"Mungu anaangalia roho haangalii mavazi" ni kauli inayohamasisha mmomonyoko wa maadili. Wakristo tuwe na msimamo juu ya mavazi kanisani

NetMaster

JF-Expert Member
Sep 12, 2022
1,454
4,853
NB: mods nawaomben msihamishe huu uzi jukwaa,kuuedit,au kutoa kipande chochote kile, kwa niloandika, Kuna funzo kubwa sana hapa kuzuia kasi ya mmomoo wa maadili (Moral Decay) ambao unazidi kumea.

Ni jukumu letu kama wakristo kujaribu kukumbusha waumini juu ya wajibu wao kuvaa mavazi yanayositiri, hili likipuuzwa litafanya makanisa yawe sehemu ya kuongeza ufuska, hapo zamani sheria kama mwanamke asivae nguo za wanaume hususani suruali zilizingatiwa na yeyote aliekiuka aligeuzwa mlangoni, lakini sasa hali imebadilika.

Mfano mimi kwa jumapili iliyopita ya ppasak niliweka mkasa nilipoenda kumpa kampani na kusikiliza neno kanisa flani ambalo lina waumini wengi hata duniani lakini nilichokutana ni mabinti kuvalia suruali, nilishangazwa kuambiwa kinachoangaliwa ni roho, moja wao nilimpiga picha hii hapa.

img_20230409_120124-jpg.2582156

Hawa wenzetu wachache wa jumamosi naona kwao suala la mavazi hawataki masikhara na kwa hili wamefanikiwa kwa kuendelea kukazia maandiko, hata iwe suruali pana utapigwa stop mlangoni! ishu iliyopo ni makanisa mengine hasa kkkt, katoliki na kwa walokole, hali ni mbaya kiasi kwamba unaona kama vile nayo makanisa yanaenda na mabadiliko ya utandawazi hata kwa mavazi (hapo zamani ukivaa ovyo unafukuzwa)

Huku mitaani tunaweza kuvumiliana lakini yatupasa tujue nyumba yoyote takatifu inabidi mtu asiende kwa namna yoyote ambayo inakera wengine ama kuwatia wengine majaribuni hasa katika mavazi

JE, KAMA MUNGU HAANGALII MAVAZI ANAANGALIA ROHO, HAYA MAVAZI NI SAWA?

Photo shared by Pisi Kali Bongo on August 11, 2020 tagging @mathaabel. (1).jpg

Photo shared by Pisi Kali Bongo on June 24, 2020 tagging @doreen_mbise..jpg


Photo shared by ππ‰πŽπŽ 𝐔𝐏𝐀𝐓𝐄 πŒπŠπ„_πŒπ‚π‡π”πŒππ€ πŸ’ on April 10, 2023 tagging @iamnkiyah. May be an image...jpg


Photo shared by Pisi Kali Bongo on March 06, 2021 tagging @shamy_bk..jpg

PAMOJA TUUNGANE KUZUIA MMONYOKO WA MAADILI
 
NB: mods nawaomben msihamishe huu uzi jukwaa,kuuedit,au kutoa kipande chochote kile, kwa niloandika, Kuna funzo kubwa sana hapa kuzuia kasi ya mmomonyo wa maadili ambao unazidi kumea....
Aisee huyo mwenye tyt nyeusi huo upaja hatari
 
NB: mods nawaomben msihamishe huu uzi jukwaa,kuuedit,au kutoa kipande chochote kile, kwa niloandika, Kuna funzo kubwa sana hapa kuzuia kasi ya mmomoo wa maadili (Moral Decay) ambao unazidi kumea...
Ni ajabu,kama Mungu hangalii mavazi kwa nini viongozi wa dini,hawaji kwenye nyumba za ibada na vichupi,hao viongozi wanavyaa kanzu ndefu, ndani suruali, halafu joho kubwa sana, huoni maeneo tatanishi.
 
Ni ajabu,kama Mungu hangalii mavazi kwa nini viongozi wa dini,hawaji kwenye nyumba za ibada na vichupi,hao viongozi wanavyaa kanzu ndefu,ndani suruali,halafu joho kubwa sana,huoni maeneo tatanishi.
Huu utamaduni umekuwa ni cancer kwa ukristo maana baadhi ya waumini waliozoea kuvaa hovyo wakienda kuanzisha makanisa yao wanachafua ukristo, Mtu kama Masanja anavaa kata k / Mlegezo / Suruali chini ya ma*****
 
Aina ya wachungaji wa siku hizi ni vijana masharobaro, wanapenda kina dada wavae hivyo. Hawa wachungaji hawapendi magauni marefu na kanga nimewasikia laivu wakiponda uvaaji wa nguo ndefu. Ukihudhuria makanisa yao utashangaa nguo tata zilivyovaliwa, matako, mapaja, matiti na miundi imebanwa, ni kichefuchefu kitupu. Zaidi utashangaa praise team wako mbele kusifu na kuabudu huku nguo walizovaa ni utata mtupu. Wakongwe wa zamani huwa hatusifu wala kuabudu tunawakodolea macho tu. Utaabudu vipi wakati ushatolewa kwenye uwepo wa Mungu? Hapo inakuwa ni utukufu wa shetani tu
 
Wasabato, mashahidi wa Yehova pia wakatoliki kwa mbaali kidogo uzingatia suala la mavazi kwingine huko wanaogopa sadaka zitapungua. Haya christianity science church yaani makanisa ya kizazi kipya hali ni mbaya kabisa kwenye mavazi, muhimu sadaka tu.
 
Aina ya wachungaji wa siku hizi ni vijana masharobaro, wanapenda kina dada wavae hivyo. Hawa wachungaji hawapendi magauni marefu na kanga nimewasikia laivu wakiponda uvaaji wa nguo ndefu. Ukihudhuria makanisa yao utashangaa nguo tata zilivyovaliwa, matako, mapaja, matiti na miundi imebanwa, ni kichefuchefu kitupu. Zaidi utashangaa praise team wako mbele kusifu na kuabudu huku nguo walizovaa ni utata mtupu. Wakongwe wa zamani huwa hatusifu wala kuabudu tunawakodolea macho tu. Utaabudu vipi wakati ushatolewa kwenye uwepo wa Mungu? Hapo inakuwa ni utukufu wa shetani tu

nimeliahuhudia hili kwenye makanisa makubwa ya hawa wazee wa mafutaa ya upako
 
Back
Top Bottom