Muasisi awashukia 'wabaya' wa CHADEMA

Muasisi awashukia 'wabaya' wa CHADEMA

Status
Not open for further replies.
hayyattullah usimlinganishe na Fisadi mtei,Kiongozi wa juu wa Iran ni Mwadilifu kuliko unavyofikiria,lkn viongozi wa chadema ni Mafisadi wanaotumia rasilimali kujiimarisha na kujineemesha wao na familia zao. Ndio mana hakuna anaestahili kutawala chadema zaidi ya mkwe wa Mzee Mtei, ukithubutu tu utaitwa umetumwa na hivyo wewe utakiwa msaliti. Chadema hawapaswi kuaminiwa hata nusu dakika maana wakishika nchi,activity ya kwanza ni kubadili katiba na kuondoa kikomo cha kutawala ktk urais,Slaa na Mbowe watatumia vyombo vya dola kubaki madarakani na Watanzania tutajuta na naamini yatatokea machafuko.
Mbowe na Slaa watatumia hii propaganda kung`ang`ania madaraka. Na kila atakae jaribu kutaka urais ataambiwa katumwa na Kagame au wamagharibi.
Mabadiliko ni lazima,mbowe must step down.

Wewe unaonekana ni mtabiri mzuri sana!
Je ulitabiri kuwa CCM haitatimiza ahadi zake kabla ya uchaguzi wa mwaka 2010?
Je,ulitabiri kuwa CCM itayafanya maisha ya watz magumu kwa kusababisha mfumuko hatari wa bei?Je,ulitabiri kuwa viongozi wa CCM kujihusisha na mambo haramu kama ujangili,ugaidi,ufisadi,uuzaji wa madawa ya kulevya,utesaji,unyang'anyi wa ardhi na wengine ubakaji wa watoto wadogo bila kuchukuliwa hatua?Je,ulitabiri kuwa CCM ikichukua madaraka itatengwa zaidi na nchi nyingine za jumuiya ya afrika mashariki?
Je ulitabiri kuwa viongozi wa CCM watapandisha kodi mbalimbali kumbana mwananchi badala ya kumpunguzia mzigo wa kodi anaolipa?

Kama sivyo,basi wewe unanufaika na mfumo huo,ambao CHADEMA ikiingia madarakani na kuuvunja utaathirika.

Simply wewe ni MCHUMIA TUMBO kama wenzio wengi waliopo CCM!

Shime watanzania,tuiondoe CCM ili tupate maendeleo ya kweli ktk nchi yetu!
 
Awali nikiri kuwa kipindi watu walipokuwa wakisema kuwa CDM ni chama cha ukanda particularly Northern TZ, jambo hilo halikuniingia kabisa akilini kwangu. Ila baada ya kufanya kazi na watu kadhaa wa ukanda huo (Northern TZ) na nikunganisha na haya yanayowatokea ZZK na Dr. Kitila sasa naanza kupata mwanga kuwa chama hiki waasisi wake walitarget kiwe ni kwa masilahi ya watu wa Northern TZ. Hii inaweza kuwa justified na sura ya uongozi wa CDM katika ngazi ya juu 1) Mbowe 2) Slaa 3) Anthony Komu 4) John Mrema. 5)...................Ni dhahiri uwepo wa ZZK katika nafasi ya Naibu katibu Mkuu ilikuwa haiwafurahishi hata kidogo hawa Northern TZ people. Yaani hawa watu hawana tofauti hata kidogo na Wakikuyu wa Kenya kwa mnaowajua Wakikuyu. Sasa njia pekee ya kuleta demokrasia ya kweli ktk hiki chama ni kupambana kwanza kuundoa hizi elements za Kinorthorn TZ. Mapambano haya ni ya muhimu kuliko hata kupigania kuchukua dola hapo 2015 Coz hata kama hiki chama kitafanikiwa kuchukua Dola 2015 definitely 75% ya viongozi wake watatoka ukanda huo kwa sababu watu hawa hawana aibu wala haya yanapokuja maslahi yao binafsi. Kwa kuusoma waraka wa Dr. Kitila na wenzake nimekuwa convinced lengo halikuwa baya kwa sababu mkakati huu pamoja na kutaka kumwondoa mwenyekiti amabaye kutokana na upeo wake na elimu ndogo hawezi kuleta changamoto zinazotakiwa kupambana na CCM tunapokaribia uchaguzi mkuu 2015. Lakini pia mkalati huo ulilenga kukipa chama hiki sura zaidi ya kitaifa kuliko kilivyo sasa. Mm nimesifu uamuzi wa ZZK aliposema hatahama Chadema...Mimi nafikiri it is a right decision at the right time. Bila kupigania kukipa chama hiki sura ya kitaifa itakuwa ni kazi ngumu kupamabana na CCM lazima tupiganie CDM kufanya uchaguzi huru na wala hatutaki Mtei atuchagulie kiongozi aache demokrasia iamue. Nawasilisha.
 
Mkuu THE BIG SHOW,

Sisi Wananchi wenzio wenye kujitambua na wenye macho yenye kuona,na wenye masikio yenye kusikia na wenye mioyo yenye shauku ya kuitaka na kuitafuta kweli...tumekufahamu na kukuelewa kwa undani mno.

Najua hapo umetumia ustaarabu na uungwana mwingi dhidi ya Chama chako ukipendacho,lakini kisichokupenda wala kukuthamini aka Chadema...ndo maana nakhis umeamua kumung'unya maneno,lakini mangi hayatoki,au ndo umeamua "kuwahifadhi"/kuwastiri wenzio!? Teh! Teh!

Mkuu,waambie "ukweli mchungu" hao jamaa zako...sasa ukiendelea kuwafichaficha hivi mtafikia vipi malengo ya chama chenu ili kiwe cha kitaifa na kuweza kukubalika nchini koote na kwa watu wenye imani/itikadi tafauti na huyo "Muasisi" aka Nabii wa Tengeru atakavyo!?

Huyo mpuuzi Mtei...unafiki,uzandiki,ufisadi na usaliti wake kwa Taifa letu hilo tunaujua kwa undani mno tangia early 1960's...labda ataendelea kuwandangaya hao misukule wake tu.

Nafikiri Mkuu Zemarcoplo,tayari anafanza shughuli njema ya kumnyambua na kutoa Ilm ya bure kuhusu huyo Nabii wa Tengeru;ili misukule wachache wanaoendela kudangayika na wasiojua historia na insights za Nchi hiyo waweze angalau kujielewa japo kiduchu!?...badala ya kushashadidia majambo bila ya maono khalisia/reality/...sidhani kama pia labda wana japo kiduchu ya historical evidences,facts guidance, and/or support!?...poor misukule! Teh! Teh!

Edwin Mtei has always known for his weird combination of wanting power and to be liked,while at the same time lacking moral integrity,transparency,responsibility and shared vision!...basically,he's a total disaster!

Hiyo level yabayana yako,amma kwa hakika ni wa hali ya juu mno kwa hao misukule wa Chadema kuweza fumbua hilo fumbolo!?

Labda waje tu na yale matusi na kashfa zao tulozoea kama wanavyotukana wale kondoo wa Bwana....Nyakageni na Nara! Teh! Teh!

Tuko pamoja Mkuu!

Ahsanta.

Cc;CHAMVIGA,Boko Haram,Kahtaan,Mzito Kabwela,Ritz

Alhabib gombesugu amani kwako ndugu yangu. Unajua sisi tunalipenda sana taifa letu kiasi kwamba saa nyingine tunatumia hata tafsida kufikisha ujumbe hasa kwenye mas'ala haya ya udini lakini inafika hatua tunashindwa hata kuvumilia na hapo sasa tukiusema ukweli ndio utasikia nyie wabaguzi, wadini n.k ila tunawavumilia sana. Zito yanampata yenye kumsibu only coz ni muislamu, si mchaga wala mkaskazini. Lakini wenzetu wao wanaendelea kuleta propaganda za kipuuzi zinazopelekea hasira kwetu. The big show kafikisha kiustarabu sana na namshukuru ila wajue kuna kuchoka.
 
With all of my due respect,baada ya salamu mimi sipo hapa kufanya propaganda wala kumchafua mtu yoyote,

Sijataumwa na yoyote,na nasimama kwa msimamo wangu binafsi katika kuelezea kile kilichopo fikran mwangu,

Kama Mtanzania mzalendo,mchukia mafisadi na muumin wa siasa bora na uongoz imara lazima nisimame kuelezea kitu nachokiona,

Hatuna shida na Mzee Mtei kama miongoni mwa waasisi wa chama hiki,na hatuna shida na wenngine wowote wale ambao kwa namna moja ama nyinine wamekuwa ni wanafamilia wa mwasisi huyo wa chama hiki,

Sisi kama Watanzania linapokuja suala la kuathirika kwa utawala m'bovu huwa tunapata athari hizo sote bila kujali umri,jinisia,kabila,kanda,dini na kadhalika,so as long as wewe na mimi tumekuwa ni wananchi na raia wataifa hili tunaathiriwa moja kwa moja kwa mamuzi ya wanasiasa either wawe wa chama tawala au chama cha upinzani,

Ni jukumu letu sisi wananchi kuhakikisha tunakuwa mabalozi wa siasa safi ili serikali itayokuwa madarakani iwe ni imara itayotuhakikishia maamuz sahihi na usalama wa taifa dhidi ya maadui wa ndan na nje ya nchi,

Ili tufikie hali kama hiyo tunahitaji chama ambacho hakiwez kuegemea kwenye maamuz ya kutoka upande mmoja ambao unajinasibisha kuwa na MORAL AUTHORITY YA KUTOA KAULI ZINAZOHIATJI KUSIKIKA KWA KUWA TUH ETI UPANDE HUO NDIO HASA ULIOPELEKEA KUASISIWA KWA CHAMA HIKO,HILI LAZIMA TULIWEKE WAZI MAPEMA SANA.


Katiba ya chadema hakuna kipengele hata kimoja kinachosema kwamba watu wapewe kipaombele kutokana na ukanda,udini na ukabila hata sehemu moja,yani kwa ufupi katiba ya chadema inapinga kwa nguvu zote mambo ya ukanda,ukabila na udini katika kulijenga taifa hili kwa kizazi cha sasa na cha baadae,hilo liko wazi na sote tunaunga mkono katiba ya namna hiyo...

Katika mukatadha huo basi yatupasa kuwaambia chadema wasimame katika misingi hiyo na kuionesha wazi wazi kwa vitedno na kila mtu aone na sio kuishia kuhubiri mambo hayo majukwaani huku upande wa pili ukionekana kuwa na malalamiko yasiyo kwisha,REJEA YA MAREHEMU CHACHA WANGWE NA HAYA MASAHIBU YANAYO WAKUTA KITILA MKUMBO,MWIGAMBA NA ZITTO KABWE KAMA MIFANO HURU KATIKA MJADALA HUU,


Chadema lazima itambue kwamba watanzania walio wengi pamoja na kuchoshwa na CCM wanahitaji m'badala thabiti na unaoijipambanua wazi wazi kiutawala,kikatiba na kitaifa.

Hoja ya AYATOLLAH ALKHAMENEI,YULE SUPRME LEADER WA IRAN NA JINSI WANAVYOENDESHA DEMOKRASIA YAO NAIFANANISHA MAJA KWA MOJA NA CHADEMA,NASEMA HIVYO KWA SABABU,

1.AYATOLLAH ALKHEMENEI.,yeye yupo juu,rais,mwnyekiti wa chama,bunge na mahakama vyote vinaripoti kwake,

Chama na bunge hawawez kupitisha jina la mgombea urais wa nchi ile bila baraka wala idhin ya YATOLLAH ALKHEMENEI KWA KUOGOPA KUWEKWA KWA MAMLUKI AU VIBARAKA WA MAREKANI KWENYE UTAWALA WA SERIKALI YA IRAN HASA KWENYE KIPINDI KAMA HIKI AMBACHO WANAPAAMBANA NA SIASA KALI ZA ISRAEL NA MAREKANI,HUSUSANI SUALA ZIMA LA NYUKLIA NA UONGOZ KWA UJUMLA,,Utakuja kuona kwamba MAHMOUD AHMEDNIJAD RASI ALIEMALIZA UTAWLA WAKE ALIKUWA MTIIFU KWA SYSTEM YA AYATOLLAH,WATU WAKADHANI KWAMBA KUJA KWA HASSAN ROUHANI RASI WA SASA WA IRAN BASI HATOKUWA MTIIFU KWA MFUMO ULE,HALI HAIKUWA HIVYO KWANI ROUHANI ALIPOINIA ALIONEKAN KUWA MODERATE TOFAUTI NA NIJADI LAKIN WOTE NI WALE WALE,WOTE WANAPOKEA AMRI KUTOKA KWA SUPREME LEADER KWA KILA HATUA..


Utaratibu ule ni mzuri kwa wairan na unawafaa kuogopa kuingizwa kwa mamluki wa kimarekani ndan yataifa lile,


Sasa nauliza swali,je utaratibu huo unafaa??na je unaweza kusaidia taifa kwa ujumla??mimi naona utaratibu huo kwa chadema kama chama una wafaa,tatizo ni kwamba je wakipewa madaraka ya nchi utaratibu huu utakuwa healthy kwa manufaa ya nchi??

Kwa maana mimi sion TOFAUTI BAINA YA MZEE MTEI NA JINS ANAVOKIENDESHA CHADEMA NA AYATOLLAH ALKHEMEI NA JINS ANAVOIENDESHA IRAN KAMA NCHI,SEMA TOFAUTI NI KWAMBA AYATOLLAH ANA SAUTI KITAIFA HUKU MZEE MTEI ANA SAUTI KICHAMA.

TUSEME WAZI NA KUMWAMBIA MZEE MTEI KWAMBA CHAMA HIKI KAMA KWELI ANATAKA KIPEWE IMAN NA WANANCHI,AKIACHIE KWA WANANCHI MOJA KWA MOJA,NA AONDOE FIKRA ZA U-YATOLLAH ALKHEMENEI,ATALIGAWA NA KULIGHARIM TAIFA.

#TEAM ZITTO...

Hapa Hakuna Cha kujadili, tutajadili vipi Utumbo kama huu...
Kila kitu kiko Clear Kabisa.
MM amevuliwa Nyadhifa zote ndani ya Chama na amepewa 14 Days ajieleze ni kwanini asivuliwe uanacahama Full Stop.
Hizi Ngonjera zenu hazitamsaidia kitu zaid ya kumungamiza kabisa.'
Two Things, Mshaurini aombe radhi kwa undumilakuwili wake aendelee na Ubunge wake kama Shibuda ama la awe Mbunge wa Mahakama.


Importantly, Mwenzake Kafulila alilia na kutoa Machozi Mbele ya Mbatia
 
Awali nikiri kuwa kipindi watu walipokuwa wakisema kuwa CDM ni chama cha ukanda particularly Northern TZ, jambo hilo halikuniingia kabisa akilini kwangu. Ila baada ya kufanya kazi na watu kadhaa wa ukanda huo (Northern TZ) na nikunganisha na haya yanayowatokea ZZK na Dr. Kitila sasa naanza kupata mwanga kuwa chama hiki waasisi wake walitarget kiwe ni kwa masilahi ya watu wa Northern TZ. Hii inaweza kuwa justified na sura ya uongozi wa CDM katika ngazi ya juu 1) Mbowe 2) Slaa 3) Anthony Komu 4) John Mrema. 5)...................Ni dhahiri uwepo wa ZZK katika nafasi ya Naibu katibu Mkuu ilikuwa haiwafurahishi hata kidogo hawa Northern TZ people. Yaani hawa watu hawana tofauti hata kidogo na Wakikuyu wa Kenya kwa mnaowajua Wakikuyu. Sasa njia pekee ya kuleta demokrasia ya kweli ktk hiki chama ni kupambana kwanza kuundoa hizi elements za Kinorthorn TZ. Mapambano haya ni ya muhimu kuliko hata kupigania kuchukua dola hapo 2015 Coz hata kama hiki chama kitafanikiwa kuchukua Dola 2015 definitely 75% ya viongozi wake watatoka ukanda huo kwa sababu watu hawa hawana aibu wala haya yanapokuja maslahi yao binafsi. Kwa kuusoma waraka wa Dr. Kitila na wenzake nimekuwa convinced lengo halikuwa baya kwa sababu mkakati huu pamoja na kutaka kumwondoa mwenyekiti amabaye kutokana na upeo wake na elimu ndogo hawezi kuleta changamoto zinazotakiwa kupambana na CCM tunapokaribia uchaguzi mkuu 2015. Lakini pia mkalati huo ulilenga kukipa chama hiki sura zaidi ya kitaifa kuliko kilivyo sasa. Mm nimesifu uamuzi wa ZZK aliposema hatahama Chadema...Mimi nafikiri it is a right decision at the right time. Bila kupigania kukipa chama hiki sura ya kitaifa itakuwa ni kazi ngumu kupamabana na CCM lazima tupiganie CDM kufanya uchaguzi huru na wala hatutaki Mtei atuchagulie kiongozi aache demokrasia iamue. Nawasilisha.

Ubarikiwe sana mkuu.
 
Hata CCM alikuwepo Nyerere na ndiye aliyetuchagulia Mkapa 1995 lakini wanaCCM walimchagua Kikwete
 
Lakini mbivu na Mbichi zitaonekana tu....ndiyo process yenyewe hiyo katika kuelekea mabadiliko yoyote...Time Will Tell
 
Shukran sana Mkuu,

Ni kweli haya yote yamenza kufumuka baada ya hili seke seke la zito na bado yataendelea kufunguka mengine mengi sana,

Zitto ni kama mwendelezo tuh,tunajua wapo waliojaribu hapo mwanzo kuuchallange mfumo kama marehem chacha wangwe lakini mwsho wa siku mungu hakupenda aendelee kubakia ulimwenguni akamchukua,

Mtei haishii tuh kuambiwa akae mbali na chama,mtei kama muasisi alimsimika mtu kama mbowe awe mwenyekiti wa chama ambae kifamilia ni mkwe wake,kwahiyo utaona jins graph inavyokwenda,

Kama hiyo haitoshi.wanapotokea watu kutangaza nia ya kutaka kumvaa huyo mwenyekiti yeye huwa kikwazo na huwa mbele mbele kuwakatisha tamaa watu hao kwa sababu mbali mbali ambazo hazina msingi jambo ambalo hutafsiriwa kama ni muendlezo wa UYATOLLAH NDAN YA CHAMA HIKI

Pamoja sana Kamanda.
Kamanda ukisema mzee Mtei alimsimika Mbowe kuwa mwenyekiti kwa sababu za kifamilia sijui upo sahihi kwa kiwango gani.
Nijualo mimi ni kuwa Mbowe alikuwa Mwenyekiti wa Vijana wa Chama kingali bado kichanga, alianza kufanya kazi ndogo ndogo kabla ya hapo.
Kwa mtu aliyeanza kuwa mwanachama wa kawaida, badae nafsi ndogo badae kuwa Mwenyekiti wa Vijana wa Chama, sidhani kama hawezi kuwa na sifa za kuwa Mwenyekiti wa Chama. Sitashangaa baada ya miaka kadhaa kumwona John Heche kuwa Mwenyekiti wa Chama.

CHADEMA wamepigiwa mdundo ambao hata baadhi ya wanachama wake waucheza, na wasipokuwa makini unaweza ukawaathiri kwa kua hawafahamu aliyeupiga alikuwa na nia gani. Suala la Ukanda na Ukabila linasemwa na hata baadhi ya Wachadema na kama viongozi nao wameshaanza kuusikiza huo mdundo kuna hatari wataacha watu wenye sifa na uwezo mzuri kwa sababu ya kuogopwa kuitwa WADINI,WAKANDA n.k. Kuna hatari siku moja wakawa na viongozi wasio na uwezo kwa sababu tu wanaogopwa kuitwa WABAGUZI. Chama kikifikia hapo basi naiona hatari yake mbele.

Tuepuke propaganda za udini,ukabila na ukanda.
 
Tutaliona anguko rasmi la CCM kabla ya uchaguzi mkuu wa 2015. Ndani ya CCM kulishakuwa na uchaguzi wa kidemokrasia tangia lini!! mwenyekiti wa sasa aligombea na nani??? kwa taarifa alipata ushindi usiozidi 58% lakini wakatangaza 99%!!! hiyo ndio demokrasia.

Subiri uone, CDM imeshazika fitina mbele kwa mbele sasa! M4c kuanza kwa nguvu zoooote. Huyo mnaempigania eti alianza CDM akiwa na umri mdogo kwa hiyo business as usual hana nguvu tena.

Mambo ya kitoto wakati watu wako serious ameshindwa tayari!
 
Maalim Gomgesugu

Asalaam aleykum,

Wallahi nimekusoma kwa dhati ya kina mno...!!

Mimi tena sifai humu ndani,,kwani sasa naitwa gaidi,mdini na mjahidina kisa naongea ukweli na ninaonekana nina iman ya kiislam kwa baadhi ya wanacjadema,japo sio wote nimeonekana kama ni INTRUDER NA SINA QUALIFICATION YA KUJIFANYA CHADEMA WALA KUZUNGMZA MAMBO YA CHADEMA,

LAKIN WALLAHI NAFANZA HIVI KWA MASLAHI YA TAIFA LETU SOTE,

SHUKRAN,NAOMBA USIBANDUKE HAPA TUWE PAMOJA KWENYE HUU MNAKASHA




Mkuu THE BIG SHOW,

Nimekusoma ndugu yangu!

Japo sina ujuzi/ufahamu wa mangi katika hiyo local politics...lakini nimejaribu kujinoa/update kiduchu,khasa tangia nimejiunga humu-JF!...kwa hili nisipoishukuru JF,basi nitakuwa mwizi wa fadhila kama Chadema! Teh! Teh!

Nimefuatilia majambo mangi kiduchu humu-JF...lakini lazim nikiri yakuwa nimehuzunishwa mno na kashfa,shutuma zisizo mantik urembeazwo kila mara,na pia kuangaliwa kwa jicho la udini, khasa kila pale utoapo hoja au ukweli ambao ni kinyume tu ati na Wana-Chadema wenzio!?

...yaani wao hawajali hata kama maoni/hoja zako ni kwa faida ya hiyo Chadema yenyewe au Taifa!?...almurad,imekua wewe unaishi ndani ya suspicious wakti woote ndani ya hicho Chama chenu!? Dah!

Lakini nimebaini pia,yawezekana yakuwa Wanataaluma wengi mno wenye stahiki zao hapo nyumbani,hawajishughulishi asilan na huu upuuzi wa malumbano/"majadiliano" ya kisiasa...nafikiri kwa mintaaraf nyingi walizonazo!? Nami najaribu pia kuwafahamu kwalo!

Wengine wenye Ilm njema na uungwana kama wewe Mkuu,ni dhiki na taabu nyingi kukubalika kiundani kwenye hiyo Chadema...sababu hiyo ni miradi tu ya wapigaji/matapeli fulani kuzidi kujitengenezea ubilionea kwa kufuja jasho la Wananchi nyuma ya pazia ati la "uzalendo"! Teh! Teh!

Kundi jingine lenye uelewa wa majambo makubwa na Wanataalauma wenye hishma/stahiki zao...nakhis hawa wengi wao wapo nje ya nchi,na kutokana na shughuli na majambo kadhaaa,inakuwa hizo local politics ni kama past time zao tu!?

Nimesoma post fulani asubuhi hii ya jamaa anaitwa nafikiri Mkandara,huyu anaelekea ni Mwanachadema mwenzio na alitujuza yakuwa yupo pale Canada nafikiri!?...alitoa uchambuzi mzuri mno,kuhusu hiyo hali ya sasa ndani ya Chadema na mgogoro wa hao akina Zitto Kabwe-MP!?

Matokeo yake...posts kadhaa zilofuata,wakaja wale misukule kadhaa ya Chadema na ati kuanza kumpinga tena kipuuzi tu bila ya hoja makini,na wengine kujaribu kumkashifu!? Dah!

Hiyo ndo Bongo/Afrika! Duh!

Tuko pamoja kwa saana tu Mkuu!

Ahsanta.
 
Kwahiyo Mkuu THE BIG SHOW cdm hakutakuwa na DEMOKRAISIA hd ZITO awe kiongozi KWELI? wanasema kupenda ni UPOFU unataka kunambia Yote anayotuhumiwa ZITO hayana ukweli hata 1! Ndg elewa jambo1 Ili m2 akuzushie lazima kutakuwa na kaUKWELI flan so kwenye hili! Naomba km kushauri tushauri kwa lengo lakujenga sio kuPAYUKA2! mara 2najiingiza kwenye mambo cjui ya DINI hv tangu hawa jamaa watuletee hz DINI zimetusaidia nini?
 
Ndugu mleta hoja, hii ni moja ya hoja zinazonipa kushangaa jinsi baadhi ya wenzetu mnavyo-react kwa mambo ya msingi na kusema haraka-haraka maneno makubwa bila kufikiri vya kutosha na kufanya uchambuzi wa jambo husika kwa makini. Hivi alichosema Mtei ni kipi cha kutosha kumlinganisha na Ayatollah ambaye neno lake ni la mwisho na linachukuliwa kama neno la Mungu? Hivi mzee Mtei kwa nafasi yake hastahili kuwa mshauri wa chama? Na kama akiona uongozi wa chama umefanya maamuzi akatoa mawazo yake kuunga mkono hilo linawezaje kutosha kumfananisha na Ayatollah? Na je, kama Mtei angekuwa amewaponda uongozi wa Chama katika hili bado mleta hoja ungemfananisha na Ayatollah, au kwa kuwa alilolisema hukulipenda unafikia conclusion hiyo?

Ni vyema tuelewe na tujenge utamaduni wa kuyapa maamuzi ya chama muda na tafakuri ya kina ili mambo yajiweke bayana machoni petu sawasawa badala ya kuropoka hovyo kwa misingi ya hisia tu. Chama kimetoa tamko la sababu ya kuwaadhibu baadhi ya viongozi wake, nao wamejieleza waliyo nayo mioyoni. Wenye busara wanajipa nafasi watafakari, wachekeche waone kulikoni kabla hawasema hili au lile. Hoja hii inaonekana wazi kuwa mwenzetu umefanya pre-mature judgement au nawe ni miongoni mwa wale walioathiriwa na propaganda zinazoenezwa kuhujumu cdm.

Tusisahau swala la Zito na uongozi halikuanza hapa. Tulitafakari taratibu kwa historia yake. Pia tukumbuke kuwa cdm kama chama kinahitaji watu wa aina zote, vijana kwa wazee. Tusidhani tutaweza kufika kama tutapuuza hazina za wazee kwa kisingizio cha haraka haraka tu kwamba eti ni saccoss ya mtu. Kwani ni chama kipi ambacho hakianzishwa na mtu?
 
Iran utaratibu ule unawasaidia kama nchi kuepuka kuingiza nchi kwenye umamluki wa marekani,ndio kwa maana ayatollah amepewa nafasi na sauti ya kusema,

Pia CHADEMA UTARATIBU HUU UNAWASAIDIA SANA,KWA MZEE MTEI KUWA NA USHAWISH NA NGUVU NDAN YA CHAMA SIO MBYA,INAWASAIDIA KUEPUKA CHAMA HIKO KUINGIZA MAMLUKI WA MAFISADI WA CCM,

JE,TUKIJAALIA HII NCHI WAKAICHUKUA CHADEMA,HATUONI KAMA TUTAKUWA TUMEWEKA REHANI KUWA MAAMUZI YATAKUWA YANATOKEA UPANDE FLANI,NA SIO MAAMUZ YA KITAIFA??

MZEE MTEI AKAE KANDO KABISA NA SIASA ZA CHADEMA ILI WATANZANIA WAKIPE IMAN YA UHAKIKA CHAMA HIKO

Mkuu Le Big Show naamini una maslahi ya dhati na CHADEMA kufuatana na michango yako mingi ingawa ningependa kuona unajiweka mbali na watu wenye ajenda zao ambazo ni dhahiri za kutaka CHADEMA ife kabisa. Kawaida yao ni kuingiza vibwagizo vya udini, ukabila na ukanda kila wakati na nawaona wakikuunga mkono sana katika uzi huu.

Kama mwenyewe ulivyogusia, hatari ya hujuma kwa chama ni ukweli ambao upo siku zote. Mamluki wanaweza kupandikizwa au hata waliomo wenye dhamana ndani ya chama wakatumiwa kuua chama. Mifano ya yaliyotokea NCCR na CUF bado ipo dhahiri sana. Watu walioaminiwa walitumika kuhujumu vyama hivyo kikamilifu kwa manufaa ya chama tawala. Na tukisema chama tawala si chama kama vyama vingine. Chenyewe kimehodhi na kinatumia vyombo na nyenzo za dola (zisizomithilika) ama kutia hofu (hata kuua) au kununua kikwazo chochote kwa bei muafaka.

Hadi sasa CHADEMA kimeshafanyiwa hujuma nyingi sana lakini kimefanikiwa kudumu zaidi ya watangulizi wake na bado kinaonekana kuwa chama tishio. Imefikia mahali watendaji wa CCM wameanza kuendesha kampeni kama za chama cha upinzani ili kushindana na CHADEMA. Sikia akina Kinana na Nape wakitangaza katika mikutano ya hadhara (badala ya kuwasiliana na mwenyekiti) ubovu wa baadhi ya mawaziri na kutaka waondolewe katika nafasi hizo.

Kuhusu Zitto hata mimi nadhani huenda suala lake halijashughulikiwa vyema. Kama tatizo ni kugombea uenyekiti au nafasi yoyote ndani ya chama basi ningependa kuona akipewa nafasi na kupitia mchakato uliopo ili utata wa kuminywa kwa demokrasia uondolewe. Naamini wakati ukifika CHADEMA hawatakuwa na budi kuruhusu hilo lifanyike; si kwa Zitto tu bali kwa yeyote anayestahili ndani ya chama.

Lakini kuna mashaka kwamba Mh. Zitto kwa nyendo zake amekuwa na ukaribu na baadhi ya viongozi wa CCM na vyombo vya dola ambao wanatuhumiwa kuendesha hujuma dhidi ya CHADEMA. Katika mazingira hayo, wewe kwa upande wako huna shaka kabisa na uwezekano wa Zitto kutumika kuhujumu chama? Kumbuka wanaotaka kuhujumu chama walio makini hawaji na mwonekano wa kishetani (mkia, mapembe, n.k.); mara nyingi wanatumia hoja thabiti kama za kuruhusu/kuimarisha demokrasia huku wakijua demokrasia kiuhalisia inaweza kuchezewa kwa fedha au hata ghilba za hisia za kibinadamu.

Pili, unaamini kweli au una ushahidi kwamba Mzee Mtei (singly) ana kauli kubwa au hata ya mwisho katika maamuzi ya Chama na kwamba CHADEMA leo hii kinaongozwa "kifamilia"? Kwa sababu kwa mtazamo wa aina hii sidhani kama mtu utakuwa na haja ya kujinasibisha na chama cha aina hiyo.
 
Na uislamu wako hauwezi kukamilika kama huitambui Injili. Injili haimbwi bali kuna miziki ya injili.

Mkuu Mtoi,

Ile safari yetu ya kula matunda Lushoto lini?

Kuna jamaa wamezusha eti wewe ndio M2. Watu wabaya sana hawa...
 
Lakini still Huyo Mzee Mtei ana nafasi yake kimawazo Chadema nani kakwambia kwamba ndiyo anatoa amri? Mbona Nyerere alisema kabisa kwamba watu kama Lowassa na Malecela hawafai nchi hii na ndiyo inasemekana yeye ndiyo aliyempendekeza Mkapa sasa unaweza kusema bado alikuwa ana command CCM?



Kamanda,

Nakusih
i embu jaribu kusoma tena hiyo bayana aloleta Bwana mleta mada, Mkuu THE BIG SHOW!?

Sasa mbona hiyo argument yako ni dhaifu mno!?...hivi unafuatilia hii migogoro,kuchafuana na malumbano ya nyinyi Chadema kwa undani!?

Au unataka tu kuanzisha "premiere league" za "malumbano ya kitoto" hapa jamvini!?...yaani wewe na akili yako timamu unashindwa kufahamu massive influence and powerful position aliyonayo huyo Nabii wa Tengeru ndani ya Chadema mpaka kesho,na jinsi anavyoitumia kizembe/kifisadi bila ya kujali democratic values and/or principals!?

...Kwa kifupi,wanachokitaka Wananchi ni Chama ambacho kitakua tafauti kabisa na hao CCM!?...kitu ambacho kwa hali halisi ya siasa hapo nchini kwa hivi sasa,ni ndoto za mchana kweupe!

Sasa wewe unajaribu kutuonyesha yakuwa,ati nyinyi Chadema/Mtei mnafanza upuuzi na upumbavu woote huo kwa sababu tu Nyerere nae alifanza kama hivyo kwa niaba ya CCM!?...sasa hapo tafauti yenu na hao mnaojaribu kutuaminisha yakuwa ati ni "wabaya" na "hawafai" kukaa madarakani ni ipi!?

Ahsanta.
 
Kwahiyo Mkuu THE BIG SHOW cdm hakutakuwa na DEMOKRAISIA hd ZITO awe kiongozi KWELI? wanasema kupenda ni UPOFU unataka kunambia Yote anayotuhumiwa ZITO hayana ukweli hata 1! Ndg elewa jambo1 Ili m2 akuzushie lazima kutakuwa na kaUKWELI flan so kwenye hili! Naomba km kushauri tushauri kwa lengo lakujenga sio kuPAYUKA2! mara 2najiingiza kwenye mambo cjui ya DINI hv tangu hawa jamaa watuletee hz DINI zimetusaidia nini?



Wewe unaleta tu insinuations na speculations...ni wapi THE BIG SHOW ametujuza yakuwa Chadema itakua haina Demokrasia ati mpaka Zitto Kabwe ndo awe Kiongozi!?

Khalaf wewe ndo "msomi" wa wapi vile!? Duh!...yaani unadai,"mtu akikuzushia jambo tu,baso ndo linakua la kweli"!? Teh! Teh!

Kwanini inakulazim ku-mention hayo mambo ya udini na kumuhusisha nayo Mkuu THE BIG SHOW!?...embu tuonyeshe ni wapi huyo mleta mada kaleta mambo ya "udini" hapa jamvini!?

Your post is the dumbest,most ignorant thing I've seen this morning! Duh!

Basically,your argument is logically invalid on so many bloody levels!

Try to re-read the whole Topic carefully and with understanding,it may help,ok!?

Ahsanta.
 
Mtei na KHOMEIN wanatofauti kama Mwinuko na Mlima.KHOMEIN analinda Taifa lake,Mtei anatetea Wizi katika lichama lake


Mkuu,

Taratibu na hizi kauli zako za ukweli!

Si unajua jamaa hawataki kusikia ukweli asilan!...yaani wanatembea na vitofali siku hizi! Teh! Teh!

Mwenzio Mwigamba anajua "khabar" hiyo! Dah!

Ahsanta.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom