JiweLinaloishi
JF-Expert Member
- May 24, 2008
- 3,737
- 2,139
Anaweza kuwa na point, ila angeelezea kwa nini ni muhimu kutoa vitalu kwa sasa badala ya kusubiri miaka 100.
Kila mtanzania anaijua gesi, lakini sio mjiolojia kujua nini kinafanyika na kinachukua muda gani katika vitalu hivyo.
Na angejaribu kuelezea kwa nini watanzania hawawezi kumiliki vitalu hivyo.
Kutukana mtu badala ya kumwelewesha ni udhaifu.
ni kweli alitakiwa atoe ufafanuzi wa kina na si kutoa matusi, tulishakosea kwenye madini huku kwenye gesi na mafuta angalau tuwe na sheria na sera nzuri za kuhakikisha tunapata tunachostahili lakini kwa mazingira ya wapuuzi kama hao wakina Muhongo tutakuja kujikuta kwenye matatizo yale yale ya madini.