Mtwara: Simbachawene azuiwa njiani!

Mtwara: Simbachawene azuiwa njiani!

Safi sana, ingekuwa Mbeya, Mwanza ama Arusha wangesema wapinzani wanachochea vurugu. Sijui huko Mtwara watasema nani anachochea, labda aende First Lady na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wakawatulize.
 
inaonekana safari ya c c m kuhamia upinzani imeanza wenye nchi wameanza kuona mwanga
 
Sokoine, Wewe yaelekea hujui ulisemalo,serikali imewatelekeza vipi na kuliko mkoa upi na kwa vigezo gani! Toa data baada research sio kulishwa maneno na CDM na unakomaa na kutolea macho vitu bila data! weka facts zako hapa!
Vipi wewe Mbona Unahara kabla ya KUJAM-BA,! Niweke facts za nini wakati ukweli wote unaujua.au umesahau kwamba miaka yote Wezi,na Mafisadi wote,wa Mali za Umma mmekua mkiwahamishia mikoa ya kusini kikazi pale wanapokosea badala ya kuwapeleka MAGEREZA! Hii inaonyesha kua Mateso yanayokuepo Mikoa ya kusini ni zaidi ya Magereza.kule kuna Bandari nzuri na yenye Kina Kirefu ambayo Meli kubwa zinaweza kutia Nanga.si hivyo tu,bado Bandari hiyo ingeweza kuhudumia Mikoa ya kusini,pamoja na nchi Jirani kama Malawi,Zambia,Congo nk.lakini kwa ufinyu wa akili ya viongozi wa Ccm na Serikali yake,mmekazania tu kila kitu Dar.Mshindwe na Mlegee!
 
Last edited by a moderator:
Hii habari ina ukweli??? mboma nyie ni rahisi kuamini iwapo habari inaipomda ccm. lakini ambayo imaisema cdm inakiwa ya uchafu. hypocrits
 
GWEN, hayo ndio madai yao ya msingi kama unakumbuka mabango yao siku ya maandamano! "GESI NI YA WAMAKOND" GESI HAITOKI MTWARA" n.k, vinginevyo wawe wameamua sasa iende Dar au wamefanyia amendment madai yao mkuu!
Madai ya gesi kubaki Mtwara kwanza ni madai yanayoungwa mkono na watanganyika wengi sana, na mimi ni mmoja wao.
Wakazi wengi sana wa Dar hawataki gesi asafirishwe kuja Dar wanataka gesi ichimbwe na ianze kurutubishwa hapo hapo Mtwara.

''Wakazi wa Mtwara wana madai ya msingi sana ni lazima wasikilizwe na waheshimiwe''
By Watanganyika, 2013.
 
Last edited by a moderator:
Kuchemachema chumni, kuchikachika chilingi, mchumali chuiii chilingi tano!! Haaaah
 
Hongereni wana ntwala,kila anayejaribu kutia pua yake na kuleta unafiki mleteeni kirambasi ya kutosha atoke baru!!!!nyambafff kabisa wamewafanya mtaji kwa miaka mingi sana.....
 
Nasisi wanzibar hyo gesi tunaitaka la sivyo tunavnja muungano.
 
Kwani mwenye matusi Kama Leyland Albion hajafika Mtwara na kusema CDM wanaongoza maandamano!!
 
BLACKTIGER, kwani sasa hivi umekufa! si nenda mtwara sasa na wewe ili pakachimbike! au kwani dhahabu zimekwisha geita? mbona hujaenda utuletee picha za maandamano na updates! peleka ubaguzi wako huko Moshi!

Inaonekana unapenda sana ukabila,kila mtu akikupinga mawazo yako unadhani katokea kaskazini.Mkuu acha uvivu wa kufikiri.
Rasillimali hizi ni za watanzania wote ila wanamtwara wanahitaji fursa au kipaumbela cha kwanza kujua au kutathimi ni kwanamna gani watanufaika na rasilimali zinazopatikana kwenye ardhi yao.
acha kuleta porojo nyiiingi kuwagawa watanzania na u CCM wako.
 
Nimewapenda wanamtwara sana kwa kujua haki zao! Nawaombea wa mikoa mingine wanakofukuzwa kwenye makazi yao kisa dhahabu imegundulika nao waamke wajue haki zao. Nawasema watu wa Shinyanga Tabora Mwanza Simiyu Geita nk. Wa kukusaidia ni wewe mwenyewe!!
 
Ranks, we usidanganye wenzako wakati we umekaa katika laptop tu! nyie Cdm mmeona m4c yenu imefeli ndo mnatumia karata ya wanamtwara! msisafirie nyota ya wenzenu mnawaponza wakina mama watoto na vikongwe kwa vurugu zenu!
Kwa hiyo wewe kwa uelewa wako hao vikongwe,kinamama,watoto,walemavu na wengineo wote wame-relxy mambo poooowa!!!It doesn't mean CHADEMA IKIFA LEO(kwa ujinga wenu mnavyoamin)MABADILIKO HAYATATOKEA.PABADILIKO YA KIMFUMO NA UTAWALA NI LAZIMA.
 
Last edited by a moderator:
Na Baraka Mfunguo,

Kilichotokea tarehe 13/1/2013 uwanja wa mashujaa ni funzo kwa wanasiasa wote wanaochukulia suala la gesi kama ajenda yao ya kisiasa. Majira ya saa 9:00 alasiri, nikiwa sina hili wala lile nashtuliwa na jirani yangu kwamba kuna mkutano wa hadhara juu ya suala lile lile la gesi. Maana kwa siku za hivi karibuni suala la gesi limekuwa gumzo huwezi kuwapita watu watano bila kusikia suala la gesi, naam mgeni rasmi ni James Mbatia mwenyekiti wa chama cha NCCR -Mageuzi.

Kabla ya Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi kuzungumza, ulifuata utangulizi wa baadhi ya wanasiasa kuzungumza akiwamo Mh Moses Machali Mbunge pamoja na viongozi wengine waandamizi walioambatana na mwenyekiti huyo. Kisha ukafuatia wakati wa Ndugu Mbatia kuzungumza, kimsingi Mbatia alikuwa na hoja ya msingi isipokuwa hakuweza kung'amua kwamba wananchi hawakutaka kusikiliza historia ama maneno ya siasa isipokuwa wao wanataka azimio moja gesi isitoke Mtwara.

Kilichofuata hapo sidhani kama atakuja kusahau katika maisha yake, blogu hii inampa pole kwani hii ndio changamoto ya kisiasa. Suala lingine wananchi walimchukulia Ndg Mbatia kama kibaraka wa CCM haswa baada ya kupata ubunge wa kuteuliwa na Rais, na hapo wananchi wakawa wanahoji uhalali wa yeye kuweza kuwa mtetezi wao.

Fundisho ni moja tu kwa wanasiasa, wawaeleze wananchi ukweli kama sepetu iite sepetu na sio kijiko kikubwa kama wanavyotaka kuwahadaa wananchi. Suala lingine ni suala la elimu lakini nadhani pia hilo ni "too late" wamechelewa mno. Kinachotaka kufanyika ni kama kutumia neno elimu kisiasa kama mbinu ya kuwalainisha wananchi ili waweze kuruhusu gesi yao itolewe Mtwara.

Taarifa zisizokuwa rasmi zinaeleza kwamba tayari makachero wa vikosi mbali mbali wapo mkoani Mtwara kwa ajili ya kufanya tathmini na namna ya kuweza kukabiliana na machafuko yoyote ambayo yanajitokeza. Ikiwamo uvunjifu wa amani unaohatarisha usalama wa taifa.

Suala hapa ni moja tu wanansiasa waelewe wananchi wanataka nini, wawatimizie wananchi, waelewe changamoto za wananchi wao na pia washirikiane na wananchi wao kuzitatua changamoto zao. Wanasiasa wakishapata madaraka yao inakuwa kana kwamba wameshajipandisha daraja na kujiweka juu ya wananchi na wao kuwa kila kitu kwa kupata stahiki za maisha bora huku wananchi wakiteseka na wao kutia pamba masikioni. Sasa suala ni moja "GESI HAITOKI MTWARA" iwe funzo kwao na wanasiasa wote ambao wanatumika kama vibaraka na wapokea rushwa kupitia wawekezaji wakubwa ambao wanawatumia kwa ajili ya kuweza kupata influence ya uwekezaji huku wao wakiwa wanafaidika kwa muda mfupi na wananchi wakichafuliwa mazingira na athari za muda mrefu pamoja na umaskini. Hao ndio akina chifu Mangungo tulionao leo hii.

 
Wanatakiwa kumpa kichapo cha mbwa mwizi huyo.

Ya ikiwezekana wamchomoe hata jicho!!
Anajifanya ana akili sana yule alimwambia Tundu Lissu eti hamuwezi kuchukua nchi kirahisi!! Sasa aangalie ngome yao ilivyosambaratishwa!!
 
Atabadilika tu na kuwa yangachawene au nyanichawene!
 
MBUNGE wa Mtwara Mjini (CCM), Hasnain Murji na Mwenyekiti wa CCM Manispaa ya Mikindani, Ali Chinkawene wamepinga kauli ya Rais Jakaya Kikwete kwamba wakazi wa Mkoa wa Mtwara hawapaswi kuzuia gesi kwenda Dar es Salaam.

Viongozi hao walisisitiza kwa nyakati tofauti kwamba, wataendelea kuunga mkono jitihada za wananchi kupinga usafirishwaji wake kwa kuwa hiyo ni haki yao.

Murji alisema yupo tayari kuvuliwa ubunge kwa kutetea masilahi ya Wanamtwara wanaopinga gesi hiyo inayovunwa katika Kijiji cha Msimbati, mkoani Mtwara huku Chinkawene akisema msimamo wa chama chake ni kuungana na wananchi kupinga gesi kupelekwa Dar es Salaam.

Alisema Serikali inapaswa kujenga mitambo ya kuzalisha umeme mkoani Mtwara badala ya Dar es Salaam...

"Tulipoona hali inakuwa tete, niliitisha kikao cha Kamati ya Siasa kujadili nini msimamo wa chama katika hili. Kamati ya Siasa wakasema hawawezi kukisemea chama kwa sababu chama ni wanachama, hivyo nikaitisha kikao cha Halmashauri Kuu ambapo pia tuliwaalika mabalozi wa mitaa."

"Katika kikao hicho, wajumbe walipinga kwa nguvu zote suala la gesi kupelekwa Dar es Salaam. Wakaniambia niseme msimamo wao kuwa hawataki gesi iende Dar es Salaam hadi pale masilahi ya Wanamtwara yatakapowekwa wazi na Serikali."

Mwenyekiti huyo alisema kwa maana hiyo, msimamo huo si wake binafsi, bali ni maazimio ya vikao halali vya chama hicho vinavyowakilisha wanachama na kwamba historia ya Mikoa ya Kusini jinsi ilivyonyimwa maendeleo ilitumiwa na wajumbe kujenga hoja hiyo.

"Wakati sisi hatuna umeme hakuna aliyefirikia kutuunganisha kwenye gridi ya Taifa… Barabara ya kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam miaka 51 ya Uhuru sasa, haijakamilika. Lakini bomba wanataka kujenga kwa miezi 18. Hivi kuna Watanzania muhimu zaidi ya wengine?" alihoji Chinkawene akinukuu kauli za wajumbe wa kikao hicho na kuongeza:

"Walizungumza mambo mengi, suala la kung'olewa kwa reli, kukatazwa kulima pamba, kuuawa kwa kilimo cha karanga na mkonge. Haya yote wanadai yamesababisha mkoa uendelee kuwa maskini na kwamba tumaini lao limebaki kwenye gesi. Wamesema wapo pamoja na wananchi."
 
Tatizo viongozi wetu hawafikiriani, wanajifikiria wao wenyewe. Kama tungekuwa tunafikiriana sisi waafrika tungekuwa mbali kuliko hata ulaya.Waafrika hatupendani,tupendaneni kama tunavyojipenda sisi wenyewe tutakuwa mbali kimaendeleo.wewe kama unamaende msaidie na yeye ajiendeleze. Hilo ndilo tatizo la viongozi wengi wanataka kujiendeleza wao wenyewe kiuchumi.kama serikali tokea mwanzo ingejenga vitega uchumi kila mkoa,kila wilaya kutokana na rasilimali zao kusingekuwa na matatizo hayo leo hii.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom