Mume wangu anatafuta kazi

Mume wangu anatafuta kazi

Samahani mpendwa, nini kilisitisha ajira yake.
Alipata ajira nyingine na kuacha Ile ya kwanza ila kampuni ikafilisika na kusababisha wao kupewa kazi Kwa mikataba midogo(short term au temporary job agreement)
 
Wewe una kazi? Kama hauna mnaishi vp? Je kipindi anafanya kazi alihifadhi hela katika assets? Viwanja/mashamba? Au hela aliitumbua yote? Je nssf/ppf hakupata? Kama alikuwa mhasibu je kapata hati chafu mpaka akafukuzwa kazi? Kwanin asitafute kazi za kawaida hiz huku akisubiria ajira ya fani yake?
 
Ni jana tu hapa nimepost kuwa mapenzi si pesa! Nashukuru dada hapa umewapa ushuuuda. Nakuombea kwa mungu shemeji apate kazi, pole kwa masikhara wanayokupa wana-JF, ndio hivo hata vidole vyetu mikononi havilingani!

Kweli nimefarijika Asante
 
Alipata ajira nyingine na kuacha Ile ya kwanza ila kampuni ikafilisika na kusababisha wao kupewa kazi Kwa mikataba midogo(short term au temporary job agreement)

Oh kwahiyo sio kwamba hana kazi ila ana kazi ya mikataba midogo. Nakushaurini wekeni akiba, mkipata mtaji mdogo muanzishe vishughuli vya ujasiriamali. Ajira hivi sasa ni majanga. Na ujasiriamali ukiuchukulia serious, inalipa sana.

Kila la kheri mpendwa.
 
Nlivyoanza kusoma nkajua unacheza na akili za watu kadri nlivyoendelea nkagundua ni mahubiri mazuri yanafaaa sana, Ubarikiwe

Mkuu nakwambia siyo wewe tu yani kadri nilivyotiririka ndivyo nilivyogundua kitu . Elimu ni mwanzo mwisho.
Copy kwa Asprin. Upo Mkubwa! Ntakuseach hewani soon!
 
Last edited by a moderator:
kazi anatafuta lakini au ndo wewe tu unakuja hapa kulalamika usaidiwe? Maana kuna watu unaweza kuta anakulalamikia hana kazi miaka 5 sasa, kumbe ukichunguza unakuta anatuma application moja kwa miezi sita, sasa hapo unategemea kweli kupata kazi? Morning glory, matangazo ya kazi yanatoka kila siku tena mengi tu. Mwambie mumeo aapply daily uone kama atamaliza miezi 6 hajapata kazi
 
Last edited by a moderator:
ana ujuzi gani wa kusomea au wa asili??hilo nadhan lingwkua la msingi wewe kulisema,lakini poa mlishawah kujaribu biashara za mitaji ya kawaida??
 
Mkuu nakwambia siyo wewe tu yani kadri nilivyotiririka ndivyo nilivyogundua kitu . Elimu ni mwanzo mwisho.
Copy kwa Asprin. Upo Mkubwa! Ntakuseach hewani soon!

Mkuu nipo na nshasevu.

Kilichobaki ni kuchukua ndoo EPL kwa kuwabamiza Chelsick na kuwanyang'anya kijiti wanaotufanya tuishi kwa tabu ndani ya ardhi yetu wenyewe.
 
Last edited by a moderator:
Habari dada, uzi wako tokea wa kwanza niliuona ila uzi huu naona kama nina mzigo wa kuchangia.
Nina mambo baadhi ninapenda nikuulize na pia nikushauri,
1. Mumeo anayo drive (Msukumo binafsi wa kutafuta ajira??) Kuna watu wengi sana wanalia hawana kazi ila ndani mwao hawana msukumo wa kutafuta ajira kwa nguvu. Msukumo kama ulionao wewe wa yeye kuwa na ajira.
2. kazi ya kwanza aliipataje na ilikuwaje akaiacha? na hivi sasa anajishughulisha na nini au ana malengo gani mbali na kutafuta kazi??
3.Mbinu gani mnazitumia kutafuta kazi?? how are you updated when it comes to the job market?? mnanunua magazeti? mitandao?? mbinu gani za kuwahabarisha?
4. Nakushauri (sijui kama umelifanya hili,) andaa Cv ya mumeo, yenye current information, muandalie na cover letter nzuri wewe ndio uchukue jukumu la kufanya application kwa niaba ya mumeo, pia uipeleke tume ya ajira mwishowe anaweza kuitwa kwenye interviews na hatimaye kupewa kazi.
5.Mshirikisheni Mungu kwa kila mnalofanya na muombe pamoja kulichukulia jambo hilo kwa uzito sana kwa sababu jambo lisiposogea kwenye ulimwengu wa roho hata ulimwengu wa mwili linabaki pale pale.

Ni matumaini yangu kazi za accounts na procurement zipo nying tu na ana advantage ya kufanya kazi miaka mitatu tena kwahiyo chances za yeye kupata kazi ni kubwa.

Nawatakia kila la heri.
 
Imezingatiwa thanks mkuu
 
Thanks dear,mume mwenyewe mzuri siwezi mkimbia aisee ntapambana mpaka mwisho wa Maisha yangu
 
Back
Top Bottom