Mume wangu huwa hatandiki kitanda

Mume wangu huwa hatandiki kitanda

Kitandike halafu chukua maji lita 60 kimwagie kila siku jioni kitabaki safi muda yote
Atakua anamkomoa nani? Njia nzuri ni kutandika kila unapoona kimevurugika hasa kama na mwenyewe unapenda ustaarabu lakini awe anamwambia jinsi anavyokereka.
 
Je ueolewa na Marioo?? Nijuavyo Mimi mwanamke huamka mapema kisha huiandalia familia breakfast na kuhakikisha Nguo kuanzia za watoto mpaka za mume zipo tayari kuvaliwa siku hiyo,kisha tunaandaa maji kwa ajili ya kuoga wewe na kisha mumeo,huku watoto nao wakijiandaa kwa muda wao, sasa huo muda mumeo anakua bafuni kuoga wewe ulipaswa ubadirishe shuka + folonya za mito na kutandika upyaa, ili hata kama mumeo atarudi tena kulala (ikiwa ni marioo) basi hatokitimua kama mlivyo kitimua usiku uliopita
Wanawake hebu tuacheni kulalamikia vitu ambavyo vipo ndani ya majukumu yetu, wanaume ni watoto zetu wakubwa na ni jukumu letu kuwatengenezea utaratibu na kuwasimamia kama tuwasimamiavyo vijana wetu
Safi sana naomba mdogod wako jamen nimekupenda
 
Hvohvo na siri zingine za ndani lazima uanike humu jiulize kwann baba na mama yako tangu wameoana mpka sasa wanaishi pamoja, na ni wazee, then jiulize wewe uko wapi kwa sasa ktk ndoa na ndoa nyingi za siku hizi kwann hazidumu, First impression matters alot, wacheni hizo mambo bhana, mnaudhi.
 
Wanawake mna mambo mengi sana,ukisema utandike utakuta katoa na kuweka shuka yenye maua kam bustani.Na akitandika yeye kosa uwahi kupanda kitandani,atakwambia amka tutandike shuka la kulalia.Bora kuwaachia wenyewe tu.
 
Aliyekwambia wanaume huwa tunatandika vitanda ni nani???!!!!

Nilitegemea uje na kesi ya mmeo kutokupa pesa ya matumizi. Akitandika kitanda kesho utakuja na kesi kuwa mmeo hakuridhishi kitandani.
 
Weka namba ya simu hapa tumpigie tumshauri maana umeshindwa kuongea nae nyumbani
 
Pumbaf kambisa...
Ngoja nikuolee mke mwenzio ili ukajifinze kwenu...
 
Katika sehemu ambayo huwa naiheshimu, ni sehemu niwekayo ubavu, kwa hilo nashukuru Mungu.
 
Jamani mume wangu kama amechelewa kuamka na mimi labda nimetoka hatandiki kitanda hadi nirudi nitandike!!

Hata nikisafiri wiki nzima hatandiki kitanda kinakuwa vuluu vuluku!!

Ananiudhi!!
Ni kweli dada wanaume wa dar hatuna desturi ya kutandika vitanda mtusamehe tu
 
Anzeni kulalia kwenye nyasi kama vipi...
 
Uwiiii, kweli watu tunatofautiana aisee! Mi ndo sitaki hata kumuona hubby anavaa viatu mwenyewe nataka nimvalishe sembuse nimlalamikie kutandika kitanda!?? Vingine vinipite kwa kweli wacha nimfanyie kila nnachoweza alimradi vipo ndani ya uwezo wangu! Ila sio kosa lako/lenu ila maisha ya tamthilia yanawaharibu mana mnakopi na ku pesti bila kutafakari! Unakuta mke wa mtu na watoto anao tena wadogo lkn ana mikucha km shetani au jini maimuna mikononi ataweza kutandika kitanda kweli? Ndo mnakuja kulia lia humu na kuiga kwenu visivyoigika!!
 
Back
Top Bottom