Mulugo: Nilifaulu peke yangu kwenda secondary

Mh. N/ Waziri wa elimu, mulugo amesema ktk kipindi cha medani za siasa na uchumi kinachorushwa na star Tv kuwa yeye alisomeshwa na padri na akafaulu pekee yake kwenda secondary.Pia amesema kuwa alichelewa kwenda chuo kikuu kwani alikuwa anatafta fedha kwa ajili ya kujisomesha. swali langu ni kwamba hivi serikali ilikuwa haitoi mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu enzi za akina mulugo?

Ukweli ni kuwa kipindi ambacho kama anasema kuwa loans for higher learning imeanza kutolewa na vyuo vikuu miaka ya 90s sina shaka kama alikuwa na sifa za kutosha basi angeweza kupata funds kufanya yeye aweze kusoma na angeweza digrii ambayo siyo BA (Economics n Education) bali BA Education with Economics sasa huyu mzee wa visiwa vya Zimbabwe na Pemba aache kwenda kwenye vyombo vya habari kujisafisha hiyo ni kazi mm ningemuona kama kudume pale tu angepima upepo na kuachia ngazi na iliarudi darasani tena na kuanza darasa la chekechea then to become a real academician.
 
bagi huwa haishindwi kuosema chochote tumuache tu maana tutaumiza vichwa
 
Mh. N/ Waziri wa elimu, mulugo amesema ktk kipindi cha medani za siasa na uchumi kinachorushwa na star Tv kuwa yeye alisomeshwa na padri na akafaulu pekee yake kwenda secondary.Pia amesema kuwa alichelewa kwenda chuo kikuu kwani alikuwa anatafta fedha kwa ajili ya kujisomesha. swali langu ni kwamba hivi serikali ilikuwa haitoi mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu enzi za akina mulugo?

mikopo ni programu ya juzi hapa....kipindi walikuwa hata hawakopeswi ilikuwa bure........ilaseme tu kwamba ahakuwa na sifa za kwenda chuo kikuu,jamaa anazidi kujidhihirisha kwamba yy ni kilaza
 
Ukweli ni kuwa kipindi ambacho kama anasema kuwa loans for higher learning imeanza kutolewa na vyuo vikuu miaka ya 90s sina shaka kama alikuwa na sifa za kutosha basi angeweza kupata funds kufanya yeye aweze kusoma na angeweza digrii ambayo siyo BA (Economics n Education) bali BA Education with Economics sasa huyu mzee wa visiwa vya Zimbabwe na Pemba aache kwenda kwenye vyombo vya habari kujisafisha hiyo ni kazi mm ningemuona kama kudume pale tu angepima upepo na kuachia ngazi na iliarudi darasani tena na kuanza darasa la chekechea then to become a real academician.

Nimecheka sana hii comment yako.

Hata hivyo nampongeza kwa kuvumilia baada ya kukosa fedha lakini hakukata tamaa ya kusoma.Ni vijana wengi sana wanakwama hapa.

Pia Sikubaliani na hii tabia ya kujisifia hivi ilihali anajua angekua that bright angepata scholarship na asingesubiri hivyo.
 
swali langu ni kwamba hivi serikali ilikuwa haitoi mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu enzi za akina mulugo?

Jamani, Mulugo wa ONE NINETEEN SEVENTY TWO "1 1972" naye ana enzi? Huyo kamaliza six juzi kati. Mimi nimentangulia darasani lakini nilipata mkopo. Anafanya maigizo ili tumuonee huruma.[/QUOTE]

mkuu kutokana na mwaka aliozaliwa na aliomaliza hastahil kuwa na cheo kikubwa kama hicho
 
Jamani kwani hakuna watu walio soma Songea Boys 1994-1996 humu JF washuhudie kuwa walikua nae darasani kutoa utata wa ukilaza wa mkuu huyu.
 
najisikia vibaya sana kusoma na mulugo shule moja-songea boys.inaniuma sana
 
Tusimwonee wivu Mulugo maana kasota sana kusoma BA (Economics of Education) 2002 - 2008 si amepata na PhD kabisa maana miaka 6 na hapo alikuwa hajawa mbunge...angekuwa mbunge angesoma miaka 18!!! Hiyo ni dalili ya nini? UKILAZA!!!!!!
 
Hivi kulikuwa na kuchaguliwa au kufaulu? Nikumbusheni wadau siku nyingi zimepita

Chama
Gongo la mboto DSM

Zamani haiikuwa kufaulu insuch kulikuwa na kuchaguliwa....yani kwa mfano nafasi za sekondari nchi nzima zilikuwa 20'000 ...mwalimu aliagiza kila mkoa upewe nafasi 1000 ....mkishafanya mtihani Kama mkoa una ushindani mmefaulu 14'000 na mnatakiwa 1000, wana chukua wenye average kubwa...,pili wana chukua makundi Maalum Kama walemavu...au wanawake..,na Kama kuna jamii dini pia inaagaliwa..
kuna mikoa mingine kiwango cha elimu lilikuwa chini ....wanapewa pia nafasi 1000 ...Tatizo limakuja unakuta hakuna wanafuzi 1000 waliofikia average ya kufaulu...hapo ndio mfumo wa kuchaguliwa inakuja tenA ...na wenye bahati kama Mulugo wanapewa nafasi...
baadaye watu wakShtuKa ...wakifeli mikoa yenye ushindani wanaenda kurudia kwenye mikoa mingine...wanafaulu..
....Tatizo linakuja form four kwenda juu hapo walikuwa wanajichuja...wenyewe.
 
Zamani ilikuwa kawaida kufaulu peke yako,mimi nilifaulu peke yangu wilaya nzima.So sio kitu cha maajabu
 
Zamani haiikuwa kufaulu insuch kulikuwa na kuchaguliwa....yani kwa mfano nafasi za sekondari nchi nzima zilikuwa 20'000 ...mwalimu aliagiza kila mkoa upewe nafasi 1000 ....mkishafanya mtihani Kama mkoa una ushindani mmefaulu 14'000 na mnatakiwa 1000, wana chukua wenye average kubwa...,pili wana chukua makundi Maalum Kama walemavu...au wanawake..,na Kama kuna jamii dini pia inaagaliwa..
kuna mikoa mingine kiwango cha elimu lilikuwa chini ....wanapewa pia nafasi 1000 ...Tatizo limakuja unakuta hakuna wanafuzi 1000 waliofikia average ya kufaulu...hapo ndio mfumo wa kuchaguliwa inakuja tenA ...na wenye bahati kama Mulugo wanapewa nafasi...
baadaye watu wakShtuKa ...wakifeli mikoa yenye ushindani wanaenda kurudia kwenye mikoa mingine...wanafaulu..
....Tatizo linakuja form four kwenda juu hapo walikuwa wanajichuja...wenyewe.

Hii kipengele cha dini SIO kweli
 
Kweli kabisa Father of All,

Enzi hizo, watu kibao walikuwa na alama ambazo siku hizi hazipatikani kirahisi (wanazipata watu wachache sana), lakini walikosa nafasi za kwenda sekondari kwa sababu hawakuchaguliwa.

Kuna mkoa mmoja ambao kuanzia kwenye mwaka 1980 hadi karibia na 1990 (kwa kadri ya kumbukumbu zangu), idadi ya watoto waliochaguliwa kwa kila wilaya haikuzidi 150 kwa mwaka. Alama ya chini za kuingia sekondari ilikuwa ni zaidi ya 76/150 (kwa masoma 3 ya Hisabati, lugha na maarifa, kila moja likiwa na alama 50).

Ngoja tuendelee kumsikiliza boss Mulugo ila muda si mrefu mambo yaliyofichika yatajifunua yenyewe!!

we umesoma lini!miaka yetu sie kufaulu na kuchaguliwa lazima angalau uwe na zaidi ya alama 115/150 kwa day schools km rungwe,njombe etc. ili kuchuguliwa boarding ilikuwa ni lazima angalau uanzie alama 120 huku Hisabati na Lugha zikiwa zinaangaliwa sana kama vigezo vikubwa!
 
Zamani haiikuwa kufaulu insuch kulikuwa na kuchaguliwa....yani kwa mfano nafasi za sekondari nchi nzima zilikuwa 20'000 ...mwalimu aliagiza kila mkoa upewe nafasi 1000 ....mkishafanya mtihani Kama mkoa una ushindani mmefaulu 14'000 na mnatakiwa 1000, wana chukua wenye average kubwa...,pili wana chukua makundi Maalum Kama walemavu...au wanawake..,na Kama kuna jamii dini pia inaagaliwa..
kuna mikoa mingine kiwango cha elimu lilikuwa chini ....wanapewa pia nafasi 1000 ...Tatizo limakuja unakuta hakuna wanafuzi 1000 waliofikia average ya kufaulu...hapo ndio mfumo wa kuchaguliwa inakuja tenA ...na wenye bahati kama Mulugo wanapewa nafasi...
baadaye watu wakShtuKa ...wakifeli mikoa yenye ushindani wanaenda kurudia kwenye mikoa mingine...wanafaulu..
....Tatizo linakuja form four kwenda juu hapo walikuwa wanajichuja...wenyewe.

Asante kwa uchambuzi wako kwa mantiki Mulugo alichaguliwa; msameheni tena ulimi uliteleza!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Pure lies if this guy is the smartest of his batch it means his was a bunch of tabularasa so to speak. By then chuo ilikuwa ni free sasa anaposema alichelewa kujiunga na chuo ili kutafuta pesa anamdanganya nani? Wakati kwenda chuo ilikuwa ni fursa ya kunenepa kwa kula bure.

Kuna jamaa yangu alijiunga na UDSM 1993. Wenzie waliokuwa na division three walipata scholarship za India. India wakati huo ilikuwa inatoa nafasi 60 kwa watz kwenda soma huko.

Wakati huo (1993) kulikuwa ndio mchakato wa uchangiaji elimu unaanza. sana sana ilikuwa ni kujilipia nauli ya kwenda na kurudi chuoni basi. Miaka hiyo kila mwanafunzi alipewa Sh.45,000/- kwa siku 70.(= na Sh.500/- kwa siku)

Je, JKT alikuwa kambi gani na ilikuwa oparesheni gani? Ajue tu kwamba njia ya mwongo ni fupi. Kunyamaza ni hekima.
 
we umesoma lini!miaka yetu sie kufaulu na kuchaguliwa lazima angalau uwe na zaidi ya alama 115/150 kwa day schools km rungwe,njombe etc. ili kuchuguliwa boarding ilikuwa ni lazima angalau uanzie alama 120 huku Hisabati na Lugha zikiwa zinaangaliwa sana kama vigezo vikubwa!

Ndugu MTENDAHAKI,

Nimeeleza vizuri kipindi ambacho nakiongelea. Na nimeshuhudia mwenyewe watu ambao walienda boarding schools na alama kama ≥78/150. Halafu enzi hizo ninazoongelea, day schools zilikuwa chache sana. Kwa mfano, DSM kulikuwa na Tambaza (both day and boarding), Azania (both), Zanaki (boarding kwa A-level tu) na shule nyingine chache sana. Kwa hiyo ni mambo ambayo nina uhakika nayo.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom