Je, Mungu wa Biblia ni Mwingi wa Rehema??
Wakristo mara zote husema kwamba Allah (SWT) si Mwingi wa Rehema kwa sababu huwaadhibu watu, na kwamba Mungu wa Biblia ndiye mwenye rehema.
Hebu tuchambue kwa mifano michache hapa chini ili tuone kama kweli ni Mwingi wa Rehema. Biblia inasema:
"Naye akawapiga watu wa Beth-shemesh, kwa sababu walikuwa wameitazama sanduku la Bwana; naam, akawapiga watu hamsini elfu na sabini. Watu wakahuzunika, kwa kuwa Bwana alikuwa amewaua watu wengi kwa pigo kuu." (1 Samweli 6:19)
Mwenyezi Mungu aliwaadhibu watu 50,070 kwa kosa la kutazama tu sanduku.
Kumbuka: Toleo jipya la Biblia kama NIV na mengine limepunguza kwa aibu idadi hii na kuifanya iwe watu 70 tu !!
"Usiwe na miungu mingine ila mimi.
Usijifanyie sanamu ya kuchonga, mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, au kilicho chini duniani, au kilicho majini chini ya dunia.
Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, nikiwaadhibu wana kwa sababu ya uovu wa baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao." (Kutoka 20:3-5)
Mungu si kwamba atawaadhibu tu wanaoshirikisha, bali atawaadhibu mpaka kizazi cha tatu na cha nne.
Kumbuka: Hapa Wakristo pia wanajumuishwa, kwa sababu wao husema Yesu NI Mungu na Roho Mtakatifu NI Mungu.
Biblia inasema:
"Na ikiwa hata baada ya hayo hamtaki kunisikiliza, ndipo nitakapowapiga mara saba zaidi kwa ajili ya dhambi zenu." (Walawi 26:18)
"Na ikiwa mtakwenda kinyume nami, wala hamtaki kunisikiliza, nitaleta juu yenu tauni mara saba zaidi kwa kadiri ya dhambi zenu." (Walawi 26:21)
"Na ikiwa kwa hayo hamtaki kurudi kwangu, bali mwende kinyume nami; basi, nami nitakwenda kinyume nanyi kwa ghadhabu, nami nitawaadhibu mara saba zaidi kwa ajili ya dhambi zenu." (Walawi 26:23-24)
Katika mistari hii tunaona kwamba Mungu haridhiki kwa adhabu ya kosa kwa kosa, bali atawaadhibu watu mara saba zaidi kwa ajili ya dhambi zao. Wakati huo huo Qur’an inasema:
"Yeye atendaye mema atapata malipo mara kumi ya mfano wake; na atendaye mabaya halipwi ila kwa mfano wake tu; wala hawatadhulumiwa." (Qur’an 6:160)
"Yeyote afanyaye mema, basi thawabu yake ni bora kuliko matendo yake; na afanyaye mabaya, basi watendao mabaya hawatalipwa ila kwa kadiri ya yale waliyoyafanya." (Qur’an 28:84)
Midomo, ulimi na pumzi ya Mungu
"Tazama, jina la Bwana linakuja kutoka mbali, na hasira yake iwakayo, na mzigo mzito; midomo yake imejaa ghadhabu, na ulimi wake ni moto uteketezao.
Pumzi yake ni kama mto unaofurika, unaofikia shingo, ili kuyapepeta mataifa katika pepeto la kuangamiza; na katikati ya taya za mataifa ataweka hatamu ya kupoteza njia." (Isaya 30:27-28)
Alhamdulillah (Sifa zote njema ni za Allah Peke Yake) — hii ndiyo sifa ya Mungu: kwamba huyazidisha mema na huadhibu madhambi tu kwa kiwango chake, ilhali Mungu wa Biblia huwaadhibu watu mara saba zaidi, na hata kuwafikia vizazi vya tatu na vya nne.