With all of my due respect,baada ya salamu mimi sipo hapa kufanya propaganda wala kumchafua mtu yoyote,
Sijataumwa na yoyote,na nasimama kwa msimamo wangu binafsi katika kuelezea kile kilichopo fikran mwangu,
Kama Mtanzania mzalendo,mchukia mafisadi na muumin wa siasa bora na uongoz imara lazima nisimame kuelezea kitu nachokiona,
Hatuna shida na Mzee Mtei kama miongoni mwa waasisi wa chama hiki,na hatuna shida na wenngine wowote wale ambao kwa namna moja ama nyinine wamekuwa ni wanafamilia wa mwasisi huyo wa chama hiki,
Sisi kama Watanzania linapokuja suala la kuathirika kwa utawala m'bovu huwa tunapata athari hizo sote bila kujali umri,jinisia,kabila,kanda,dini na kadhalika,so as long as wewe na mimi tumekuwa ni wananchi na raia wataifa hili tunaathiriwa moja kwa moja kwa mamuzi ya wanasiasa either wawe wa chama tawala au chama cha upinzani,
Ni jukumu letu sisi wananchi kuhakikisha tunakuwa mabalozi wa siasa safi ili serikali itayokuwa madarakani iwe ni imara itayotuhakikishia maamuz sahihi na usalama wa taifa dhidi ya maadui wa ndan na nje ya nchi,
Ili tufikie hali kama hiyo tunahitaji chama ambacho hakiwez kuegemea kwenye maamuz ya kutoka upande mmoja ambao unajinasibisha kuwa na MORAL AUTHORITY YA KUTOA KAULI ZINAZOHIATJI KUSIKIKA KWA KUWA TUH ETI UPANDE HUO NDIO HASA ULIOPELEKEA KUASISIWA KWA CHAMA HIKO,HILI LAZIMA TULIWEKE WAZI MAPEMA SANA.
Katiba ya chadema hakuna kipengele hata kimoja kinachosema kwamba watu wapewe kipaombele kutokana na ukanda,udini na ukabila hata sehemu moja,yani kwa ufupi katiba ya chadema inapinga kwa nguvu zote mambo ya ukanda,ukabila na udini katika kulijenga taifa hili kwa kizazi cha sasa na cha baadae,hilo liko wazi na sote tunaunga mkono katiba ya namna hiyo...
Katika mukatadha huo basi yatupasa kuwaambia chadema wasimame katika misingi hiyo na kuionesha wazi wazi kwa vitedno na kila mtu aone na sio kuishia kuhubiri mambo hayo majukwaani huku upande wa pili ukionekana kuwa na malalamiko yasiyo kwisha,REJEA YA MAREHEMU CHACHA WANGWE NA HAYA MASAHIBU YANAYO WAKUTA KITILA MKUMBO,MWIGAMBA NA ZITTO KABWE KAMA MIFANO HURU KATIKA MJADALA HUU,
Chadema lazima itambue kwamba watanzania walio wengi pamoja na kuchoshwa na CCM wanahitaji m'badala thabiti na unaoijipambanua wazi wazi kiutawala,kikatiba na kitaifa.
Hoja ya AYATOLLAH ALKHAMENEI,YULE SUPRME LEADER WA IRAN NA JINSI WANAVYOENDESHA DEMOKRASIA YAO NAIFANANISHA MAJA KWA MOJA NA CHADEMA,NASEMA HIVYO KWA SABABU,
1.AYATOLLAH ALKHEMENEI.,yeye yupo juu,rais,mwnyekiti wa chama,bunge na mahakama vyote vinaripoti kwake,
Chama na bunge hawawez kupitisha jina la mgombea urais wa nchi ile bila baraka wala idhin ya YATOLLAH ALKHEMENEI KWA KUOGOPA KUWEKWA KWA MAMLUKI AU VIBARAKA WA MAREKANI KWENYE UTAWALA WA SERIKALI YA IRAN HASA KWENYE KIPINDI KAMA HIKI AMBACHO WANAPAAMBANA NA SIASA KALI ZA ISRAEL NA MAREKANI,HUSUSANI SUALA ZIMA LA NYUKLIA NA UONGOZ KWA UJUMLA,,Utakuja kuona kwamba MAHMOUD AHMEDNIJAD RASI ALIEMALIZA UTAWLA WAKE ALIKUWA MTIIFU KWA SYSTEM YA AYATOLLAH,WATU WAKADHANI KWAMBA KUJA KWA HASSAN ROUHANI RASI WA SASA WA IRAN BASI HATOKUWA MTIIFU KWA MFUMO ULE,HALI HAIKUWA HIVYO KWANI ROUHANI ALIPOINIA ALIONEKAN KUWA MODERATE TOFAUTI NA NIJADI LAKIN WOTE NI WALE WALE,WOTE WANAPOKEA AMRI KUTOKA KWA SUPREME LEADER KWA KILA HATUA..
Utaratibu ule ni mzuri kwa wairan na unawafaa kuogopa kuingizwa kwa mamluki wa kimarekani ndan yataifa lile,
Sasa nauliza swali,je utaratibu huo unafaa??na je unaweza kusaidia taifa kwa ujumla??mimi naona utaratibu huo kwa chadema kama chama una wafaa,tatizo ni kwamba je wakipewa madaraka ya nchi utaratibu huu utakuwa healthy kwa manufaa ya nchi??
Kwa maana mimi sion TOFAUTI BAINA YA MZEE MTEI NA JINS ANAVOKIENDESHA CHADEMA NA AYATOLLAH ALKHEMEI NA JINS ANAVOIENDESHA IRAN KAMA NCHI,SEMA TOFAUTI NI KWAMBA AYATOLLAH ANA SAUTI KITAIFA HUKU MZEE MTEI ANA SAUTI KICHAMA.
TUSEME WAZI NA KUMWAMBIA MZEE MTEI KWAMBA CHAMA HIKI KAMA KWELI ANATAKA KIPEWE IMAN NA WANANCHI,AKIACHIE KWA WANANCHI MOJA KWA MOJA,NA AONDOE FIKRA ZA U-YATOLLAH ALKHEMENEI,ATALIGAWA NA KULIGHARIM TAIFA.
#TEAM ZITTO...