Sadaka itakayokuokoa siku ya Tabu

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,103
22,542
Salaam, Shalom!

INTRODUCTON.

Mungu ameweka sadaka kuwa kitu kinachoendeleza kipato Cha mtoaji maisha yake yote.

(Luke 6:38) Yesu asema, wapeni watu vitu,nanyi mtapewa, kipimo Cha kujaa, na kushindiliwa, na kusukwasukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile mpimacho, ndicho mtakachopimiwa.

Ukipata Laki Moja, ukalipa ZAKA na sadaka 15000k Kwa Mfano, ukabaki na 85,000k matumizi, Ile 15,000k uliyotoa, Mungu huibadili kuwa 100,000k na kukupa tena next time Ili utoaji uendelee, na kamwe hutapungukiwa, usipofanya hivyo, uhitaji na Umaskini utakukumba.

Wapo watu wabaya, wengine agents, wanaodanganya watu wapuuze Kutoa sadaka na ZAKA.

Kila mtu anazo siku njema, na zipo pia siku za taabu mbele yetu, Leo nitazungumzia sadaka kama funguo Moja wapo muhimu itakayokutoa katika siku za taabu mbele Yako.

MADA: JINSI GANI SADAKA INAVYOWEZA KUKUSAIDIA WAKATI WA TAABU.

Mpendwa, tupitie shuhuda ZIFUATAZO zitakazoongeza Imani Yako na uhakika wa kupita salama wakati Ule mbaya.

SHUHUDA NO. 1

(Matendo ya mitume 9:36-43)

Hapa Petro, anamfufua Dorkas aliyekuwa amekufa baada ya kuombwa sana na watu waliokuwa wakinufaika na sadaka alizokuwa akitoa Dorkas. Na sadaka hizo, hazikuwa pesa, Bali alitoa nguo alizokuwa akishona na kuwapa wajane na watumishi na watu wengine Kwa Upendo.

Alipokufa, watu waligoma kumzika wakisema, Mama huyu hakustahili kufa sababu ya sadaka zake. Na Kweli, Petro alimwombea Kwa Jina la YESU na akafufuka na kurudi kuwa hai tena.

USHUHUDA No. 2

Mama mmoja aliyekuwa tasa, alimwomba Mungu apewe mtoto Kwa miaka mingi bila kuchoka, Ilipofikia muda wa Mungu kumjibu ombi lake, alimtuma Malaika wake aliyekuja nyumbani Kwa mwonekano wa mtu maskini, asiye na uwezo wa kukodi nyumba ya kulala. Mama yule pamoja na kuwa katika shida na uhitaji wa pesa, alimpokea mtu yule na kumkaribisha nyumbani Yeye na familia yake, walishiriki naye chakula na Kisha, walimpa chumba Cha kulala, na siku iliyofuata, mtu yule aliaga na kuondoka, hazikupita siku kadhaa, mama yule alishika ujauzito Kutoka Kwa mume wake wa NDOA na baada ya miezi tisa,alizaa mtoto wa kiume Kwa uwezo wa Mungu. Jiulize asingetoa sadaka Kwa kumkarimu mgeni, nini kingetokea?

USHUHUDA NO. 3

Mtu mmoja alizoea kuwapa chakula watoto yatima mtaani, Kila alipowaona, aliwaita na kununua chakula Kwa ajili Yao Kwa furaha, na hakuwa tajiri, HAPANA, alipenda kufanya hivyo kama sadaka yake Kwa BWANA sababu Yesu aliagiza kuwajali yatima na wajane.

Siku moja, Jirani ya mtu huyo aliyekuwa mshirikina, alimwendea Kwa mganga na Kutoa sadaka Ili mtu huyo auliwe kichawi, mganga alipokea sadaka na kutuma kundi la mapepo Ili wamtoe uhai.

Mtu yule alipokuwa amelala, aliota ndoto kuwa, kundi la mapepo wenye silaha wamekuja nyumbani kwake, walifika katika nyumba yake hiyo alivyokuwa akiishi pekeake, na baada ya mapepo hayo kufika, yalikwenda kitandani alipolala mtu yule Ili yamuue,

Cha kushangaza, kitandani, mapepo Kila yalipoangalia, alionekana mtoto mdogo amelala Badala ya mtu yule.

Mapepo Yale yalizunguka chumba kizima kumtafuta mtu yule na yasimwone na yakaondoka kumrudia mganga.

Mtoto yule aliyeonekana kitandani Badala ya mlengwa, ilikuwa ni ushahidi juu ya sadaka iliyofanyika msaada wakati wa TAABU, kuwa sadaka Kwa watoto yatima, ilimwokoa na MAUTI wakati wa TAABU.

USHUHUDA NO. 4

Baba mmoja wa familia, akapata uvimbe katika mguu wake, maumivu yalipozidi, Akaenda hospitali, baada ya vipimo, Daktari alimwambia baba yule kuwa, mguu wako unatakiwa ukatwe haraka maana una cancer inayokua Kwa Kasi sana.

Mtu yule, allimwambia daktari ampe muda Ili aishirikishe familia yake. Alipomshirikisha mkewe ambaye alikuwa mwana maombi, alimtia moyo na kumwambia tuombe, Mungu anaweza kukuponya cancer usikatwe mguu.

Waliomba Kwa siku kadhaa na mabadiliko hayakuonekana Kwa haraka, wakakubaliana kuendelea na maombi. Mtu yule siku moja akiwa njiani kuelekea kufanya check up ya mguu wake, akakutana na mtu mmoja njiani aliyemsimamisha na kumwomba pesa kidogo Ili anunulie chakula, mgonjwa yule wa mguu alimjibu Kwa hasira mtu yule akisema, Sina pesa Mimi, Mimi Nina matatizo na ninaenda hospitali, usinisunbue.

Alipofika hospitali, daktari alimwambia inabidi mguu ukatwe haraka, na Kweli akakubali mguu wake ukatwe na kupuuza maombi.

Kumbe, Mungu alikwisha sikia maombi yake walipoomba na mkewe, akamtuma Malaika ambaye ndiye mtu yule aliyemjaribu njiani Kwa kuomba sadaka kidogo ya CHAKULA na hakutoa, Malaika yule alikuwa amekuja na mguu mpya, spea Kutoka Mbinguni ambayo ingewekwa ikiwa angeshinda jaribu. Mtu yule alibaki na ulemavu na baadae alikufa Kwa cancer iliyorudi tena sehemu ingine. Sadaka ni muhimu, hata Ukiwa katika magumu, sadaka itakutoa katika magumu siku ya Taabu.

NB: Usisubiri nyakati za taabu ndo utoe sadaka, utakuwa umechelewa. Anza sasa.

Ikiwa hujampa Yesu maisha Yako, fuatisha Sala ifuatayo;

EE MUNGU KATIKA JINA LA YESU KRISTO, NINAKUKIRI WEWE KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE, NINAOMBA UNISAMEHE, ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU, ULIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA, NIPE UWEZO WA KUISHI MAISHA MATAKATIFU, DHAMBI ISINISHINDE. NINAOMBA HAYO KUPITIA JINA LA YESU KRISTO. AMEN

Amen.🙏
 
(Luke 6:38) Jesus says,

Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa,kipimo Cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwasukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu,

Kwa kuwa kipimo kile mkipomacho, ndicho mtakachopimiwa.

Amen
Kusaidia watu nasaidia sana ila sio kwa kutegemea kupata chochote , ni ubinadamu tu.
 
Kusaidia watu nasaidia sana ila sio kwa kutegemea kupata chochote , ni ubinadamu tu.
Na ndicho Mungu atakacho, tusaidiane.

Tena anasisitiza kusaidia watu usiotegemea wakurudishie chochote baadae, ni sadaka Kwa ajili ya Upendo.

Sadaka utoazo, zitakusaidia wakati wa TAABU muda ambapo hutakuwa na msaada, ndipo Mungu atakusaidia akikukumbusha wema uliotenda zamani.

Amen
 
Na ndicho Mungu atakacho, tusaidiane.

Tena anasisitiza kusaidia watu usiotegemea wakurudishie chochote baadae, ni sadaka Kwa ajili ya Upendo.

Sadaka utoazo, zitakusaidia wakati wa TAABU muda ambapo hutakuwa na msaada, ndipo Mungu atakusaidia akikukumbusha wema uliotenda zamani.

Amen
Hizo habar za Mungu kwangu ndio sizipi nafasi kabisa, OK upo sawa kwa upande wako👍
 
Mtu mmoja,alimuuliza yesu ofanye nn ili niweze kuurithi ufalme wa mbinguni, akamwbia zitii amri 10 kumi za mungu. Yule mbwana akajibu haya yote niliyafanya tangu nikiwa bado mdogo je nifanye nn kingine? Akamwambia uza mali zalo na uwagawie masikini, hakusema peleka kanisani,hii ina maana sadaka hutoleqa kwa masikini wasiojiweza , uaipelwkw sadaka kanisani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtu mmoja,alimuuliza yesu ofanye nn ili niweze kuurithi ufalme wa mbinguni, akamwbia zitii amri 10 kumi za mungu. Yule mbwana akajibu haya yote niliyafanya tangu nikiwa bado mdogo je nifanye nn kingine?? Akamwambia uza mali zalo na uwagawie masikini, hakusema peleka kanisani,hii ina maana sadaka hutoleqa kwa masikini wasiojiweza , uaipelwkw sadaka kanisani

Sent using Jamii Forums mobile app
(Warumi 10:14-15)
14:Basi wamwiteje Yeye wasiyemwamini?

Tena wamwaminije Yeye wasiyemsikia?

Tena wamsikieje pasipo mhubiri?

15: Tena wahubirije, wasipopelekwa?

Maana imeandikwa, ni mizuri kama nini miguu Yao wahubirio habari ya mema.

Mwisho wa kunukuu......

Ndipo sasa ujue sadaka hutolewa Kwa wajane na yatima, lakini pia sadaka hutolewa Ili kuwapeleka watumishi na vitendea KAZI kuhubiri INJILI.

Next time ukikutana na HOJA inayofanana na hii, usisahau hili pia maana ni agizo la Mungu.

Amen
 
Ubarikiwe Sana Brother, nami naanza tena kutoa sadaka
Usiache mwana wa Mungu.

Usipotoa lazima upitie mkwamo, Mimi Nina ushuhuda, siwezi kuanza shughuli yoyote, ujenzi Kwa Mfano bila kwanza Kutoa sadaka na ZAKA,

Nisipotoa, hata kama Nina pesa lundo bank, siwezi fanya chochote Hadi nitoe kwanza.

Amen
 
Sidhani!
Umechanganya vitu hapo! Kutoa vitu na kuwapa watu ni kama kutoa Sadaka ni tofauti na kutoa Zaka!
Na utalipwa sawa sawa na ulivyotoa! Ukitoa vingi utalipwa vingi na zaidi, ukitoa kidogo utalipwa kidogo!
Kwa hiyo kwa mifano uliyotoa ni Mungu kukumbuka SADAKA zao walizokuwa wakitoa siyo ZAKA zao!

Zaka unalipa lakini siyo Sadaka!
Sadaka ni kitu cha hiari!

Naona uko katika lile dhehebu ambalo wanasistiza sana kulipa Zaka kuliko hata kutoa Sadaka! Madhehebu ya usipotoa Zaka utalaaniwa, (Malaki 3:8-10)
Na baada ya hapo unaambiwa umekufa kizaka toka Kanisani kajifufue!😀😀
SADAKA NI TOFAUTI NA ZAKA!
Lakini tusiache Kutoa Zaka! Hiyo ni sawa na kutoa Kodi, Ushuru serikalini, ile ni kwa ajilli ya maendeleo! Hivyo tunapotoa Zaka ni Kodi ya BWANA kwa ajili ya kujenga Kanisa,kulipia umeme na maji, na huduma nyinginezo!
(LAKINI SIYO KUMNENEPESHA MCHUNGAJI NA FAMILIA YAKE)🙏🙏🙏
 
Sidhani!
Umechanganya vitu hapo! Kutoa vitu na kuwapa watu ni kama kutoa Sadaka ni tofauti na kutoa Zaka!
Na utalipwa sawa sawa na ulivyotoa! Ukitoa vingi utalipwa vingi na zaidi, ukitoa kidogo utalipwa kidogo!
Kwa hiyo kwa mifano uliyotoa ni Mungu kukumbuka SADAKA zao walizokuwa wakitoa siyo ZAKA zao!

Zaka unalipa lakini siyo Sadaka!
Sadaka ni kitu cha hiari!

Naona uko katika lile dhehebu ambalo wanasistiza sana kulipa Zaka kuliko hata kutoa Sadaka! Madhehebu ya usipotoa Zaka utalaaniwa, (Malaki 3:8-10)
Na baada ya hapo unaambiwa umekufa kizaka toka Kanisani kajifufue!😀😀
SADAKA NI TOFAUTI NA ZAKA!
Lakini tusiache Kutoa Zaka! Hiyo ni sawa na kutoa Kodi, Ushuru serikalini, ile ni kwa ajilli ya maendeleo! Hivyo tunapotoa Zaka ni Kodi ya BWANA kwa ajili ya kujenga Kanisa,kulipia umeme na maji, na huduma nyinginezo!
(LAKINI SIYO KUMNENEPESHA MCHUNGAJI NA FAMILIA YAKE)🙏🙏🙏
Point imeeleweka.

Hayo mengine umeongezwa wewe!!

Ahsante.
 
Back
Top Bottom