Mungu hayupo? Atheist njooni mthibitishe

Mungu hayupo? Atheist njooni mthibitishe

Nmekwambia kitu rahis uwez kuamin dini pamoja na vitab vya mungu haliyakuwa mungu huamin kam yupo.

Usijipe mzgo mzito wa kutak kuamin mungu yupo kupitia qur'an utajichangany. Hata nikileta ushahid kutoka kweny qur'an juu ya uwepo wa mung bado utoamin simply because huamin uwepo wa mung alileta hayo maelekezo

Huko kweny dini bado uwezo wenu ni mdgo.Mung huthibitishwa kwa normal life la kila siku kama nguvu iliyopo nyuma ya kila kitu

Ukishaanza kuelewa super power iliyopo nyuma ya maisha ya viumbe na vitu vingne. Ndo dini inashika hatamu kueleza hio super power ni ipi

Even qur'an inasema hili mitume walimtafuta mungu kweny vitu vingi sana, maisha ya dunian yalizishughurisha akili zao wapo waliohis hio nguv ni mwez ,but baada ya kuamini kuna nguv ndipo mungu alijidhihirisha kwako kwa maandiko

Mwanzo nimewauliza vitu rahis vilivyoko ndan ya uwezo wenu wa utambuz mkaanza kujing'ata. Mmeleta inshu za dini mnaishia kujikoroga

Nyie kwa akili zenu mnaona dunia inajiendea tu. Yan mfumo wa uzazi ulijiamulia mwanadam azae mtu direct na kwa kuku atotoe yai kwanza [emoji848]

Msijipe mzigo mzito kumtafuta mungu kweny dini. Dini inavit ving ambavyo kuna watu wamevichomeka inahitaj kuwa huru kichwan kuving'amua

Super power haiitaji akili kubwa kuelewa juu ya uwepo wake ,ni uwezo wa reasoning tu

Anzeni kufaham hio super power then mje kweny dini kuijua hio super power ni ipi.Unless mtazid kupotea

Yatafakar mazingira yako, tafakar mifumo ndan ya mwili wako then somen hizo theory kisha mjiulize who organised hiv vitu. Nan kaviprogram hiv vitu

Mkuu,,

Wewe huelewi tofauti ya imani na ujuzi.

Huelewi tofauti ya dini na mantiki.

Huelewi kuwa ukitumia reasoning dhana ya kuwepo Mungu inakupa contradictions zinazoonesha Mungu hayupo?
 
Senses hizo tano hazitoshi kuthibitisha kila kitu, kuna matukio mengi supernatural na ambayo yameshuhudiwa hayaelezeki kwa kutumia senses tano hizo.
Matukio gani hayo supernatural? Kama hayelezeki Kwa hizi senses tano basi ni mambo ya dhahania!
 
Mkuu,,

Wewe huelewi tofauti ya imani na ujuzi.

Huelewi tofauti ya dini na mantiki.

Huelewi kuwa ukitumia reasoning dhana ya kuwepo Mungu inakupa contradictions zinazoonesha Mungu hayupo?
Unatak kulinganisha iman na ujuzi

Dini na mantik

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Nmekwambia keep reasoning utajua hii dunia kuna power behind everything.

Hizo contradictions ulizopata baada ya reasoning ni zipi?
 
Mimi ni mmoja kati ya wanaoamini uwepo wa Mungu. Ila nikiangalia hoja za wenzangu mnaoamini, nikalinganisha na za hao atheists (wasioamini), niwe mkweli tu, wenzangu mko na hoja dhaifu sana!

Mtu anathibitisha vipi kitu ambacho haamini uwepo wake? Nikisema ndani kwangu kuna tembo, basi ni jukumu langu kuthibitisha kwamba kweli tembo yupo. Sio niseme eti ndani kwangu kuna tembo, alafu niseme "ambae haamini kama ndani kwangu kuna tembo athibitishe". Huo ni utoto!

Ukimtuhumu mtu kua ni mwizi, basi ni jukumu lako kuthibitisha kwamba mtu huyo ni mwizi. Sio useme fulani ni mwizi, alafu tena useme "kama sio mwizi, athibitishe ". That's a simple judicial logic!
Acha ujinga hiyo milango ya fahamu unayoiamini kama macho still ina udhaifu wake mkubwa tyu mfano mach yako hayana uwezo wa kuona bacteria na viumbe wengine wadogo lakini pia katika kipindi cha jua kali kwenye lami huona kuna maji wakati kiuhalisia hakuna maji yote ni madhaifu ya milango yetu ya fahamu na ndo maana hata mungu huna uwezo wa kumuona
 
Matukio gani hayo supernatural? Kama hayelezeki Kwa hizi senses tano basi ni mambo ya dhahania!
Bacteria na virusi umewaona kwa macho au kuwasikia kwa maskio au kuwahis kwa ngozi ,je umewaonja au kuwanusa if not Why unaamin wapo really na sio dhahania
 
Mkuu,

Nakushukuru sana kuelewa Mungu hayupo.

Tunakubaliana katika hilo. Nafurahi kuona tunaokubaliana katika hili tunazidi kuongezeka hapa JF.

Lakini kuna mengine tunapishana. Na hapo najisikia nina wajibu wa kunyambulisha mambo tueleweshane zaidi na kubadikishana mawazo.

Sifikiri kwamba sense pekee zinatosha kusema kitu kipo au hakipo.

Kuna mengi hatuyafahamu kwa sense tano, lakini tunaweza kutambua kuwa yapo kwa kutumia mantiki.

Kesho tunafahamu inakuja, lakini hatujaiona, hatujaisikia, hatujainusa, hatujaigusa, wala hatujaionja.

Kwa hivyo, zaidi ya senses tano, kuna akili, kuna mantiki.

Tunajua 1 + 1 = 2. Lakini hakuna hata mtu mmoja aliyewahi kuiona 1 (namaanisha 1 yenyewe, si chungwa moja, au namba moja inayowakilisha moja yenyewe)

Kwa hivyo, inawezekana kitu kikathibitishwa kimantiki, k8mahesabu, bila kuthibitishwa wala kujulikana kwa senses. Watu wanaofanya mahesabu ya juu wanajua hili. Waliweza kuthibitisha spacetime ina bend ukiwa kwenye high gravity, kwa mahesabu, bila kujua hilo kupitia senses. Kwa mahesabu tu. Ukimsima Albert Einstein na Relativity utaona hilo.

Kwa hivyo, ingawa nakubakiana nawe Mungu hayupo, sikubakuani nawe kwamba tunathibitisha mambo kwa senses tu.

Ukiindoleea senses zote tano, ukapewa uwezo wa jufanya hesabu tu, unaweza kuthibitisha mambo mengi sana kimatiki na kimahesabu.

Tatizo la dhana ya kuwapo Mungu si kwamba haonekani, haonjeki, hanusiki, hagusiki, hasikii.
Kuna vitu havionekani na vipo.

Kuna vitu havionekani, havionjeki, havinusiki, havigusiki nahavisikiki na vipo.

Tatizo la dhana ya kuwapo Mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote ni la kifalsafa na kimantiki zaidi.

Tatizo ni kwamba, dhana ya kuwapo kwake haina logical consistency. Tabia zake, tunazoambiwa anazo a zinapingana zenyewe, pia, zinapingana na ulimwengu tunaouona kwa namna ambayo, Mungu huyo angekuwepo, ulimwengu huu tunaouona usingeweza kuwapo.

Unaambiwa Mungu ni kilele cha perfection, halafu unaambiwa Mungu anakasirika.

Kukasirika ni uthibitisho wa impwrfection, sasa Mungu perfect anakasirikaje?

Mungu perfect maana yake hawezi kukasirika. Kukasirika ni imperfection. Halafu hapo hapo unaambiwa Mungu ni perfect, halafu anakasirika. Cintradiction.

Unaambiwa Mungu huyu ni mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote. Logically Mungu huyu ni mwenye kugawa mazuri tu, mabaya hagawi. Ana neema kuu.

Sasa Mungu huyu imekuwaje kaumba ulimwengu ambao unaruhusu mabaya, wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao hauruhusu mabaya?

Kati ya anayeumba ulimwengu unaoruhusu mabaya na anayekuja kujikuta katika ulimwengu huo tu, na kufanya mabaya, lakini hajaumba ulumwengu unaoruhusu mabaya, nani ana kosa kubwa zaidi?

Hivi, huyu aliyeumba ulimwengu ambao unaruhusu mabaya, angeumba ulimwengu ambai mabaya hayawezi jufanyuka, viumbe ambao wangetokea katika ulimwengu huo wangeweza kufanya mabaya?

Kati ya Mungu na viumbe hapa, nani ana makosa makubwa zaidi?

Kuna mtu al8niambia kwamba napinga uwepo wa Mungu kwa sababu sijamuona.

Nikamwambia si kweli, unaweza kwenda jangwani, ukaona mbele yako kuna chemchemi ya maji kwa mirage, kumbe hakuna maji, ni mauzauza ya mwanga nanjoto tu.

Unaweza kuona Bob Marley anaimba mbele yako kwenye TV au computer, kumbe Bob Marley amefariki tangu May 11 1981.

Kwa hivyo, hizi five senses, kuona, kusikia, kuonja, kunusa na kugusa si vitu vya kuhakiki na kuthibitisha kitu kipo.

Vitu vinaweza kuhakikiwa na kuthibitishwa vizuri zaidi kwamba vipo kweli kwa kutumia hizo senses, pamoja na kitu kikubwa zaidi.

Akili. Mantiki.

Logical consistency. Contradictions.

Na pingamizi langu kubwa kabisa dhidi ya hoja ya uwepo wa Mungu, si ka senses, ni la kiakili na kimantiki.

Ninapopinga uwepo wa Mungu kwa kuangalia "the problem of evil", si kwa sababu simuoni, simuonji, simgusi, simsikii wala simnusi.

Babu za babu zangu wote siwaoni, siwaonji, siwagusi, siwasikii na wala siwanusi.

Lakini, kwa kutumia logical consistency, naweza kusema nina uhakika waliishi.

So.

Mungu hayupo.

Si kwa sababu simuoni, simuonji, simgusi, simsikii au simnusi.

Bali, kwa sabaju, habari za kuwapo kwake zina logical inconsistencies na contradictions kibao.
Mkuu, nakubaliana na wewe.
Primary source yetu ya uthibitisho wa vitu ni senses zetu. Kisha hapo ndipo mantiki na logical consistency inafuata. So ahsante kwa hii icing juu ya cake yangu.
 
Bacteria na virusi umewaona kwa macho au kuwasikia kwa maskio au kuwahis kwa ngozi ,je umewaonja au kuwanusa if not Why unaamin wapo really na sio dhahania
Bacteria na virus wanaonekana chini ya Microscope mkuu. Pia, logically madhara tunayoambiwa wanayafanya Kwa mwili wa binadamu au mnyama mwingine yako consistent. Ndiyo maana symptoms za magonjwa mi universal kwa watu wote tu.
 
Okay so dhahania inaweza isiwepo ikitokea kuna logical consistency

Microscope + logical Consistency =Ni kweli bacteria na virus wapo

Actually akili huonesha mungu (super natural power) yupo ila mnsema logical Consistency ndo hamna. Zipi logical zinaku contradicts juu ya uwepo wa mungu mpka useme no logical Consistency juu ya uwepo wa mungu?
 
Hujawahi ona Giza muda wa mchana?
Ile mwaka 2020 kupatwa kwa jua haukuwepo duniani?
Kijana unajua maana ya Giza au unajua Giza ni nini ?

Ukitaka kujua maana ya ujinga waangalie au soma hona za Wakana Mungu.
 
Binadamu tunathibitisha mambo kupitia senses zetu tano ambazo wote tunazijua.

Linapokuja swala la Mungu, binafsi sijawahi kumuona, kumsikia, kumuonja, kumuhisi wala kusikia harufu yake.

Hii inanipa hitimisho kwamba Mungu ni dhana tu iliyoanzishwa na binadamu walipokosa majibu ya asili ya mambo mbalimbali. Kisha akaingizwa kwenye hadithi mbalimbali na kupewa sifa za mamlaka na zingine za kuogofya.

So naamini Mungu haexist physically ila dhana ya Mungu inaishi kwenye vichwa vya mamilioni ya watu duniani Kwa kuwa stori za Mungu zinasimuliwa toka utotoni na dhana ya Mungu imebidhaishwa na watu mbalimbali Kwa manufaa yao binafsi ya kisiasa, kiuchumi na kadhalika.
Unafahamu kuwa hapo ulipo una nguvu kubwa beyond your body and mind(hizo five senses unazo zungumzia) ?
 
Binadamu tunathibitisha mambo kupitia senses zetu tano ambazo wote tunazijua.
Unakubali ya kuwa milango ya fahamu Ina ukomo ? Kwa akili yako unataka kutuambia ya kuwa vile ambavyo milango ya fahamu haiwezi kuvidiriki ni kwamba havipo ? Hii akili ha wapi ?
Linapokuja swala la Mungu, binafsi sijawahi kumuona, kumsikia, kumuonja, kumuhisi wala kusikia harufu yake.
Wewe una akili au huna ? Akili ushawahi kuihisi ? Kuionja ? Kuiona ? Harufu ya akili unaijua ? Ushawahi kuisikia ?
inanipa hitimisho kwamba Mungu ni dhana tu iliyoanzishwa na binadamu walipokosa majibu ya asili ya mambo mbalimbali. Kisha akaingizwa kwenye hadithi mbalimbali na kupewa sifa za mamlaka na zingine za kuogofya.
Huu ujinga huwa naona mnapenda sana kuandika. Naomba unithibitishie ya kuwa dhana ya Mungu chanzo chake ni binadamu walipo kosa majibu ya asili ya mambo mbalimbali na uniambie ilikuwa lini kwa mara ya kwanza.

Sasa msilete dhana kuelezea dhana na kithibitisha Shana zenu.
 
Acha ujinga hiyo milango ya fahamu unayoiamini kama macho still ina udhaifu wake mkubwa tyu mfano mach yako hayana uwezo wa kuona bacteria na viumbe wengine wadogo lakini pia katika kipindi cha jua kali kwenye lami huona kuna maji wakati kiuhalisia hakuna maji yote ni madhaifu ya milango yetu ya fahamu na ndo maana hata mungu huna uwezo wa kumuona

Mimi sio mtu uliyemquote ila napenda kukubali hoja yako hii, kisha nikuulize swali unijibu.

Unasema hatuwezi kumuona Mungu kutokana na udhaifu wa milango yetu ya fahama, nakubali. Je ni kwa njia ipi tunaweza kumuona au kuthibitisha kuwa yupo ?

Na kama haukuna namna yoyote ile ya kumuona au kuthibitisha kuwa yupo, hauoni kwamba maelezo yenu (waamini Mungu yupo) yamejikita kwenye KUAMINI tu na sio uelewa?
 
Senses hizo tano hazitoshi kuthibitisha kila kitu, kuna matukio mengi supernatural na ambayo yameshuhudiwa hayaelezeki kwa kutumia senses tano hizo.
Yeah,ndo maana meditators practice going beyond the mind and body.
 
Mtu anathibitisha vipi kitu ambacho haamini uwepo wake? Nikisema ndani kwangu kuna tembo, basi ni jukumu langu kuthibitisha kwamba kweli tembo yupo. Sio niseme eti ndani kwangu kuna tembo, alafu niseme "ambae haamini kama ndani kwangu kuna tembo athibitishe". Huo ni utoto!
Swali la msingi huyo mtu anakuwa amejuaje ya kuwa hicho kitu hakipo ?

Wewe ukisema hayupo huna wajibu wa kuthibitisha ya kuwa hayupo ? Tena yule ambaye anakusha mara nyingi hutangulizwa kwenye kuthibitisha sababu yeye hudhaniwa ni mjuzi zaidi kuliko yule anaye sadikisha. Someni Elimu za utafiti na mijadala mtaona hivi vitu.

Yaani unaanzaje kuamini kutokuwepo kwa kitu ? Kwa ujinga au kwa Elimu yaani kujua ? Utaamini vipi kitu Fulani hakipo bila Elimu ? Huu ni ujinga ambao umeandika hapa.
 
Unafahamu kuwa hapo ulipo una nguvu kubwa beyond your body and mind(hizo five senses unazo zungumzia) ?
Nguvu gani hiyo mkuu? Inaitwaje? Nipe mbinu ya kuthibitisha hiyo nguvu tafadhali.
 
Nguvu gani hiyo mkuu? Inaitwaje? Nipe mbinu ya kuthibitisha hiyo nguvu tafadhali.
Inaitwa Consciousness ama Ufahamu..kila binadamu amezaliwa nayo. Huwezi kuipokonya,huwa inaoperate 24/7 na inabaki hata baada ya wewe kufa (physical body death).

Ili kujifunza,fuatilia kitu kinaitwa MEDITATION. Naweza kukufudisha buree tukipata muda
 
Unakubali ya kuwa milango ya fahamu Ina ukomo ? Kwa akili yako unataka kutuambia ya kuwa vile ambavyo milango ya fahamu haiwezi kuvidiriki ni kwamba havipo ? Hii akili ha wapi ?

Wewe una akili au huna ? Akili ushawahi kuihisi ? Kuionja ? Kuiona ? Harufu ya akili unaijua ? Ushawahi kuisikia ?

Huu ujinga huwa naona mnapenda sana kuandika. Naomba unithibitishie ya kuwa dhana ya Mungu chanzo chake ni binadamu walipo kosa majibu ya asili ya mambo mbalimbali na uniambie ilikuwa lini kwa mara ya kwanza.

Sasa msilete dhana kuelezea dhana na kithibitisha Shana zenu.
Mkuu,
1. Milango yetu ya fahamu inatuthibitishia uwepo wa vitu physical. Beyond physical realities ni abstract thinking ambayo huhitaji kutumia logic ili kufikia conclusion. Kiufupi ni kwamba tutatumia senses kuthibitisha uhalisia wa physical beings na logic Kwa ajili ya vitu abstract.

2. Kuhusu akili, akili ni dhana abstract. So huwezi kuiona au kuihisi. Ila tunathibitisha uwepo wa akili Kwa kufuata logic na Kuna vipimo vya kupima uwezo wa akili.

3. Kuhusu binadamu kutumia dhana ya Mungu kuelezea mambo wasiyoweza kuyaeleza. Hili liko wazi katika jamii mkuu.
Huko makanisani mnakoenda si kila mara mnaambiwa ukame au mafuriko (Kwa mfano) ni matokeo ya hasira za Mungu. Hiyo attribution ni lame na tunajua ni kwa vile viongozi hao wa kiroho hawajui au wameamua kupuuza sababu za mafuriko au ukame zinazoweza kuthibitika.
 
Mkuu
Inaitwa Consciousness ama Ufahamu..kila binadamu amezaliwa nayo. Huwezi kuipokonya,huwa inaoperate 24/7 na inabaki hata baada ya wewe kufa (physical body death).

Ili kujifunza,fuatilia kitu kinaitwa MEDITATION. Naweza kukufudisha buree tukipata muda
Mkuu,
Consciousness haiendi beyond senses zetu kama unavyosema. Binadamu tunapata ufahamu Kwa kupitia milango yetu ya fahamu na logical reasoning. Hivyo, huwezi kutenganisha ufahamu na milango ya ufahamu.
Pia sikubaliani na wewe unaposema kwamba hata mtu aliyekufa anabaki na ufahamu wake. Unless unithibitishie Hilo au uniambie namna isiyo na mashaka nikathibitishe kwamba maiti ina ufahamu.
 
Okay so dhahania inaweza isiwepo ikitokea kuna logical consistency

Microscope + logical Consistency =Ni kweli bacteria na virus wapo

Actually akili huonesha mungu (super natural power) yupo ila mnsema logical Consistency ndo hamna. Zipi logical zinaku contradicts juu ya uwepo wa mungu mpka useme no logical Consistency juu ya uwepo wa mungu?
Ndugu,
Mkuu Kiranga na wengine wameeleza logical contradictions za dhana ya uwepo wa Mungu katika Uzi huu huu na zingine pia. Naomba urudi juu kidogo usome comments kadhaa walau or else, nitakuja kukuwekea angalau list fupi ya hoja hizo.
 
Back
Top Bottom