Mungu anafanya miujiza au anatumia sayansi?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
11,622
Reaction score
20,570
Kuna stori kuwa Columbus alipokuwa anaondoka kisiwa fulani huko Amerika aliwaambia wenyeji wampe chakula cha safari. Wakagoma. Akasema mkigoma kesho nitafanya miujiza. Nitautia mwezi giza. Kweli kesho yake mwezi uliingiwa giza. Wenyeji wakamsujudu Columbus na kumpa chakula. Waliona miujiza mtu kuutia mwezi giza. Lakini Columbus alitumia sayansi. Alijua habari za kupatwa kwa mwezi na mzunguko wake.

Binadamu anaweza kurusha mzinga na ukaenda kutua sehemu anayotaka. Anaangalia umbali alipo adui, spidi ya mzinga, joto, mgandamizo wa hewa, spidi ya upepo nk. Anaingiza yote haya(Variables)kwenye formula na kupata angle anayopaswa kuweka mzinga wake. Na kweli mzinga unaenda kutua alipopanga.

Si Mungu naye anapotabiri mambo hutumia formula kama hiyo. Anapotabiri mfano kifo anaingiza mabilioni ya variables kumhusu mtu huyo kwenye formula. Alichokula, mawazo yake(Brain waves) maneno anayoongea, afya yake, watu wanaomzunguka, hali ya hewa. . . Yaani anaingiza kila kitu kinachomhusu mtu huyo kwenye formula kisha anapata jibu kuwa kesho Absalomu mwana wa Daudi atakufa kwa kunaswa kwenye mti. Hafanyi miujiza, anafanya hesabu. "Miujiza" inawezekana bila sayansi?
 
Kuna stori kuwa Columbus alipokuwa anaondoka kisiwa fulani huko Amerika aliwaambia wenyeji wampe chakula cha safari. Wakagoma. Akasema mkigoma kesho nitafanya miujiza. Nitautia mwezi giza. Kweli kesho yake mwezi uliingiwa giza. Wenyeji wakamsujudu Columbus na mumpa chakula. Waliona miujiza mtu kuutia mwezi giza. Lakini Columbus alitumia sayansi. Alijua habari za kupatwa kwa mwezi na mzunguko wake.

Binadamu anaweza kurusha mzinga na ukaenda kutua sehemu anayotaka. Anangalia umbali alipo adui, spidi ya mzinga, joto, mgandamizo wa hewa, spidi ya upepo nk. Anaingiza yote haya(Variables)kwenye formula na kupata angle anayopaswa kuweka mzinga wake. Na kweli mzinga unaenda kutua alipopanga.

Si Mungu naye anapotabiri mambo hutumia formula kama hiyo. Anapotabiri mfano kifo anaingiza mabilioni ya variables kumhusu mtu huyo kwenye formula. Alichokula, mawazo yake(Brain waves) maneno anayoongea, afya yake, watu wanaomzunguka, hali ya hewa. . . Yaani anaingiza kila kitu kinachomhusu mtu huyo kwenye formula kisha anapata jibu kuwa kesho Absalomu mwana wa Daudi atakufa kwa kunaswa kwenye mti. Hafanyi miujiza, anafanya hesabu. "Miujiza" inawezekana bila sayansi?
Thibitisha huyo Mungu yupo kwanza.
 
Ijapokuwa Biblia ni hadithi za watu zilizosukwa kwa ustadi wa hali ya juu na kuwa compiled pamoja... na hizi dini tumeletewa ili tutawalike...

But haiondoi dhana ya kuwa MUNGU Hayupo! Mungu amekuwa proved beyond reasonable doubt za mwanadamu kwa vitu vingi sana!

Ni mpumbavu/taahira pekee anaweza kukataa/kupinga uwepo wa Mungu!
Hata babu zetu tangu enzi na enzi waliabudu miungu.

Naamini Katika uwepo wa miungu wengi...NA SI HUYU MMOJA TUNAEHUBIRIWA!
 
Mungu ni zaidi ya Science
Anauwezo wa ku control chochote na ni creative

Mfano mdogo hapa duniani kuna mimea ya aina nyingi sana
Hayo kisa kusema Neno
Tu Ardhi itoe mimea
Na Ardhi ikatoa

Anachosema vitu vinatii
He manipulates matter
Katika kumanipulate matter huko anafuata kanuni za sayansi?
 
He does what he likes.those formula obey him to the fullest
Ulimwengu haupo shaghalanghala. Unafuata kanuni za kisayansi ambazo ndiyo kwanza tumeanza kuzigundua. Hii haionyeshi kuwa aliyeutengeneza alikuwa anafuata kanuni za kisayansi?
 
Kuna stori kuwa Columbus alipokuwa anaondoka kisiwa fulani huko Amerika aliwaambia wenyeji wampe chakula cha safari. Wakagoma. Akasema mkigoma kesho nitafanya miujiza. Nitautia mwezi giza. Kweli kesho yake mwezi uliingiwa giza. Wenyeji wakamsujudu Columbus na kumpa chakula. Waliona miujiza mtu kuutia mwezi giza. Lakini Columbus alitumia sayansi. Alijua habari za kupatwa kwa mwezi na mzunguko wake.

Binadamu anaweza kurusha mzinga na ukaenda kutua sehemu anayotaka. Anaangalia umbali alipo adui, spidi ya mzinga, joto, mgandamizo wa hewa, spidi ya upepo nk. Anaingiza yote haya(Variables)kwenye formula na kupata angle anayopaswa kuweka mzinga wake. Na kweli mzinga unaenda kutua alipopanga.

Si Mungu naye anapotabiri mambo hutumia formula kama hiyo. Anapotabiri mfano kifo anaingiza mabilioni ya variables kumhusu mtu huyo kwenye formula. Alichokula, mawazo yake(Brain waves) maneno anayoongea, afya yake, watu wanaomzunguka, hali ya hewa. . . Yaani anaingiza kila kitu kinachomhusu mtu huyo kwenye formula kisha anapata jibu kuwa kesho Absalomu mwana wa Daudi atakufa kwa kunaswa kwenye mti. Hafanyi miujiza, anafanya hesabu. "Miujiza" inawezekana bila sayansi?

Miujiza ndiyo Sayansi.
Mungu ndiye Mwanasayansi Mkuu. Binadamu wanamuiga kwa mbali sana .

Kufanya matrilioni ya vitu kuelea angani ni sayansi kubwa sana . Dunia ingekua peke yake basi ingeanguka anguko lisilo na mwisho lakni vitu au objects huko angani zinazunguka katika mivutano isiyo na mwisho hivyo kuvifanya vielee angani bila kupoteza uelekeo wake na mifumo kuendelea katika usahahi wake .

Muujiza haufanywi na binadam bali ni Mungu .
Ukiona binadam anasema kuwa anafanya muujiza basi hayo ni mazingaumbwe au kiini macho. Janja janja tu.

Muujiza Mkubwa wa kisayansi unaoiathiri majira na siku na miaka katika dunia mpaka leo ni ule wa Nabii Joshua kumwomba Mungu ili jua na mfumo wake usimame na kuendelea na vita kwa masaa sita .
Joshua 10:12-14
Yaani alirudisha Jua nyuma masaa sita kuanzia saa kumi na mbili jioni na kurudisha jua kuwa saa sita mchana.
Mpaka leo kuna mwaka wenye upungufu wa masaa 6 wenye siku mia 365¼ Ndio unaoitwa mwaka mfupi kuna masaa sita yanayoelea elea katika masaa 24.
Huo ulikuwa ni muujiza mkubwa sana wa kisayansi . Huo unafanywa na nguvu za Mungu Mwanyewe kupitia Malaika wake waliopewa kazi ya kusimamia mifumo katika uumbaji wake wa ajabu.
 
Katika kumanipulate matter huko anafuata kanuni za sayansi?
Ndio
Vya kiroho ili vije kimwili kwa kimwili zinatumia kanuni za kisanyansi
Na pia kanuni za kiroho zinaweza zikavunja kanuni za kisanyansi

Mfano Yesu alipaa , alitembea Juu ya maji (Jaribu kutembea juu ya maji utaniambia)
Samak 2 na mikate 5 kulisha maelfu ya watu
 
Mpangilio wa ulimwengu unaonyesha kuwa Kuna nguvu inayojitambua imehusika kupanga.
Mpangilio gani? Unajuaje ni mpangilio na si anthropic bias/ anthropic principle tu? Nguvu gani? Unajuaje inajitambua? Unajuaje imehusika kupanga?

Kama kila kilicho na order kinahitaji kupangwa, unaelewa kuwa, ujiondoa special pleading fallacy, hiyo ni hoja ya kwamba Mungu mpanga vyote hawezi kuwepo?
 
Ndio
Vya kiroho ili vije kimwili kwa kimwili zinatumia kanuni za kisanyansi
Na pia kanuni za kiroho zinaweza zikavunja kanuni za kisanyansi

Mfano Yesu alipaa , alitembea Juu ya maji (Jaribu kutembea juu ya maji utaniambia)
Samak 2 na mikate 5 kulisha maelfu ya watu
Siyo kwamba "kupaa," na kutembea juu ya maji na kuduplicate samaki na mikate kulitumia sayansi ambayo hatuijui bado? Kwa watu wa kale sayansi iliyopo Leo kwao ni miujiza mikubwa.
 
Mpangilio gani? Unajuaje ni mpangilio na si anthropic bias/ anthropic principle tu? Nguvu gani? Unajuaje inajitambua? Unajuaje imehusika kupanga?

Kama kila kilicho na order kinahitaji kupangwa, unaelewa kuwa, ujiondoa special pleading fallacy, hiyo ni hoja ya kwamba Mungu mpanga vyote hawezi kuwepo?
Si sayansi inasema anthropy inaegemea kwenye disorder. Bila nguvu ya kuweka mambo sawa ulimwengu ungekuwa shaghalabaghala. Ila siku zote vitu na viumbe vimepangika vyema.

Utasema Mungu mpanga vyote naye alitakiwa kupangwa, aliyempanga naye alitakiwa kupangwa. . . Hatuijui yalivyoanza. Ila ushahidi unaonyesha mambo haya yamepangwa vyema na nguvu inayojitambua. Kama ambavyo tukiona gari tunafahamu kuwa limepangwa vyema na kiumbe kinachojitambua.
 
Kama kila chenye order kinatakiwa kuwa na mpangaji hiyo maana yake Mungu hawezi kuwepo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom