Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,341
- 51,907
MUNGU HAHITAJI ZAKA NA SADAKA YAKO, SADAKA NA ZAKA NI MALIPO YA WATUMISHI WA DINI.
Anaandika, Robert Heriel
Kuhani
"Mtolee Mungu"
" Hiyo ni sadaka Kwa Mungu wako"
" Unamnyima Mpaka Mungu anayekupa uhai"
Na kauli zingine kama hizo, ni Utapeli mtupu.
Kuna Ile unaambiwa" mtolee Mungu ili akubariki" huo ni Uchawi na ushirikina mkubwa. Kwamba ati unampa Mungu rushwa kama Samunge, labda Ile miungu ya Kwa msisi.
Mungu hahitaji chochote Kutoka Kwako, endapo Mungu huyo atahitaji chochote Kutoka Kwako basi anapoteza vigezo vya kuwa Mungu. Kwa sababu moja ya Sifa ya Mungu ni kuwa sio mhitaji.
Sadaka au Zaka ni MALIPO tunayowalipa viongozi wa dini tunazoabudia ili waweze kuendesha Maisha Yao kama Sisi tunavyofanya kazi katika shughuli zetu.
Viongozi wa dini wanafamilia zao, wanamahitaji Yao, wanahitaji vyakula, nguo, nyumba, magari na mahitaji mengine
Ukienda Kanisani, au msikitini au madhabahuni popote pale, lazima uingie makubaliano na huyo kuhani au mchungaji, au nabii au Mtume kwamba kwako ninakuja Kwa ajili ya Kupata mambo 1,2,3.
Mfano, unakuja Kwa Kuhani Taikon, unaniambia, Kuhani Taikon wa Mungu wa Tibeli, Mungu Mkuu, nimekuja kwako Kwa sababu zifuatazo;
1. Nataka uniombee nipone ugonjwa Fulani,
2. Nataka Njia zangu na kazi za mikono yangu ifanikiwe, nataka ndani ya miaka Hii Mitano niwe ninanyumba au Gari.
3. Nataka ulinzi katika familia yangu.
Hapo nitaingia chumba cha Siri kumuuliza Mungu wa Tibeli kama atakusaidia au Laa. Kama akisema atakusaidia, nitakujia nitakuambia Mungu wa Tibeli kasema atakusaidia, kisha nitakuambia nenda alafu Mungu atakapokusaidia ndio ulete malipo(sadaka) ya Kazi niliyokufanyia ya kuwa Dalali baina yako na Mungu wa Tibeli.
Nitakupa sheria na masharti ya kufuata kadiri nitakavyoagizwa na huyo Mungu wa Tibeli.
Mfano nitakuambia Mungu atakujibu ndani ya mwaka mmoja, atakapokujibu utaleta Sehemu ya ishirini ya Mapato yako ndani ya miaka mitatu.
Kisha utaondoka, utaamua kutoa shukrani au usitoe ni wewe mwenyewe, kwani hapo ulikuja kufanya agano/mkataba na Mungu wa Tibeli. Haukuja kutoa Sadaka wala Zaka wala dhabihu.
Sio nikuombe Sadaka na Zaka Wakati hakuna kazi niliyoifanya, huo ni Utapeli.
Kufumba macho na kuanza kuomba hiyo sio kazi. Hiyo kila MTU anaweza Kufanya, hata mtoto Mdogo anaweza kufumba macho akaomba.
Mchungaji au nabii anayetanguliza umlipe Kabla ya Kazi huyo ni Mhuni, tapeli.
Manabii na mitume wakweli anakupa Huduma kisha wewe mwenyewe utaamua uvunja makubaliano au uwe mwaminifu. Hii ni Kwa sababu, kama wanauwezo wa kukupa Mali au kukusaidia basi ni hakika Wanauwezo wa kuvichukua vyote walivyokupa.
Hata hivyo, kama umeenda Kanisani au msikitini kusikiliza Mawaidha au kufundishwa Neno la Mungu basi itakupasa uwalipe Kwa kazi hiyo ya kukufundisha, ndio Yale mambo ha kwenda kila mwisho wa juma Kanisani au misikitini ili mfundishwe habari za miungu yenu. Hivyo lazima muwalipe sadaka na Zaka zao Kwa kazi ya kuwafunza.
Ila kama haukuenda kujifunza, ulienda kutafuta Maisha mazuri, au unatatizo unataka litatuliwe basi hakikisha tatizo Hilo linatatuliwa ndio utoe sadaka au Zaka kama malipo ya Kazi waliyoifanya.
Zingatia, sio lazima kwenda kujifunza neno la Mungu ikiwa tangu ukiwa mtoto ulifundishwa habari za Mungu wako. Utapewa hadithi zilezile na mafunzo yaleyale tuu.
Manabii na watumishi wa Mungu wapo kwaajili ya Kutatua matatizo ya jamii ili nao walipwe Kwa kazi Yao.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam