Tanzania: Adui yetu ni nani na tuna fursa gani za kumshinda? Tunamlenga au tunamkwepa?

Kichuguu wewe uko Alaska nini...?

Hapana, nadhani kwenye hayo masaa nimechanganya na kuisha kwa twilight. Nilikuwa Anchorage mwezi wa tano mwaka juzi, jua likazama kama saa nne na nusu hivi lakini twilight iliendelea mpaka kwenye majira ya around saa tano na nusu hivi.

Back to ujinga (ignorance) wa raia: Unakumbuka kuwa 80% ya raia walisema kuwa wanataka mfumo wa chama kimoja? Kwa aibu, serikali iliamua kuwa-overide na kuingiza mfumo wa vyama vingi kwa vile ilikuwa ni wazi kabisa serikali ilifahamu kuwa wananchi hawa hawajui wasemalo.
 
Kuna wakati wa kuongea na kuna wakati wa kutenda.
Mpaka dakika hii hatujaongea mengi ya kutosha.
Kwa hiyo mtu asifikiri tunaongea sana.
Kitu cha kufanya miezi 6 kupangwa katika miaka 10 si hoja kubwa.

Hata tukipata jibu la maswali yetu bado tuna kazi nyingine kubwa,
kushawishi.

Ni ngumu sana kumshawishi Mtanzania wa kawaida popote pale alipo.
Kwake ni vema aiunge mkono CCM inayomliza kuliko kuunga mkono teory yeyote mpya.

Kumshawishi Mtanzania wa kawaida mpka akubali ni One on One Task.
Unachukua watu wawili watatu unawapa shule mkielewana unawageuza kuwa walimu.
Kwa hiyo hii si kazi ya jukwaani ni ya grass root level.
 
Kumshawishi Mtanzania wa kawaida mpka akubali ni One on One Task.
Unachukua watu wawili watatu unawapa shule mkielewana unawageuza kuwa walimu.
Kwa hiyo hii si kazi ya jukwaani ni ya grass root level.

Hiyo ndiyo inayotakiwa. I am sorry kuwa sikusisitiza hivyo katika post yangu ndefu. jambo hili ndilo upinzani wanakosa. Trip za helicopter alizafanya Mbowe nchi nzima mwaka 2005 hazikuwa zinafika kwenye grasroot level.
 
Mzee Kitila Mkumbo, heshima yako tena Baba! Naona umenena haswa.

Mzee Kitila, Frankly speaking, this is a courtesy call to let you know that, no good deeds go unnoticed. Pili, Mzee Kichuguu, Mzee Masatu, na wewe, mmeweka hoja ambazo lazima zijibiwe bila kuvungavunga. Nitajitahidi kuzijibu kwa hoja zilizobeba ushahidi na mifano ya hali halisi katika nchi yetu na nchi zote nitakazo ziongelea. Leo nimechagua vipengele vichache, ila nitaendelea kesho.

Binafsi, naamini katika haki za wananchi (wanasiasa na taasisi nyingine zikiwemo). Kila mtu au kundi la watu linayo haki ya kujiamulia mambo yake. Sioni tatizo kwa wanasiasa, au taasisi mbalimbali kuunganisha wananchi kwa lengo la kuongoza. Tatizo langu kwa wanasiasa ni pale wanapowatenga wananchi katika masuala ya uongozi. Wanapokataa kuwasikiliza wananchi wanasema nini. Wanafanya hila za kuwanyima wananchi haki ya uwakilishi wakati wao wako tayari kutoa hata hongo kununua hiyo haki. Wako tayari kutoa roho za watu kwa kutumia Magobori ili kupata hiyo haki. Eti wananchi wakitaka kujiongoza, lazima wafanane na wanasiasa; yaani wajiunge na vyama vya siasa. What a mess?

Zamani wananchi waliotaka kuwa wanachama, walipata mafunzo ili kuelewa misingi, kanuni, na imani za chama kabla ya kupewa kadi ya chama. Siku hizi kadi zinagawiwa kama Njugu mikutanoni. Wakati mwingine unapewa fedha kabla ya kupewa kadi. Zamani vyama vilichangiwa fedha na wanachama wake (mfano; TAA). Serikali ya kikoloni haikutoa ruzuku kwa TAA. Zamani watu waliingia kwenye chama kwa nia ya kuunganisha nguvu ili kumshinda adui. Siku hizi watu wanaingia kwenye chama ili kupata ruzuku au utajiri wa haraka. Wengine wanahongwa ili wapewe kadi kwenye mikutano ya hadhara ili kuonyesha idadi kubwa ya wanachama.

Nakumbuka Adamjee (Mbunge Kawe -CCM), alishindwa kutaja imani ya CCM katika mkutano wa kampeni. Ndiyo! kwasababu aligombea ubunge kutokana na fedha aliyokuwa nayo, na wala si kutokana na imani yake katika sera za CCM. Viongozi wa CCM walitaka mtu wa kushinda jimbo la Kawe, hivyo wakamgongea mlango nyumbani kwake. Alipofungua akapewa kadi ya uanachama papo kwa papo. Na busara za kuwawakilisha wananchi wa Kawe zikamjia papo kwa papo. Sera na ubora wa wanachama havizingatiwi tena, bali fedha na idadi ya wanachama ndio imegeuka kuwa dira na imani za vyama.

Kadili ya viraka ndani ya katiba yetu, baadhi ya vibaka waliopewa kadi na Kikwete pale Kigoma, wamepata hekima na busara za kutatua matatizo ya wakulima wa Kigoma. Lakini wakulima wenyewe wa kigoma wanaotaabika kila siku, hawana busara na hekima za kujisemea. Ati hawana hekima kwasababu hawajajiunga na vyama vya siasa. Wale wanawake wa Kigoma wanaobeba mizigo, kutwanga, na kukoboa nafaka, hawana hekima na busara. Isipokuwa wale wanawake wa "upendeleo maalumu" ndio wana hekima na busara.

Vyama vya siasa vilitakiwa kuchukuwa nafasi ya uongozi katika jamii yetu. Badala yake vinawagawa wananchi katika vibaba vya wenye itikadi na wasio nayo. Wenye haki ya kuwasemea wenzao na wasio nayo. Wenye haki ya kujiamulia mambo yao na wasio nayo. Wenye haki ya kuwawakilisha wenzao na wasio nayo. Vyama vya siasa vinapata fedha, nguvu, na mamlaka kutoka kwa wananchi. Lakini vinazitumia hizo fedha na hiyo nguvu kwa lengo la kuwatenga na kuwakandamiza wengine. Huu hauwezi kuitwa ujemedari, wala hauwezi kuitwa uongozi. Huu ni upuuzi.

Leadership endeavors to be inclusive, not exclusive. Leadership makes the effort to identify, recognize, and properly utilize the strengths of the constituent's component members. Leadership harnesses the collective brain power of the constituent and unleashes the harnessed force on the problems of the constituent. Leadership surmounts what divides but cements what unites the constituent. Leadership is more proactive than it is reactive. Leadership is sorely needed in our country.

Wananchi walikuwepo kabla ya vyama vya siasa. Kihistoria, Afrika ina mifano ya dola zilizostaarabika kuzidi dola nyingi nje ya Afrika. Nyingine zilipiga hatua kubwa kimaendeleo katika ujenzi na biashara. (mfano; pyramids - Egypt). Wakati huo havikuwepo vyama vya siasa. Hakuna mashine zilizojenga yale maajabu ya dunia. Ni nguvu za asili za binadamu zilizotumika. Walishirikiana na kuunganisha vipaji na nguvu za jamii bila kuwagawa na kuwatenga wananchi katika vibaba. Egypt sasa hivi kuna vyama vya siasa, mashine za kisasa, mafuta, na fedha. Lakini wananchi wa Egypt hawawezi kulima tuta la viazi vitamu bila kupata mfadhili wa kuja kuwapa fedha za kuwasaidia kulima. Kazi ya wananchi siku hizi ni kusubili maendeleo kutoka kwa wanasiasa, ambao nao wanasubiri kutoka kwa wafadhili.

Ingawa Watanzania hawakuwa na umoja baina ya kabila na kabila, lakini katika kabila moja, waliishi kwa pamoja kwa kuunganisha nguvu za kijamii. Hawakuwa na vyama vya siasa, lakini walitembeza mkirikiti wa kupambana na uvamizi, utumwa, na ukoloni. Hakukuwa na vyama vya siasa wakati Kimweri anawaongoza Wasambaa katika vita dhidi ya wavamizi. Wakati Mkwawa anawaongoza Wahehe katika mapambano dhidi ya wakoloni. Wakati Kinjekitile, Mputa, na Kibasila wanaongoza vita ya Majimaji. Huo ndio ulikuwa mwanzo wa juhudi zilizokuja kuzaa matunda ya uhuru.

Wananchi walijitoa muhanga kwa kupoteza maisha yao. Wakoloni walitambua kwamba wananchi wako tayari kufa kuliko kubuluzwa. Baada ya miaka michache, ndipo ikaundwa TAA na kuweza kuunganisha watu zaidi. Hakuna mtu anayebisha kuwa wananchi waliungana na TAA kwa kujituma bila kujali wangepata nini. Kinachonishangaza ni kuwa, vyama vyote vya siasa vinahitaji wananchi ili kushinda. TANU ilihitaji wananchi ili kushinda. Chiluba alihitaji wananchi ili kushinda. Kibaki alihitaji wananchi ili kushinda. Waade alihitaji wananchi ili kushinda. Kila mtu anahitaji wananchi wote ili kushinda.

Tanzania vyama vya upinzani vimedoda kwasababu wananchi bado hawajaviunga mkono kuishinda CCM. Nimesoma wadau wanasema hicho ni kitendo cha ujinga. Ina maana kwamba, vyama vya siasa popote pale duniani haviwezi kushinda bila wananchi wote kujitokeza kwa wingi ili kuviunga mkono. Kama wanasiasa peke yao hawawezi kushinda bila msaada wa wananchi wote, inakuwaje wanaweza kuongoza bila msaada wa wananchi wote? Kama kuongoza mnaweza peke yenu, kwanini kushinda peke yenu hamuwezi? Kama mtu hawezi kuwa na busara za kuwawakilisha wenzake mpaka awe mwanasiasa, atapata wapi busara za kukusaidia wewe ushinde uchaguzi? Kwa nini msiwaite wanasiasa peke yao wakawasaidia kushinda? Na watu wakiwapuuza, mnasema ni wajinga.

Je mnataka kuwatumia watu au mnataka kushirikiana na watu? Mna bima gani ya kuwawekea watu kinga, alafu wakaamini kwa dhati kuwa ninyi ni tofauti na CCM? Kwamba nia yenu sio kuwatumia, bali mkiingia madarakani mtashirikiana nao, badala ya kuwapiga teke. Je mtu anayewaangalia machoni na asiwaamini, badala yake akasema bora Zimwi likujualo, ni mjinga? Mnafikiri kwasababu watu hawawezi kuchanganua mambo, basi hawajuhi kinachowasibu? Animals will be animals. Lakini binadamu ana utashi. Inawezekana wasiweze kuchanganuwa mambo, but they have feelings. They feel it and we have to feel with them.

Kwa hiyo sipingi vyama vya siasa, ila nasema vyama vya siasa visiteke madaraka. Unakumbuka Nyerere aliposema kuwa CCM sio baba wala Mama. Nchi kwanza, alafu CCM baadae. Hata katiba ya Chadema (attached pdf format), inasisitiza umuhimu wa watu kuwa na nguvu. Sura ya tatu ya Katiba ya Chadema, kifungu (3A) kidogo 3.1 kinasema, " Falsafa ni fikra na mtazamo wa chama ambayo ni kuamini katika nguvu na mamlaka ya umma (people's power), katika kumiliki, kuendesha, kubuni, na kuendeleza maamuzi, mawazo na rasilimali, uchumi, na siasa ya nchi yao".

Katika katiba ya Chadema, kuanzia kifungu kidogo 3.1 mpaka 3.8 wanapigilia msumali juu ya nguvu za wananchi. Binafsi, nakubaliana na hivi vipengele katika katiba ya chadema, hata kama sina chama. Mzee kitila, umeandika mahala kwamba wewe ni mwanachama wa Chadema. Sasa inakuwaje huamini falsafa ya chama chako? Kwani mimi kutokuwa na chama, inaninyima fursa ya kutetea vipengele muhimu ndani ya katiba ya chama chochote? Huoni kwamba mimi nimekuwa muhubili mzuri wa chama chako kuliko hata wewe mwenyewe?

Katika katiba ya CCM, imani yao ya kwanza ni kuwa "Ujamaa na kujitegemea ndio njia pekee ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru". Lakini mambo wanayoyafanya hayafanani na hii imani. Unataka kuniambia kuwa kuna hata vyama vya vingine vya siasa vilivyoazima busara za CCM za kuandika kile wasichoamini? Alafu wananchi wakiwapuuza kwa kuona mnafanya mambo yasiyotofautiana na ya CCM, mnawaita wajinga? Au mnadhani ni wajinga kwasababu mnaona hawawezi kuchanganua mambo? Always remember-(People feel). Ndio maana nasema, kabla ya 2010, yatupasa kuruhusu fikra mpya zipenye.

Kama ilivyo kawaida yangu. Leo nanamalizia na mfano wa nchi iliyoendelea duniani kwa sababu ya wananchi kuwa na nguvu kuliko vyama vya siasa na Serikali. Hivi Mzee kitila ulikuwa unafahamu kuwa katika katiba ya Marekani neno SIASA (POLITICS) lilipigwa marufuku. Hakuna sehemu yoyote katika katiba yao ambapo kumeandikwa hilo neno. Hata vyama vya siasa (political parties), hakuna. Nimeambatanisha katiba ya Marekani (pdf format). Si umeniuliza tunaweza kufanya je bila siasa, kwani wao wanafanya je? Tofauti ni kwamba wao wana wawakilishi wa wananchi (Representatives), na sisi tuna wawakilishi wa vyama vya siasa wanaoviwakilisha vyama badala ya kuwawakilisha wananchi.

Rais wao wa kwanza George Washington alitawala nchi vipindi vitatu. Katika muda wote wa utawala wake, hakukuwa na chama cha siasa hata kimoja. Katiba yao ilitungwa bila chama cha siasa. Rais wao wa kwanza akatawala nchi bila chama cha siasa. Misingi ya uongozi waliyoiweka, na katiba waliyoitunga, ndivyo vinaiongoza Marekani mpaka leo. Wakati Geroge Washington anang'atuka, aliwahonya kuwa makini kuhusu vyama vya siasa (Refer to Washington farewell address - attached pdf format). Alisema visije vikachukuwa nafasi ya wananchi na kuanza kujiwakilisha vyenyewe. Ni kweli, angalia yanayo wapata sasa hivi. Vyama vimenunuliwa na big corporations. Wanaanza kupoteza mwelekeo kwa kupunguza nguvu za watu.

Wamarekani walipomfukuza mkoloni, walitupa Jongoo na mti wake. Sisi tulitupa Jongoo tukabaki na mti. Hawakutaka Serikali yenye madaraka kuzidi watu. Walisema hiyo ilikuwa Serikali ya mkoloni. Mkutano wa kutunga katiba ya Marekani ulifanyika Pennsylvania mwezi mei 1787. Mwakilishi wa wananchi kutoka Virginia bwana George Mason, alipinga kupitishwa kwa katiba mpaka iwe na haki za msingi za binadamu. Kilichotoka Pennsylvania siku hiyo ilikuwa siyo katiba bali "article of confederation" kwasababu haikuwa na haki za msingi za binadamu.

Ulipoletwa mswada wa haki za binadamu (bills of rights), ndipo ilitamkwa rasmi kuwa hii ni katiba ya Marekani. Kumbuka bills of right ilikuwa na mapendekezo 12, lakini mawili yalitupwa nje na yakakubaliwa kumi. Moja kati ya mawili yaliyokataliwa, lilikuwa ni kiinua mgongo na maslahi ya wabunge (wawakilishi) vinahalalishwa. Lakini mwaka 1992, vyama vya siasa vikapitisha mabadiliko ya 27 ya katiba ya Marekani kwa kufufua muswada uliokataliwa miaka miambili iliyopita. Wakajiwekea hayo malupulupu ambayo waasisi wao waliyakataa.

Kwa Marekani, hata Mahakamani, mwananchi anachagua, ama ahukumiwe na Jaji au ahukumiwe na wananchi. Wananchi wanaruhusiwa kumiliki siraha, ili siku Serikali ikiwaletea mauzauza, wanaingia barabarani kuiondoa madarakani. Chini nimetoa nukuu ya swali wanalojiuliza wamarekani mara kwa mara kuhusu katiba na haki zao za msingi.

Does not the Constitution give us our rights and liberties?

A. No, it does not, it only guarantees them. The people had all their rights and liberties before they made the Constitution. The Constitution was formed, among other purposes, to make the people's liberties secure-- secure not only as against foreign attack but against oppression by their own government. They set specific limits upon their national government and upon the States, and reserved to themselves all powers that they did not grant. The Ninth Amendment declares: "The enumeration in the Constitution, of certain rights, shall not be construed to deny or disparage others retained by the people."
 

Attachments

  • Copy of Katiba ya Chadema.pdf
    84 KB · Views: 499
  • George Washington Speech.pdf
    46.5 KB · Views: 43
  • The United States of America-Constitution.pdf
    98.6 KB · Views: 47
Kyoma,

Hizi ndio sauti ambazo laiti zingekuwa zinasikika kwa uhuru kwenye mitaa ya
Tanzania kama sauti ya ndege jua linapochomoza, naamini tusingelikuwa hapa tulipo.

Tume suppress mawazo ya watu, tulichopata ni mawazo ambayo yako corrupted. Watu wanaangalia kwanza kiongozi ana mawazo gani ndio wanatoa mawazo yao. Mawazo ya watu kama akina Kyoma hayawezi kutolewa freely kwenye jamii yetu.

Kyoma, haya maandishi yako kaka ni msumari kweli kweli. Laiti sauti kama hizi zingelikuwa zinasikika kila siku na kurudiwa na kurudiwa, tusingelikuwa hapa tulipo.

Well done brother!
 
--------------------------------------------------------------------------------

mhu!!!!!!!!!! mhu!!!!!!!!!! mhu!!!!!!!!!! mhu!!!!!!!!!!

Bado nipo, nakohoa tu, ila nitaongea baadaye kidogo.
 
Kichuguu,

Una uhakika gani kwamba wananchi ni wajinga? Hili linanipa taabu sana
kukubaliana na watu ambao wanaona kwasababu wananchi wanaendelea
kuipigia kura CCM basi ni wajinga.

Ukitaka kumtwanga bingwa kwenye ngumi inabidi umtoe kwa knock out, vinginevyo atapewa ubingwa wa points.

Sasa kama vyama vingine vya siasa vinafanana fanana na hiyo CCM, kwanini wananchi wasiamue kuendelea na CCM ambayo angalau wanaijua?

Tunapotumia muda mwingi kujadili ujinga wa raia, tunapoteza mwelekeo, tunachotakiwa hapa ni kujadili ujinga wa vyama vya siasa. Vyama ambavyo vinashindwa kuelewa kwamba ili vipate madaraka inatakiwa viende kwa wananchi na kupata baraka zao. Ni kawaida ya mwanadamu kuchukua credits kwa mafanikio yoyote na ku blame wengine kwa failures. Vyama vya upinzani na wasomi mbalimbali wameshindwa kuiondoa CCM kwasababu ya failurs zao kuelewa wananchi wa TZ wanataka nini, badala ya kukubali hayo makosa na kujifunza wanaona jibu rahisi ni kulaumu ujinga wa raia.

Ni kweli watu wetu wengi hawana elimu za kutosha, lakini kuelewa siasa huhitaji elimu kubwa. Kama alivyosema Kyoma feelings au instincts vinatosha kuwafanya waelewe nani yuko upande wao.

Tunaweza kubadili mwelekeo wa siasa TZ kama tu tutakubali kurudi kwa wananchi, kuishi nao, kukaa nao, kuwasikiliza wanataka nini na kushauriana nao. Kwasasa uchaguzi ukiisha TZ wanasiasa wanafunga virago, wanarudi mijini mpaka baada ya miaka mitano tena.
 
Mimi hizi shule ninazopata hapa, basi bana. Mzee Mwanakijiji hiyo shule yako ya ujuha na ujinga nimeikubali. Kichuguu palepale panapotakiwa. Kyoma hilo ni darasa la masters' degree. Of course kuna sehemu kadhaa ninatofautiana na wewe. Nitarudi.

Hivi ndivyo tunavyopaswa kuendesha mijadala yetu. Guys you have made my day with your ideas, I am walking taller and fatter the whole of thie weekend!
 
Mimi naamini watanzania sio wajinga na wala sio majuha, if anything Watanzania ni welevu mahiri!

Welevu wao huu ndio uliopelekea kung'amua kuwa kuna ubabaishaji mkubwa sana ktk uongozi wa vyama mbalimbali vya upinzani. Wakati mkoloni wazee walitambua kuwa kwa kumuondoa mkoloni kutoboresha maisha yao.

Katika wakati tulionao sasa (wa vyama vingi) wananchi naamini wanaona kuna mapungufu mengi ktk CCM, maisha yanakuwa magumu kadiri siku zinavyosonga wengine tushaanza kuamini kuwa hilo zimwi CCM limeharibika beyond repair. Si kweli kuwa watanzania hawalijui hili, wasiwasi wao ni kuwa wasije ruka maji na kuingia ktk matope halafu wakayahitaji maji kunawa! na hapo ndio swali kubwa linabaki palepale.. where are the alternative? Pengine wananchi wanachofanya hapa ni ku apply wait and see.


Sio siri upinzani umeshindwa kuwashawishi watanzania utayari wao wa kushika madaraka. Kuna mtu kakumbusha uchaguzi wa mwaka 1995 wakati Mrema na NCCR wanatingisha nchi. Mwamko ulikuwa mkubwa sana na pengine kama sio personal intervention ya mwalimu, Mrema akingekuwa Rais. Sasa hebu tu refresh memories zetu hapa, hivi kweli ulikuwa ni uamuzi sahihi Mrema kukosa Urais na kumpa Mkapa au tulichemsha? Yaliyofuata baada ya pale nadhani ndio jibu la swali. Watanzania wakaja ona kuwa Mrema na genge lake walikuwa wababaishaji, wenye uchu wa madaraka, ruzuku na tamaa ya uongozi. Once again watanzania walifanya uamuzi sahihi.

Leo hii tuna some credible opposition parties kama Chadema, CUF, UDP, TLP, NCCR etc hebu tuwaangalie utayari wao mmoja, mmoja au kwa kuungana. Kwangu mimi natofautiana na Mwalimu Kichuguu kwenye hili la uwezekano wa muungano wa vyama, tuache muungano ktk level ya Urais huo una complications zake tuangalie muungano unaonekana rahisi zaidi wa ngazi mitaa, udiwani na ubunge. The biggest stumbling block hapa bila kuuma maneno ni RUZUKU. Na hii CCM wameiweka kama chambo. Ruzuku za vyama zinakuwa determine na ushindi na viti vya udiwani na ubunge. Suala la kuachiana hapo ndio unakuwa mtihani. Kitendo cha M-cuf kumpisha M-chadema kwenye kiti cha ubunge ni kupunguza ruzuku ya chama. Matokeo yake kila chama kitadai kila sehemu wao ndio strong hold yao na vigezo vya kujua hii ni strong hold ya chama fulani ni mtihani mwingine. Kwa mfano mwaka 1995 Jimbo la Ubungo lilikuwa ni strong hold ya NCCR, then ikaja by election (baada ya Lamwai kushindwa kesi) Ubungo ikawa strong hold ya CUF same as ktk uchaguzi wa 2000. Ilipofika 2005 Young Mnyika na Chadema wameliteka jimbo la Ubungo na sasa ni strong hold yao, mifano ipo mingi.

Tatizo jingine la upinzani ni viongozi wenyewe, juzi tumeshuhudia hapa idea tu ya kuungana imeleta mtafaruku mkubwa kila mmoja analeta tafsiri yake. Kuna tatizo la viongozi makini ktk upinzani, nikiangalia Chadema napata just handful ya viongozi, the like of Slaa, Mnyika, Akwilombe, Mdee, Zitto (despite of all mapungufu) etc. Im sorry to me Mbowe is not Presidential material, lakini anafit sana kwenye level ya ubunge. CUF nako I cant see much apart from Lipumba, Lwakatare, Duni, Seif, Hamad, Khalifa, Machano, Miraj nk. Hata hivyo wengi wa hawa washaanza kuchoka na hii tag ya udini waliyovishwa na CCM wana struggle kuivua. Hivyo They still have a long way to go. TLP is more abt Mrema, same as UDP for Cheyo. NCCR is all abt Mvungi na Mbatia. The only way kuwa na upinzani thabiti ni hivi vichwa kuungana lakini hilo halitawezekana kwa kuwa RUZUKU itawavunja vunja wote.

Kwa msingi huo hapo ndipo welevu wa watanzania unapokuja kuona HERI YA ZIMWI LIKUJUALO........
 
Laiti watu wangefungasha virago vyao na kurudi nyumbani na kuyaweka wayasemayo humu katika vitendo kwa kweli tungekuwa mbali...

But until then jamboforums remains to be a talk shop....
 
Wanabodi,

Binafsi naamini sana kuwa sisi sote kinachotusumbua ni ignorance! sasa ikiwa ignorance ni Ujinga ama Ujuha mimi sielewi. Ignorance imetokana na nini sielewi pia! lakini yote kwa pamoja naamini kabisa kuwa adui yetu mkubwa ni UMASKINI. Umaskini umetufanya kuwa woga, vipofu, mabubu, tusiokuwa na hisia za aina yeyote zaidi ya umaskini wenyewe. Sawa na mfa maji ambaye hu-grab anything floating!..

Kwa nini nasema hivi basi.
Ni kutokana na kukubali kwangu kujitazama mimi mwenyewe ktk kioo na kukubali kuwa kile nachokiona ndio mimi. An ignorant person! ignorant kwa sababu naelewa kabisa kuwa napata maumivu makali ya Umaskini lakini sikubali kwamba mwili wangu una maradhi!....sipendi kusikia jina la Ugonjwa huo kabisaa!... na kweli wachache sana wanaoweza penda kujulikana wana HIV?..ndio umaskini ulivyo!

Ndugu zangu sisi sote hapa tunaelewa kwa mapana matatizo yetu, wengine wasomi wazuri,wana exposure, elimu dunia, U name it lakini inapofikia kujikomboa hapa kila mmoja anakuja na somo lake. Hakuna anayekubali unyonge wa kufikiri na kutenda,tumekuwa wazito ktk maamuzi yetu na dharau kubwa ktk kukubali kuwa matokeo ya ukimya huu utakuwa ni madhara makubwa sana baadaye....na cha ajabu sote tunaelewa kuwa kisipofanyika kitu hadi 2010 basi CCM wanachukua tena UTAWALA kwa asilimia kubwa vilevile.
Yet, hakuna kinachofanyika!..tumebaki kutazamana na kila mmoja anasubiri mtume!.mtu ambaye alichaguliwa na Mungu kuja tuokoa Wadanganyika!..

Jamani, tukubaliane sote kwa pamoja na imani ya Kiislaam japokuwa kwa hili moja dogo la elimu kuwa - HAKUNA MITUME WA MUNGU watakao kuja!.that era is gone! book closed.
Mitume ni nyie wenyewe ktk uzio wenu na elimu mliyokuwa nayo ni tosha kabisa ktk kumkomboa Mdnganyika. Sisi tupo ktk fungu la wanaojua lakini hawajui kama wanajua! - Wanaoweza lakini hawajui kama wanaweza. Njabu Ngabu is right!.....very right.
Na kama unabisha go look in the mirror!..ndugu zangu wakombozi ni sisi wenyewe isipokuwa hatujui kama tunaweza!..acheni ushamba!,Ujinga Ujuha na Ulimbukeni wa kuendekeza kesho-kesho. Hii ni ignorance!..
tumepewa zana zote na Mwenyezi Mungu, uwezo wa kutambua matatizo na dawa zake lakini sote tumekaa giiiih! wakati upande wa pili wa hao WATAWALA - viongozi ndio wanazidi kuwa ignorant kama makaburu ama KKK. Sikiliza majibu yao kwa ria waliowachagua! sikiliza majibu ya mawaziri wabunge huko bungeni? wamefikia kuwaita wabunge wengine kuwa hawana UPeo mkubwa!.. tena basi cha ajabu ni kwamba hawatoi maelezo yanayoweza kutuonyesha sisi wananchi kuwa wale wabunge kweli wana upeo mdogo wa kufikiri!
Ikiwa kweli waziri amefikia kusema hivyo! hii ni dharau kwa wabunge wengi sana wanaowakilisha hoja zao. Hata siku moja Upeo mdogo hautokani na swali ila hutokana na JIBU!..mbunge kuuliza swali asipewe jibu ila kuitwa ana upeo mdogo ni matusi ya nguoni!
Hata hivyo nitamalizia kwa kusema kuwa sisi tupo ktk fungu la Washamba kutokana na usemi wa Mwanakijiji (nimenukuu).WANAOJUA lakini HAWAJUI kama WANAJUA!
 
:mad: Si vizuri kama tukiendela kua wasemaji kuliko Utendaji...
Africa ina tabia ya kufahamu matatizo...na kubuni matatizo...Lakini Kwenye Utatuzi wa matatizo kwetu ni siasa....!!Hii ina tokana na kufanana Tabia na Adui...!!

Itakuaje ? itawezekanaje mimi nisimame ku piga vita rushwa wakati mimi Mwenyewe Ndio Mla Rushwa wa chini chini ?...Uta ikosoaje CCM wakati wewe mwenyewe una fanana na CCM...

Tuna shindwa kusogea kwasababu ya kuogopa kuusogelea Ukweli...

Nashangaa!! Wabunge walishindwa Kuibana Vizuri wizara ya Miundombinu...!!
Ok! lets go...
 
Masatu,

Maneno mazito!

Niliwahi kuanzisha thread hapa inayoelezea jinsi gani "pesa katika siasa inavyoisambaratisha Tanzania" lakini kwa sababu uchwara, ikaunganishwa na nyingine ili kuimaliza nguvu. Nilijenga hoja na kuonyesha ni jinsi gani kwa sasa ukombozi wa nchi yetu kwa njia ya siasa ni hakuna. Wengi unaowaona wanajitokeza, ni kwamba wanakimbia njaa kwenye taaluma zao kwa vile siasa zimegeuka "ajira" inayolipa sana. Sasa kwa vile watanzania wamewashtukia, leo wanaitwa "majuha", "wajinga", na matusi mengi tu. Nadhani kama siyo kukata tamaa, basi ni kufilisika kiakili na kisera.

Lakini, the only time in history ambapo upinzani ulikuwa na uwezo wa kuitingisha CCM ni 1995 na ni kwa vile watu wengi walihitaji mabadiliko bila kujali nani atawaongoza almradi CCM iondoke madarakani. Kushindwa kule lilikuwa ni kama pigo ambalo limeuhujumu upinzani hadi leo. Waliovaa ngozi za "kondoo" na kuja kama wakombozi, baada ya uchaguzi ule walizivua na kuonyesha "ufisi" wao halisi. Na kuanzia hapo, wale wote waliopata ubunge/udiwani 1995 kupitia upinzani wakaanza kupukutika taratibu kwa kuondolewa na kura hizo hizo zilizowaingiza; na wanaondolewa na watu wale wale ambao leo hii wanaitwa "wajinga". Demokrasia ipo wapi? Mtu kutumia uhuru wake kufanya analota almradi hajavunja sheria unamuita mjinga. Halafu kesho eti uje tena kwa mtu yule yule umwambie akuchague. Kawaulize waliowaita wananchi "kuku wa kienyeji", "wamepigika", etc. wameambulia nini.

Umeongelea ruzuku za vyama. Hilo ni jinamizi ambalo hadi leo hii silielewi. Tunakosa hospitali za maana, shule za maana, barabara nzuri, lakini kila mwisho wa mwezi mabilioni ya shilingi yanaingia kwenye vyama vya siasa, eti ruzuku ya vyama. Na sijawahi kusikia chama chochote, iwe CCM ama vingine vinavyopata ruzuku hiyo vikihoji uhalali wa sheria hiyo!!! Zaidi ni kwamba kumekuwepo na vilio vingi kutaka hiyo ruzuku vipewe vyama vyote vya siasa hata ambavyo havina wawakilishi/wabunge.

Mishahara na marupurupu ya wanasiasa: siasa imegeuka "taaluma" inayolipa sana kiasi cha kila mtu kukimbilia huko. Mbali na maipo yaliyo wazi, kuna yaliojificha nyuma ya pazia. Siasa imgeuka kuwa muhimili wa maendeleo ya Tanzania. Kila kitu kimekuwa siasa.
 
Je yawezekana kuwa tumekata tamaa na tumekubali yaliyokuwa yawe, na liwalo na liwe, kila mtu na vyake ila Mungu ni wetu sote? Yawezekana kuwa tatizo letu siyo ujinga, ujuha, ulimbukeni n.k bali ni tatizo la kukata tamaa? Kwamba whatever happens to us that is our fate and whatever gonna happen to us that is our destiny? Je twafikiri twaweza kubadilisha kilicho mbele yetu tu tuyupe mikono kwa kungojea hisani ya muda, huku tukipiga magoti tukisubiri muda utuonee huruma? Yawezekana basi kuwa baada ya kupima chaguzi mbalimbali na jinsi wanasiasa wanavyotenda tumefikia mahali pa kusema "haiepukiki" na "hakuna mlango wa kutokea".

Kama tatizo ni kukata tamaa na kukubali kilichopo kwa vile kile tunachotumainia hakipo na hakitakuwepo kwa muda mrefu, tutafanya nini kurejesha matumaini?
 
Mzee mwana kijiji,

Watu hawaja kata tamaa hata kidogo ila tumegubikwa na wingu la Umaskini wa akili na mali.
Ukisoma maelezo mengi yaliyotangulia utagundua kuwa vichwa vipo na watu hawajakata tamaa kabisa kwani kama wangekuwa wameisha kata tamaa vyombo kama hii JF visingekuwepo kabisa!...Tatizo ni kutojua kama tunaweza. Sawa na mtoto mwenye kipaji cha Udaktari ama sheria lakini kaamua kuwa mfuga kuku, akisingizia mazingira na soko la biashara hiyo. Kuna mchangiaji mmoja aliwahi toa mfano wa Nyerere ambaye aliacha kazi yake ya Ualimu na kujiunga na TAA akitegemea michango ya chakula na usafiri toka kwa kina Bomani, Sykes na kadhalika!..hawa ndio watu Walijua na walijua kuwa Wanajua....

Masatu,
Swala la vyama na ruzuku mimi sioni kabisa tatizo hapa, ikiwa hesabu ya ruzuku ipo determined kutokana na USHINDI wa viti vya udiwani na Ubunge..bado CUF wanapata ruzuku za ushindi sio ruzuku kutokana na kusimamisha mgombea. Hesabu ya washindi haiwezi kupungua ama kuongezeka ikiwa mshindi ni mmoja tu kwa hesabu kamili ya wilaya na Majimbo. Na kizuri zaidi ni kwamba wakiungana kama chama kimoja ruzuku itakuwa kulingana na vyama vilivyopo. Mathlan millioni 5 ukizigawa kwa vyama 5 ni chache ktk mgawanyo kuliko hizohizo 5m kwa vyama 2 hapa wamepunguza sana hesabu ya matumizi na heasabu kubwa ya uongozi usiotakiwa. Chama hiki kitakuwa na fedha zaidi ya kujiandaa kama chama kimoja!
Fanya utakavyo fanya hesabu inabaki ile ile isipokuwa kuna unafuu zaidi ktk kuwa kitu kimoja.. CUF hawezi kuchukua strong hold za Chadema ama vise verse! na hata kama kutakuwepo na mabadiliko ya mgombea kama ulivyoelezea kumbuka hawa jamaa watafanya uchaguzi wao mdogo wa mwakilishi ktk kila ngazi kabla ya kumchagua mwakilishi. Mathlan leo hii J.J Mnyika kashika Ubungo lakini kabla hajawakilisha Ubungo atapambana na wawakilishi wa CUF, NCCR-Mageuzi, TLP ktk uchaguzi wao mdogo ama Convesitional. Ushauri mkubwa ni kuwaacha walioshinda kuendelea kuwakilisha sehemu walizoshinda na wengine ktk strong hold za CCM kuwachagua watu wanaoweza shindana kwa vigezo vya Wadanganyika!....forget about sera!.. vyama vya upinzani lazima vigeuze mpango wa wawakilishi wao uwe ule wa ushindani kwa sifa za CCM. Kutafuta MTU anayekubalika mtu anayeuzika kama CCM wanavyofanya!.
 
Nadhani tatizo ni mchanganyiko wa mambo yote mliyoyaainisha humu (ujinga, ujuha, uwoga, ulimbukeni, umaskini, n.k.). Katika baadhi ya pande matatizo haya yawezekana kuwa yamekatisha watu matumanini lakini haina maana wamesalimu amri na kusema liwalo na liwe.

Je twafikiri twaweza kubadilisha kilicho mbele yetu? Absolutely! Nchi ni ya wananchi na ni sisi wananchi ambao ndio wenye neno la mwisho. Tunachohitaji ni kusema kwamba sasa imetosha, muda wa kuichukua nchi yetu umefika....waporaji bye nye! Sasa..kusema maneno tu peke yake haitoshi. Maneno hayo inabidi yafuatiwe na vitendo madhubuti. Kwa hiyo siyo kwamba hakuna mlango wa kutokea. Mlango upo, sababu tunayo, na kilichobaki ni kupata ujasiri wa kutafuta njia inayoeleka kwenye mlango huo. Tukishaipata hiyo njia ya kueleka huko kwenye lango kuu na kuziba mabonde yaliyopo na kutoa vizingiti na miamba inayoziba njia hiyo, hakika matumaini yatarejea kwani wenye macho wataona kuwa inawezekana.
 
Leo hii rasmi natangaza kuomba kadi ya Chadema!...
Mh. Freeman, Zitto, J.J.Mnyika, Mwanasisa naomba tuwasiliane!
Mkandara sina kuficha wala mpango wa kupitia mlango wa nyuma.Nataka kutiwa maji ya ubatizo..
Ila tu kumbukeni Mkandara nina sifa moja!.......BABU UBISHI!

Tupo pamoja 2010!
 
Back
Top Bottom