Mume wangu anatafuta kazi

Mume wangu anatafuta kazi

Mkuu Morning Glory, sikumbuki kama nilichangia kwenye uzi wako wa mwanzo ambao, kama sikosei, ulitoa kwenye Jukwaa la MMU.

Kwa kuwa ni hulka yetu kumtanguliza MUNGU hasa tunapokwama, hivyo, na mimi, usiku huu wa manane ninamtanguliza MUNGU kwenye ushauri wangu mfupi.

Kukosa ajira kwa Mumeo huenda ni Mpango wa MUNGU. Huenda MUNGU amekusudia makubwa katika Maisha yenu lakini sio kupitia ajira rasmi ya Mumeo ya Mshahara kwa kila mwisho wa Mwezi, Mkataba wa Kazi, kuripoti kazini kila kukicha, kuvaa Shati na Suruali - mkanda nje, kupokea Salary Slip kila tarehe 25 ya mwezi, kukimbizana na Mikopo ya Benki kwa Wafanyakazi, n.k., n.k.

Huenda MUNGU anawaepushia mabaya kwa kukosekana kwa ajira hiyo.

Jaribuni kuliangalia suala hili kwa mtazamo tofauti - mtazamo chanya. Cha msingi ni kuangalia fursa nyingi zilizopo na kuingia huko. Mwanzo siku zote ni mgumu, lakini uvumilivu na kumtumainia MUNGU ndiyo silaha. Hakuna haja ya kuanza parefu, anzieni chini - mdogomdogo. Jishusheni ili mpande. Hiyo PGD (haijalishi ni ya Masomo yepi) ni Mtaji kwa kuwa upana wa kuyaona na kuyapembua mambo pengine ni mkubwa kuliko wasio na kiwango hicho cha Elimu.

Kuna Mtu ninamfahamu. Alisoma Digrii ya Uchumi hapo UDSM na kuongezea Vyeti kadhaa baada ya hiyo Digrii. Aliacha yote, akaenda kusoma Kozi ya Mwaka mzima ya Kilimo kwenye Chuo kimoja cha Kilimo hapa Nchini. Akaanza kwa Bustani ndogo ya kukodi hapo Dar. Sasa hivi ingawa siyo Tajiri wa kusifiwa kwenye Vyombo vya Habari ana Mradi wa Shamba na Mifugo wa kutosha kabisa huko Arusha unaoifanya Familia yake iishi maisha ya neema na Watoto wasome Ulaya. Hii siyo fiksi - ni ukweli!

Sijui kama ninaeleweka. Hivyo ninaomba niishie hapa!
Ningeandika mengi!
 
Acha umbumbumbu na umbulumundu wewe! Nani kakuambia kazi ya house boy ni kashfa? We mbona unadharau kazi za wenzako? au kwakuwa ww ni manager? Hiyo postgraduate ndo inakutisha? Acha mawazo mgando watu wanalisha family zao kwa hizo kazi. Hata wabeba box wengi mtoni ni wapishi na wanaleta huge amount of money kwa familia zao
Kipi bora kukaa jobless au kuwa house boy na kupata chochote kitu? Nenda India huko na middle east uone Phd za wahindi wanavyouza magenge ya nyanya na kazi za upishi mahotelini utajua nn namaanisha
Shirikisha akili yako unapochangia mada sensitive.

Kushirikisha akili si kutoa mifano ya india, asia na ya wabeba mabox ulaya. Hii no Tanzania na si kawaida mtu mwenye postgraduate akawa houseboy. Huenda ukawa wa kwanza hapa TZ.
 
Kubali umezingua mkubwa,acha kujitetea,this is not INDIA,Give out a postive way jinsi ya kumsaidia Ndugu hapa,we utamlipa nini kwa taaluma yake ?
 
Hii huyo mumeo mpaka unamtafutie kazi wewe ina maana ni kilema au vipi, ajitume hata zege ababe mradi familia iende chooni bwana alaaa,yani kitendo cha wewe kumwombea kazi naona hatakuwa mfanya kazi mzuri
 
Kua na heshima ndugu yangu
Kwani umeambiwa yeye (mumewe) hatafuti?
 
Samahani kama nitakukwaza ila naomba nikuulize ili suala la kujiajili unalichukuliaje wee unaetoa mawazo hayo???kujiajili kunataka Plan, Pesa, na vinginezo...sasa mtu anakwambia hana mbele wala nyuma ile kupata mlo shida unamwambia akajiajili atawezaje au kujiajili mie sikuelewi nini napotoka jaman wadau hebu nisaidieni maana watu wengi wanasema sana suala la kujiajili mtu hana chochote zaidi ya yeye mwenyewe yaani Human Resource tu sasa combination ya Capital ataipata wapi hebu fikilieni bana sio mnakurupuka tu JIAJILI...ajiajili na Hewaaaa!!!😕

Asante umesaidia kujibu!
 
Kubali umezingua mkubwa,acha kujitetea,this is not INDIA,Give out a postive way jinsi ya kumsaidia Ndugu hapa,we utamlipa nini kwa taaluma yake ?

Mtu mwenye PGD awe houseboy Tanzania hii watu hawapo serious,halafu atalipwaje?
 
Kubali umezingua mkubwa,acha kujitetea,this is not INDIA,Give out a postive way jinsi ya kumsaidia Ndugu hapa,we utamlipa nini kwa taaluma yake ?
Kwani anavyokaa nyumbani miaka nenda anapata nini kwa taaluma yake?Kwani nilivyotoa mfano wa India nina maana hapa ni India? Jitambue mkuu
 
Kushirikisha akili si kutoa mifano ya india, asia na ya wabeba mabox ulaya. Hii no Tanzania na si kawaida mtu mwenye postgraduate akawa houseboy. Huenda ukawa wa kwanza hapa TZ.

Hivi nyie mnashirikisha ubongo mnavyojibu mada? Nimetoa mifano ya watu wenye Phd kwamba hawadharau kazi ili mradi anapata chochote kitu cha kuendeshea maisha. Sasa hiyo PG yake inamsaidia nini anakaa tu nyumbani? Mpaka mke anahangaika kule na kule....Tatizo elimu zetu zimekomaa na mfumo wa kuajiriwa tu ndio maana mtu mwenye PG anaona kufanya kazi za kawaida ni kudhalilishwa. Anyway
 
Samahani kama nitakukwaza ila naomba nikuulize ili suala la kujiajili unalichukuliaje wee unaetoa mawazo hayo???kujiajili kunataka Plan, Pesa, na vinginezo...sasa mtu anakwambia hana mbele wala nyuma ile kupata mlo shida unamwambia akajiajili atawezaje au kujiajili mie sikuelewi nini napotoka jaman wadau hebu nisaidieni maana watu wengi wanasema sana suala la kujiajili mtu hana chochote zaidi ya yeye mwenyewe yaani Human Resource tu sasa combination ya Capital ataipata wapi hebu fikilieni bana sio mnakurupuka tu JIAJILI...ajiajili na Hewaaaa!!!😕

Wala hata hujanikwaza. Kujiajiri si lazima awe na mtaji mkubwa. So long mkewe ana kakibarua at least naamini anaweza japo kukopesheka. Kuna jamaa hapa jirani alianza na genge la mtaji wa chini ya 150k, akajikuta kafungua kamgahawa na sasa anamiliki hardwares 2 zenye akili.

Tukijitoa kwenye tabia ya kuamini vikazi vidogo kama kuuza chips, genge, kufuga vikuku na kutumia elimu tulofanikiwa kuipata kuanzia kwenye vimradi hivyo, naamini kwa kiasi kikubwa tutakuwa tumejitoa kwenye utumwa wa ajira.

Swali na tatizo kubwa ni moja, TUNATHUBUTU????

BtW, umeisoma thread vizuri mkuu au umeibuka juu kwa juu. hakuna sehemu mleta mada kasema familia yake iko hoi hohehahe. Ye mwenyewe ana kibarua chake kinachoendesha maisha ya familia yake. Mjadala hapa ni ajira kwa mmewe na sio uhohehahe wa kipato.

Ahsanta.
 
Hapana kaka we ni zaidi ya kichwa
Be blessed bro
 
STORY FUPI YENYE MAFUNZO....
KUNA WIZI UMETOKEA BENKI

•••••••••••••••••••••• Jambazi "wote laleni chini pesa ni za serikali na maisha ni ya kwenu".
Wote wakalala chini.
HII INAITWA DHANA YA USHAWISHI - kubadilisha
njia ya kawaida ya kufikiria.
•••••••••••••••••••••

Kuna dada, kwa woga, akawa amelala chini
kimitego, jambazi akamwambia, "dada hebu kuwa na adabu, chukua kanga jifunike, hili ni tukio la ujambazi na sio la ubakaji.”
HUU UNAITWA WELEDI -
zingatia ulichofundishwa
kufanya.
••••••••••••••••••••••

Walipotoka kwenye wizi
jambazi mdogo, ambaye
anashahada ya uzamili ya
biashara, akamwambia
mwenzake, "tuzihesabu hizi fedha.” Yule mkubwa akamcheka kwa dharau na kumjibu, "wewe. mjinga sana hizo hazina haja ya kuhesabu, saa mbili
watatutangazia kwenye
taarifa ya habari tumeiba
kiasi gani.
HUU INAITWA UJUZI - Siku
hizi ujuzi ndio bora kuliko
vyeti.
•••••••••••••••••••••••

Baada ya majambazi kuondoka, meneja akamwambia mhasibu wa bank, "ujumlishie na zile milioni 80 tulizo iba sisi.”
HUKU KUNAITWA KUOGELEA NA MKONDO WA MAJI - kushabihiana na mazingira magumu kwa faida binafsi.
•••••••••••••••••••••••

Mhasibu akafurahi na kusema, "dah wizi ukitokea kila mwezi itakuwa burudani sana.”
HUKU KUNAITWA KUWA NA MAWAZO CHANYA - Furaha ndio kitu cha muhimu zaidi.
•••••••••••••••••••••••

Meneja kafurahi sana kwakuwa sasa matatizo yake yametatuliwa na wizi uliojitokeza.
HUKU KUNAITWA KUTHUBUTU - shikilia nafasi pale inapojitokeza hata kama ni hatari kiasi gani.
•••••••••••••••••••••••

Haya usiku wake taarifa ya habari ikatangaza kuwa wizi mkubwa sana wa million 100 umetokea leo benki.
Majambazi kuskia hivyo
wakaanza kuhesabu zile pesa lakini wakajikuta na milioni 20 tu. Yule jambazi mkubwa akashtuka na kusema, "dah! yaani meneja kaiba mara nne zaidi yetu bila kuchezesha msuli? Bora umeneja kuliko ujambazi.
”HII INAITWA ELIMU NDIYO KILA KITU - ishike sana elimu, ina nguvu kuliko dhahabu.

ISHIKE SANA ELIMU, MWAMINI SANA MUNGU, IKO SIKU UTAFANIKIWA.

DHIHAKA KWA BINADAMU NI KITU CHA KAWAIDA, ZISIKUKWAZE MPENDWA.

Mwalimu aliingia darasani akiwa tafrani amechoka sana akawataka w'funzi wote wakae kimya kilikuwa ni kipindi cha dini mara usingizi ukamchukuwa pale pale darasani, ghafla mkaguzi akaingia akasimama pembeni kwa yule mwalim. Mara mwalim alizinduka huku akipiga miayo alipotupa macho pembeni alimuona mkaguzi ndipo alipojibabaisha na kuwaambia w'funzi: "Na Hivi ndivyo walivyolala WANAFUNZI wa YESU, walipokua wanamsubiri kule mlimani, Jee kuna mwenye swali"? mkaguzi akapiga makofi na kumsifia kwa kufundisha kwa vitendo.

Nikutakie mafanikio mema. Mungu aendelee kukubariki na kukutia moyo. usikate tamaa.

Amina.

Amen
mtumishi
Hyo asprin inaponyesha kweli
God is everything!
 
Wadau wote wa JF Nliwahi kupost Uzi Hapa wa mume wangu kutokuwa na kazi na Huu ni mrejesho.Tunaendelea kuumia kadri siku zinavyoenda mbele na msaada wangu unakuwa haitoshi Kwa familia yangu.Watu wengi waliahidi kunisaidia lakini mpaka Leo nimeishia kuambulia ahadi hewa tu na uchokozi na utani mwingi kutoka Kwa wadau humu JF.Wenye nafasi tafadhali msaidieni mume wangu yani karibu tunaumbuka na ukizingatia tunaishi nyumba ya kupanga

PLAN B IMAMUHUSU SANA
Si kwamba ukienda Chuo basi ni lazima uajiriwe, Unaweza anza biashara yako mwenyewe, na biashara sio mtaji ila ni uvumilivu ndo mataji mkubwa kuliko hata pesa, Mme wako unaweza mpatia hata mtaji wa elfu 20 akiwa kweli siriasi hiyo pesa inaweza kuja kumtoa kabisa, kinacho takiwa na malengo na si kingine Dada, mme wako anaweza hata anza kuuza vocha stend, anaweza hata kuuza karanga au kuuza maji kama mko Dar.

Kinacho takiwa aweke pembeni hiyo elimu yake yote, lakini akijiona kwamba yeye amesoma na haweza uza hata vocha basi endeleeni kutafuta hiyo kazi.

HUO NDO USHAURI WANGU, SORY KAMA NITAKUA NIMEKUKWAZA
 
uyo mumeo kwa vile umemsifia ni mzuri ndo maana anachagua kazi hata kuuza genge hawezi anasubiri white kola job zimfuate!

Mkuu ndo tatizo la Watanzania, Dada anaweza mpatia mtaji hata wa 20,000/ mzee aanze kutembeza vocha mjini, akiwa na malengo atafika mbali, anaweza hata kuuza maji, kuwa na degree sio ishu.

Tatizo kubwa ninalo liona ni watu kuogopa kwamba sasa marafiki, ndugu na jamaa watanionaje kwamba nina degree na ninauza maji town.
 
Back
Top Bottom