Mtwara kumekucha; Maandano ya kupinga kusafirisha gesi yaja

Status
Not open for further replies.
Nami naunga mkono maandamano haya kwa sababu:
1. badala ya kusafirisha gesi kwa zaidi ya KM 550 toka mtwara hadi dar kwa zaidi ya dola 1.2 bilioni na kuja kujenga kituo cha kuzalisha umeme wa 3900MW ni bora hizi pesa zingetumika kuweka hii mitambo ya Gesi palepale mtwara kwa sababu ni karibu na pia kwa kutumia pesa hiyo hiyo tumaweza jenga mitambo ya gesi kuzalisha UMEME mara 2 zaidi ya hiyo gharama ya kujenga pipepline hadi Dar.
2. Kama umeme wote unaoingia katika gridi ya Taifa wote unakuwa controlled DAR sioni umuhimu wa ulazima kusafirisha gesi hadi dar then kuzalisha huo umeme....maana unaweza zalishwa palepale mtwara na unaingwizwa katika gridi ya taifa na kama nilivyosema wote unakuwa monitored from DAR

Kwa kweli huwa sijui kama mipango yetu ya Kitaifa hasa ya maendeleo kama hufanywa na watalaamu. Kama ndivyo basi hatuna watalamu kitu ambacho siamini. Kwa mtu wa akili ya kawaida tu siye mtaalamu wa uchumi wala wa nishati hawezi kutotambua yafuatayo kuhusu gesi au mafuta yaliyogunguliwa huko kusini mwa Tanzania:

1. Tunataka yazalishe umeme ili tupate unafuu wa bei ya umeme. Umeme huo unaweza kuzalishwa huko huko kusini na kuingizwa kwenye grid ya Taifa huko huko kusini. Kwani mbona huko Mtera, Tanga n.k. wanazalisha umeme huko huko na kuingizwa kwenye grid ya Taifa? Sasa sijui sisi ni majuha au vipi, tunataka umeme huo tukauzalishie Dar kwa kuisafirisha hiyo gesi gafi kwenye bomba lenye kipenyo cha urefu wa mtu (over 1.5 m) na urefu wa over 550 km la gharama ya over TShs 3 trions! Mitambo iliyopo pale Ubungo ya Symbions, PTL, Songas n.k. bei yake kila moja haizidi TShs 150 billion. At most yote kwa pamoja haizidi TShs 1 trion. Tungeweza hata kui dismantle na kuisafirisha na kuifunga huko Mtwara kwa gharama ndogo zaidi. Au tungeweza kununua mitambo mingine mipya mingi kuliko iliyopo Ubungo na kuifunga huko Mtwara kwa chini ya bei ya hilo bomba, na kuweza kuzalisha umeme kwa gharama ndogo. Viwanda vya Dar vinaweza kuendelea kupata gesi kwa kutumia meli toka Mtwara ambazo gharama zake ni nafuu kuliko bomba au lori. Wastage kwenye bomba ni mkumbwa sana, kwanza lazima lijae (over 1 trion cubic metre) excess ndiyo itafika Dar. Njiani cho chote kinaweza kutokea kwenye hilo bomba na inaweza ikawa disaster tupu.

2. Matumizi mengine ya hiyo gesi ni majumbani, kupikia hivyo kuokoa mazingira kwa kupunguza kukata miti kwa ajili ya mkaa au kuni hasa kule vijijini. Kuna sababu gani gesi hiyo isijazwe kwenye hiyo mitungi au containers za gas za Oryx n.k. huko huko Mtwara na kusafirishwa kwa meli au malori hadi huko Dar na kwingineko ambako inahitajika?

3.Kwa hiyo hata mafuta ya petroli yatakapoanzwa kuchimbwa huko kusini yatabidi yasafirishwe gafi kwenye bomba hadi Dar kwa refinary badala ya hizo refineries kujengwa Mtwara?

4. Mhhhh, ndiyo maana tunashindwa kufunga mitambo ya kufua umeme unaosemekana wa zaidi Megawatts 5,000 huko kwenye mafuriko ya Steinghlet kwa sababu tunashindwa kuyahamishia hayo mafuriko Dar? Vivyo hivyo kwa makaa ya mawe na hata uranium zingekuwa Dar mambo yangekuwa poa! Jamani Tanzania si Dar peke yake na wawekezaji waambiwe hivyo, wapo watakaoelewa tu. Wasiolewa waachane na sisi, yote ni kwa faida yetu sote kwani gharama zitakuwa nafuu kwa wote wala si Mtwara peke yao. Vinginevyo wananchi watashindwa kuwaelewa kwa maamuzi kama haya yasiyokuwa na logic. Watafikiri kuna mlungura umetembea! Si vizuri, muwaelimishe.

Big up Mtwara corridor, keep up and we all stand to benefit.
 
Naungana na wana Mtwara kupinga Gas kusafirishwa Bagamoyo na huko ndiyo wazalishe UMEME na umeme huo usafirishwe tena Mtwara. Ni heri kuzalisha umeme hukohuko Kusini na gharama iwe kusafirisha umeme tu.

Yaleyale ya kuipa kiwanda cha NYUZI Tabora wakati Pamba inazalishwa Mwanza na Shinyanga. Na wakati huohuo, kiwanda cha kuchambua Tumbaku wakajenga Morogoro badala ya Tabora. Hii mijitu pana wakati namuamini Masaburi kuwa wanatumia Makalio yao kufikiri na Kichwa kinatumika tu kuotesha nywele.

Watu wa Mwanza, Mara, Shinyanga na Tabora mmeshaona jinsi wenzenu wanafanya. Mbuguni na nyie huko kwenye Tanzanite na nyie anzeni kukomaa ili mfaidike na madini na siyo watu wanajenga Dar na nyie mnakufa kwenye vibanda vya nyasi. Kila watu wafaidike kwanza wao kwa utajiri huo na sehemu kidogo ndiyo iende kwenye bajeti ya Taifa.

KITAELEWEKA TU SIKU MOJA.
 
Acha CCM oyeeeeeeeeee iwatokee puani. Mchiteme, wala mchitafune. Mkichezea cherikali mtakula nchale kama pungo. Ama!
 
maandamano yasio na tija wala faida.
mnalia umeme kila siku mnategemea mtambo
aliofungua JK pale kinyerezi utatumia maji kuzalisha umeme?
gesi tayari inatumika mtwara mna mtambo wa kuzalisha
umeme mbona nyumba zenu za nyasi na makuti hamjaweza kutumia umeme?
tukiwawekea processing industry Mtwara nmategemea kupata ajira wakati hamtaki kusoma?
si ndio nyie mko dar mnajiita wamachinga? mbona mmekimbia kwenu?
Kuna mama ntilie wa kigeni kwenye zile blocks za kuchimba gesi ndio wanagawa vyakula kule
mlishaomba hizo tenda mkanyimwa??

mnajidanganya tu madini,gesi na mafuta ni kwa manufaa ya watanzania wote, rudini darasani
mkasome mjue namna ya kutumia rasilimali na kuepusha mikoa yenu na umaskini
mna ardhi yenye rutuba, mna korosho hata kuzipalilia hamwezi

mikoa yenu wangepewa wasukuma,wanyakyusa na wachaga ingekuwa mikoa tajiri.
kila siku mnavaa nguo za kijani mnaimba chama chajenga nchi mnalalamika nini
maji mmeyavulia nguo ingieni muoge bakini na umaskini wenu
hata mkipigwa mabomu mmeyataka wenyewe

atakaetukana na atukane ukipigwa bun shauri yako mmezidi uvivu afu mnataka bwerere
kaeni vijiweni endeleeni kunywa gahawan gesi lazima ije dar penda msipende
ss hatupingi watanzania wenzetu wasipate umeme toka mtwara.tunachotaka ni kwamba umeme utoke mtwara had dar na sio gesi ghaf.hii itasaidia pia mikoa ya kusini kuingia ktk grid ya taifa.na mkumbuke miaka ya 60 kulikuwa na reli toka mtwara hadi nachingwea serikal ikaindoa sjui waliipeleka wapi! Bandar yet nayo imeuzwa!!tunasema sasa basi imetosha.
 
Hawa Watu wa Kusini wacha watie adabu sasa, maana wao hujiona ndio CCM hata kumzidi Rizione. Hapa ndipo watakapojua kwamba ujinga si sifa nzuri.
:majani7::majani7::majani7::majani7::majani7::majani7::majani7::majani7::majani7::majani7::majani7::majani7::majani7::majani7::majani7::majani7::majani7::majani7::majani7::majani7::majani7::majani7:
 
Watu wa kusini nendeni shule nyie. Acheni ubinafsi na uchoyo usio wa maana. Hivi kila mtu akisema ang'ang'anie kilicho chake, tutafika kweli?
:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa
 
Nyie watu wa Mtwara ni wa ajabu sana, Serikali ndio wenye mali na maamuzi juu ya utajiri wa nchi kwa maendeleo ya wote
 
acheni ushenzi gesi ni lazima iletwe DAR nyinyi baadaye mbona sisi Mwanza tunakula mapanki samaki wanakula wazungu alafu maendeleo tunashea wote acheni kujipendelea Tanzania ni nchi moja, labda nanyi mjitenge kama zanzibar.
lugha jamani, tuwe makini! maneno hayo hayo ukiambiwa wewe lazima utapandwa na hasira!
 
Muachane na mawazo ya KIKANDA ambazo ni sera za CHADEMA, msije kuponzwa na siasa za vyama vingi, CCM na wana Mtwara tuna undugu wa jadi na wa kihistoria, dukuduku zenu pelekeni kwa Kamanda Simbakalia, Ghasia na Kapteni Mkuchika watachukua hatua
 
fuatilia kwa makini kabla hujapost

Wepo dachi!! lete sababu za kukataa gesi kusafirishwa hadi kwa wateja (DSM); muwe wakweli gharama za uchimabi gesi hazitaweza kurudi kwa kuuza gesi yote Mtwara na Lindi
 
Mtwara ni kwetu na Gesi ni yetu, watuachie wenyewe!!!!!!!

mnataka kupikia chikandanga!! Ikibidi FFU watatumika ili mradi bomba la gesi lijengwe na kufika Kinyerezi kwa ajili ya matumizi husika jijini Dar na Tanga
 
Naona kuna ushamba kidogo hapa wa Gesi ya asilia. Gesi haisafirishwi na matenka kama mafuta sasa mnataka Gesi iende vipi kwenye matumizi ya nyumba zaidi ya pipeline. Kwa matumizi ya nyumbani Gesi inabidi kusafirishwa kwa pipeline lakini kwa kupekeza nchi za nje wawekezaji watajenga kituo cha kuifanya gesi kuwa liquid na kuishafirisha nje hii itajegwa hukohuko inakotokea ni miradi tofauti. Gesi ya Dar ni kwa matumizi ya umeme na nyumbani tu.

Mkuu kwani unafikili hawalijui hilo! Niliwahi kuona kwenye TV wakiwekewa Umeme vijijini unao zalishwa hapo hapo MTWARA; lakini wakumbuke gas inatumika kwenye shughuli nyingine zaidi ya kusaidia kuzalisha UMEME, mimi nafikili sio busara kutumia mali asili kwa malengo ya kisiasa. KILA MKOA WENYE MALI ASILI NYINGI UKIAMUA kujifanyia wapendalo nchi itatawalika kweli!
 
Umeme kutokana na gesi unaweza ukazalishwa Mtwara na kuingizwa kwenye grid ya taifa ili wananchi wale wafaidi ajira. Kwa upande wa gesi kwa matumizi ya nyumbani uangaliwe utaratibu utakaowezesha uzalishaji wenye tija kama ni pale pale Mtwara au kwa njia ya bomba hadi Dar. Kwa matazamo wangu, gesi kwa matumizi ya nyumbani kwa sasa Dar panafaa kuliko Mtwara kutokana na miundombinu ya usafiri kuwa kwa wingi na inayowezesha bidhaa kufika kirahisi sehemu nyingi za nchi kutoka Dar.
 
Wepo dachi!! lete sababu za kukataa gesi kusafirishwa hadi kwa wateja (DSM); muwe wakweli gharama za uchimabi gesi hazitaweza kurudi kwa kuuza gesi yote Mtwara na Lindi

dachi chamani, unataka tuoongee kimakonde na kimalaba ndo mtuelewe?
 
Nyie watu wa Mtwara ni wa ajabu sana, Serikali ndio wenye mali na maamuzi juu ya utajiri wa nchi kwa maendeleo ya wote

ndio mtuache na uajabu wetu. hv serikali ni nan? Rais,mawaziri na wabunge bila wananchi?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom