Mungu nisamehe kwa nilichotaka kufanya

Mungu nisamehe kwa nilichotaka kufanya

Binafsi kifo cha Mpauko kimenipa funzo sana. Nimepitia nyuzi zote na comment Mungu naomba tu unisamehe kwa mawazo niliyokua nayo.

Binafsi nilizaa 2014 mume akafariki ghafla kwa ajali nikabaki na mtoto. Nilihangaika sana sababu sikuwa na pakushika.

Mama yangu alikuwa Mtendaji alistaafu 2015, bahati nzuri akanipa mtaji milioni 1.5 nikafungua duka la dawa. Mungu akanisaidia nikawa naenda vizuri na maisha, 2016 nikapata mchumba aliyekuwa tempo TANESCO. Mshahara ulikuwa haukidhi na maisha ya kwao yalikuwa duni sana hivyo yeye ndio alikuwa tegemezi.

Kidogo mimi biashara haikunitupa hivyo akikwama nilikuwa namsaidia. Mungu akamsaidia Januari 2018 akapata ajira ya Uengineer mkoa mwingine. Turifurahi sababu tulimuomba sana Mungu.

Baada ya mwaka akanitolea mahari nikahamia anapoishi. Duka nikaweka mtu akaniiibia nikabaki ikabidi nilifunge. Jamaa akanifungulia duka lingine huku tulipohamia. Jamaa mshahara ukawa mzuri hakosi milioni 4 kwa mwezi pamoja na overtime, marupurupu kibao.

Akabadilika akawa hanishirikishi tena, hatupangi pamoja kama zamani tukipata kidogo tunapanga pamoja.

Changamoto ikawa uzazi ukagoma tangu 2018 mwenzangu ana hamu sana ya mtoto. Last year nikapata ujauzito Juni 26 ukatoka. Nimehangaika hospitali, dawa za kienyeji, tiba lishe, bila mafanikio.

Jamaa kaanzisha mahusiano na mfanya kazi wake mpaka kumleta ndani. Nikimuuliza anadai anatafuta mtoto.

Duka nililofungua jamaa hela zote anachukua.
Mtoto wangu shule mwaka huu kasimama. Nikimpigia mama anadai vumilia sasa utaenda wapi ushapoteza kila kitu?

Inafikia hatua unaona dunia imekutenga, huna thamani tena hasa inapofikia usiku jamaa analala nje ukimpigia anadai anatafuta mtoto.

Nilikata tamaa nikaamua nimpe sumu mtoto wangu na mimi ninywe ili haya maumivu yapotee. Juzi nimechukua mtoto tukaja guest house ili tufe wote. Kila nikitaka nimpe anywe anakuja na story nzuri tunacheka naogopa jamani.

Nisamehe Mungu wangu natubu mimi mbele zako. Eee Mungu baada ya kusoma kifo cha mpauko nisamehe mimi. Acha nipambane tu bado Mungu una makusudi na maisha yangu. Sasa hivi saa 11 sijafumba macho hata tone moja.

Jamani tupeane tu moyo haya maisha hatujui tunapitia yapi. Wewe unaweza kuwa na furaha usifikiri ni wote. Mtu akiomba ushauri humu tufarijiane tu wengine JF inatupa faraja sana.

Mbarikiwe
Pole sana dada, yatapita yote hayo na kubaki historia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
God bless the Woman. Lucky Dube

In the middle of the night I heard her pray
So bitterly and so softly, yeah
She prayed for her children
She prayed for their education
Then she prayed for the man
That left her with her children
We praise heroes everyday
But there are those that we forget to praise
The women of this world
They don't run from anything
They stand and fight for what's right
Oh oh oh
God bless the women
Even when times are so hard
They are so cool, calm and collected
They don't run from anything
They stand and fight for what is right
They do not run from responsibilities
They stand and fight for what Is right
Oh oh oh
God bless the women
 
Wana jf mmebadilika, kila mtu kaingiwa na huruma, hakuna comments za kejeli tena. [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]. Mtarudi tu mule mule soon. Ngoja na mimi nishushe uzi wangu kuhusu marehemu mpauko. Huko aliko anawachora tu kwa unafiki wenu

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo mpauko kweli nimemfahamu Jana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole kwa mitihani unayopitia ndugu, kikubwa mshinde shetani na majaribu yake. Sali sana mlilie Mungu ndie atoae na atupae hujui mbele kuna nini. Kingine usiwe mnyonge kama mauzo ya siku chukua kidogo zako tunza zikusaidie wewe na mtoto.
Huyo mme wako na wasiwasi yeye ndo mwenye tatizo[emoji19].
Toa address uliyopo huwezi jua kuna mwanajf akavutika kukusaidia chochote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole dada lakini unachokosea ni kumfanya huyo jamaa kama mungu mtu. Yeye asipoona thamani yako, kwa mtoto au ndugu zako una thamani sana. Kusanya mtaji wako, mpe jamaa nafasi ya kujitanua fanya mambo yako. Unaye mtoto mmoja. Kuna watu hawana kabisa hata mmoja. Acha kukumbatia tatizo. Jihesabu umekosea, fanya maisha mengine. Binadamu muda wowote wanakufa, hatuna haja ya kuwekeza furaha zetu kwao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi kifo cha Mpauko kimenipa funzo sana. Nimepitia nyuzi zote na comment Mungu naomba tu unisamehe kwa mawazo niliyokua nayo.

Binafsi nilizaa 2014 mume akafariki ghafla kwa ajali nikabaki na mtoto. Nilihangaika sana sababu sikuwa na pakushika.

Mama yangu alikuwa Mtendaji alistaafu 2015, bahati nzuri akanipa mtaji milioni 1.5 nikafungua duka la dawa. Mungu akanisaidia nikawa naenda vizuri na maisha, 2016 nikapata mchumba aliyekuwa tempo TANESCO. Mshahara ulikuwa haukidhi na maisha ya kwao yalikuwa duni sana hivyo yeye ndio alikuwa tegemezi.

Kidogo mimi biashara haikunitupa hivyo akikwama nilikuwa namsaidia. Mungu akamsaidia Januari 2018 akapata ajira ya Uengineer mkoa mwingine. Turifurahi sababu tulimuomba sana Mungu.

Baada ya mwaka akanitolea mahari nikahamia anapoishi. Duka nikaweka mtu akaniiibia nikabaki ikabidi nilifunge. Jamaa akanifungulia duka lingine huku tulipohamia. Jamaa mshahara ukawa mzuri hakosi milioni 4 kwa mwezi pamoja na overtime, marupurupu kibao.

Akabadilika akawa hanishirikishi tena, hatupangi pamoja kama zamani tukipata kidogo tunapanga pamoja.

Changamoto ikawa uzazi ukagoma tangu 2018 mwenzangu ana hamu sana ya mtoto. Last year nikapata ujauzito Juni 26 ukatoka. Nimehangaika hospitali, dawa za kienyeji, tiba lishe, bila mafanikio.

Jamaa kaanzisha mahusiano na mfanya kazi wake mpaka kumleta ndani. Nikimuuliza anadai anatafuta mtoto.

Duka nililofungua jamaa hela zote anachukua.
Mtoto wangu shule mwaka huu kasimama. Nikimpigia mama anadai vumilia sasa utaenda wapi ushapoteza kila kitu?

Inafikia hatua unaona dunia imekutenga, huna thamani tena hasa inapofikia usiku jamaa analala nje ukimpigia anadai anatafuta mtoto.

Nilikata tamaa nikaamua nimpe sumu mtoto wangu na mimi ninywe ili haya maumivu yapotee. Juzi nimechukua mtoto tukaja guest house ili tufe wote. Kila nikitaka nimpe anywe anakuja na story nzuri tunacheka naogopa jamani.

Nisamehe Mungu wangu natubu mimi mbele zako. Eee Mungu baada ya kusoma kifo cha mpauko nisamehe mimi. Acha nipambane tu bado Mungu una makusudi na maisha yangu. Sasa hivi saa 11 sijafumba macho hata tone moja.

Jamani tupeane tu moyo haya maisha hatujui tunapitia yapi. Wewe unaweza kuwa na furaha usifikiri ni wote. Mtu akiomba ushauri humu tufarijiane tu wengine JF inatupa faraja sana.

Mbarikiwe

Pole sana new hamida...karibia kila mtu anapitia changamoto...jambo la msingi ni kupiga moyo konde na kuendelea kupambana...mahusiano mengi ndo chanjo cha watu wengi kujiuwa...mnaanza vizuri mkiwa hamna kitu...ila maisha yanapoanza kuwachangania shetani na vikwazo vinainuka...

Rudi kwa hiyo mwanaume...lakini this time ukiwa na strategy nzuri...nenda kapambane upate mtaji wa biashara..na kwa kuwa tayari wewe ni mfanya biashara mzuri...hakika utasimama tena..

IN GOD WE TRUST..
 
Back
Top Bottom