Muda umefika sasa kukagua vyeti vya waheshimiwa walioko bungeni ili kuhakiki elimu ya kila mmoja

saidoo25

JF-Expert Member
Jul 4, 2022
602
1,407
Wiki hii tumeshudia bungeni wabunge na mawaziri wakiringishiana viwango vya elimu wengine wakitamba na PHD zao kwamba ni za darasani sio za kupewa na wengine wakiambiwa hawana elimu ni waganga wa kienyeji.

Ni muhimu Spika wa Bunge kuruhusu uhakiki wa vyeti vya elimu kwa wabunge ili kujua ukweli wa elimu ambazo zimekuwa zikitajwa bungeni kama kinga ya kutisha wengine na watanzania wajue ukweli kuhusu wawakilishi wao.

Uhakiki huo ukague cheti cha Darasa la 7, Kidato cha 4, Kidato cha 6, Astashahada, Stashahada, Shahada, Shahada za uzamili, Shahada za Uzamivu nk.

Pia TCU ihakiki vyeti vya waliodaiwa kusoma nje ya nchi na kupata ukweli kuhusu elimu zao na uhalali wao.
 
Unajua Huo Mhimili Ndiyo Pekee Unaringa
Posho Mlima, Bima Ya Juu, Matibabu Nje, Hakuna Kulipa Kodi
Elimu Zao KK Mbili, Anachosema Ni Kinga Hakihojiwi
 
Mjue mbunge wa CCM alieishia chekechea😁😁😁
 
Wiki hii tumeshudia bungeni wabunge na mawaziri wakiringishiana viwango vya elimu wengine wakitamba na PHD zao kwamba ni za darasani sio za kupewa na wengine wakiambiwa hawana elimu ni waganga wa kienyeji.

Ni muhimu Spika wa Bunge kuruhusu uhakiki wa vyeti vya elimu kwa wabunge ili kujua ukweli wa elimu ambazo zimekuwa zikitajwa bungeni kama kinga ya kutisha wengine na watanzania wajue ukweli kuhusu wawakilishi wao.

Uhakiki huo ukague cheti cha Darasa la 7, Kidato cha 4, Kidato cha 6, Astashahada, Stashahada, Shahada, Shahada za uzamili, Shahada za Uzamivu nk.

Pia TCU ihakiki vyeti vya waliodaiwa kusoma nje ya nchi na kupata ukweli kuhusu elimu zao na uhalali wao.
Vyeti ndiyo vinaongea au mtu anajenga hoja? Kishimba ni la saba lakini hoja zake haziwezi kujibiwa na Makamba wala Bashe
 
Back
Top Bottom