Cecil David Mwambe - Wawekezaji Mradi wa LNG badala ya Kutumia Bandari ya Dar es Salaam Watumie Bandari ⛵ na Uwanja wa Ndege wa Mtwara na Lindi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
943

MHE. CECIL MWAMBE - MRADI WA LNG WAWEKEZAJI WATUMIE BANDARI NA UWANJA WA NDEGE WA MTWARA NA LINDI BADALA YA DAR ES SALAAM

Mbunge wa Jimbo la Ndanda, Mhe. Cecil David Mwambe wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Nishati amesema ni vyema wawekezaji wa mradi wa LNG badala ya kutumia Bandari ya Dar es Salaam watumie Bandari ⛵ na Uwanja wa Ndege wa Mtwara na Lindi

"Niwapongeze REA, Mradi wetu wa kuweka taa kwenye Jimbo la Ndanda wenye thamani ya Shilingi Milioni 400 tunategemea kuusaini hivi karibuni. Ndanda kwenye Kata zote za eneo la barabara Kuu inayoelekea Masasi linakwenda kuwaka" - Mhe. Cecil David Mwambe, Mbunge wa Jimbo la Ndanda

"Kazi ya kuweka Umeme kwenye Vijiji vyote vya Kata ya Mpanyani na Vijiji vyote vya Kata ya Msikisi inaendelea, kuna baadhi ya maeneo wameshaanza kuwasha na ifikapo mwezi Julai na mimi nitakwenda kushiriki zoezi la uwashaji" - Mhe. Cecil David Mwambe, Mbunge wa Jimbo la Ndanda

"Bado kuna mahitaji makubwa ya umeme katika Vijiji vya Ndanda hasa Vijiji vya Mbemba , Mbaju na Vijiji vingi vinavyozunguka Jimbo la Ndanda tuna mahitaji ya Umeme. Mheshimiwa Rais ameamua ugomvi" - Mhe. Cecil David Mwambe, Mbunge wa Jimbo la Ndanda

"Mtwara tuna tatizo kubwa, umeme umekuwa unakatika kila mara maeneo yote ya Mkoa wa Mtwara hasa kwenye Wilaya Masasi, Newala, Mtwara Mjini na Wilaya zingine zote. Waziri wa Nishati umetuhakikishia ndani ya miezi 3 ijayo utapeleka Turbine ya Megawatts 20 kama suluhisho la awali kuhakikisha Mkoa wa Mtwara unapata umeme wa uhakika" - Mhe. Cecil David Mwambe, Mbunge wa Jimbo la Ndanda

"Mama Samia ametuamulia ugomvi, Mradi wa REA unaotokea Songea wa Grid ya Taifa kuleta Umeme Masasi, Waziri wa Nishati umepata fedha nyingine ya kutoa Umeme Masasi kupeleka Maumbika. Maeneo ya Ndanda, Chikukwe, Chigugu na Vijiji vingine vitakuwa vinapata Umeme wa Uhakika" - Mhe. Cecil David Mwambe, Mbunge wa Jimbo la Ndanda

"Mradi wa LNG na faida zake. Wabunge wa Mtwara tulikuwa hatueleweki kwa wananchi wote wa Mkoa wa Mtwara. Miaka 10 iliyopita Mkoa ulikuwa juu kimaendeleo kwasababu ya miradi mbalimbali ya Gesi Asilia. Walikuwa na hamu ya kuona utekelezaji. Ndoto kubwa tuliyoisubiri kwa muda mrefu sasa inakwenda kutimia na kuwa kitu halisi" - Mhe. Cecil David Mwambe, Mbunge wa Jimbo la Ndanda

"Nampongeza Mhe. Hamida na Waziri wa Nishati kuhakikisha zinapatikana fedha za fidia kwa ajili ya wananchi wa eneo zenye thamani ya Shilingi Bilioni 5.5, hii tafsiri yake ni kwamba sasa Mradi wa LNG unakwenda kutekelezwa" - Mhe. Cecil David Mwambe, Mbunge wa Jimbo la Ndanda

"Tunakushauri Waziri wa Nishati hakikisha shughuli za kutia saini, utekelezaji wa miradi na maandalizi yanafanyika kwenye maeneo ya Lindi na Mtwara ili kuweza kuchechemua uchumi wa maeneo haya" - Mhe. Cecil David Mwambe, Mbunge wa Jimbo la Ndanda

"Shughuli za Mradi wa LNG badala ya kutumika uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam, Bandari ya Dar es Salaam, Waziri uwasisitize wawekezaji ikiwezekana kwa Mikataba Maalum kwamba Mizigo yao na Shehena zao zishukie Bandari ya Mtwara, Bandari ya Lindi na Uwanja wa Ndege wa Lindi" - Mhe. Cecil David Mwambe, Mbunge wa Jimbo la Ndanda

"Katika miradi mikubwa ya kimkakati, Mradi wa Mchuchuma na Liganga ya Ludewa, mradi huu umekuwa unatajwa lakini hautekelezwi. Tunaomba Serikali kwasababu wawekezaji wameshapatikana, jambo hili lifanyike kwa haraka ili tuanze kuona manufaa ikiwezekana kabla ya kuanza mwaka wa fedha 2024-2025 kazi zianze kufanyika" - Mhe. Cecil David Mwambe, Mbunge wa Jimbo la Ndanda

"Kwa sasa hivi mahitaji ya umeme ni makubwa, hatujakamilisha Mradi wa LNG Lindi, Mradi wa Mtwara Megawatts 300 haujakamilika na Mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere haujakamilika. Waziri ona namna ya kukaa na SONGAS boresheni Mikataba ili wananchi waendelee kunufaika " - Mhe. Cecil David Mwambe, Mbunge wa Jimbo la Ndanda

"Jukumu la Vinasaba lilikuwa EWURA mwanzoni lilipelekwa TBS. TBS ameshindwa kufanya hii kazi ndiyo maana gharama za mafuta zinaongezeka. Tuachane na TBS kwenye hili jambo tuwape watu ambao wana uwezo wa kulifanyia kazi ili twende nao sambamba" - Mhe. Cecil David Mwambe, Mbunge wa Jimbo la Ndanda

"Kuna maeneo ambayo kuna tatizo kubwa la Umeme, tukakamilishe maeneo haya. Mkoa wa Mtwara una Vijiji zaidi ya 780+ lakini karibia Vijiji 300 havina Umeme. Tatizo la Umeme Mkoa wa Mtwara sasa linakwenda kuisha" - Mhe. Cecil David Mwambe, Mbunge wa Jimbo la Ndanda

"Wawekezaji wa Mradi wa LNG Ofisi zao ziwe Lindi na Mtwara. Kwa kipindi kirefu tumetegemea Korosho tu lakini sasa tunakwenda kutegemea mazao ya Gesi Asilia ikiwa ni pamoja na Masuala ya Mbolea, Usafirishaji, Bandari ya Mtwara Serikali imeweka fedha nyingi sana kuhakikisha inatumika" - Mhe. Cecil David Mwambe, Mbunge wa Jimbo la Ndanda
 
Attachments

  • maxresdefaultaswer.jpg
    maxresdefaultaswer.jpg
    57.2 KB · Views: 5

Hii point ya kutumia Bandar I na airport.. Ni Habari nzuri Sana, kipindi wazungu wako kule kufanya utafiti.. Mtwara palinoga... Wageni kila siku hadi pakachangamka... Akifanya hivi Ile Hali ya uzembe wa wamakonde itapungua kama sio kubisha.. Maana wageni wengi watachangamkia fursa wao wakiendelea kulala
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom