Kwenye singularity kanuni za kisayansi hazifanyi kazi. Zinakwama. Lakini hawaachi kuzitumia. Kwa waamini Mungu, inapofika chanzo cha Mungu ushahidi unaoonyesha kuwa vitu tata vyote vinaumbwa unakwama, lakini hatuachi kuutumia kutuaminisha kuwa tumeumbwa na ulimwengu umeumbwa.
Kwa sababu katika sayansi kuna kanuni kwamba hatujui kila kitu. Tunaweza kuwa tumekosea lakini tukajua zaidi tukajiongeza.
Ndiyo maana kanuni za Newtonian classical mechanics zinafanya kazi katika context ya Newtonian classical mechanics, hazifanyi kazi katika Einstenian Relativistic physics, lakini hilo halitufanyi tutumie Einsteinian Relativistic physics popote pale.
Kwa sababu hatuhitaji Einsteinian Relativistic physics kwenye non Relativistic setting.
Kwenye sayansi kama nyundo inatosha kung'oa msumari huhitaji kutumia winch hata kama winch lina nguvu zaidi.
Kanuni kutofanya kazi si kanuni kuwa contradicted. Hayo ni mambo mawili tofauti.
Kanuni za Newton hazifanyi kazi katika speeds zinazokaribia speed ya mwanga, hapo tunahitaji kanuni za Einstein.
Lakini, ukweli huo hau contradict kanuni za Newton, unatuonesha tu kuwa kanuni za Newton domain yake si Relativistic speeds zikizo karibu na speeds za mwanga, domain yake ni speeds ndogo za kila siku hapa duniani.
Unachanganya suala la domain ya kanuni na kanuni kuwa contradicted.
Tofauti ya mfano wako na habari za kila kitu tata kuhitaji kusababishwa na muumba ni kwamba kanuni hii ina contradict uwepo wa Mungu.
Ukisema kila kilicho tata ni lazima kiumbwe na kingine hapo umeshasema kuwa Mungu muumba vyote hawezekani kuwapo.
Na kusema hujui Mungu katokeaje hujaepuka logic kwamba kanuni hii ina contradict uwepo wa Mungu. Inawezekana hujui Mungu katokeaje kwa sababu hayupo. Ni muhisika katika hadithi ya kuungaunga tu. Ushawahi kufikiria hilo?
Huelewi wapi hapo?