Steven Robert Masatu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2009
- 2,458
- 1,826
Nipo ndani ya ukumbi wa mikutano wa JK nyerere, ambako dakika chache Waziri muhongo amewaambia baadhi ya watu waliokuwa wakimuuliza maoni yake kuhusu ndugu Mengi kumshauri yeye na wizara kusitisha mnada wa vitalu. haya ndo maneno yake, Hatuwezi kuwasikiliza wapuuzi. Mda wa mjadala umekwisha, serikali haiwezi kuongea na wapumbavu wasiojua maswala ya gesi. Hawana uwezo kuingia kwenye miradi ya gesi na Tanzania haiwezi kusubiri miaka 100 kufaidika na gesi yake. Hawa wapiga kelele ni wa kupuuzwa amesema muhongo
Tutawajuza zaidi kutoka humu ndani. Kaeni mkao wa kula
Mkuu mie naomba uwasilishe ombi letu local suppliers, tunahitaji wasiwaruhusu hao wawekezaji waje na vifaa ili wapewe exemption, instead tupewe sie local suppliers kuwasambazia vifaa vyote watavyohitaji katika utafutaji na uchenjuanji wa hizo maliasili. Mwambie makampuni ya supplies yapo mengi sana na yanamilikiwa na wazawa tunahitaji support ya wizara kwenye hili suala, muwekezaji anakuja hadi na magnifying lens jamani.