuna aqida ya Uislamu inayosema hivi. Sababu hapo mnapingana na aya, maana yake kama Imamu Qurtubiy amesema haya amekosea, anakuwa amefanya "taawili" katika aya.

Tamko kustawi lina maana yake.

Hapa naona unataka kumsingizia Imam Abul Fida Ismail Imaad diin Ibn Kathiir, katika aya hii yeye anafata uelewa wa wema walio tangulia ambao ni Malik, Al-Awza`i, Ath-Thawri, Al-Layth bin Sa`d, Ash-Shafi`i, Ahmad, Ishaq bin Rahwayh na wengine kwa kuchukua maana ya wazi kama ilivyo kuja katika Qur'aan, na maana hiyo iko wazi na tamko "Istawa" liko wazi. Rejea katika tafsiri yake alipokuwa anafasiri aya hiyo.

Sasa swali langu kwako hiyo kauli yako inayokwenda sambamba na kauli ya Imam Ibn Kathir ni ipi ? Imam Ibn Kathir hana kauli hiyo, sasa kama hujasoma vitabu umekopi marejeo bila kusoma, nenda kasome tena.

Allab hayupo juu ya Arshi kwa ushahudi gani ? Maana huna ushahidi wowote unao utoa zaidi ya maoni ya hao Wanachuoni, huku ukimsingizia uongo Imam Ibn Kathir.

Haya si madhebeu ya wema walio tanguli, hili amelithibitisha Imam Ibn Kathir, kadhalika Imam Shafii hakuwa na itikadi hiyo.

Nikirudi nakuja kukuelezea wapi hii Itikadi waliitoa. Nilikuuliza unamjua Jahm Ibn Saf'wan ? Huyu ndiyo mwenye itikadi hii na hawa waliathirika na Wanafalsafa na Wakrsito.
Unachokifanya ni ujanja wa kujificha kwenye kivuli cha dokezo la kudokoa hapa na pale aina fulani ya maneno kwa kuvisha vazi la ujuzi ili ionekane kuna kitu unajaribu kukiweka sawa kwa kuonesha kuna kitu kipo wrong. Brother, huo mwenendo si mzuri na Mimi si aina ya watu ambao wa kuwachezea mchezo huo.

Maadamu haya masuala ni ya kisomi na yana dalili maneno pekee hayatoshi, inabidi yafungamane na ushahidi.

Kabla ya kunijia mimi na kuyasema niliyoyaweka ni uzushi au uongo au chochote kitakachothibiti kwa tafsiri ya namna hizo inakubidi kwanza uje na ushahidi madhubuti juu yangu.

Nimekupatia ushahidi wa vitabu, hujavisoma na unakuja kukanusha na kusema nina andika uongo. Nimekupatia Juzuu na kurasa zake unadai nimekopi sijasoma. Lakini wewe hauji na ushahidi unakuja na maneno matupu!

Uislamu haumruhusu mtu kuingia kwenye masuala yoyote bila ushahidi na haumruhusu kutoka kwenye masuala yoyote bila ushahidi.

Kikubwa fahmu kuwa hatafutwi bingwa wale aliye mjuzi zaidi. Unaotafutwa ni usahihi. Ukirudi nitag kwa herufi kubwa Hammaz inshallah nitafika.

Ukija njoo na ushahidi.
 
kwa ilo jambo kila jamii zitabashiri kwa imani zao, muislam atasema ivi, mkristo vile n k.

hii siri binadamu kwa akili izi za kimwili sio rahis, tufanye meditation tuongee ktk ulimwengu wa roho
 
Hao watoto wakiwa tumboni walijuaje kama kuna kitu kinaitwa kuzaliwa?
Who certainly informed them about birth?
How did the awareness of birth came to them?
kuwa ipo siku watazaliwa baada ya miezi tisa?

Huenda sijaelewa, naona hiyo nadharia yako Ina ukakasi...ukuilinganisha na suala la mwanadamu kujua kuwa ipo siku atakufa.

Tunajua tutakufa kwa sababu tunaona watu wakifa.
Mapacha waliotungwa mimba, na kujikuta ndani ya mji wa uzazi, wana habari gani kuhusu kuzaliwa? Wanajuaje kama wao ndio mimba ya kwanza au ya pili? Wanaexperience gani ya kuwafanya wapate kujadili afterbirth?

Labda nimekuwa too literal.....huenda pengine ni tafakuri tu kama tafakuri nyingine kuhusu maisha.

Bro uko na akili kubwa sana mm kdg jamaa alitaka kunitingisha n kweli nani amewaambia kua kuna kuzaliwa
 
Hadithi iliyopokelewa na Ibn Jarud, Imam Al Bayhaqii na Bukhari Mtume anasema: "Kana llahu walam ghayrahu shay'aa"
Yaani; alikuwepo Mungu pasipo chochote kuwepo. Kwa maana pasipo Mbingu, Arshi, na kila chochote kuwepo alikuwepo.

Katika msingi wa sheria ya Kiislamu Mungu habadiliki! kama alivyokuwa ndivyo alivyo. Kwa maana; hatuwezi kusema kabla ya Mungu kuanza kuumba haimaanishi kuwa hakuwa na uwezo wa kuumba na alivyoupata ndivyo akaanza kuumba. Msingi wa sheria ya Kiislamu unakataa, unasema Mungu kama alivyokuwa ndivyo alivyo(Tazama aqida katika kitabu cha Imam Tahawi).

Ikiwa hiyo ndiyo hali, kipi kimemfanya abadilike? Yaani; alikuwepo kabla ya chochote na kisha baada ya kuumba akawa juu ya Arshi kama unavyosema. HAYA NI MABADILIKO! Ikiwa hiyo ndiyo hali basi msingi wa sheria ya Kiislamu si sahihi kwani utakuwa umeongopa kwa kusema Mungu habadiliki.

Daaah kuna watu mnauwezo wa kuchamgha mambo mm pia niliwaza mungu baasa ya kukaa muda mrefu ndo akafikiria kuumba dunia kwahy hata yeye anatabia ya kubadilika anafikiria kama sisi
 
"Kana llahu walam ghayrahu shay aa"

"Kana llahu wala qablahu shay aa"

-Alikuwepo Mungu pasipo chochote kuwepo.

-Alikiwepo Mungu kabla ya chochote kuwepo.

Ni hadithi za Mtume.

Kisha baada ya kuumba thumma stawaa al arshi. Kwa hili ukasema Mungu yupo juu ya Arshi.

-Tunafafanuaje hapa?
Ufafanuzi ni kuwa kuna hali mbili: (1)Pasipo/kabla ya chochote
Kwa maana uwepo wake haukutegemea chochote.

(2) Yupo juu ya Arshi
Kutoka katika pasipo au kabla ya chochote mpaka kuwa juu ya chochote ambacho ni Arshi: Haya ni mazingira au hali mbili tofauti. Pengine tuseme "walam ghayrahu shay aa na kqbla huu shay aa tuipe herufi A. Na juu ya Arshi tuipe herufi B. Hivyo, Mungu alikuwa herufi A kisha akawa herufi B. Huko ni kubadilika.

Tuje kwenye msingi wa sheria ya Kisslamu kuwa Mungu habadiliki. Tukikusanya hadithi za Mtume na maneno yako wewe yanaonyesha Mungu yupo herufi B baada ya kutoka herufi A. Swali linakuja; Haya kwako unayaitaje?

Bro ww noma yaan alitokea from nothing akaja akatengeneza arshi yake
 
Unachokifanya ni ujanja wa kujificha kwenye kivuli cha dokezo la kudokoa hapa na pale aina fulani ya maneno kwa kuvisha vazi la ujuzi ili ionekane kuna kitu unajaribu kukiweka sawa kwa kuonesha kuna kitu kipo wrong. Brother, huo mwenendo si mzuri na Mimi si aina ya watu ambao wa kuwachezea mchezo huo.

Maadamu haya masuala ni ya kisomi na yana dalili maneno pekee hayatoshi, inabidi yafungamane na ushahidi.

Kabla ya kunijia mimi na kuyasema niliyoyaweka ni uzushi au uongo au chochote kitakachothibiti kwa tafsiri ya namna hizo inakubidi kwanza uje na ushahidi madhubuti juu yangu.

Nimekupatia ushahidi wa vitabu, hujavisoma na unakuja kukanusha na kusema nina andika uongo. Nimekupatia Juzuu na kurasa zake unadai nimekopi sijasoma. Lakini wewe hauji na ushahidi unakuja na maneno matupu!

Uislamu haumruhusu mtu kuingia kwenye masuala yoyote bila ushahidi na haumruhusu kutoka kwenye masuala yoyote bila ushahidi.

Kikubwa fahmu kuwa hatafutwi bingwa wale aliye mjuzi zaidi. Unaotafutwa ni usahihi. Ukirudi nitag kwa herufi kubwa Hammaz inshallah nitafika.

Ukija njoo na ushahidi.

Bro we n hatar yaan huwa nakaa jamii forums naona watu wamesoma
Mm sjasoma sana na ninazipinga dini
 
Kwanza kabisa tangu uanze kujadili hili hujaweka ushahidi hata mmoja, zaidi ya kauli za wanazuoni tena kwa kuwaelewa vibaya. Mimi nimekuwekea aya ambayo iko wazi kabisa inayosema Allah amestawi juu ya Arshi yake, wewe unasema Imam Qurtubiy amekataa hilo, bila kuelezea yeye ameegemea wapi ?

Kadhalika ukamzulia uongo Imam Ibn Kathiri, tafuta kitabu chochote alichoandika Imam Ibn Kathiri hapingi hilo na anakubali ya kuwa Allah yuko juu ya Arshi yake na haki.

Sasa maana ya ushahidi ni Qur'aan, Sunnah, kauli za Maswahaba na maneno ya Wanazuoni yasiyo pingana na hivyo vitatu vya mwanzo. Sasa huwezi kusema umeweka ushahidi maneno ya wanachuoni halafu yanapingana na Wahayi ukasema huo ni ushahidi, hakuna ushahidi wa hivyo kijana.

Sasa unapoanza kujihami kwa kusema mimi naleta ujanja wakati jambo liko wazi, wewe unaonekana haya mambo hujayasoma, au unanakili sehemu ndiyo maana huwezi kuelezea na kujibu maswali ninayo kuuliza.

Kwahiyo hapo hujaweka ushahidi wowote kijana.

Kitu kingine nilichokiona kwako ni kuwa hivyo vitabu unavyo vinukuu hujavisoma, mfano ulipo sema ya kuwa Imam Ibn Kathiri anaenda sambamba na kauli yako, hili kwa mtu tu ambaye anamjua vizuri Imamu Ibn Kathir hata bila kusoma au kurejea katika kitabu chake, hawezi kukubali ya kuwa Imam Ibn Kathir anaweza kusema hayo au kuunga mkono hilo, sababu Imam Ibn Kathir alikuwa mtu wa hadithi na watu wa Hadithi walikuwa wanafata ufahamu wa wema walio tangulia, ndiyo maana hicho ulicho kinasibisha na Imam Ibn Kathir tena kwenye Tafsiri yake hakipo, sasa nakuuliza wewe umekipata wapi ?

Sasa kuna mapote (firaq) yanajinasibisha na Uislam lakini kiuhalisia wako mbali na Uislamu mapote haya yanakanusha baadhi ya sifa za Allah, na katika hili wapo Jahmiyah, hawa wanakataa ya kuwa Allah hayupo juu, lakini hawana hoja zaidi ya Falsafa, watu hawa waliathiriwa na Falsafa za kina Aristotle, wakaja kuingiza mfumo wa kuhoji huo katika Uislamu. Watu hawa tunawaita "Mutakalimiin au Ahlul Kalaam" yaani watu wa maneno maneno na kucheza na maneno, na wewe ndiyo upo humo, yaani mwanzo mwisho hutoi ushahidi na ukiweka ushahidi unapotosha maana.

Sasa nitakuuliza kuna ushahidi gani katika dini yetu kuzidi Qur'aan na Hadithi ? Sasa tuwekee aya na Hadithi zinazo pinga kwamba Allah hayuko juu ?

Nikirudi nakuja kukuonyesha namna mlivyo mzulia Imam Abuu Jaafari Twahawiy Allah amrehemu, wala hapingi ya kuwa Allah hayuko juu. Huenda humjui Imam huyu, huyu alikuwa na itikadi ya Salaf na alikuwa mtu wa Hadithi wala hakuwa Jahmiya, wala Ashaariya, wala Kulabiyya wala hakuwa Muutazila.
 
Hiki kitabu kipo ukihitaji tukipitie tutakipitia hapa hapa na hakuna shaka Mkuu ni kuelimishana tuu!
Siyo tu kipo mimi ninacho hard copy, sherehe maarufu iitwayo "Sharhu aqidat st-Twahawiyah" sherehe ya Imam Abul 'Izz al Hanafiy mwenye kitabu Al-Urjuzat al-Miiyah fiy dhikri haali ashrafu al-Baariyah".

Kwahiyo cha msingi ni kusoma kilichomo, wewe utaniambia unayo matini au na Sherehe ?
 
Kwanza kabisa tangu uanze kujadili hili hujaweka ushahidi hata mmoja, zaidi ya kauli za wanazuoni tena kwa kuwaelewa vibaya. Mimi nimekuwekea aya ambayo iko wazi kabisa inayosema Allah amestawi juu ya Arshi yake, wewe unasema Imam Qurtubiy amekataa hilo, bila kuelezea yeye ameegemea wapi ?
Kwenye dini kuna kitu kinaitwa Isnaad. Utasikia miongoni mwa watu wanasema wanafuata Quran na Sunnah! Anafungua Quran mwenyewe na kuisoma. Anafungua hadithi na kuisoma, na ili ajue kinachozungumziwa ni kipi anatafuta translation ya Quran au hadithi na kilichofanyika ni ukalimani wa kutoka lugha ya kiarabu kuja kwenye lugha ambayo anayoielewa.

Vipi kama wale walioishi karne 3 bora zilizopita wasingewafuata wanawachuoni ingelikuwaje kama kila mtu angelisema nafuata Quran na Sunna kwa kutohoa aya na kwa kusema ewaaa! Aya imelisema hivi basi ndio ipo hivyo! Jawabu ni kuwa watu wangelisema chochote wanachokitaka lakini ni nani angelihakiki kwa kusema hiki kilichozungumzwa ni sahihi? Ni wanawazuoni pekee, na hii ni kwa sababu kuna Isnaad: Kama Imam Shafii kasoma kwa Imam Malik, Malik kasoma kwa Ibn Maula, Ibn Maula kwa Abdallah ibn Umar ambaye ni sahaba ambaye kasoma kwa Mtume. Kwa hili Mtume akasema; Wanawazuoni ni warithi wa Mitume.

Quran huwezi kuielewa inasema nini kama hujapatiwa fafanuzi kutoka kwa wanawazuoni na hadithi hauwezi kuielewa inasema nini kama haujapata fafanuzi kutoka kwa wanawazuoni. Ikiwa kama utabeba maneno ya Quran na hadithi literally kuwa makini kuna baadhi ya aya zinazungumzia mapambano zitazame nyayo zako usijeukaangukia kwenye úgaidi. Na ikiwa utakataa maneno ya wanawazuoni tambua útakuwa miongoni mwa watakaokuwa majangani.

Pia tambua: Criticising is the job that requires zero qualifications. Unasema nimewaelewa wanawazuoni vibaya hauoneshi huo uzuri. Haya si mashindano! Kukazania huko pengine unaona ni uzalendo wa dini kumbe suala ni dogo tu nalo ni tusome. Kuna aya inasema "Allahu nuru ssamawaati wal ardh"-Mungu ndiye nuru ya mbinguni na ardhini. Hii ni tarjama! Umebadilisha lugha tu kutoka Kiarabu kuja Kiswahili lakini ukiitakidi hivi utakua umekosea kwa sababu "laysa ka mithlihi shay aa" Mungu hamithiliki na chochote. Iyyaka na abudu wa iyyaka nastaiin- Wewe tu ndiye tunaekuabudu na wewe tu ndie tunaekuomba msaada. Ikiwa Yee ukiondoa shadda maana yake itabadilika, itakuwa "Mwangaza tunakuabudu, mwangaza tunakuomba msaada". Kinachoangaza ni chenye nuru lakini ikiwa hii aya ukiitamka hivi utakuwa umekosea na wanawazuoni wengine wanasema umeingiza shirki. Kwa sababu Mungu hamithiliki na chochote. Tafsiri sahihi ya mfano wa aya ya kwanza ni "Mungu ndiye mpatishanaji wa nuru ya Mbinguni na ardhini".

Kwa kusema Imam Qurtubi ameegemea wapi(?) hili swali linaonyesha dhahiri tunahitaji kukaa chini kusoma. Quran tafsiri yake yote ni kauli thabiti haina kusema imeegemea wapi! Tafsiri za aya si rai/jitihada za wanawazuoni bali ni kama zilivyopokelewa na maswahaba kutoka kwa Mtume. Wanawazuoni wanasema aya 1 ya Quran kwa uchache ina maana zaidi ya 7 na kila moja ni tofauti na ipo deep. Imam Qurtubi kakusanya takribani zote na ndiyo maana kwa tafsiri za Quran huyu Imam yeye ndiye anayeitwa Beberu kwa Imam wote Mufassoruun basi yeye ndiye Beberu.

MManeno sehemu nyengine yanaweza kisomeka kama yenye ukakasi, yasikutishe! Mwili na akili vimechoka kutokana na majukumu. Hivyo ninaandika nikiwa katika hali ya machovu.

Mungu hayupo juu ya Arshi.
 
Kwenye dini kuna kitu kinaitwa Isnaad. Utasikia miongoni mwa watu wanasema wanafuata Quran na Sunnah! Anafungua Quran mwenyewe na kuisoma. Anafungua hadithi na kuisoma, na ili ajue kinachozungumziwa ni kipi anatafuta translation ya Quran au hadithi na kilichofanyika ni ukalimani wa kutoka lugha ya kiarabu kuja kwenye lugha ambayo anayoielewa.
Hili liko wazi na linajulikana. Sasa hiyo aya inayosema Allah baada ya kuumba mbingu na ardhi akastawi juu ya Arshi yake, kisichoeleweka hapo ni nini ? Yaani kabla hujaenda kwa Wanachuoni aya inamaanisha nini ? Aya iko wazi.

Ukitaka ufafanuzi sasa ndiyo unarudi kwa Maswahaba kwanza, hawa wali muona Mtume na Mtume aliwafasiria Qur'aan, sasa tutaka tujue je Maswahaba walielewa vipi hiyo aya au Maswahaba wanasema Allah hayupo juu ya Arshi ? Jibu ni kinyume wanakubali Allah yuko juu ya Arshi. Maimamu wote wanne wanakubali Allah yuko juu ya Arshi, lakini wao husema ya kuwa ukiona kauli zao zinapingana na maneno ya Mtume basi acheni kauli zao na mfate nususi. Hii ndiyo itikadi yetu sisi Waislamu.

Sasa kauli za Wawanachuoni zinachukuliwa endapo hazija pingana na Qur'aan na Hadithi za Mtume.

Sasa ulipata wapi ujasiri wa kumzulia Imam Ibn Kathir ? Ukapata wapi ujasiri wa kumzulia Imam Abuu Jaafar Tahawi ? Hili najua wewe umecopy sababu nawajua wenye itikadi hizi ni kina nani.

Sasa kitabu cha Imam Abuu Jaafari at-Twahawiy hiki hapa na sherehe yake imefanywa na Imam Ibn Abil 'Izz al Hanafi, hukuti maana ya maneno yako kama ulivyo muelezea Imam.

Taaliq ya Sherehe hii imefanywa na Imam Al-Albaaniy, tafuta isome.
 
Attachments

  • IMG_20220607_092105.jpg
    IMG_20220607_092105.jpg
    778.2 KB · Views: 25
Vipi kama wale walioishi karne 3 bora zilizopita wasingewafuata wanawachuoni ingelikuwaje kama kila mtu angelisema nafuata Quran na Sunna kwa kutohoa aya na kwa kusema ewaaa! Aya imelisema hivi basi ndio ipo hivyo! Jawabu ni kuwa watu wangelisema chochote wanachokitaka lakini ni nani angelihakiki kwa kusema hiki kilichozungumzwa ni sahihi? Ni wanawazuoni pekee, na hii ni kwa sababu kuna Isnaad: Kama Imam Shafii kasoma kwa Imam Malik, Malik kasoma kwa Ibn Maula, Ibn Maula kwa Abdallah ibn Umar ambaye ni sahaba ambaye kasoma kwa Mtume. Kwa hili Mtume akasema; Wanawazuoni ni warithi wa Mitume.
Sasa ulitakiwa kwanza ulete maana ya hiyo aya toka kwa Swahaba je wanaifasiri vipi hiyo aya. Lakini hili huna, hakuna Imam wa Ahlul Sunnal, wenye kuelewa hiyo aya kama unavyosema wewe, hakuna si Imam Shaafi wala Ibn Kathiir.

Jina la mwalimu wa Imam Maalik siyo Maula sahini ni Nafi hilo Mawla siyo jina lake bali alikuwa ni mtumwa wa swahaba Ibn Umar.
 
Quran huwezi kuielewa inasema nini kama hujapatiwa fafanuzi kutoka kwa wanawazuoni na hadithi hauwezi kuielewa inasema nini kama haujapata fafanuzi kutoka kwa wanawazuoni. Ikiwa kama utabeba maneno ya Quran na hadithi literally kuwa makini kuna baadhi ya aya zinazungumzia mapambano zitazame nyayo zako usijeukaangukia kwenye úgaidi. Na ikiwa utakataa maneno ya wanawazuoni tambua útakuwa miongoni mwa watakaokuwa majangani.
Hili siyo lazima sana sababu aya ziko wazi kama vile Mola wetu ni mmoja au hajazaa wala hajazaliwa au amestawi juu ya Arshi yake.

Sasa wewe nitakuuliza swali, ni nani katika Maswahaba walikuwa na uelewa huo juu ya aya hiyo ? Sasa usandike maneno mengi ambayo hayana maana yoyote.
 
Siyo tu kipo mimi ninacho hard copy, sherehe maarufu iitwayo "Sharhu aqidat st-Twahawiyah" sherehe ya Imam Abul 'Izz al Hanafiy mwenye kitabu Al-Urjuzat al-Miiyah fiy dhikri haali ashrafu al-Baariyah".

Kwahiyo cha msingi ni kusoma kilichomo, wewe utaniambia unayo matini au na Sherehe ?
Nimeshakuambia na nairejea tena haya hayatakusaidia! Mimi sihimiliwi kwenye hoja kwa mfano wa unayoyafanya. Aliyesoma vitabu iwezo wake unakwenda sambamba na hoja anazozitoa uwiano wake upo kwa kiasi gani! Ukiwa uwiano ni mashariki na magharibi jawabu lipo wazi ya kuwa mhusika anajaribu kututumua misuli. Mimi sishindani na wala si kuonekana mjuzi Jf. Nitakusanya ninachokijua hatua hatua ushahidi kwa ushahidi pindi nitakapopata muda inshaallah ili kukupatia.
 
Sasa ulitakiwa kwanza ulete maana ya hiyo aya toka kwa Swahaba je wanaifasiri vipi hiyo aya. Lakini hili huna, hakuna Imam wa Ahlul Sunnal, wenye kuelewa hiyo aya kama unavyosema wewe, hakuna si Imam Shaafi wala Ibn Kathiir.

Jina la mwalimu wa Imam Maalik siyo Maula sahini ni Nafi hilo Mawla siyo jina lake bali alikuwa ni mtumwa wa swahaba Ibn Umar.
Naona Mzee unaleta ligi!

Anaitwa Nafii Ibn Mawla ambaye mwalimu wake ni ibnu Umar (Abdallah Ibn Umar).

Ushahidi wa aya nitakupatia tu nitakupigia na picha na usikimbie humu. Kesho au kesho kutwa nitakupatia humu Inshaallah! Na Uzuri Imam Qurtubi ndivyo alivyotafsiri Aya!
 
Ukitaka ufafanuzi sasa ndiyo unarudi kwa Maswahaba kwanza, hawa wali muona Mtume na Mtume aliwafasiria Qur'aan, sasa tutaka tujue je Maswahaba walielewa vipi hiyo aya au Maswahaba wanasema Allah hayupo juu ya Arshi ? Jibu ni kinyume wanakubali Allah yuko juu ya Arshi. Maimamu wote wanne wanakubali Allah yuko juu ya Arshi, lakini wao husema ya kuwa ukiona kauli zao zinapingana na maneno ya Mtume basi acheni kauli zao na mfate nususi. Hii ndiyo itikadi yetu sisi Waislamu.
Upo wapi ushahidi?
 
Sasa ulitakiwa kwanza ulete maana ya hiyo aya toka kwa Swahaba je wanaifasiri vipi hiyo aya. Lakini hili huna, hakuna Imam wa Ahlul Sunnal, wenye kuelewa hiyo aya kama unavyosema wewe, hakuna si Imam Shaafi wala Ibn Kathiir.

Jina la mwalimu wa Imam Maalik siyo Maula sahini ni Nafi hilo Mawla siyo jina lake bali alikuwa ni mtumwa wa swahaba Ibn Umar.
Kuwa na mipaka!

Mwenye elimu huwa anasema mimi kwangu haikunifikia, kama unaelimu nalo tupatie ushahidi.

Inshaallah nitakueletea ushahidi ila usikimbie humu! Tuwekane wazi kabisaaa usikimbie humu!
 
Back
Top Bottom