Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 4,956
- 4,330
Nami naunga mkono maandamano haya kwa sababu:
1. badala ya kusafirisha gesi kwa zaidi ya KM 550 toka mtwara hadi dar kwa zaidi ya dola 1.2 bilioni na kuja kujenga kituo cha kuzalisha umeme wa 3900MW ni bora hizi pesa zingetumika kuweka hii mitambo ya Gesi palepale mtwara kwa sababu ni karibu na pia kwa kutumia pesa hiyo hiyo tumaweza jenga mitambo ya gesi kuzalisha UMEME mara 2 zaidi ya hiyo gharama ya kujenga pipepline hadi Dar.
2. Kama umeme wote unaoingia katika gridi ya Taifa wote unakuwa controlled DAR sioni umuhimu wa ulazima kusafirisha gesi hadi dar then kuzalisha huo umeme....maana unaweza zalishwa palepale mtwara na unaingwizwa katika gridi ya taifa na kama nilivyosema wote unakuwa monitored from DAR
Kwa kweli huwa sijui kama mipango yetu ya Kitaifa hasa ya maendeleo kama hufanywa na watalaamu. Kama ndivyo basi hatuna watalamu kitu ambacho siamini. Kwa mtu wa akili ya kawaida tu siye mtaalamu wa uchumi wala wa nishati hawezi kutotambua yafuatayo kuhusu gesi au mafuta yaliyogunguliwa huko kusini mwa Tanzania:
1. Tunataka yazalishe umeme ili tupate unafuu wa bei ya umeme. Umeme huo unaweza kuzalishwa huko huko kusini na kuingizwa kwenye grid ya Taifa huko huko kusini. Kwani mbona huko Mtera, Tanga n.k. wanazalisha umeme huko huko na kuingizwa kwenye grid ya Taifa? Sasa sijui sisi ni majuha au vipi, tunataka umeme huo tukauzalishie Dar kwa kuisafirisha hiyo gesi gafi kwenye bomba lenye kipenyo cha urefu wa mtu (over 1.5 m) na urefu wa over 550 km la gharama ya over TShs 3 trions! Mitambo iliyopo pale Ubungo ya Symbions, PTL, Songas n.k. bei yake kila moja haizidi TShs 150 billion. At most yote kwa pamoja haizidi TShs 1 trion. Tungeweza hata kui dismantle na kuisafirisha na kuifunga huko Mtwara kwa gharama ndogo zaidi. Au tungeweza kununua mitambo mingine mipya mingi kuliko iliyopo Ubungo na kuifunga huko Mtwara kwa chini ya bei ya hilo bomba, na kuweza kuzalisha umeme kwa gharama ndogo. Viwanda vya Dar vinaweza kuendelea kupata gesi kwa kutumia meli toka Mtwara ambazo gharama zake ni nafuu kuliko bomba au lori. Wastage kwenye bomba ni mkumbwa sana, kwanza lazima lijae (over 1 trion cubic metre) excess ndiyo itafika Dar. Njiani cho chote kinaweza kutokea kwenye hilo bomba na inaweza ikawa disaster tupu.
2. Matumizi mengine ya hiyo gesi ni majumbani, kupikia hivyo kuokoa mazingira kwa kupunguza kukata miti kwa ajili ya mkaa au kuni hasa kule vijijini. Kuna sababu gani gesi hiyo isijazwe kwenye hiyo mitungi au containers za gas za Oryx n.k. huko huko Mtwara na kusafirishwa kwa meli au malori hadi huko Dar na kwingineko ambako inahitajika?
3.Kwa hiyo hata mafuta ya petroli yatakapoanzwa kuchimbwa huko kusini yatabidi yasafirishwe gafi kwenye bomba hadi Dar kwa refinary badala ya hizo refineries kujengwa Mtwara?
4. Mhhhh, ndiyo maana tunashindwa kufunga mitambo ya kufua umeme unaosemekana wa zaidi Megawatts 5,000 huko kwenye mafuriko ya Steinghlet kwa sababu tunashindwa kuyahamishia hayo mafuriko Dar? Vivyo hivyo kwa makaa ya mawe na hata uranium zingekuwa Dar mambo yangekuwa poa! Jamani Tanzania si Dar peke yake na wawekezaji waambiwe hivyo, wapo watakaoelewa tu. Wasiolewa waachane na sisi, yote ni kwa faida yetu sote kwani gharama zitakuwa nafuu kwa wote wala si Mtwara peke yao. Vinginevyo wananchi watashindwa kuwaelewa kwa maamuzi kama haya yasiyokuwa na logic. Watafikiri kuna mlungura umetembea! Si vizuri, muwaelimishe.
Big up Mtwara corridor, keep up and we all stand to benefit.