Mume wangu huwa hatandiki kitanda

Mume wangu huwa hatandiki kitanda

Kutandika kitanda lazima upinde mgongo...unaruhusu mumeo apinde mgongo ilhari wewe upo!
Huna adabu kabisa.
 
Watu watakuponda kwakuwa wengi hawatandiki vitanda na huona ndi uanaume. Ila ni uchafu wa kimataifa kulala hapohapo kama mnyama kisa mke hayupo si utandike hata vibaya!.

Mtoa mada nawewe jifunze kukua kama mke wa mtu haya uliowaeleza hapa watakusaidia nini? Mwambie mumeo. Kwenye mahusiano kuna siri nyingi watu hugombana hata miezi 5 hawaongei hawasalimiani ila hutunza siri nakuelewana amani irudi.
Wewe issue ya kitanda mitandaoni? Shame on you and your ramshackle husband.
 
Aisee inafaa aongeze mke mwengine aje kukusaidia kutandika kitanda....
 
Wanaume tunatandika kitanda tukiwa tunaishi wenyewe(mabachela) tukioa huo utamaduni unakufa wenyewe,duh ivi zile kitchen party hua mnafundishwa nini siku hizi hawa wanawake tunaowaoa kama masela wetu tu yaani ushindani tu tena wa kibwege unaweza kukuta hii kesi imefika mpaka ukweni
 
Ujue kuna mambo mengine kama ni mtu mzima, huna haja ya kuomba ushauri nje tena humu mtandaoni.
 
Shoga yangu umefundwa kweli??
Kutotandika kitanda nayo ni big issue kwa mumeo mpk likukere uje JF...
Hilo mbona ni dhaifu dogo sanaaaaa....
Utaweza vumilia makubwa kweli wewe...
Jifunze kukaa kimyaaa..kitu kidogo sans hichoo...
Mpk umekuja JF sitoshangaa kusikia una mkera mumeo kwa maneno kisa hatandiki..utamkimbiza nje shauri yako.
Achana na kumind vitu vidogo....unless km humpendi
Ukitandika unapungukiwa nini.....
 
Wanaume tunatandika kitanda tukiwa tunaishi wenyewe(mabachela) tukioa huo utamaduni unakufa wenyewe,duh ivi zile kitchen party hua mnafundishwa nini siku hizi hawa wanawake tunaowaoa kama masela wetu tu yaani ushindani tu tena wa kibwege unaweza kukuta hii kesi imefika mpaka ukweni
Tatizo mnaoa wanawake mnaokutana nao kwenye majumba ya anasa...
Full makope ya bandia..nywele bandia...kila kitu kwenye mwili wake fake mpk tabia fake...
Ukiulizwa umempendea nini eti ooh dem yuko km Kim kardashian...lafudhi yake kama jlo...
Hamjuagi kuna zaidi ya hayooo ndani ya mke mwema....
Tizama huyu sasa hata siri ndogo km hii anashindwa itunza...
Hahaha wanaume hebu kuwen makin mchaguapo wake....msikurupuke
 
Ndio maana nimemshangaa kua hata kutandika kitanda analeta ushindani na nikamuuliza ivi kitchen party hua wanafundishwa madudu gani kama analalama kutandika kitanda huyu atakua wale kucha za kubandika
 
Huyo tunafanana,ni mojawapo ya sababu iliyotufanya tuoe
au huyo wa kwako umemuoa wewe?
Kuna mambo mengine kwenye ndoa yanaongeza thamani
ya mwanamke,kama unadhani nakutania
tafuta HG afu mpe kazi ya kuwatandikia utaniambia
 
Mie mwenyewe huwa sitandiki kitanda aisee, mke wangu anatandika kila siku, mie nikifika tu nyumbani ni mshedede kwa kwenda mbele
 
Naomba nikuambie, Chumba chenu ni chako weye na huyo mumeo tu. Hivyo, swali safi la kujiuliza ni; Nnani anaingia chumbani kwetu aone hicho kitanda?? Ka umesafiri, ukajakuta shuka zimefuliwa na kitanda katandika, utakuwa na amani kweli au ndo mwanzo wa kuanza kunusa hadi godoro??
Tupeane majukumu; Mume alete sabuni weye ufue, mume alete fagio, weye ufagie na mume anunue pasi na kulipia umeme, wewe upasi na kutandika kitanda.
Huo ndo ushauri wangu
 
Moja kati ya mambo yanayonifanya nihitaji kuoa ni hili la kutake care kitanda na accessories zake (hili ninakiri limenishinda kabisaa). Mengine ni kufua, kupika na kuosha vyombo. Sasa mwanamke akija na mambo kama hizi sidhani kama hali itakuwa shwari. Though nafahamu umuhimu wa kusaidiana lakini sio kwa style hii.
 
Jamani mume wangu kama amechelewa kuamka na mimi labda nimetoka hatandiki kitanda hadi nirudi nitandike!!

Hata nikisafiri wiki nzima hatandiki kitanda kinakuwa vuluu vuluku!!

Ananiudhi!!
hapo dawa yake ni kutumia gundi unayagundisha hayo mashuka kitandani nayeye kma bado kalala gundisha vyote uone kma keaho yake atarudia
 
Duu kama mimi mke wangu haniamkii shikamoo over vile tunalingana!!! Et baby mambo? za asubuhi! za kazi? za kushinda?? Ananiboa kama nini, mi namwangalia tuu....
 
Duu kama mimi mke wangu haniamkii shikamoo over vile tunalingana!!! Et baby mambo? za asubuhi! za kazi? za kushinda?? Ananiboa kama nini, mi namwangalia tuu....
Hivi nitamwamkiaje mume wangu? Kama unataka nikuamkie usinivue nguo.
 
Back
Top Bottom