SoC03 Elimu ya Kidato cha Tano na Sita ibadilishwe kuwa Elimu ya Vyuo vya kutoa ujuzi

Stories of Change - 2023 Competition

Colly 7

Member
Jul 27, 2022
88
442
Kwa muda mrefu nimekuwa najiuliza nini maana ya elimu wa kidato cha tano na sita (yaani "Advanced Level"), nilikuwa sipati majibu zaidi ya kwamba ni daraja la kujiunga na chuo kikuu (kama ufaulu ni mzuri), na kurudi kwenda kusomea Stashahada, sawa na wale walimaliza kidato cha nne (kama ufaulu ni wa kawaida au wa chini).

Pia nilikuwa ninajiuliza, ni kwa nini watu wanamaliza kidato cha sita hawana ujuzi katika fani yoyote? Nikagundua kwamba masomo yanayofundishwa katika ngazi hii ya juu ya elimu, ni yaleyale ya kidato cha kwanza hadi cha nne; lakini pia katika Elimu ya Msingi, tofauti ni kwamba masomo yanafundishwa kwa kina zaidi. Kama ilivyo kwa shule ya msingi, na kidato cha kwanza hadi cha nne, masomo haya yanafundishwa kwa nadharia zaidi kuliko kwa vitendo. Masomo yanayofundishwa katika ngazi hii ya elimu ni matatu kati ya haya hapa chini:

Jiografia; Kiswahili, Kiingereza, Hisabati, Fizikia, Kemia, Biolojia, Historia, Kilimo, Biashara, nk.
Mengine ni: Uraia....

Kwa nini napendekeza elimu ya kidato cha 5 na 6 kuwa elimu ya chuo?
Kwa mtizamo wangu, elimu katika ngazi hii, inachangia ongezeko la vijana wasio na kazi mitaani. Hii ni kwa sababu, kijana anapomaliza kidato cha sita, kama hakufaulu kujiunga na chuo, anaweza kukata tamaa na kujikuta kajiingiza katika makundi ya kiuhalifu; katika makundi ya uzururaji, na/au katika biashara ndogondogo zisizokuwa na tija, ukilinganisha na kiwango cha elimu yake.

Nikizungumzia zaidi wanafunzi waliosoma masomo ya sayansi na kumaliza kidato cha sita katika mchepuo wa sayansi, mfano: Fizikia, Kemia na Hisabati; Mtu aliyehitimu kidato cha sita katika masomo haya na kupata alama "A" masomo yote, hana uwezo wa kutengeneza hata sabuni ya maji au ya kipande.

Nimekuwa najiuliza, kama utengenezaji wa sabuni, ni kemia tupu, inakuwaje mtu amesoma hadi kidato cha sita, somo la kemia, pamoja na masoma mengine, anashindwa kuitengeneza? Badala yake, elimu kama hii inapatikana mitaani kutoka kwa watu wa kawaida na wenye elimu ya kawaida (hata elimu ya msingi) kwa muda usiozidi siku moja!

Ni ukweli usiopingika kwamba vijana wengi wanajiunga na vyuo vikuu, ni wahitimi wa kidato cha sita; na kwa muda mrefu nashuhudia vijana wengi wanamaliza vyuo vikuu, wakizunguka mitaani wakisaka ajira, huku baadhi yao (ambao naweza kuwaita ni majasiri) wakifanya biashara ndogondogo, maarufu kama umachinga. Sasa huwa najiuliza, hivi hili ndio lengo la kuhitimu chuo kikuu? Kwa upande mwingine, nimeshuhudia vijana wengi walihitimu vyuo vya kati wakiweza kujiajiri na hata kuajiriwa kuliko wale walihitimu kidato cha sita na chuo kikuu.

Niligundua kwamba baadhi ya waajiri hupendelea kuajiri vijana wenye astashahada na stashahada kuliko wale wenye vyeti vya kidato cha sita na shahada. Moja ya sababu ni kwamba wanaamini kwamba wana umahiri zaidi katika kazi na hawana matarajio makubwa sana.

Hizi ni miongoni mwa sababu zilizonifanya nione haja ya kubadili elimu hii, ili iwe na tija zaidi si tu kwa wahitimu, bali pia kwa maendeleo ya nchi. Maana hainiingi akilini kwamba serikali inatumia gharama nyingi (muda na fedha) kumwezesha kijana kuhitimu kidato cha sita na hata chuo kikuu, ili akauze dawa za mbu mitaani, au kuendesha Bodaboda! Ninaamini lengo la serikali la kusomesha watu wake hadi viwango vya elimu ya juu, ni kupata watu watakaofanya mambo makubwa katika sekta za kimkakati, mfano, kuwezesha taifa kufikia uchumi wa Buluu; uchumi wa viwanda, kilimo cha kisasa, uchumi wa gesi asilia, uchumi wa madini, uchumi wa utalii, uchumi wa sanaa, na kadhalika.

Mahitaji ya Sasa Yamebadilika
Miaka ya 1980 na kurudi nyuma, wahitimu wa ngazi zote, yaani, darasa la saba, kidato cha nne, kidato cha sita, vyuo vya kati na vyuo vikuu waliweza kuajiriwa na sekta za umma na za binafsi. Kipindi hicho sekta za umma ... kwa maana ya serikali, ilikuwa mwajiri mkubwa na wa kutegemewa. Baada ya kipindi hiki, uwezo wa serikali wa kuajiri ulianza kupungua kila mwaka, kufuatia viwanda na mashirika mengi kufa, kubinafsishwa au kupunguza uzalishaji.

Kutokana na hali hii, ajira za umma zilianza kupungua kwa kasi, na hivyo kusababisha wahitimu wa darasa la saba kuachwa kuajiriwa; hali ya ajira iliendelea kuwa mbaya, na hivyo baadaye wale wahitimu wa kidato cha nne nao wakawa hawapati ajira; na hatimaye wahitimu wa kidato cha sita nao hawaajiriki.

Kutokuajirika kwa makundi haya, haimaanishi kuwa elimu yao ni duni, la hasha, ni kwamba nafasi za ajira ni haba! Maana kipindi wanaajiriwa, walipatiwa mafunzo kazini, baadaye walipatiwa fursa za kwenda kujiendeleza katika vyuo mbalimbali.

Kwa kuwa serikali imebakiwa na ajira kidogo sana, na sekta binafsi katika nchi yetu bado ni changa sana, kuweza kuajiri vijana wengi kila mwaka, kuna haja ya kuangalia upya mfumo wetu wa elimu, ili umwandae kijana kuajirika au kujiajiri anapohitimu kiwango chochote cha elimu.

Na kwa kuzingatia makala yangu, nazungumzia zaidi elimu ya kidato cha tano na sita, kwamba imtoe kijana atakayeajirika, kujiajiri, na akipenda aendelee na elimu ya juu. Kwa maana hiyo, haitaitwa tena kidato cha tano na sita (maarufu kama "Advanced Level"), bali elimu ya chuo itakayompatia mhitimu stashahada katika fani mbalimbali.

Mapendekezo
1. Shule zote za "A Level" zibadilishwe na kuwa vyuo vya fani mbalimbali, vitakavyowezesha wahitimu kuajirika, kujiajiri na/au kujiunga na vyuo vikuu.
2. Waalimu wa shule hizi wapelekwe kuongeza nguvu kidato vya kwanza hadi cha nne katika shule mbalimbali, na wengine wajengewe uwezo waweze kufundisha baadhi ya kozi katika vyuo hivyo.
3. Kwa kuwa vyuo hivi vitakuwepo kila wilaya, viandaliwe na kuwa vya kimkakati; kama vipo maeneo ya uchimbaji wa madini, pamoja na nyingine, kuwe na kozi zinazohusiana na uchimbaji wa madini; kama ni maeneo ya kilimo, ufugaji, vyuo viwe na kozi za kilimo na ufugaji... nk.

Hitimisho
Elimu ya kidato cha tano na sita haimsaidii tena kijana kujikomboa kiuchumi, na haina tena tija kwa taifa, kumbe inaweza ikabadilika bila kuathiri miundombinu iliyopo, ikawa ya ujuzi zaidi, na hivyo kumuongezea mhitimu thamani zaidi.

Rejea
Benard Semen, swahilihub (August 9, 2022), Elimu ya Tanzania ni Butu?

"The Citizen (April 13, 2021), Why Tanzania Needs Vocational, Technical Skills"
 
Kwa muda mrefu nimekuwa najiuliza nini maana ya elimu wa kidato cha tano na sita (yaani "Advanced Level"); nilikuwa sipati majibu zaidi ya kwamba ni daraja la kujiunga na chuo kikuu (kama ufaulu ni mzuri), na kurudi kwenda kusomea stashahada, sawa na wale walimaliza kidato cha nne (kama ufaulu ni wa kawaida au wa chini).
Pia nilikuwa ninajiuliza, ni kwa nini watu wanamaliza kidato cha sita hawana ujuzi katika fani yoyote? Nikagundua kwamba masomo yanayofundishwa katika ngazi hii ya juu ya elimu, ni yaleyale ya kidato cha kwanza hadi cha nne; lakini pia katika Elimu ya Msingi, tofauti ni kwamba masomo yanafundishwa kwa kina zaidi. Kama ilivyo kwa shule ya msingi, na kidato cha kwanza hadi cha nne, masomo haya yanafundishwa kwa nadharia zaidi kuliko kwa vitendo. Masomo yanayofundishwa katika ngazi hii ya elimu ni matatu kati ya haya hapa chini:
Jiografia; Kiswahili, Kiingereza, Hisabati, Fizikia, Kemia, Biolojia, Historia, Kilimo, Biashara, nk.
Mengine ni: Uraia....

Kwa nini napendekeza elimu ya kidato cha 5 na 6 kuwa elimu ya chuo?
Kwa mtizamo wangu, elimu katika ngazi hii, inachangia ongezeko la vijana wasio na kazi mitaani. Hii ni kwa sababu, kijana anapomaliza kidato cha sita, kama hakufaulu kujiunga na chuo, anaweza kukata tamaa na kujikuta kajiingiza katika makundi ya kiuhalifu; katika makundi ya uzururaji, na/au katika biashara ndogondogo zisizokuwa na tija, ukilinganisha na kiwango cha elimu yake.
Nikizungumzia zaidi wanafunzi waliosoma masomo ya sayansi na kumaliza kidato cha sita katika mchepuo wa sayansi, mfano: Fizikia, Kemia na Hisabati; Mtu aliyehitimu kidato cha sita katika masomo haya na kupata alama "A" masomo yote, hana uwezo wa kutengeneza hata sabuni ya maji au ya kipande.
Nimekuwa najiuliza, kama utengenezaji wa sabuni, ni kemia tupu, inakuwaje mtu amesoma hadi kidato cha sita , somo la kemia, pamoja na masoma mengine, anashindwa kuitengeneza? Badala yake, elimu kama hii inapatikana mitaani kutoka kwa watu wa kawaida na wenye elimu ya kawaida (hata elimu ya msingi) kwa muda usiozidi siku moja!
Ni ukweli usiopingika kwamba vijana wengi wanajiunga na vyuo vikuu, ni wahitimi wa kidato cha sita; na kwa muda mrefu nashuhudia vijana wengi wanamaliza vyuo vikuu, wakizunguka mitaani wakisaka ajira, huku baadhi yao (ambao naweza kuwaita ni majasiri) wakifanya biashara ndogondogo,.. maarufu kama umachinga. Sasa huwa najiuliza, hivi hili ndio lengo la kuhitimu chuo kikuu? Kwa upande mwingine, nimeshuhudia vijana wengi walihitimu vyuo vya kati wakiweza kujiajiri na hata kuajiriwa kuliko wale walihitimu kidato cha sita na chuo kikuu.
Niligundua kwamba baadhi ya waajiri hupendelea kuajiri vijana wenye astashahada na stashahada kuliko wale wenye vyeti vya kidato cha sita na shahada. Moja ya sababu ni kwamba wanaamini kwamba wana umahiri zaidi katika kazi na hawana matarajio makubwa sana.
Hizi ni miongoni mwa sababu zilizonifanya nione haja ya kubadili elimu hii, ili iwe na tija zaidi sii tu kwa wahitimu, bali pia kwa maendeleo ya nchi. Maana hainiingi akilini kwamba serikali inatumia gharama nyingi (muda na fedha) kumwezesha kijana kuhitimu kidato cha sita na hata chuo kikuu, ili akauze dawa za mbu mitaani, au kuendesha Bodaboda!! Ninaamini lengo la serikali la kusomesha watu wake hadi viwango vya elimu ya juu, ni kupata watu watakaofanya mambo makubwa katika sekta za kimkakati, mfano, kuwezesha taifa kufikia uchumi wa Buluu; uchumi wa viwanda, kilimo cha kisasa, uchumi wa gesi asilia, uchumi wa madini, uchumi wa utalii, uchumi wa sanaa, na kadhalika.

Mahitaji ya Sasa Yamebadilika
Miaka ya 1980 na kurudi nyuma, wahitimu wa ngazi zote, yaani, darasa la saba, kidato cha nne, kidato cha sita, vyuo vya kati na vyuo vikuu waliweza kuajiriwa na sekta za umma na za binafsi. Kipindi hicho sekta za umma ... kwa maana ya serikali, ilikuwa mwajiri mkubwa na wa kutegemewa. Baada ya kipindi hiki, uwezo wa serikali wa kuajiri ulianza kupungua kila mwaka, kufuatia viwanda na mashirika mengi kufa, kubinafsishwa au kupunguza uzalishaji.
Kutokana na hali hii, ajira za umma zilianza kupungua kwa kasi, na hivyo kusababisha wahitimu wa darasa la saba kuachwa kuajiriwa; hali ya ajira iliendelea kuwa mbaya, na hivyo baadaye wale wahitimu wa kidato cha nne nao wakawa hawapati ajira; na hatimaye wahitimu wa kidato cha sita nao hawaajiriki.
Kutokuajirika kwa makundi haya, haimaanishi kuwa elimu yao ni duni, la hasha, ni kwamba nafasi za ajira ni haba! Maana Kipindi wanaajiriwa, walipatiwa mafunzo kazini, baadaye walipatiwa fursa za kwenda kujiendeleza katika vyuo mbalimbali.
Kwa kuwa serikali imebakiwa na ajira kidogo sana, na sekta binafsi katika nchi yetu bado ni changa sana, kuweza kuajiri vijana wengi kila mwaka, kuna haja ya kuangalia upya mfumo wetu wa elimu, ili umwandae kijana kuajirika au kujiajiri anapohitimu kiwango chochote cha elimu.
Na kwa kuzingatia makala yangu, nazungumzia zaidi elimu ya kidato cha tano na sita, kwamba imtoe kijana atakayeajirika, kujiajiri, na akipenda aendelee na elimu ya juu. Kwa maana hiyo, haitaitwa tena kidato cha tano na sita (maarufu kama "Advanced Level"), bali elimu ya chuo itakayompatia mhitimu stashahada katika fani mbalimbali.

Mapendekezo
1. Shule zote za "A Level" zibadilishwe na kuwa vyuo vya fani mbalimbali, vitakavyowezesha wahitimu kuajirika, kujiajiri na/au kujiunga na vyuo vikuu.
2. Waalimu wa shule hizi wapelekwe kuongeza nguvu kidato vya kwanza hadi cha nne katika shule mbalimbali, na wengine wajengewe uwezo waweze kufundisha baadh i ya kozi katika vyuo hivyo.
3. Kwa kuwa vyuo hivi vitakuwepo kila wilaya, viandaliwe na kuwa vya kimkakati; kama vipo maeneo ya uchimbaji wa madini, pamoja na nyingine, kuwe na kozi zinazohusiana na uchimbaji wa madini; kama ni maeneo ya kilimo, ufugaji, vyuo viwe na kozi za kilimo na ufugaji... nk.

Hitimisho
Elimu ya kidato cha tano na sita haimsaidii tena kijana kujikomboa kiuchumi, na haina tena tija kwa taifa, kumbe inaweza ikabadilika bila kuathiri miundombinu iliyopo, ikawa ya ujuzi zaidi, na hivyo kumuongezea mhitimu thamani zaidi.

Rejea
Benard Semen, swahilihub (August 9, 2022), Elimu ya Tanzania ni Butu?

"The Citizen (April 13, 2021), Why Tanzania Needs Vocational, Technical Skills"
Hii imeendaa
 
Kwa muda mrefu nimekuwa najiuliza nini maana ya elimu wa kidato cha tano na sita (yaani "Advanced Level"), nilikuwa sipati majibu zaidi ya kwamba ni daraja la kujiunga na chuo kikuu (kama ufaulu ni mzuri), na kurudi kwenda kusomea Stashahada, sawa na wale walimaliza kidato cha nne (kama ufaulu ni wa kawaida au wa chini).

Pia nilikuwa ninajiuliza, ni kwa nini watu wanamaliza kidato cha sita hawana ujuzi katika fani yoyote? Nikagundua kwamba masomo yanayofundishwa katika ngazi hii ya juu ya elimu, ni yaleyale ya kidato cha kwanza hadi cha nne; lakini pia katika Elimu ya Msingi, tofauti ni kwamba masomo yanafundishwa kwa kina zaidi. Kama ilivyo kwa shule ya msingi, na kidato cha kwanza hadi cha nne, masomo haya yanafundishwa kwa nadharia zaidi kuliko kwa vitendo. Masomo yanayofundishwa katika ngazi hii ya elimu ni matatu kati ya haya hapa chini:

Jiografia; Kiswahili, Kiingereza, Hisabati, Fizikia, Kemia, Biolojia, Historia, Kilimo, Biashara, nk.
Mengine ni: Uraia....

Kwa nini napendekeza elimu ya kidato cha 5 na 6 kuwa elimu ya chuo?
Kwa mtizamo wangu, elimu katika ngazi hii, inachangia ongezeko la vijana wasio na kazi mitaani. Hii ni kwa sababu, kijana anapomaliza kidato cha sita, kama hakufaulu kujiunga na chuo, anaweza kukata tamaa na kujikuta kajiingiza katika makundi ya kiuhalifu; katika makundi ya uzururaji, na/au katika biashara ndogondogo zisizokuwa na tija, ukilinganisha na kiwango cha elimu yake.

Nikizungumzia zaidi wanafunzi waliosoma masomo ya sayansi na kumaliza kidato cha sita katika mchepuo wa sayansi, mfano: Fizikia, Kemia na Hisabati; Mtu aliyehitimu kidato cha sita katika masomo haya na kupata alama "A" masomo yote, hana uwezo wa kutengeneza hata sabuni ya maji au ya kipande.

Nimekuwa najiuliza, kama utengenezaji wa sabuni, ni kemia tupu, inakuwaje mtu amesoma hadi kidato cha sita, somo la kemia, pamoja na masoma mengine, anashindwa kuitengeneza? Badala yake, elimu kama hii inapatikana mitaani kutoka kwa watu wa kawaida na wenye elimu ya kawaida (hata elimu ya msingi) kwa muda usiozidi siku moja!

Ni ukweli usiopingika kwamba vijana wengi wanajiunga na vyuo vikuu, ni wahitimi wa kidato cha sita; na kwa muda mrefu nashuhudia vijana wengi wanamaliza vyuo vikuu, wakizunguka mitaani wakisaka ajira, huku baadhi yao (ambao naweza kuwaita ni majasiri) wakifanya biashara ndogondogo, maarufu kama umachinga. Sasa huwa najiuliza, hivi hili ndio lengo la kuhitimu chuo kikuu? Kwa upande mwingine, nimeshuhudia vijana wengi walihitimu vyuo vya kati wakiweza kujiajiri na hata kuajiriwa kuliko wale walihitimu kidato cha sita na chuo kikuu.

Niligundua kwamba baadhi ya waajiri hupendelea kuajiri vijana wenye astashahada na stashahada kuliko wale wenye vyeti vya kidato cha sita na shahada. Moja ya sababu ni kwamba wanaamini kwamba wana umahiri zaidi katika kazi na hawana matarajio makubwa sana.

Hizi ni miongoni mwa sababu zilizonifanya nione haja ya kubadili elimu hii, ili iwe na tija zaidi si tu kwa wahitimu, bali pia kwa maendeleo ya nchi. Maana hainiingi akilini kwamba serikali inatumia gharama nyingi (muda na fedha) kumwezesha kijana kuhitimu kidato cha sita na hata chuo kikuu, ili akauze dawa za mbu mitaani, au kuendesha Bodaboda! Ninaamini lengo la serikali la kusomesha watu wake hadi viwango vya elimu ya juu, ni kupata watu watakaofanya mambo makubwa katika sekta za kimkakati, mfano, kuwezesha taifa kufikia uchumi wa Buluu; uchumi wa viwanda, kilimo cha kisasa, uchumi wa gesi asilia, uchumi wa madini, uchumi wa utalii, uchumi wa sanaa, na kadhalika.

Mahitaji ya Sasa Yamebadilika
Miaka ya 1980 na kurudi nyuma, wahitimu wa ngazi zote, yaani, darasa la saba, kidato cha nne, kidato cha sita, vyuo vya kati na vyuo vikuu waliweza kuajiriwa na sekta za umma na za binafsi. Kipindi hicho sekta za umma ... kwa maana ya serikali, ilikuwa mwajiri mkubwa na wa kutegemewa. Baada ya kipindi hiki, uwezo wa serikali wa kuajiri ulianza kupungua kila mwaka, kufuatia viwanda na mashirika mengi kufa, kubinafsishwa au kupunguza uzalishaji.

Kutokana na hali hii, ajira za umma zilianza kupungua kwa kasi, na hivyo kusababisha wahitimu wa darasa la saba kuachwa kuajiriwa; hali ya ajira iliendelea kuwa mbaya, na hivyo baadaye wale wahitimu wa kidato cha nne nao wakawa hawapati ajira; na hatimaye wahitimu wa kidato cha sita nao hawaajiriki.

Kutokuajirika kwa makundi haya, haimaanishi kuwa elimu yao ni duni, la hasha, ni kwamba nafasi za ajira ni haba! Maana kipindi wanaajiriwa, walipatiwa mafunzo kazini, baadaye walipatiwa fursa za kwenda kujiendeleza katika vyuo mbalimbali.

Kwa kuwa serikali imebakiwa na ajira kidogo sana, na sekta binafsi katika nchi yetu bado ni changa sana, kuweza kuajiri vijana wengi kila mwaka, kuna haja ya kuangalia upya mfumo wetu wa elimu, ili umwandae kijana kuajirika au kujiajiri anapohitimu kiwango chochote cha elimu.

Na kwa kuzingatia makala yangu, nazungumzia zaidi elimu ya kidato cha tano na sita, kwamba imtoe kijana atakayeajirika, kujiajiri, na akipenda aendelee na elimu ya juu. Kwa maana hiyo, haitaitwa tena kidato cha tano na sita (maarufu kama "Advanced Level"), bali elimu ya chuo itakayompatia mhitimu stashahada katika fani mbalimbali.

Mapendekezo
1. Shule zote za "A Level" zibadilishwe na kuwa vyuo vya fani mbalimbali, vitakavyowezesha wahitimu kuajirika, kujiajiri na/au kujiunga na vyuo vikuu.
2. Waalimu wa shule hizi wapelekwe kuongeza nguvu kidato vya kwanza hadi cha nne katika shule mbalimbali, na wengine wajengewe uwezo waweze kufundisha baadhi ya kozi katika vyuo hivyo.
3. Kwa kuwa vyuo hivi vitakuwepo kila wilaya, viandaliwe na kuwa vya kimkakati; kama vipo maeneo ya uchimbaji wa madini, pamoja na nyingine, kuwe na kozi zinazohusiana na uchimbaji wa madini; kama ni maeneo ya kilimo, ufugaji, vyuo viwe na kozi za kilimo na ufugaji... nk.

Hitimisho
Elimu ya kidato cha tano na sita haimsaidii tena kijana kujikomboa kiuchumi, na haina tena tija kwa taifa, kumbe inaweza ikabadilika bila kuathiri miundombinu iliyopo, ikawa ya ujuzi zaidi, na hivyo kumuongezea mhitimu thamani zaidi.

Rejea
Benard Semen, swahilihub (August 9, 2022), Elimu ya Tanzania ni Butu?

"The Citizen (April 13, 2021), Why Tanzania Needs Vocational, Technical Skills"
Naunga mkono hoja
 
Nyerere muona mbali alikuwa ameyaona haya miaka karibu hamsini kabla hayajatufikia. Aliweka Elimu ya Kujitegemea, Shule zote zikawa na Michepuo ya kufundisha stadi mbalimbali, ufundi, kilimo biashara na kadhalia. Walipokuja vipofu wakadai Nyerere alikuwa amekosea wakafuta kila alichoweka. leo ndiyo hivyo elimu yetu imekuwa ni kichekesho. Walisahau kuwa professionally Nyerere alikuwa Mwalimu na alikuwa anajua sana umuhimu wa elimu katika jamii, ndiyo maana akawa ametangaza kuwa adui mmojawapo ni ujinga. Aitaka kufuta kabisa ujinga nchini hadi anaondoka literacy rate yetu ilikuwa karibu 90% lakini leo hata mtoto anamaliza form 4 hawezi kuandika wala kujenga hoja. Vivyo hivyo kuna form 6 wanamaliza na Div 1 lakini hawawezi kujenga hoja. Iwapo huwezi kujenga hoja, hutaweza hata kuanzisha kitu cha maana labda kwa kudra za Mungu tu.

Maoni yako ni kuonyesha kutoelewa maana ya elimu, na unadhani kuwa elimu maana yale ni stadi. Kuna stream mbili za elimu; academic stream na trade stream. Wakati wa Nyerere trade stream ilikuwa na vyuoa kama Technical Colleges (ambazo zilikuwa zinafundisha trades katika ngazi ya FTC na diploma), Veta maarufu ikijulikana wakati huo kama Chang'ombe ambayo ilikuwa inafundisha Trade Test Grade 3, Grade 2, na Grade 1 na Technical Foreman. Vyuo vya Kilimo Uyole, na vinginevyo vingi.

Baada ya kubadilisha technical colleges zote kuwa academic colleges za kutoa digrii; wacha tule ya chuya sasa.
 
Na tutakula chuya sana kama serikali haitofunguka kifikra.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom