Mungu hayupo? Atheist njooni mthibitishe

Mungu hayupo? Atheist njooni mthibitishe

Mkuu

Mkuu,
Consciousness haiendi beyond senses zetu kama unavyosema. Binadamu tunapata ufahamu Kwa kupitia milango yetu ya fahamu na logical reasoning. Hivyo, huwezi kutenganisha ufahamu na milango ya ufahamu.
Pia sikubaliani na wewe unaposema kwamba hata mtu aliyekufa anabaki na ufahamu wake. Unless unithibitishie Hilo au uniambie namna isiyo na mashaka nikathibitishe kwamba maiti ina ufahamu.
Siwezi kubishana mimi. Have a good Day mkuu.
 
Habari

Mimi ni muumini mzuri wa dini ya kikristo, nimezaliwa na kukulia katika dini. Hiyo haikuwa sababu ya kunizuia kusoma maandiko na machapisho ya dini zengine.

Nimesoma Quran pale nilipo bahatika, nikasoma maandiko ya freemasons yale niliyokutana nayo, nimesoma vitabu vya wahindu kwa uchache wake.

Vyote hivyo vinamuelezea Mungu vizuri kabisa na vimejitosheleza. Lakini hawa jamaa "Atheist" watu wasioamini uwepo wa Mungu.

Maandiko yao yamekuwa yakinipa ukakasi sana. Leo naomba Atheist mje hapa nanithibitishie kuwa Mungu hayupo.

Nipe sababu ikikupendeza nielezee kwanini unasema Mungu hayupo, nithibitishie kuwa hakuna, hajawahi kuwa Mungu wa aina yoyote ile.

Thibitisha kuwa Allah hayupo, hayupo Yehovah, hayupo Shiva, Vinshu. Yaani hii dunia haiendeshwi na Mungu
Hajawahi onekana...
 
Hata mtu ambae hajaenda shule, atajibu kuwa mateso na maafa duniani inathibitisha Mungu hayupo.
 
Matukio gani hayo supernatural? Kama hayelezeki Kwa hizi senses tano basi ni mambo ya dhahania!

Wacha kujitoa ufahamu kama kwamba haujui haya mavitu, nenda hata hapo kwa mganga yeyote akufanyie mavitu supernatural utie akili.
 
Ndugu,
Mkuu Kiranga na wengine wameeleza logical contradictions za dhana ya uwepo wa Mungu katika Uzi huu huu na zingine pia. Naomba urudi juu kidogo usome comments kadhaa walau or else, nitakuja kukuwekea angalau list fupi ya hoja hizo.
Nishawajibu nahitaji zako
 
Habari

Mimi ni muumini mzuri wa dini ya kikristo, nimezaliwa na kukulia katika dini. Hiyo haikuwa sababu ya kunizuia kusoma maandiko na machapisho ya dini zengine.

Nimesoma Quran pale nilipo bahatika, nikasoma maandiko ya freemasons yale niliyokutana nayo, nimesoma vitabu vya wahindu kwa uchache wake.

Vyote hivyo vinamuelezea Mungu vizuri kabisa na vimejitosheleza. Lakini hawa jamaa "Atheist" watu wasioamini uwepo wa Mungu.

Maandiko yao yamekuwa yakinipa ukakasi sana. Leo naomba Atheist mje hapa nanithibitishie kuwa Mungu hayupo.

Nipe sababu ikikupendeza nielezee kwanini unasema Mungu hayupo, nithibitishie kuwa hakuna, hajawahi kuwa Mungu wa aina yoyote ile.

Thibitisha kuwa Allah hayupo, hayupo Yehovah, hayupo Shiva, Vinshu. Yaani hii dunia haiendeshwi na Mungu
Kuna maneno mawili watu huyachanganya.

Atheism na blasphemy.

Atheism hawana uthibitisho wa uwepo wa Mungu..

Blasphemy ni kumtukana Mungu na hunywa na wale walioamini uwepo wake kisha wakakanusha kwa maana ni waislam na wakristo waliokufuru.

Sasa wewe ndie mwenye wajibu wa kuwathibitishia uwepo wa M.Mungu.

Utaweza?!?
 
Habari

Mimi ni muumini mzuri wa dini ya kikristo, nimezaliwa na kukulia katika dini. Hiyo haikuwa sababu ya kunizuia kusoma maandiko na machapisho ya dini zengine.

Nimesoma Quran pale nilipo bahatika, nikasoma maandiko ya freemasons yale niliyokutana nayo, nimesoma vitabu vya wahindu kwa uchache wake.

Vyote hivyo vinamuelezea Mungu vizuri kabisa na vimejitosheleza. Lakini hawa jamaa "Atheist" watu wasioamini uwepo wa Mungu.

Maandiko yao yamekuwa yakinipa ukakasi sana. Leo naomba Atheist mje hapa nanithibitishie kuwa Mungu hayupo.

Nipe sababu ikikupendeza nielezee kwanini unasema Mungu hayupo, nithibitishie kuwa hakuna, hajawahi kuwa Mungu wa aina yoyote ile.

Thibitisha kuwa Allah hayupo, hayupo Yehovah, hayupo Shiva, Vinshu. Yaani hii dunia haiendeshwi na Mungu
Na wewe thibitisha Mungu yupo kwanza...sio useme una amini Mungu yupo.!

Thibitisha Mungu yupo.

Ukisema una amini Mungu yupo kwa imani tu na Atheist wana amini Mungu Hayupo kwa imani.
 
Mimi ni mmoja kati ya wanaoamini uwepo wa Mungu. Ila nikiangalia hoja za wenzangu mnaoamini, nikalinganisha na za hao atheists (wasioamini), niwe mkweli tu, wenzangu mko na hoja dhaifu sana!

Mtu anathibitisha vipi kitu ambacho haamini uwepo wake? Nikisema ndani kwangu kuna tembo, basi ni jukumu langu kuthibitisha kwamba kweli tembo yupo. Sio niseme eti ndani kwangu kuna tembo, alafu niseme "ambae haamini kama ndani kwangu kuna tembo athibitishe". Huo ni utoto!

Ukimtuhumu mtu kua ni mwizi, basi ni jukumu lako kuthibitisha kwamba mtu huyo ni mwizi. Sio useme fulani ni mwizi, alafu tena useme "kama sio mwizi, athibitishe ". That's a simple judicial logic!
Kama una amini Mungu yupo na huwezi kuthibitisha uwepo wake, Tambua kwamba na Atheist pia wana amini Mungu hayupo na hawawezi kuthibitisha kutokuwepo kwake.

Unataka uthibitisho wa Mungu kutokuwepo wakati na wewe binafsi huwezi kuthibitisha uwepo wa Mungu.

Kila mtu na imani yake.
 
Hayupo wa kuthibitisha kuwa hayupo.

Watakuja kukosoa ushahidi wa yeye kuwepo.

Watashindwa kujibu maswali ya msingi kama imekuaje tuna huu ulimwengu

Hawana ushahidi zaidi watata kasoro za kiimani ilhali nao hawana chochote kuthibitisha vinginevyo.

‘It’s fascinating to listen to them’
Wewe una uthibitisho na ushahidi wa uwepo wa Mungu???

Usiseme una imani ya uwepo wa Mungu,Imani sio uthibitisho ni illusion tu,leta uthibitisho wa Mungu kuwepo...!!
 
Wacha kujitoa ufahamu kama kwamba haujui haya mavitu, nenda hata hapo kwa mganga yeyote akufanyie mavitu supernatural utie akili.
Mkuu, hao waganga tumeishi nao na tunajua kwamba wanachezea watu akili tu. Wakati mwingine wanatumia vitu vya kawaida (mchanganyiko wa dawa za mitishamba) vya kuweza kuleta madhara Kwa binadamu na kujifanya ni mizimu imefanya.
 
Na wewe mleta mada Thibitisha Mungu yupo.

Leta uthibitisho wa Mungu kuwepo.
 
Mkuu, hao waganga tumeishi nao na tunajua kwamba wanachezea watu akili tu. Wakati mwingine wanatumia vitu vya kawaida (mchanganyiko wa dawa za mitishamba) vya kuweza kuleta madhara Kwa binadamu na kujifanya ni mizimu imefanya.

Nimekushauri nenda kilingeni kabisa umjaribishe yeyote, acha wale wa mitishamba ambao hamna kikubwa zaidi ya kulisha watu majani, naongea kuhusu wale wa mazingaombwe unaingia kwake anakutajia majina ya watu wenu na kukuonyesha kabisa kwenye kioo unawaona, supernatural phenomena do exist, the type that science can not explain, and can not be comprehended by use of our five senses.

Magics kama hizi ni some of them

Wewe una uthibitisho na ushahidi wa uwepo wa Mungu???

Usiseme una imani ya uwepo wa Mungu,Imani sio uthibitisho ni illusion tu,leta uthibitisho wa Mungu kuwepo...!!
Kwani unaielewaje dhana ya Mungu mkuu?

Mungu ni nini kwako?
 
Sio mcheke [emoji23][emoji23][emoji23]

Fanyen kuthibitisha mumg hayupo jukwaa ni huru
Mkuu upo serious kweli?[emoji23]
Ushaambiwa kitu hakipo unataka aliyesema hakipo ndo athibitishe.....
Sasa athibitishe nini wakati hakipo?

Hapo wa kuthibitisha ni aliyesema kipo
Maana ana uhakika kama kipo na ana uwezo wa kuthibitisha kama kipo

Nakuambia ndani kwangu hakuna redio unaniambia nithibitishe kama haipo?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Mim nathibitisha uwepo wa mungu wew unanambia namuomba mtu athibitishe why mungu hayupo.

Nin kimekuonesha mim nmemwambia mtu athibitishe mungu hayupo. Nanukuu "Usiku na mchana kunadhihirisha mungu yupo sabab hakujawai kutokea mchana mda wa usiku na usiku mda wa mchana means vipo organised.Who organised this?"

Hio who organised this? Ndo inakuchangany au

Mnajua mnanifrahisha nyie watu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mkuu,
1. Milango yetu ya fahamu inatuthibitishia uwepo wa vitu physical. Beyond physical realities ni abstract thinking ambayo huhitaji kutumia logic ili kufikia conclusion. Kiufupi ni kwamba tutatumia senses kuthibitisha uhalisia wa physical beings na logic Kwa ajili ya vitu abstract.
Jaribu kuwa una jibu maswali ninayo kuuliza ili mjadala uende vizuri. Nimekuuliza unakubali ya kuwa milango ya fahamu Ina ukomo ?

Kingine umeongelea kuhusu logic, logic ni nini ? Unaweza kutumia logic kujua ukweli wa jambo kama lilivyo ?

Katika aya ya kwanza unasema beyond physical realities huhitaji kutumia logic lakini mwisho unasema kwa abstract unatumia logic, Sasa kipi ni kipi ? Mimi nakupa kazi tumia logic kuujua ukweli wa chanzo Cha ulimwemgu.

2. Kuhusu akili, akili ni dhana abstract. So huwezi kuiona au kuihisi. Ila tunathibitisha uwepo wa akili Kwa kufuata logic na Kuna vipimo vya kupima uwezo wa akili.
Labda sijui maana ya dhana, unaposema akili ni dhana una maanisha nini ?

Tumia logic kuthinitisha uwepo wa akili, ni vipimo gani mnatumia kujua uwezo wa akili ?
3. Kuhusu binadamu kutumia dhana ya Mungu kuelezea mambo wasiyoweza kuyaeleza. Hili liko wazi katika jamii mkuu.
Huko makanisani mnakoenda si kila mara mnaambiwa ukame au mafuriko (Kwa mfano) ni matokeo ya hasira za Mungu. Hiyo attribution ni lame na tunajua ni kwa vile viongozi hao wa kiroho hawajui au wameamua kupuuza sababu za mafuriko au ukame zinazoweza kuthibitika.
Shida yenu Wakana Mungu huwa ni kwenye kujibu maswali yaani hamjibu maswali mnayo ulizwa. Soma tena swali langu nililo kuuliza Kisha ujibu nilicho kuuliza.
 
Back
Top Bottom