Muhongo: Ni upumbavu kusema Mnada Wa Vitalu Usitishwe

Muhongo: Ni upumbavu kusema Mnada Wa Vitalu Usitishwe

Muhongo tatizo lake ni mkweli sana
alichosema ni kweli kwa lugha ya wazi kabisa
labda katumia maneno makali lakini ukweli hakuna mtanzania anaeweza kuwekeza kwenye gas
Ni mtanzania gani na yupi mwenye utajiri wa kufikia USD Billion 540??
hata makampuni ya nje yanasaidiwa na serikali zao kupata hiyo mitaji.
mengi anachotaka apewe kitalu ili afanyie udalali lakini uwezo hana
Tukiwaamba watanzania waungane kama makampuni ni wabishi na wabinafsi..
kwa tulio na elimu ya mambo ya gas tunaona waziri kasema ukweli
tatizo serikali imekimbilia kugawa vitalu bila kuwa na sheria mathubuti inayoanisha mpewa tenda,kodi inayolipwa,mirahaba,ajira,mazingira,nk.

kuna Tatizo gani serikali ya Tanzania kuwasaidia wazawa kama kina Mengi katika kuendeleza vitalu?Kwanini tukimbile kuwagawia wawekezaji bila kuwawezesha wazawa ambao uchumi wao utabakia nchini kuliko kuwafaidisha wageni ambao wataondoka na uchumi wetu na kutuacha watanzania tukitaabika!
Nashauri Mengi asikilizwe na wazawa wapewe kipaumbele tusikimbilie wawekezaji kwa kila kitu ni Colonial legacy ambayo haijatuisha Waafrica juu ya wawekezaji
 
Duh msomi wetu busara na hekima zero, huyo naye ameamua kujipima kwa Dr. Mengi tutamuona 2015 akifuata walikopotelea kina Masilingi na Masha ktk medani za siasa.
 
Uwaziri na Ubunge wa viti maalum umemlevya sana Prof.Muhongo.
Sio Utu, Heshima wala Busara kwa Waziri kuwaita Watanzania wanyonge kuwa wao ni Wapumbavu.., Wapuuzi.., Wajinga... nk.

Ipo siku kitanuka tu, na huyo huyo Muhongo atakuja kumbembeleza Mengi ampe Airtime kwenye media zake ili kilio chake kiwafikie watanzania ili wamwonee huruma. Aende akamuulize Sumaye, Mramba, nk.
 
professor mulongo has insulted all tanzanian ni bora kuliko kututukana angetoa maelezo kwa kina on what is happening & it's advantage for the country,why this hapening now ktk vyombo vya habari,is this the way gov't runt? Is this openness <ogp> as we sign that agreement
 
Muhongo

Ni mtanzania gani na yupi mwenye utajiri wa kufikia USD Billion 540??
mkuu,
tutakuaminije unachoongea kuhusu gasi kama ni kweli wakati wewe figures tu zinakupa matatizo!

Angalizo: Most valuable company kama sijakosea kwa sasa ni Apple ni dola 500b!

Hivi unaelewa dola 540b? Wanatumia icho kiasi kwenye nini..wakati wa exploration,drilling au nikujenga offshore platform?

Unasema wanasaidiwa na serikali zao.Makampuni ya Norway wanatoa wapi huo mtaji wakati budget ya nchi yao haifikii hata nusu ya dola 540b!
Kuna big exaggeration ya figures kwenye haya makampuni ili wasilipe kodi stahiki,kuboost share prices na kuwakatisha tamaa wazawa kuingia kwenye hii business.
Na Muhongo anawasaidi kufanya hivyo!!

Mtaji sio lazima uwe pesa, kuna watu mtaji wao ni Knowledge.Founders wa Ophir Energy walikuwa ni waajiriwa kwenye oil industry, wakaungana na kuanzisha kampuni ambayo sasa hivi ina worth billions. Sisi mtaji wetu ni gasi!
 
mkuu,
tutakuaminije unachoongea kuhusu gasi kama ni kweli wakati wewe figures tu zinakupa matatizo!

Angalizo: Most valuable company kama sijakosea kwa sasa ni Apple ni dola 500b!

Hivi unaelewa dola 540b? Wanatumia icho kiasi kwenye nini..wakati wa exploration,drilling au nikujenga offshore platform?

Unasema wanasaidiwa na serikali zao.Makampuni ya Norway wanatoa wapi huo mtaji wakati budget ya nchi yao haifikii hata nusu ya dola 540b!
Kuna big exaggeration ya figures kwenye haya makampuni ili wasilipe kodi stahiki,kuboost share prices na kuwakatisha tamaa wazawa kuingia kwenye hii business.
Na Muhongo anawasaidi kufanya hivyo!!

Mtaji sio lazima uwe pesa, kuna watu mtaji wao ni Knowledge.Founders wa Ophir Energy walikuwa ni waajiriwa kwenye oil industry, wakaungana na kuanzisha kampuni ambayo sasa hivi ina worth billions. Sisi mtaji wetu ni gasi!

Hizi figure wanazimanipulate ili kutisha watu. Huyo Lokissa mara aseme $ 540 Bil, mara $ 540 Mil.
Kuna mahali nimesoma mwingine anadai ni $ 11-12 Mil. Mwingine aliwahi kusema ni $ 100 Mil. Yaani ni full utata!
 
Last edited by a moderator:
Hivi hii nchi ina sera ya gesi na mafuta? Kama hakuna, wanatumia vigezo gani kuingia mikataba?
 
Wapumbavu waache kuchelewesha wabongo kufaidi gesi yao!
 
Niliedit mkuu pale . Figure inayokisiwa kwa sasa ni hiyo USD 540 Billion..
inaweza kuwa chini ya hapo but sio kwa kiwango cha mtu mmoja kuweza kuwa na hizo hela
makampuni makubwa wanawezeshwa na nchi zao na wanaungana sio rahisi kwa mtu binafsi au kampuni moja kuweza yenyewe..
Hizi figure wanazimanipulate ili kutisha watu. Huyo Lokissa mara aseme $ 540 Bil, mara $ 540 Mil.
Kuna mahali nimesoma mwingine anadai ni $ 11-12 Mil. Mwingine aliwahi kusema ni $ 100 Mil. Yaani ni full utata!
 
Hizi dharau za mkwaya sasa zinapita boundaries.....Yeye kama jiologia maarufu duniani awaeleimishe watu wasiojua anachokijua yeye. Lakini sasa yeye anaingiza zile dharau za Mugango kwenye interests za Taifa.
 
Hapana mkuu
kabla ya kupewa kitalu lazima wahakikishe financial capacity yako, hapo lazima udocument kiasi ulichonacho bank kama kinawiana na garama halisi,labda kwa Tanzania ndio wafanye ujinga huo wasiangalie vigezo hivo, kigezo kingine kikubwa ni technical capacity kwa nchin zenye gas kama Norway mfano mwombaji mpya halazimiki kuweka mitambo mipya ya kusafirisha gas au kuchimba,kuna kampuni zipo zilishaweka mitambo hiyo na zina meli za kufanyia tafiti na kuchimba, wao wanalease tu sasa wanaita (Access to facility)
kwa Tanzania someone has to start a new kila kitu....Mkuu siko huko unakofikiri mimi kibaka tu natoa mawazo kulingana na upeo wangu nliouona nchi zingine..
Since TPDC wamebeba ridhaa yetu watu kama kina Mengi can work with them
KInachotakiwa kwa sasa ni ushirikishwaji wa wananchi wajue watafaidikaje na gas hiyo
tuwe na sheria ilio wazi tujue kampuni ikipewa tender wanalipa kodi kiasi gani na hizo fedha zinapelekwa wapi
pia sheria iangalie hao wageni wanajulikana na TRA na walipe kodi kama wazawa ili tufaidi fedha zao nk.......
nawashauri kina Mengi na wewe ndugu muungane muwe kama watu 10 walau mkishaonyesha mna uwezo itakuwa rahisi kukopesheka na bank ya dunia au AFD nk ili nanyi mpewe kitalu chenu....
huwezi kupewa kitalu kwanza kama hujatimiza vigezo hivo
ukisema uweke block au kitalu dhamana in case of default watakuja wakiuze? kumbuka kitalu kinakuwa leased na sio purchased, can you obtain a loan in a leased block???
What I think that can be accepted as collateral in mitambo hiyo wanayoinstall baharini na assets zingine za kampuni kama hisa na sio block...correct me if Im wrong
....
Mkuu tatizo lako na tatizo la watanzania wengi ni business skills, kwa akili yako ndogo unaamini kuwa mzungu au mchina atatoa hela mfukoni mwake kununua kitalu cha gesi kumbe ukweli ni kwamba atabid then akishinda anatumia kitalu hicho hicho kama dhamana ya kukopa na kutajirika na gesi yetu. Kitu ambacho hata mtanzania anaweza akipewa nafasi. Ni upuuzi huu wa kujizuia kuthubutu ndio umeifanya nchi yetu maskini. Wataalam kama wewe Lokissa hamjawahi kufanya hata biashara ya karanga na ndio mko kwenye ofisi kubwa mnakaa meza moja na wafanyabiashara wakubwa wa kimataifa bila kushauriwa na watu kama Reginald Mengi au Ally Mufuruki ndio maana mnaishia kudanganywa na kuiingiza nchi hasara. Mitaji ya biashara zote duniani uko bank na sio kwa makampuni au watu, the difference is dhamana tu, na kwenye gesi dhamana ni kitalu.
 
Lugha ya waziri sio mzuri,Mengi na Uchaga wake wote lkn yopo tofauti,anasaidia maskini na mkarimu,chakujiuliza uwezo anao au anataka kuwa mtukati???historia inaonyesha Madalali wengi walitajirika kupindukia kwa ujanjaujanja.wengi wao wakawekeza Ulaya na kununua klabu za mpira majuma na poti za anasa na kuwaacha mamilioni ya watu maskini.
 
Unaona unavyojichanganya na kudanganya watu!?
Awali tuliambiwa na wizara kwamba uwekezaji katika sekta ya gesi unahitaji capital ya atleast USD 100 Bilioni,wewe inayedai kuwa mtaalamu katika mambo ya gesi umesogeza goal post kwamba ni USD 540 Bilioni! Sasa hapa tumuamini nani Kati yako na wizara? Ngoja nimuite msemaji wa wizara ya Nishati na Madini atuweke sawa kwa taarifa sahihi.

PIa unadai kuwa hata hayo makampuni ya nje yanayokuja kuwekeza kwenye gesi yanafadhiliwa na serikali zao,unaweza kutuambia ni kwanini serikali yetu haitaki kuwadhamini watanzania wazawa ili nao wafaidi utajiri wa rasilimali yetu? NA bila shaka pesa watakayoivuna itabaki hapa hapa nchini na kuchangia maendeleo ya nchi yetu wakati wageni watakwenda kujenga kwao.

Kama wizara kwa maana ya serikali wanamuona Mengi hana uwezo, kwanini wasiwape watanzania wengine? Kwanini serikali inashindwa kuwasapoti wazawa kwa kujificha kwenye udhaifu wa mtu mmoja?
Hii inatosha kutuambia kwamba wasomi wa kitanzania bado ni watumwa wa wazungu hata kama wamesoma kwa kiwango cha juu sana kama ndugu yangu Prof. Muhongo. NA hapa ndipo nataka kukubaliana na wadau kwamba Prof. Muhongo anawapigia chapuo zaidi wageni kwakuwa 10% yake itakuwa guaranteed rather than kwa waswahili wenzake ambao ni aghalabu kumpa chochote na hata kama watampa italuwa hela mbuzi tu.
Mkuu Mwita Maranya, nakubaliana na wewe kwa 100%. Mambo ya gesi, nimeisha yapigia kelele sana humu!, tayari tumishaingia mikataba ya PSA (Production Sharing Agreements) na makampuni 22 ya utafutaji gesi wakati hatuna sera wala sheria!. Ni ukweli Watanzania hatuna "capacity" kwenye mambo haya ya gesi, sioni kwa nini tusisubiri kwanza performance ya hizo PSA 22 wakati huo tukijenga local capacity!, tukiandaa sera na kutunga sheria, tena kama ya Arabuni inayolazimisha mwekezaji lazima awe na local partner!.

Hizi PSA zilizopo, mwekezaji anachukua 100% na TPDC 0.0% kwa kipindi chote cha deni la uwekezaji (labda miaka 100!, investiment ikishalipa, then inakuwa 75% mwewkezaji na 25% TPDC for the rest of the life!, huku ni kuibiwa kule kule kama kwenye madini!. Hili nimelipigia kelele sana hapa Gesi asili: Is it "day light robbery?!"- watanzania tunaibiwa

Kwa taarifa tuu, hayo makampuni ya uwekezaji, nayo yanakopa!, Watanzania tungekuwa na capacity, sisi ndio tungekopa na kuyaajiri hayo makapuni kwa kuwalipa mishahara!, umiliki ungekuwa 100% ni gesi yetu!. Through colective investmen ts schemes, pensions funds zinge team up, zinaweza ku rais such capital!.

Kwenye bomba la mafuta nimesema hivyo hivyo!, Mkopo ni wa thamani ya 1.2 bilion dollars toka Exim Bank ya Uchina, tumepewe kwa riba ya 1% per annum!. Tumepewa grace period ya lazima ya 20 years, na repayment period ya 80 years!, total is 100 years!. Kama interest ni 1% kwa mwaka, total interest tutakayolipa ni 100% interest!. Kwa uchumi wa gesi ulivyo, deni la 1.2 bilions lingeweza kulipika lote within 6 months!, why lipa kwa miaka 100!.

Kipindi chote hiki cha miaka 100 ya mkopo, bomba litakuwa chini ya usimamizi wa mwekezaji!. Gharama halisi za utandazaji wa hilo bomba ni dola milioni 600! tuu, zimepanda marambili kwa sababu ni mkopo, with risk factor na ma 10% lukuki kuanzia "ghorofani mpaka chini!".

Hivi kweli serikali yetu ilishindwa kuzimobilize pension funds zetu kutoa hiyo kutoa hiyo dola milioni 600 na bomba likawa letu milele?.

Mchina sio mjinga kutengeneza mikataba mirefu ya kifisadi, na kwa taarifa, kwa umasikini tulionao, hii mikopo tuilipia kwa mtindo wa "mali kwa mali" barter trade kwa kuwapa gesi badala ya pesa at very low price karibu na bure!.
Hili pia nililipigia kelele hapa! Tetesi: Bomba la Gesi Mtwara:A "20 -Year Grace Period" ya Mkopo ...

Pasco.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Inabidi watu kuwa na uelewa mpana. The Mineral right or whatever is not an asset hii ipo kiuchumi. Your share will sound on capital investment. Huwezi kunyoosha suluari tu unasema nina share kwenye mradi kisa tu una jina kwenye leseni. india wana TPDC yao inaendeshwa vizuri tu na inakuwa na share hata Uarabuni kwenye visima vya mafuta. Sasa sisi tukisema tu TPDC intamiliki bila kuweka hata mia tutaambulia zero share. Angalia NDC kwenye Chuma ya Liganga tutakuwa wasindikizaji tu.


Wewe ungekuwa waziri wa wizara hiyo ungefanya hivi kama yeye???!!!!
 
Muhongo tatizo lake ni mkweli sana
alichosema ni kweli kwa lugha ya wazi kabisa
labda katumia maneno makali lakini ukweli hakuna mtanzania anaeweza kuwekeza kwenye gas
Ni mtanzania gani na yupi mwenye utajiri wa kufikia USD Billion 540??
hata makampuni ya nje yanasaidiwa na serikali zao kupata hiyo mitaji.
mengi anachotaka apewe kitalu ili afanyie udalali lakini uwezo hana
Tukiwaamba watanzania waungane kama makampuni ni wabishi na wabinafsi..
kwa tulio na elimu ya mambo ya gas tunaona waziri kasema ukweli
tatizo serikali imekimbilia kugawa vitalu bila kuwa na sheria mathubuti inayoanisha mpewa tenda,kodi inayolipwa,mirahaba,ajira,mazingira,nk.

Lokisa please dont provoke us! Unataka watanzania wawe na uwezo gani zaidi ya umiliki wa rasilimali hii waliyo nayo? Unajua kuna asset/capital za aina ngapi wewe? Ebu acheni kututania bwana!

Hakuna kitu ambacho nchi hii kingeshindwa kukifanya kama ingejua jinsi ya ku transfer hii capital kwenda kwenye aina nyingine tena tungeweza kabisa kuwa na umiliki wa 100% kama tungetaka!

Unaposema watanzania ni wabishi maana yake nini? Nani anayepaswa kutupa muongozo? Individual ama wizara kupitia sera? Umesema mwenyewe hapo chini tungekuwa na sera sasa hapo ubushi wa watanzania unaingiaje? Wamekataa kusiwe na sera?

Kama mtu hajui chakufanya akubali na ku consult wengine lakini acheni kuwapa watanzania matusi ya nguoni!
 
Lokissa, wewe ni mmoja wa wale mnaojiona hauwezi na hautakaa uweze milele, ondoa huo umasikini wa fikra ktk kichwa chako otherwise uko na Muhongo kudanganya watanzania wajinga kama wewe.
 
Last edited by a moderator:
kuna Tatizo gani serikali ya Tanzania kuwasaidia wazawa kama kina Mengi katika kuendeleza vitalu?Kwanini tukimbile kuwagawia wawekezaji bila kuwawezesha wazawa ambao uchumi wao utabakia nchini kuliko kuwafaidisha wageni ambao wataondoka na uchumi wetu na kutuacha watanzania tukitaabika!
Nashauri Mengi asikilizwe na wazawa wapewe kipaumbele tusikimbilie wawekezaji kwa kila kitu ni Colonial legacy ambayo haijatuisha Waafrica juu ya wawekezaji

Actualy siyo kuwasaidia bali ni wajibu wake serikali kuwawezesha raia wake tena siyo wale wenye cash peke yake bali kila mmoja katika nafasi yake na hasa wale wamahala gesi ilipopatikana.

Tanzania ina wataalamu hiyo ni capital ina wenye cash kidogo kama kina Mengi lakini ina wananchi kwenye vijiji ambapo gesi ilipatikana ambao ni proprietors wa hiyo land ambayo kwao ni capital vyote hivi in aggregate pamoja na government yenyewe wangeweza kupata mikopo mikubwa waka join hands na hizo kampuni ili kupunguza burden na kufanya trade in comparative advantage ku invest kwenye gesi!

Hapo kina sumbua ni 10% tu na ufupi wa maono pamoja na kukosa political will basi hakuna longolingo yoyote zaidi
 
Hii ni moja ya Big Result kwa kuondolewa UHAI mtu mmoja aliyekuwa anaitwa Julius Kambarage Nyerere.
"HATUWEZI SUBIRI miaka 100".
Ili tufanye sisi au tufanyiwe na Mataifa ya nje??
Tanzania itajengwa na Mchina not Mtanzania.
cc J.M. Kikwete
 
Back
Top Bottom