Mungu hayupo? Atheist njooni mthibitishe

Mungu hayupo? Atheist njooni mthibitishe

Jifunze kwanza maan ya hijja.

Qur an ni ya mtume Muhammad yeah but ina- complies vitabu vya mitume wote na dini zao kabla ya uislam.

Kabla ya uislam kulikua na iman nyingine nying, baada ya kuja uislam hizo iman zote zikawa terminated japo wapo watu walioendelea nazo kama wayahud na ukristo

Before mungu alikua anatuma mitume kimakundi mtume huyu anaenda mfano kenya mwingine anaenda uganda,lakin Muhammad alikuja kwa ajili ya dunia nzima

Mungu hutuma mtume baada ya jamii kupotea. Hao maquraish walikua wanabud masanam kabla ya mtume kuja
Huyo mtume aliyekuja kwaajili ya Dunia nzima alitembelea wapi na wapi kufikisha huo ujumbe aliotumwa na mungu wake ili tuamini kweli aliletwa kwaajili ya dunia nzima? Mtu kazunguka Maka na Madina unaniaminishaje kuwa katumwa kwa Dunia nzima!? Hizo dini zinawafanya muwe wajinga.
 
Huyo mtume aliyekuja kwaajili ya Dunia nzima aliyembelea wapi na wapi kufikisha huo ujumbe aliotumwa na mungu wake ili tuamini kweli aliletwa kwaajili ya dunia nzima? Mtu kazunguka Maka na Madina unaniaminishaje kuwa katumwa kwa Dunia nzima!? Hizo dini zinawafanya muwe wajinga.
Mwambie huyo
Hakujua kwamba Kuna Amerika Wala Australia.

Hakujua kama Kuna Afrika kusini mwa jangwa la Sahara wanaishia Misri na Somalia kama walizidi sana

Halafu wanakwambia katumwa na yeye mtume na Mungu kwa ajili ya Dunia nzima.

Hawakujua hata habari za Mijusi mikubwa(Dinosaur)
 
According tu makaratas yaliyowashika akili dunia ina muda wa zaid ya 4+ billion years though hii dunia ipo zaid ya hiyo miak.Kweny hii dunia walianza kuishi viumbe wengine tofaut na wanadam
Halafu wewe makaratasi yako yaliyoshushwa hayajakushika akili?!

Ama kweli.....
 
Nina swali

Kwanini katika kutoa kalenda na tarehe za matukio unatumika mfumo wa B.C na A.D?

(Kuacha baadhi ya matukio yale ya kusadikika ambayo hayatumii mfumo huo)

Jibu:-
Anno Domino(A.D) na Before christ (B.C) viashirio hivi hutumika kuonyesha miaka katika kalenda ya julian na gregorian ambazo ndo kwa asilimia kubwa zinatumika duniani..Kifupisho cha A.D au Anno domino ni katika lugha ya kilatini inayomaanisha "Katika mwaka wa bwana" au "katika siku za Bwana" japo asili yake kwa urefu ilikuwa inaitwa "Anno domini nostri jesu christi" yaani maana yake katika Mwaka/Miaka ya bwana wetu yesu kristo, mpaka pale ilipofupishwa kuwa A.D na neno B.C ni (kabla ya kuwepo kwa kristo) {Japo zamani iliitwa kwa kilatin ante christum natum, ambapo kwa siku hizi haitumiki tena bali hutumika version ya kiinglish)

Japo sio Jamii zote hutumia A.D Na BC kuna jamii nyingi kama zile za Kiyahudi na zingine ambao wao kulingana na imani yao Hawasadiki uwepo wa Bwana yesu na wengine ambao hawaamini Mungu wao hutumia Vifupisho kama C.E na B.C.E nadhani Tetramelyz ushakutana navyo hivyo vifupisho

ambavyo kwa wao A.D Huita C.E yaani Common Era yaani Zama za kawaida na BC wao huita BCE yaani before Common Era means kabla ya zama za kawaida

natumai umenielewa
 
Hakuna atakayethibitisha zaidi ya kukupa nadharia na kuanza kukuhoji tena badala ya kuthibitisha hilo.
Wakitoka hapo watakupa maneno ya falsafa na physics kisha wataongeza blah blah za hapa na pale mchezo umeisha.

Ndio maana Mathematician tunaamini Mungu yupo na natural numbers (1,2,3,...9) ziliumbwa na Mungu.
Mathematical operations nyingine ni man's manipulations.
Kwanza kabisa, mantiki ya uthibitisho ipo kwa mtu anayesema kitu kipo.

Wewe ukisema kuwa wewe ni mtoto wa kibaiolojia wa Donald Trump, wewe uliyesema kwamba wewe ni ntoto wa Donald Trump ndiye una wajibu wa kuthibitisha hilo.

Mimi nikikuona kwamba mbona wewe Muafrika mweusi tii, na Donald Trump mzungu, imekuwaje awe baba yako mzazi, ninachofanya ni kukuhoji tu, nakudai uthibitisho.

Wewe unayesema kitu kipo ndiye una wajibu wa kutoa uthibitisho.

Huna haki wala mantiki ya kunidai mimi ambaye sikubali kwamba wewe ni mtoto wa Donald Trump nitoe uthibitisho kwamba wewe si mtoto wa Donald Trump.

Hii mantiki ndiyo inayofanya Polisi wakija nyumbani kwako wakisema kwamba wewe una madawa ya kulevya, wao wanaosema hivyo ndio wana wajibu wa kuthibitisha hilo.

Wanakuja, wanafanya msako, wakiyapata wanakuwa wamethibitisha kuwa una madawa ya kulevya wanakupa kesi.

Hakuna hata sehemu moja inayotumia mantiki ambapo Polisi atakuja nyumbani kwako, atakwambia kwamba wewe una madawa ya kulevya kwenye nyumba hii, halafu huyo Polisi aliyetoa madai hayo akakupa mzigo wa kuthibitisha kwamba huna madawa ya kulevya.

Yeye amesema una madawa ya kulevya, yeye ana mzigo wa kuthibitisha madawa ya kulevya yapo kweli.

Sasa hapa unachofanya wewe, ni kama vile Polisi anayesema mtu ana madawa ya kulevya, halafu akiambiwa kuthibitisha hizo tuhuma, anamoa mzigo mtuhumiwa kuthibitisha kwamba hana madawa ya kulevya.

Kabla ya kudai atheists wathibitishe Mungu hayupo, elewa kwamba wewe unayesema Mungu yupo ndiye mwenye mzigo wa kuthibitisha Mungu yupo.

Lakini pia, soma post ya pili ya uzi huu, nimeweka link sehemu nilipomjibu mtoa mada swali hili la kuthibitisha Mungu hayupo.
 
Binadamu tunathibitisha mambo kupitia senses zetu tano ambazo wote tunazijua.

Linapokuja swala la Mungu, binafsi sijawahi kumuona, kumsikia, kumuonja, kumuhisi wala kusikia harufu yake.

Hii inanipa hitimisho kwamba Mungu ni dhana tu iliyoanzishwa na binadamu walipokosa majibu ya asili ya mambo mbalimbali. Kisha akaingizwa kwenye hadithi mbalimbali na kupewa sifa za mamlaka na zingine za kuogofya.

So naamini Mungu haexist physically ila dhana ya Mungu inaishi kwenye vichwa vya mamilioni ya watu duniani Kwa kuwa stori za Mungu zinasimuliwa toka utotoni na dhana ya Mungu imebidhaishwa na watu mbalimbali Kwa manufaa yao binafsi ya kisiasa, kiuchumi na kadhalika.

Mkuu,

Nakushukuru sana kuelewa Mungu hayupo.

Tunakubaliana katika hilo. Nafurahi kuona tunaokubaliana katika hili tunazidi kuongezeka hapa JF.

Lakini kuna mengine tunapishana. Na hapo najisikia nina wajibu wa kunyambulisha mambo tueleweshane zaidi na kubadikishana mawazo.

Sifikiri kwamba sense pekee zinatosha kusema kitu kipo au hakipo.

Kuna mengi hatuyafahamu kwa sense tano, lakini tunaweza kutambua kuwa yapo kwa kutumia mantiki.

Kesho tunafahamu inakuja, lakini hatujaiona, hatujaisikia, hatujainusa, hatujaigusa, wala hatujaionja.

Kwa hivyo, zaidi ya senses tano, kuna akili, kuna mantiki.

Tunajua 1 + 1 = 2. Lakini hakuna hata mtu mmoja aliyewahi kuiona 1 (namaanisha 1 yenyewe, si chungwa moja, au namba moja inayowakilisha moja yenyewe)

Kwa hivyo, inawezekana kitu kikathibitishwa kimantiki, k8mahesabu, bila kuthibitishwa wala kujulikana kwa senses. Watu wanaofanya mahesabu ya juu wanajua hili. Waliweza kuthibitisha spacetime ina bend ukiwa kwenye high gravity, kwa mahesabu, bila kujua hilo kupitia senses. Kwa mahesabu tu. Ukimsima Albert Einstein na Relativity utaona hilo.

Kwa hivyo, ingawa nakubakiana nawe Mungu hayupo, sikubakuani nawe kwamba tunathibitisha mambo kwa senses tu.

Ukiindoleea senses zote tano, ukapewa uwezo wa jufanya hesabu tu, unaweza kuthibitisha mambo mengi sana kimatiki na kimahesabu.

Tatizo la dhana ya kuwapo Mungu si kwamba haonekani, haonjeki, hanusiki, hagusiki, hasikii.
Kuna vitu havionekani na vipo.

Kuna vitu havionekani, havionjeki, havinusiki, havigusiki nahavisikiki na vipo.

Tatizo la dhana ya kuwapo Mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote ni la kifalsafa na kimantiki zaidi.

Tatizo ni kwamba, dhana ya kuwapo kwake haina logical consistency. Tabia zake, tunazoambiwa anazo a zinapingana zenyewe, pia, zinapingana na ulimwengu tunaouona kwa namna ambayo, Mungu huyo angekuwepo, ulimwengu huu tunaouona usingeweza kuwapo.

Unaambiwa Mungu ni kilele cha perfection, halafu unaambiwa Mungu anakasirika.

Kukasirika ni uthibitisho wa impwrfection, sasa Mungu perfect anakasirikaje?

Mungu perfect maana yake hawezi kukasirika. Kukasirika ni imperfection. Halafu hapo hapo unaambiwa Mungu ni perfect, halafu anakasirika. Cintradiction.

Unaambiwa Mungu huyu ni mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote. Logically Mungu huyu ni mwenye kugawa mazuri tu, mabaya hagawi. Ana neema kuu.

Sasa Mungu huyu imekuwaje kaumba ulimwengu ambao unaruhusu mabaya, wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao hauruhusu mabaya?

Kati ya anayeumba ulimwengu unaoruhusu mabaya na anayekuja kujikuta katika ulimwengu huo tu, na kufanya mabaya, lakini hajaumba ulumwengu unaoruhusu mabaya, nani ana kosa kubwa zaidi?

Hivi, huyu aliyeumba ulimwengu ambao unaruhusu mabaya, angeumba ulimwengu ambai mabaya hayawezi jufanyuka, viumbe ambao wangetokea katika ulimwengu huo wangeweza kufanya mabaya?

Kati ya Mungu na viumbe hapa, nani ana makosa makubwa zaidi?

Kuna mtu al8niambia kwamba napinga uwepo wa Mungu kwa sababu sijamuona.

Nikamwambia si kweli, unaweza kwenda jangwani, ukaona mbele yako kuna chemchemi ya maji kwa mirage, kumbe hakuna maji, ni mauzauza ya mwanga nanjoto tu.

Unaweza kuona Bob Marley anaimba mbele yako kwenye TV au computer, kumbe Bob Marley amefariki tangu May 11 1981.

Kwa hivyo, hizi five senses, kuona, kusikia, kuonja, kunusa na kugusa si vitu vya kuhakiki na kuthibitisha kitu kipo.

Vitu vinaweza kuhakikiwa na kuthibitishwa vizuri zaidi kwamba vipo kweli kwa kutumia hizo senses, pamoja na kitu kikubwa zaidi.

Akili. Mantiki.

Logical consistency. Contradictions.

Na pingamizi langu kubwa kabisa dhidi ya hoja ya uwepo wa Mungu, si ka senses, ni la kiakili na kimantiki.

Ninapopinga uwepo wa Mungu kwa kuangalia "the problem of evil", si kwa sababu simuoni, simuonji, simgusi, simsikii wala simnusi.

Babu za babu zangu wote siwaoni, siwaonji, siwagusi, siwasikii na wala siwanusi.

Lakini, kwa kutumia logical consistency, naweza kusema nina uhakika waliishi.

So.

Mungu hayupo.

Si kwa sababu simuoni, simuonji, simgusi, simsikii au simnusi.

Bali, kwa sabaju, habari za kuwapo kwake zina logical inconsistencies na contradictions kibao.
 
Si ungewathibitishia wewe kwanza kuwa yupo au unatafuta kiki mwanangu?
Mkuu umeandika kitu kikubwa sana.

Ila wasiojua mantiki ya uthibitisho wanaweza wasikuelewe.

Mzigo wa uthibitisho upo kwa yule anayedai, anayesema kitu kipo.

Anayebisha na kusema kitu hakipo hana mzigo wa uthibitisho.

Ndiyo maana, Polisi wakija nyumbani kwako na kusema kwamba nyumba hii ina madawa ya kulevya, wao ndio wana mzigo wa kuthibitisha hilo.

Watafanya msako mpaka wayapate, wathibitishe kwa kanuni zote za kimantiki kwamba nyumba hii ina madawa ya kulevya.

Polisi hawatakiwi kuja nyumbani kwako, kukutuhumu wewe kwamba nyumba yako ina madawa ya kulevya, halafu kukupa wewe mzigo wa kuthibitisha kwamba nyumba yako haina madawa ya kulevya.

That is ridiculous.

Wanachofanya hawa wanaotaka atheists wathibitishe Mungu hayupo ni sawa na Polisi anayekuja nyumbani kwako na kukutuhumu kwamba una madawa ya kulevya, halafu kukutaka uthibitishe huna madawa ya kulevya.

They are asking you to prove a negative.

Hawa watu hawajui hata logic ya proof and the fact kwamba you can't prove a negative!

Lakini.

Licha ya yote.

Nimeweka link post # 2, n8meelezea prpof in context.

Sijaona mtu anaijadili hiyo proof kimantiki so far.

cc Enkulu
 
Mimi ni mmoja kati ya wanaoamini uwepo wa Mungu. Ila nikiangalia hoja za wenzangu mnaoamini, nikalinganisha na za hao atheists (wasioamini), niwe mkweli tu, wenzangu mko na hoja dhaifu sana!

Mtu anathibitisha vipi kitu ambacho haamini uwepo wake? Nikisema ndani kwangu kuna tembo, basi ni jukumu langu kuthibitisha kwamba kweli tembo yupo. Sio niseme eti ndani kwangu kuna tembo, alafu niseme "ambae haamini kama ndani kwangu kuna tembo athibitishe". Huo ni utoto!

Ukimtuhumu mtu kua ni mwizi, basi ni jukumu lako kuthibitisha kwamba mtu huyo ni mwizi. Sio useme fulani ni mwizi, alafu tena useme "kama sio mwizi, athibitishe ". That's a simple judicial logic!
Watu hawaelewi hata "burden of proof" nini na iko wapi.
 
Kiakili tu lazima uhisi kuna super power kweny hii dunia.

Kuzaliwa,kuishi,kufa na kufufuliwa ni dalili tosha yupo mungu (Allah (saw) according to islam)

Kweny uislam kuna dalili za kuwepo mungu

01.Maisha ya mwanadam
02.Kuwepo usiku na mchana

Zipo nying izo ni chache.Ukifikir maisha ya mwandam unagundua kuna kitu kipo nyuma,hiko kitu ni Allah kwa hakika

Why allah (sw).
Sabab qur an iloleta habar za Allah(sw) na mafundisho yake imefanikiwa kutushawishi kuwa kuna mungu(allah)

muingiliano mkubwa wa 100% wa hayo mafundisho na maisha ya kila siku ya wanadam imetufanya tukiamin hiko kitabu pamoja na maelezo yake juu ya uwepo wa mungu. Si kila kitu usithibitishwa kwa kuonwa kwa macho

Wew unaamin binadam tunaroho Je ushawah kuiona. Tukianza kuelezea science ya mawasiliano tutaishia kusema kuna waves zinasafirisha sauti je tukiomba uthibitisho wa hizo waves zipoje utapatikan?

Kama swala ni kuzuka tu mbona hakuzuki kitu kingine kila siku ni binadam hawa hawa, wanyama hawa hawa means hiv vitu vipo organised je whow organised.
Hata ukikubali kuna superpower.

Kwa nini hiyo superpower iwe Mungu na isiwe kitu kingine chochote, pengine hata ambacho hukielewi kabisa?
 
Mkuu umeandika kitu kikubwa sana.

Ila wasiojua mantiki ya uthibitisho wanaweza wasikuelewe.

Mzigo wa uthibitisho upo kwa yule anayedai, anayesema kitu kipo.

Anayebisha na kusema kitu hakipo hana mzigo wa uthibitisho.

Ndiyo maana, Polisi wakija nyumbani kwako na kusema kwamba nyumba hii ina madawa ya kulevya, wao ndio wana mzigo wa kuthibitisha hilo.

Watafanya msako mpaka wayapate, wathibitishe kwa kanuni zote za kimantiki kwamba nyumba hii ina madawa ya kulevya.

Polisi hawatakiwi kuja nyumbani kwako, kukutuhumu wewe kwamba nyumba yako ina madawa ya kulevya, halafu kukupa wewe mzigo wa kuthibitisha kwamba nyumba yako haina madawa ya kulevya.

That is ridiculous.

Wanachofanya hawa wanaotaka atheists wathibitishe Mungu hayupo ni sawa na Polisi anayekuja nyumbani kwako na kukutuhumu kwamba una madawa ya kulevya, halafu kukutaka uthibitishe huna madawa ya kulevya.

They are asking you to prove a negative.

Hawa watu hawajui hata logic ya proof and the fact kwamba you can't prove a negative!

Lakini.

Licha ya yote.

Nimeweka link post # 2, n8meelezea prpof in context.

Sijaona mtu anaijadili hiyo proof kimantiki so far.
Shukrani mkuu kwa kunielewa na kumwelewesha mtoa mada. Maada mwanzoni alijitahidi kutumia kutoelewa maelezo yangu kama jibu la kutaka nikubaliane na hoja yake wakati haikubaliki. Anatumia kisu kumshambulia mtu ambaya anamnyang'anya hicho kisu na kukitumia. Akifanya hivyo, anaanza kulalamika. Hoja ya uwepo au kutokuwepo Mungu inajijibu kirahisi kwa kuangalia uwepo wa Mungu unavyotumia nadharia huku ukitaka wanaopinga wasitumie nadharia bali vitendo. Ni sawa ni ile kesi ya Waislam kusema Biblia ni kitabu kilichotungwa na binadamu jambo ambalo ni kweli lakini bado wakasema kitabu hicho kimemtabiri mtume wao. Kwa mjuzi wa mambo unashangaa mantiki hapa.
 
Mnaosema mungu yupo ndio mthibitishe sio kumrushia mzigo ambaye haamini ngano zenu zilizoandikwa miaka 2000 iliyopita
 
Shukrani mkuu kwa kunielewa na kumwelewesha mtoa mada. Maada mwanzoni alijitahidi kutumia kutoelewa maelezo yangu kama jibu la kutaka nikubaliane na hoja yake wakati haikubaliki. Anatumia kisu kumshambulia mtu ambaya anamnyang'anya hicho kisu na kukitumia. Akifanya hivyo, anaanza kulalamika. Hoja ya uwepo au kutokuwepo Mungu inajijibu kirahisi kwa kuangalia uwepo wa Mungu unavyotumia nadharia huku ukitaka wanaopinga wasitumie nadharia bali vitendo. Ni sawa ni ile kesi ya Waislam kusema Biblia ni kitabu kilichotungwa na binadamu jambo ambalo ni kweli lakini bado wakasema kitabu hicho kimemtabiri mtume wao. Kwa mjuzi wa mambo unashangaa mantiki hapa.
Shukurani kwako pia mkuu kwa uchambua mambo kwa kina.

Watetezi wa uwepo wa Mungu ni mabingwa wa contradiction.

Wanakwambia Mungu ana uwezo mkuu, ujuzi mkuu, na upendo mkuu.

Halafu, baada ya tabia hizo ambazo zinampa uwezo wa kuumba ulimwengu wowote anaotaka. Wanakuonesha ulimwengu ambao kimsingi unatuonesha kwamba kama umeumbwa na Mungu huyo, basi ame fail vibaya sana.

Mungu ambaye ana uwezo, ujuzi na upendo kuumba ulimwengu ambao hauna cancer anaumbaje ulimwengu ambao unaweza kuwa na cancer?

Mungu anayeweza kuumba ulimwengu wowote anaotaka kwa nini aumbe ulimwengu huu kati ya options zote alizonazo?

I mean Mungu amabye ana uwezo wa kuumba ulimwengu ambao rangi nyekundu haipo, ulimwengu ambao muda unarudi kinyumenyume tu na watu wanazaliwa makaburini na kufa matumboni mwa mama zao, ulimwengu ambao hauna mabaya na kinachojulikana ni mazuri tu.

Kwa nini aumbe ulimwengu huu kati ya options zote alizokuwa nazo?

Na akishaumba hivyo hakuna atakayejua tofauti, wote titakubali tu kwamba hivi ndivyo ulimwengu ulivyo.

Yani tupo katika ulimwngu ambao rangi nyekundu haipo, halafu hakuna mtu hata anayehoji kwa nini ulimwengu huu hauna rangi nyekundu.

Kwa sababu hakuna mtu anayeijua rangi nyekundu.

Kwa sababu hakuna rangi nyekundu.

Kwa sababu Mungu hajaumba ulimwengu unaoweza kuwa na rangi nyekundu.

Sasa.

Mungu menye uwezo huo, kwa nini kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawez akufanyika, wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani kufanyika?

Yani Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao haiwezekani hata mtu mmoja aishie motoni, halafu, haumbi ulimwengu huo, anaenda kuumba ulimwengu ambao mabilioni ya watu yanaishia motoni.

Hivi watu wanaamini vipi contradiction hii?
 
Huwa nawachallenge wamuache Mungu huyu mwenye uwezo usiomithalika ajitetee au aendelee kunyamaza. Ni ujinga wa kujifanya wanajua na wana jipya wakati hakuna lolote zaidi ya kubabaisha na kubangaiza. Ndiyo maana dini hutegemea na kuhimiza imani badala ya maarifa au welewa. Kwanini kuamini wakati nataka kuelewa? Yote. hadithi za Ibn Waas
 
Kwani wanajua hata kama kuna tofauti ya kuamini na kuelewa?

Mimi nimejadiliana na watu wengi sana hapa JF ambao hawajui kama kuna tofauti, na kama kuna tofauti, tofauti ni nini.

Mpaka sasa nakuwa selective nani najadiliana naye, maana wengine kujadiliana nao ni kupunguza viwango vya majadiliano tu.
 
Halafu wewe makaratasi yako yaliyoshushwa hayajakushika akili?!

Ama kweli.....
Nmekwambia kitu rahis uwez kuamin dini pamoja na vitab vya mungu haliyakuwa mungu huamin kam yupo.

Usijipe mzgo mzito wa kutak kuamin mungu yupo kupitia qur'an utajichangany. Hata nikileta ushahid kutoka kweny qur'an juu ya uwepo wa mung bado utoamin simply because huamin uwepo wa mung alileta hayo maelekezo

Huko kweny dini bado uwezo wenu ni mdgo.Mung huthibitishwa kwa normal life la kila siku kama nguvu iliyopo nyuma ya kila kitu

Ukishaanza kuelewa super power iliyopo nyuma ya maisha ya viumbe na vitu vingne. Ndo dini inashika hatamu kueleza hio super power ni ipi

Even qur'an inasema hili mitume walimtafuta mungu kweny vitu vingi sana, maisha ya dunian yalizishughurisha akili zao wapo waliohis hio nguv ni mwez ,but baada ya kuamini kuna nguv ndipo mungu alijidhihirisha kwako kwa maandiko

Mwanzo nimewauliza vitu rahis vilivyoko ndan ya uwezo wenu wa utambuz mkaanza kujing'ata. Mmeleta inshu za dini mnaishia kujikoroga

Nyie kwa akili zenu mnaona dunia inajiendea tu. Yan mfumo wa uzazi ulijiamulia mwanadam azae mtu direct na kwa kuku atotoe yai kwanza [emoji848]

Msijipe mzigo mzito kumtafuta mungu kweny dini. Dini inavit ving ambavyo kuna watu wamevichomeka inahitaj kuwa huru kichwan kuving'amua

Super power haiitaji akili kubwa kuelewa juu ya uwepo wake ,ni uwezo wa reasoning tu

Anzeni kufaham hio super power then mje kweny dini kuijua hio super power ni ipi.Unless mtazid kupotea

Yatafakar mazingira yako, tafakar mifumo ndan ya mwili wako then somen hizo theory kisha mjiulize who organised hiv vitu. Nan kaviprogram hiv vitu
 
Hata ukikubali kuna superpower.

Kwa nini hiyo superpower iwe Mungu na isiwe kitu kingine chochote, pengine hata ambacho hukielewi kabisa?
Nmekwambia kitu rahis uwez kuamin dini pamoja na vitab vya mungu haliyakuwa mungu huamin kam yupo.

Usijipe mzgo mzito wa kutak kuamin mungu yupo kupitia qur'an utajichangany. Hata nikileta ushahid kutoka kweny qur'an juu ya uwepo wa mung bado utoamin simply because huamin uwepo wa mung alileta hayo maelekezo

Huko kweny dini bado uwezo wenu ni mdgo.Mung huthibitishwa kwa normal life la kila siku kama nguvu iliyopo nyuma ya kila kitu

Ukishaanza kuelewa super power iliyopo nyuma ya maisha ya viumbe na vitu vingne. Ndo dini inashika hatamu kueleza hio super power ni ipi

Even qur'an inasema hili mitume walimtafuta mungu kweny vitu vingi sana, maisha ya dunian yalizishughurisha akili zao wapo waliohis hio nguv ni mwez ,but baada ya kuamini kuna nguv ndipo mungu alijidhihirisha kwako kwa maandiko

Mwanzo nimewauliza vitu rahis vilivyoko ndan ya uwezo wenu wa utambuz mkaanza kujing'ata. Mmeleta inshu za dini mnaishia kujikoroga

Nyie kwa akili zenu mnaona dunia inajiendea tu. Yan mfumo wa uzazi ulijiamulia mwanadam azae mtu direct na kwa kuku atotoe yai kwanza [emoji848]

Msijipe mzigo mzito kumtafuta mungu kweny dini. Dini inavit ving ambavyo kuna watu wamevichomeka inahitaj kuwa huru kichwan kuving'amua

Super power haiitaji akili kubwa kuelewa juu ya uwepo wake ,ni uwezo wa reasoning tu

Anzeni kufaham hio super power then mje kweny dini kuijua hio super power ni ipi.Unless mtazid kupotea

Yatafakar mazingira yako, tafakar mifumo ndan ya mwili wako then somen hizo theory kisha mjiulize who organised hiv vitu. Nan kaviprogram hiv vitu
 
Huyo mtume aliyekuja kwaajili ya Dunia nzima alitembelea wapi na wapi kufikisha huo ujumbe aliotumwa na mungu wake ili tuamini kweli aliletwa kwaajili ya dunia nzima? Mtu kazunguka Maka na Madina unaniaminishaje kuwa katumwa kwa Dunia nzima!? Hizo dini zinawafanya muwe wajinga.
[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
Maka na madina [emoji23][emoji23]

Amini kwanza ipo nguv nyuma ya huu ulimwengu kisha ndo tudiscuss dini, unless utajikoroga

Narudia tena mungu kumtafuta kweny qur'an ambayo huiamin utofikia conclusion. Mtafute mung kweny mazingira yako ya kila siku

Jiulize maswali Why uende toilet. Why ulale. Why ule chakula normal questions then ukipata majib jiulize tena why why nying itafika hatua hizo theory zenu mtaona ni za kitoto

Tumien akili kwanza sawa sawa
 
Hakuna theory ambayo haijaletwa na mwanadamu.

Kuanzia
Mungu
mungu
Mizimu
Majini
Sayansi
Falsafa

Zote zimeletwa na wanadamu tunachoangalia ni mantiki
Cha kukusaidia ukiwa unasoma hizo theory zako jaribu kuipa akili yako uhuru wa kuzichambua hiz theory

Big bang theory ni uongo mtu

Em ifanye akili yako kuwa huru kwanza.

Nimekujib toka mwanzo nadharia ni makisio tu sio uhalisia ni lazima mwanadam ahusike kweny haya makisio sabab ni mdhaif kimwili mpka kielimu
 
Kwahiyo aliyeandika quran (kutoka kwa malaika) ni nani? Na mna uhakika gani kama hayakuwa mawazo yake?
Uthibitisho wa hayakuwa mawazo yake upo,ila jikite kweny kuijua hio supernatural power kwa kujiuliza maswali juu ya maish yako ya kila siku

Then utakuja tukwambie dini ni nn na hio super natural power ni nn

Ukiruka vitu utajikoroga
 
Back
Top Bottom