Mungu anafanya miujiza au anatumia sayansi?

Nimesema ushahidi unaonyesha(sikumbuki kusema lazima) vitu tata huwa vimeumbwa. Lakini ushahidi huu haufai kuelezea chanzo cha Mungu ambaye tunasema hajaumbwa na mwanzo wa vitu vyote. Inafanana na ulivyosema. Kanuni za Newton haziwezi kuelezea Relativistic Speed.

Ushahidi huo unatosha kutuaminisha kuwa ulimwengu na sisi tumeumbwa. Tutakapokuja kwa muumbaji ushahidi huu hauwezi kufanya kazi kama ambavyo kanuni za Newton zinavyokwama kuelezea Quantum Mechanics. Lakini haimaanishi hazifai. Wala ushahidi wetu kushindwa kufafanua uwepo wa Mungu haimaanishi haufai.

Waamini Mungu hatusemi tunajua kila kitu kumhusu. Amesema njia zake hazichunguziki. Tunaamini tu.
Unajuaje kuwa ushahidi huo unatosha kutufanya tuamini kuwa ulimwengu na sisi tumeumbwa? Threshold ni ipi? Kwa nini unataja habari ya kuamini wakati kuamini ni kitu subjective?

Na kama ulimwengu na sisi tumeumbwa, kwa nini unaunganisha moja kwa moja sisi kuumbwa na Mungu kuwapo?

Huoni kuwa kurukia habari ya Mungu kwa sababu inaonekana tumeumbwa bila kujua tumeumbwaje ni logical non sequitur fallacy, kwamba unakimbilia conclusion ya kuwa tumeumbwa na Mungu wakati hata kama tumeumbwa, inawezekana hatujaumbwa na Mungu?

Kama kilicho tata ni lazima kiwe kimeumbwa, huoni kuwa hiyo kanuni inakataza kuwepo kwa Mugu tata ambaye hajaumbwa?
 
Ni suala la imani. Watu tofauti wanahitaji kiwango tofauti tofauti cha ushahidi kuamini jambo.

Tunaamini creator=Mungu.

Sijasema kilicho tata lazima kiwe kimeumbwa. Nimesema ushahidi kuwa vitu tata huumbwa ni ushahidi tosha kutuaminisha/kuniaminisha kuwa ulimwengu na viumbe vimeumbwa. Ushahidi huu haufanyi kazi linapokuja suala la kumuelezea Mungu. Umeongea huko juu. Kanuni hazifanyi kazi kwenye kila domain.
 
Binadamu anaweza kurusha mzinga na ukaenda kutua sehemu anayotaka. Anaangalia umbali alipo adui, spidi ya mzinga, joto, mgandamizo wa hewa, spidi ya upepo nk. Anaingiza yote haya(Variables)kwenye formula na kupata angle anayopaswa kuweka mzinga wake. Na kweli mzinga unaenda kutua alipopanga.

Si Mungu naye anapotabiri mambo hutumia formula kama hiyo. Anapotabiri mfano kifo anaingiza mabilioni ya variables kumhusu mtu huyo kwenye formula. Alichokula, mawazo yake(Brain waves) maneno
Ingefaa ufafanue:
Mungu ni nini?
Mtu ni nini?
Muujiza ni nini?
Sayansi ni nini?
 
Kuna stori kuwa Columbus alipokuwa anaondoka kisiwa fulani huko Amerika aliwaambia wenyeji wampe chakula cha safari. Wakagoma. Akasema mkigoma kesho nitafanya miujiza. Nitautia mwezi giza. Kweli kesho yake mwezi uliingiwa giza. Wenyeji wakamsujudu Columbus na kumpa chakula. Waliona miujiza mtu kuutia mwezi giza. Lakini Columbus alitumia sayansi. Alijua habari za kupatwa kwa mwezi na mzunguko wake.

Binadamu anaweza kurusha mzinga na ukaenda kutua sehemu anayotaka. Anaangalia umbali alipo adui, spidi ya mzinga, joto, mgandamizo wa hewa, spidi ya upepo nk. Anaingiza yote haya(Variables)kwenye formula na kupata angle anayopaswa kuweka mzinga wake. Na kweli mzinga unaenda kutua alipopanga.

Si Mungu naye anapotabiri mambo hutumia formula kama hiyo. Anapotabiri mfano kifo anaingiza mabilioni ya variables kumhusu mtu huyo kwenye formula. Alichokula, mawazo yake(Brain waves) maneno anayoongea, afya yake, watu wanaomzunguka, hali ya hewa. . . Yaani anaingiza kila kitu kinachomhusu mtu huyo kwenye formula kisha anapata jibu kuwa kesho Absalomu mwana wa Daudi atakufa kwa kunaswa kwenye mti. Hafanyi miujiza, anafanya hesabu. "Miujiza" inawezekana bila sayansi?
Mmmh
 
Ni suala la imani. Watu tofauti wanahitaji kiwango tofauti tofauti cha ushahidi kuamini jambo.

Tunaamini creator=Mungu.

Sijasema kilicho tata lazima kiwe kimeumbwa. Nimesema ushahidi kuwa vitu tata huumbwa ni ushahidi tosha kutuaminisha/kuniaminisha kuwa ulimwengu na viumbe vimeumbwa. Ushahidi huu haufanyi kazi linapokuja suala la kumuelezea Mungu. Umeongea huko juu. Kanuni hazifanyi kazi kwenye kila domain.
Imani ni irrelevant katika facts.

Kwa sababu unaweza kuamini hata uongo.

Sasa kwa nini unaona imani kuwa kitu muhimu katika kutafuta facts?

Unaweza kuamini kwa kuangalia mambo kwa anthropic bias.

Wewe mpaka sasa unaangalia mambo kwa anthropic bias tu.

Unaangalia kwa level ya mtu unaona kila kilicho tata ni lazima kiumbwe.

Hujaangalia at the quantum level vitu vinatokea tu bila kuumbwa.

Hujaangalia huko ambako dhana nzima za time na causality kama unavyozielewa wewe zinakuwa challenged na kuonekana hazina maana.

Hujaweza hata kujibu swali kwamba hata kama vitu vimeumbwa, unajuaje vimeumbwa na Mungu? That is a logical non sequitur leap, a logical fallacy.

Yani ni kama unasema wewe Mndengereko wa Rufiji, baba yako mzazini James Bond 007 mzungu. Kwa nini? Kwa sababu kila mtu lazima awe na baba mzazi.

Sawa, inawezekana ni lazima kila mtu awe na baba mzazi. Lakini hilo halimfanyi James Bond 007 kuwa baba yako mzazi. Inabidi ututhibitishie James Bond 007 yupo, na kama yupo ni baba yako mzazi.

Usirukie tu kusema James Bond 007 ni baba yako mzazi, kwa sababu kila mtu ni lazima awe na baba mzazi.
 
Huwezako wa Mungu kuwepo hakuna ila akili ya mwadamu ya kutochamgamkia awarenessau uelewa wa anayayona ndo unampa biased conclusion ndo udhaifu wetu.
Na aya mambo kila mtu wa kufikiri anayaona ila sasa jamii inayotuzunguka tunaendana nayo hivohivo.
 
Ha
Unajuaje kuwa ushahidi huo unatosha kutufanya tuamini kuwa ulimwengu na sisi tumeumbwa? Threshold ni ipi? Kwa nini unataja habari ya kuamini wakati kuamini ni kitu subjective?

Na kama ulimwengu na sisi tumeumbwa, kwa nini unaunganisha moja kwa moja sisi kuumbwa na Mungu kuwapo?

Huoni kuwa kurukia habari ya Mungu kwa sababu inaonekana tumeumbwa bila kujua tumeumbwaje ni logical non sequitur fallacy, kwamba unakimbilia conclusion ya kuwa tumeumbwa na Mungu wakati hata kama tumeumbwa, inawezekana hatujaumbwa na Mungu?

Kama kilicho tata ni lazima kiwe kimeumbwa, huoni kuwa hiyo kanuni inakataza kuwepo kwa Mugu tata ambaye hajaumbwa?
Hapa kiongozi ulivyosema hoja ni subjective upo sahihi sana. Hoja za kiimani ni ngumu kuzithibitisha isipokuwa mtu abaki kwenye misingi ya anachoamini kuwa ni sahihi. Mfano hata kwenye Maandiko MUNGU halazimishi mtu amuamini au amfuate, la hasha!.(MUNGU hataki walio vuguvugu.(kwa wenye imani ya kuamini uwepo wake).

Hapa ukindelea kujiuliza maswali mengi ni huwezi pata majibu yatakayokuridhisha maana ni hayapo(Labda kiroho ambapo IMANI itahitajika tena- kitu ambacho huwezi thibitisha tena...hivyo kitategemea maoni binafsi mwisho ambayo yatairudisha hoja yako kwenye A kutoka Z.

SASA.
Kukujaribu kukuchallenge naweza kuuliza baadhi ya maswali ambayo bado yatarudi kwenye imani😅

1. Unaamini uchawi/ulozi upo?? Au ushawahi kuona mtu aliorogwa?? Ama kurogwa??
Ama Kuhisi kitu cha ushirikina kutoka kwa watu wako wa karibu au mtu yoyote ambaye wewe binafsi ulikiri kuwa kuna nguvu isiyo ya kawaida imehusika hapa...

Kama jibu ni NDIO. Umeshawahi waza chanzo mama cha ushirikina(hiyo source kama unavyohoji kuhusu MUNGU).

2. Pia kwa wakazi wa maeneo yanayoamini hizo mambo za MIUNGU(gods)
Umeshawahi kaa nao karibu ukauliza kama ni kweli wanachokiamini kinanguvu au kinawasikiliza.??

Kama jibu ni NDIO/ama unahisi HIVYO japo bado hukubaliani nao...

Je??
Hiyo miungu nguvu inatoa wapi???
Au ushawahi simuliwa source ya nguvu za miungu fulani??

Kama jibu ni NDIO basi sawa...lakini kama jibu ni HAPANA jaribu kuwaza... Kwanini hujawahi ambiwa source za Miungu hiyo lakini una amini kama IPO na inanguvu??

Haijalishi nani alisambaza hizo nguvu...
Je ni nani au asili ya hizo nguvu ni wapi??
Nini kilitenengeneza hizo nguvu??
Nani alikitengeneza??
(Japo haya yatakuja kama ukiamini kuwa zipo japo inawezekana usizisisadiiki).

Hivyo basi kama ilivyo ngumu kuthibitisha hayo mambo basi ndivyo ilivyongumu...
Kuthibitisha doughts zako.....
Japokuwa zinalogic.

Sasa ndio waza kwa wanaoamini kwenye MUNGU sasa.
Tunachokoseana ni kulazimishana
Maana kwenye uwepo wa Hizi nguvu
Ukiweka mbele LOGIC pekee itakuwa ni ngumu kama hauna BELEIF.
 
Au ukianza kuwaza namna moyo unafanya kazi na kwanini sayansi zinashindwa kutengeneza moyo halisi kama unaoutumia ama figo etc...
Namna zinavyofanya kazi
Inaeleweka lakini,,,,kitu gani kilizifanya zianze kufanya kazi ndio hutopata majibu
zaidi ya maswali zaidi yasiyo na majibu ya moja kwa moja....

Yaani ukiwaza mashine labda ili ianze kufanya kazi inabidi SWITCH iwashwe...
je hiyo nguvu ya kuenda kuiwasha iliyokea wapi???
Na nani aliwasha??

hapa ndio unaona kuna nguvu ya ziada
Huenda ipo kwenye kufanya ukamlisho...

swali hiyo nguvu ya ziada unaweza ithibitisha??

jibu ni HAPANA.

Au fusion ya gametes mbili kuleta zygote baadae mtoto....

Ukaanza kuwaza .....mbona ni maji maji yanayoingia...

Je??

Mechanism ya mfupa inatokea wapi??
ni kweli tunaona hatua kwa hatua mfupa unapojiumba...

Je hiyo mechanism au nguvu ya kuanza kuumba huo mfupa imetokea wapi??
(Kisayansi inaelezeka lakini baada ya kitendo fulani). (Sasa nguvu ya kabla inayosema sasa..ni wakati wa mfupa..sasa ni wakati wa moyo...sijui brain...kianze hiki kifate hiki...unaweza tafakari ukapata majibu??

Lakini hata ukikataa bado....utaona bado kuna utashi wa ajabu upo hapo sio??

Lakini kuulezea ndio huwezi...

Basi waza pia kwenye MUNGU na Uwepo wake na namna ilivyongumu kuielezea SOURCE yake...kama unavyohoji.

Nadhani tulivyoumbwa Akili zetu zinaukomo wa fikra...ndio maana hata kuna mambo hata ukisema uyachunguze...hutopata majibu zaidi ya maswali zaidi ambayo hayana majibu zaidi ya maswali zaidi na zaidi.

1. Maswali kama yupo ama hayupo hapo
Ni wewe sasa..unavyochanganya (logic zako na imani zako). Maana ukisema uache kimoja huwezi fika.

LAKINI...

Yupo ndio...je Alitoka wapi??
Tutarudi kuanza kuhoji
Je ni nini kilifanya uchawi uwe uchawi??
Sijui blah blah blah....
Ni maswali magumu sana kama hayo ya uumbwaji wa binadamu kutoka kwenye mbegu.
 
Huenda hata ukielezewa namna ye anasema hajawahi umbwa...
Bado hutoelewa kulingana na uwezo wa akili zetu.
Mfano rahisi...
Utakuwa ushasikia kwamba dunia imeumbwa kimahesabu na fizikia....
Je kuna mwanasayansi alishawahi thibitisha how???

So unakuta vingi tupo juu juu...
Tu hata jibu likitoka kesho hutolielewa..
 
Ha

Hapa kiongozi ulivyosema hoja ni subjective upo sahihi sana. Hoja za kiimani ni ngumu kuzithibitisha isipokuwa mtu abaki kwenye misingi ya anachoamini kuwa ni sahihi. Mfano hata kwenye Maandiko MUNGU halazimishi mtu amuamini au amfuate, la hasha!.(MUNGU hataki walio vuguvugu.(kwa wenye imani ya kuamini uwepo wake).

Hapa ukindelea kujiuliza maswali mengi ni huwezi pata majibu yatakayokuridhisha maana ni hayapo(Labda kiroho ambapo IMANI itahitajika tena- kitu ambacho huwezi thibitisha tena...hivyo kitategemea maoni binafsi mwisho ambayo yatairudisha hoja yako kwenye A kutoka Z.

SASA.
Kukujaribu kukuchallenge naweza kuuliza baadhi ya maswali ambayo bado yatarudi kwenye imani😅

1. Unaamini uchawi/ulozi upo?? Au ushawahi kuona mtu aliorogwa?? Ama kurogwa??
Ama Kuhisi kitu cha ushirikina kutoka kwa watu wako wa karibu au mtu yoyote ambaye wewe binafsi ulikiri kuwa kuna nguvu isiyo ya kawaida imehusika hapa...

Kama jibu ni NDIO. Umeshawahi waza chanzo mama cha ushirikina(hiyo source kama unavyohoji kuhusu MUNGU).

2. Pia kwa wakazi wa maeneo yanayoamini hizo mambo za MIUNGU(gods)
Umeshawahi kaa nao karibu ukauliza kama ni kweli wanachokiamini kinanguvu au kinawasikiliza.??

Kama jibu ni NDIO/ama unahisi HIVYO japo bado hukubaliani nao...

Je??
Hiyo miungu nguvu inatoa wapi???
Au ushawahi simuliwa source ya nguvu za miungu fulani??

Kama jibu ni NDIO basi sawa...lakini kama jibu ni HAPANA jaribu kuwaza... Kwanini hujawahi ambiwa source za Miungu hiyo lakini una amini kama IPO na inanguvu??

Haijalishi nani alisambaza hizo nguvu...
Je ni nani au asili ya hizo nguvu ni wapi??
Nini kilitenengeneza hizo nguvu??
Nani alikitengeneza??
(Japo haya yatakuja kama ukiamini kuwa zipo japo inawezekana usizisisadiiki).

Hivyo basi kama ilivyo ngumu kuthibitisha hayo mambo basi ndivyo ilivyongumu...
Kuthibitisha doughts zako.....
Japokuwa zinalogic.

Sasa ndio waza kwa wanaoamini kwenye MUNGU sasa.
Tunachokoseana ni kulazimishana
Maana kwenye uwepo wa Hizi nguvu
Ukiweka mbele LOGIC pekee itakuwa ni ngumu kama hauna BELEIF.
Mimi siamini uchawi. Imani za uchawi ni ujinga tu.

Na kuhusu nguvu, imani inaweza kutengeneza nguvu kisaikolojia hata baadhi ya magonjwa yakapona, hiyo ni saikolojia tu, haihitaji Mungu awepo. Inaitwa placebo effect.

Mimi simlazimishi mtu kuamini kitu. Najua imani ni haki ya binadamu, ipo katika katiba na Universal Declaration of Human Rights tangu December 10 1948.

Mimi siamini Mungu lakini namtetea Gwajima awe na haki ya kuabudu anavyotaka. Kwa sababu haki yake ya kuamini anavyotaka ni upande mmoja tu wa shilingi, uoande w apili ni haki yangu ya kutoamini. Pande hizi mbili zipo katika haki ya freedom of conscience.

Sipo hapa kuingilia imani ya mtu au kutaka kumbadiklisha. Ukifikiria hivyo utakuwa hujanielewa. Mambo ya imani hayafai hata kujadiliwa. Kwa sababu ni mambo ya uhuru na faragha ya mtu binafsi.

Mimi naongelea ukweli. Falsafa ya epistemology. Unaposema naamini hiki, unajuaje hicho unachoamini ni kweli na si hadithi tu?
 
Kuna stori kuwa Columbus alipokuwa anaondoka kisiwa fulani huko Amerika aliwaambia wenyeji wampe chakula cha safari. Wakagoma. Akasema mkigoma kesho nitafanya miujiza. Nitautia mwezi giza. Kweli kesho yake mwezi uliingiwa giza. Wenyeji wakamsujudu Columbus na kumpa chakula. Waliona miujiza mtu kuutia mwezi giza. Lakini Columbus alitumia sayansi. Alijua habari za kupatwa kwa mwezi na mzunguko wake.

Binadamu anaweza kurusha mzinga na ukaenda kutua sehemu anayotaka. Anaangalia umbali alipo adui, spidi ya mzinga, joto, mgandamizo wa hewa, spidi ya upepo nk. Anaingiza yote haya(Variables)kwenye formula na kupata angle anayopaswa kuweka mzinga wake. Na kweli mzinga unaenda kutua alipopanga.

Si Mungu naye anapotabiri mambo hutumia formula kama hiyo. Anapotabiri mfano kifo anaingiza mabilioni ya variables kumhusu mtu huyo kwenye formula. Alichokula, mawazo yake(Brain waves) maneno anayoongea, afya yake, watu wanaomzunguka, hali ya hewa. . . Yaani anaingiza kila kitu kinachomhusu mtu huyo kwenye formula kisha anapata jibu kuwa kesho Absalomu mwana wa Daudi atakufa kwa kunaswa kwenye mti. Hafanyi miujiza, anafanya hesabu. "Miujiza" inawezekana bila sayansi?
Astrology

Na hiyo ndio system inayo tumiwa na baadhi ya wachungaji mashekhe waganga na makuhani

Yaani hapo lazima akupige Hela , Hayo mambo kafanya sana Muhammad and the likes
 
Kuna stori kuwa Columbus alipokuwa anaondoka kisiwa fulani huko Amerika aliwaambia wenyeji wampe chakula cha safari. Wakagoma. Akasema mkigoma kesho nitafanya miujiza. Nitautia mwezi giza. Kweli kesho yake mwezi uliingiwa giza. Wenyeji wakamsujudu Columbus na kumpa chakula. Waliona miujiza mtu kuutia mwezi giza. Lakini Columbus alitumia sayansi. Alijua habari za kupatwa kwa mwezi na mzunguko wake.

Binadamu anaweza kurusha mzinga na ukaenda kutua sehemu anayotaka. Anaangalia umbali alipo adui, spidi ya mzinga, joto, mgandamizo wa hewa, spidi ya upepo nk. Anaingiza yote haya(Variables)kwenye formula na kupata angle anayopaswa kuweka mzinga wake. Na kweli mzinga unaenda kutua alipopanga.

Si Mungu naye anapotabiri mambo hutumia formula kama hiyo. Anapotabiri mfano kifo anaingiza mabilioni ya variables kumhusu mtu huyo kwenye formula. Alichokula, mawazo yake(Brain waves) maneno anayoongea, afya yake, watu wanaomzunguka, hali ya hewa. . . Yaani anaingiza kila kitu kinachomhusu mtu huyo kwenye formula kisha anapata jibu kuwa kesho Absalomu mwana wa Daudi atakufa kwa kunaswa kwenye mti. Hafanyi miujiza, anafanya hesabu. "Miujiza" inawezekana bila sayansi?
...Mungu Hana haja ya kufanya mahesabu yote hayo. Ya Nini ? Mtu kamtengeza yeye akitaka kumuondoa anamuondoa TU! Hesabu mtafanya nyinyi Kutafuta Sababu za Kifo chake, Sio yeye....!
 
Naomba afanye miujiza ili tupate katiba mpya na TANGANYIKA ibaki mikono salama.
Kashindwe kufanya miujiza huko Gaza Palestine miaka na miaka watu wanakufa hovyo licha ya watu hao kuwa ni waumini wake ndio ataweza ktk katiba mpya !?? Uwepo wa Mungu ni fiction story
 
Hawafi hovyo,wanauliwa
 
Nimesema ushahidi unaonyesha(sikumbuki kusema lazima) vitu tata huwa vimeumbwa. Lakini ushahidi huu haufai kuelezea chanzo cha Mungu ambaye tunasema hajaumbwa na mwanzo wa vitu vyote. Inafanana na ulivyosema. Kanuni za Newton haziwezi kuelezea Relativistic Speed.

Ushahidi huo unatosha kutuaminisha kuwa ulimwengu na sisi tumeumbwa. Tutakapokuja kwa muumbaji ushahidi huu hauwezi kufanya kazi kama ambavyo kanuni za Newton zinavyokwama kuelezea Quantum Mechanics. Lakini haimaanishi hazifai. Wala ushahidi wetu kushindwa kufafanua uwepo wa Mungu haimaanishi haufai.

Waamini Mungu hatusemi tunajua kila kitu kumhusu. Amesema njia zake hazichunguziki. Tunaamini tu.
Mungu hayupo kwasababu uwepo wake unaotajwa ktk vitabu vinavyo muelezea na kuelezea sifa zake una contradiction nyingi nyingi tena sana

Mfano mungu Mjuzi wa yote mwenye upendo Kwa wote inakuwaje aruhusu watu wanao muambudu wagawanyike na kuwa na madhehebu /Dini tofauti Duniani !?

Kama Anaupendo Kwa wote -- amefeli wapi kutumia hiyo nguvu kuwaunganisha watu wote waliopo Duniani waweze kuwa ktk Dini Moja Waka muabudu pamoja bila ya kuwa na mpasuko au Utengano wa kiimani !?

Mzazi Bora Tangu lini akaruhusu Kizazi chake kiweze kutengana ilhali Ana uweze wa kutoruhusu hizo hitlafu zisiweze kutokea !? Ina maana kimantiki mungu anashindwa Kifikra hata na binaadamu!?

Huo uwezo wake wa yote uko wapi upendo wake wa yote uko wapi !? Ikiwa tu anashindwa kuwa unganisha watu na kuwa kitu kimoja ktk Imani !?

Na Kwanini kuhusu habari za mahubiri yake Asikuambie yeye mwenyewe wakati anauwezo wa yote na ujuzi wa yote !?

Kwanini Ameshindwa kutumia uwezo wake wa yote ktk kutufikishia habari zake na badala yake Amechagua watu ndio waje kumsemea na kutuambia habari zake !?

Kitu ambacho kinazidi kuleta mkanganyiko na kuwafanya watu wazidi kuwa na wasiwasi Nae kuhusu huo U-mungu wake na uweza wake wa yote tulio elezwa kuwa anao !?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom