Munde Tambwe: Sheria itungwe kudhibiti mauaji ya mapenzi

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,112
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Munde Tambwe ameomba mwongozo wa Spika wa Bunge akitaka chombo hicho cha kutunga sheria kujadili ongezeko la mauaji ya wivu wa mapenzi.

Mbunge huyo ameomba mwongozo huo leo Ijumaa Juni 4, 2021 mara baada ya kipindi cha maswali na majibu.

Munde amesema kuna ongezeko la mauaji ya wivu wa mapenzi siku za hivi karibuni akitoa mfano wa vifo vilivyotokea mkoani Ruvuma na Iringa.

Juni 2, 2021 katika Chuo Kikuu Iringa Prudence Patrick (22) mwanafunzi wa mwaka wa pili wa chuo hicho alikamatwa na polisi kwa tuhuma za kumnyonga hadi kufa mpenzi wake, Petronia Mwanisawa ambaye pia ni mwanafunzi wa chuo hicho ikidaiwa sababu ni wivu wa mapenzi.

Huku akiwataka wabunge kulaani mauaji ya aina hiyo mbunge huyo amesema, “kumejengeka tabia ya mwanaume kumpiga mwanamke kuwa kawaida kabisa katika jamii yetu na jambo hili husababisha wanaume kuwaua wanawake kwa kipigo.”

Amesema hata wanawake wenye macho mekundu wamekuwa wakiuawa kwa kudhaniwa ni wachawi, “huwa najiuliza hivi hakuna wanaume wachawi.”

Hata hivyo, naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amesema hoja hiyo ni muhimu na nzito lakini si jambo la dharura kujadiliwa bungeni kulingana na kanuni za chombo hicho.

“Niombe Serikali mjitahidi kwanza kuelimisha jamii, mnapotoa elimu kuhusu uhalifu na hili mliseme na wanaothibitika kufanya vitendo hivi wachukuliwe hatua ili mtu ajue akifanya kitendo hicho ni mwisho wa maisha yake pia,” amesema.

Dk Tulia amesema si vyema mtu kufanya jambo la ukatili na kuendelea kuwepo katika jamii, akitaka hatua kuchukuliwa.

Chanzo: Mwananchi

Baadhi ya mauji yaliyotokana na wivu wa mapenzi, soma
 
Wanawake wachawi kuliko wanaume, Hata wenye mapepo ni wanawake, Wanaume wachache sana kwenye hizi mambo.
 
Eti wanawaomba viongozi wa dini kusaidia! Hawa viongozi wa dini siku hizi ni pumbav kabisa! Kila siku kuzungumzia ndoa na ngono na wanajiona wana akili timamu.
 
Sio kila tatizo linatatuliwa kwa kutunga sheria!

Tunayo sheria kali dhidi ya bangi lakini ndio tunaongoza Africa kwa matumizi ya hayo majani.
 
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Munde Tambwe ameomba mwongozo wa Spika wa Bunge akitaka chombo hicho cha kutunga sheria kujadili ongezeko la mauaji ya wivu wa mapenzi.

Mbunge huyo ameomba mwongozo huo leo Ijumaa Juni 4, 2021 mara baada ya kipindi cha maswali na majibu.

Munde amesema kuna ongezeko la mauaji ya wivu wa mapenzi siku za hivi karibuni akitoa mfano wa vifo vilivyotokea mkoani Ruvuma na Iringa.

Juni 2, 2021 katika Chuo Kikuu Iringa Prudence Patrick (22) mwanafunzi wa mwaka wa pili wa chuo hicho alikamatwa na polisi kwa tuhuma za kumnyonga hadi kufa mpenzi wake, Petronia Mwanisawa ambaye pia ni mwanafunzi wa chuo hicho ikidaiwa sababu ni wivu wa mapenzi.

Huku akiwataka wabunge kulaani mauaji ya aina hiyo mbunge huyo amesema, “kumejengeka tabia ya mwanaume kumpiga mwanamke kuwa kawaida kabisa katika jamii yetu na jambo hili husababisha wanaume kuwaua wanawake kwa kipigo.”

Amesema hata wanawake wenye macho mekundu wamekuwa wakiuawa kwa kudhaniwa ni wachawi, “huwa najiuliza hivi hakuna wanaume wachawi.”

Hata hivyo, naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amesema hoja hiyo ni muhimu na nzito lakini si jambo la dharura kujadiliwa bungeni kulingana na kanuni za chombo hicho.

“Niombe Serikali mjitahidi kwanza kuelimisha jamii, mnapotoa elimu kuhusu uhalifu na hili mliseme na wanaothibitika kufanya vitendo hivi wachukuliwe hatua ili mtu ajue akifanya kitendo hicho ni mwisho wa maisha yake pia,” amesema.

Dk Tulia amesema si vyema mtu kufanya jambo la ukatili na kuendelea kuwepo katika jamii, akitaka hatua kuchukuliwa.

Chanzo: Mwananchi

Baadhi ya mauji yaliyotokana na wivu wa mapenzi, soma
Ungeshauri wanawake wenzako waache KUDANGA! Unawapanga wanaume 20 unawadanganya unawachuna vihela vyao vya kudunduliza masikini wakihoji wanajibiwa kunya, unategemea wasikasirike kusalitiwa! Chanzo cha mauaji mengi ni USALITI WA MAPENZI / UKAHABA NA SIYO unaoitwa WIVU wa mapenzi.
 
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Munde Tambwe ameomba mwongozo wa Spika wa Bunge akitaka chombo hicho cha kutunga sheria kujadili ongezeko la mauaji ya wivu wa mapenzi.

Mbunge huyo ameomba mwongozo huo leo Ijumaa Juni 4, 2021 mara baada ya kipindi cha maswali na majibu.

Munde amesema kuna ongezeko la mauaji ya wivu wa mapenzi siku za hivi karibuni akitoa mfano wa vifo vilivyotokea mkoani Ruvuma na Iringa.

Juni 2, 2021 katika Chuo Kikuu Iringa Prudence Patrick (22) mwanafunzi wa mwaka wa pili wa chuo hicho alikamatwa na polisi kwa tuhuma za kumnyonga hadi kufa mpenzi wake, Petronia Mwanisawa ambaye pia ni mwanafunzi wa chuo hicho ikidaiwa sababu ni wivu wa mapenzi.

Huku akiwataka wabunge kulaani mauaji ya aina hiyo mbunge huyo amesema, “kumejengeka tabia ya mwanaume kumpiga mwanamke kuwa kawaida kabisa katika jamii yetu na jambo hili husababisha wanaume kuwaua wanawake kwa kipigo.”

Amesema hata wanawake wenye macho mekundu wamekuwa wakiuawa kwa kudhaniwa ni wachawi, “huwa najiuliza hivi hakuna wanaume wachawi.”

Hata hivyo, naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amesema hoja hiyo ni muhimu na nzito lakini si jambo la dharura kujadiliwa bungeni kulingana na kanuni za chombo hicho.

“Niombe Serikali mjitahidi kwanza kuelimisha jamii, mnapotoa elimu kuhusu uhalifu na hili mliseme na wanaothibitika kufanya vitendo hivi wachukuliwe hatua ili mtu ajue akifanya kitendo hicho ni mwisho wa maisha yake pia,” amesema.

Dk Tulia amesema si vyema mtu kufanya jambo la ukatili na kuendelea kuwepo katika jamii, akitaka hatua kuchukuliwa.

Chanzo: Mwananchi

Baadhi ya mauji yaliyotokana na wivu wa mapenzi, soma
Mbunge muongo sana huyu,!!!! kupiga wanawake siku haipo kawaida ni tofauti na zamani, wazee wa zamani mke akikosa anamcharaza mikwaju mbele ya hadhara na hakuna anayeingilia ila sasa ukimgusa kibao kimoja tu mwanamke unakamatwa unatupwa polisi dawati la jinsia mashitaka teleeee umenyanyasa kijinsia umedhuru mwili shambulio nk nk bila kujali huyo mwanamke alikutukana matusi ya nguoni ambalo nalo ni kosa la jinai.
 
Back
Top Bottom