Mtwara kumekucha; Maandano ya kupinga kusafirisha gesi yaja

Status
Not open for further replies.
acheni hizo, gesi ni lazima iletwe DAR nyinyi baadaye mbona sisi Mwanza tunakula mapanki samaki wanakula wazungu alafu maendeleo tunashea wote acheni kujipendelea Tanzania ni nchi moja, labda nanyi mjitenge kama zanzibar.
 
Pamoja sana wana wa Kusini. Naona pia chembechembe za matokeo chanya ya M4C Operesheni Okoa Kusini pamoja na hotuba za Kambi ya Upinzani Bungeni, hasa kwenye Bunge la Bajeti mwaka huu 2012.
 
Hawa wakazi wasikilizwe hata bila ya kuandamana wafuatwe ,kwani watakuwa wamejifunza mererani pamoja na tanzanite kuwa inatoka tanzania tu duniani mji mdogo una baki na mahandaki yenye historia ya pekee .hali ni mbaya kuliko maelezo barabara hazipitiki ,.pili angalia wale wenzetu wanaolala juu ya almasi na dhahabu no strategically plan ,watu wanavuna tu kama vile hamna wenyewe .
 
maandamano yasio na tija wala faida.
mnalia umeme kila siku mnategemea mtambo
aliofungua JK pale kinyerezi utatumia maji kuzalisha umeme?
gesi tayari inatumika mtwara mna mtambo wa kuzalisha
umeme mbona nyumba zenu za nyasi na makuti hamjaweza kutumia umeme?
tukiwawekea processing industry Mtwara nmategemea kupata ajira wakati hamtaki kusoma?
si ndio nyie mko dar mnajiita wamachinga? mbona mmekimbia kwenu?
Kuna mama ntilie wa kigeni kwenye zile blocks za kuchimba gesi ndio wanagawa vyakula kule
mlishaomba hizo tenda mkanyimwa??

mnajidanganya tu madini,gesi na mafuta ni kwa manufaa ya watanzania wote, rudini darasani
mkasome mjue namna ya kutumia rasilimali na kuepusha mikoa yenu na umaskini
mna ardhi yenye rutuba, mna korosho hata kuzipalilia hamwezi

mikoa yenu wangepewa wasukuma,wanyakyusa na wachaga ingekuwa mikoa tajiri.
kila siku mnavaa nguo za kijani mnaimba chama chajenga nchi mnalalamika nini
maji mmeyavulia nguo ingieni muoge bakini na umaskini wenu
hata mkipigwa mabomu mmeyataka wenyewe

atakaetukana na atukane ukipigwa bun shauri yako mmezidi uvivu afu mnataka bwerere
kaeni vijiweni endeleeni kunywa gahawan gesi lazima ije dar penda msipende
 
Sasa gesi yote ikibaki Mtwara mna viwanda vya kuitumia izo 7TCF jamani au ushabiki tuu!
Mtwara itakuwa tuu gradually sio ghafla kama mtakavyo ninyi
So nao jamaa wa Iringa waseme Mtera Dam ni kwa ajili ya wana Iringa tuu
Jamaa zangunkule Ngaka Mbinga waseme mkaa ni kwa wana mbinga tuu
Same to Chuma Liganga,Mkaa Mchuchuma,Dhahabu Kahama,Oil and Gas Nyasa na Tanganyika Lakes kama zikipatikana halinkadhalika Rukwa
Natumtumbo waseme Uranium ni yao tuu
Tutafika kweli?
 
What is Dar by the way! hata watu wa maeneo mengine wanahitaji maendeleo kwa haraka zaidi! sio kila kitu Dar halafu hamtaki kuwasikiliza wananchi. Eti utasikia ikipelekwa dar ndio raisi kuingizwa kwenye gade ya Taifa. sasa iandaliwe kulekule mtwara , sio mnaleta maamuzi ya kihunu hapa.
 
Haya ni matatizo ya kutokuwa na serikali za mtaa zenye mamlaka. Mf majimbo chini ya magavana wenye kuwajibika moja kwa moja kwa wananchi ndio imesababisha maendeleo yote yawe Dar. mfano kama chuo cha IFM kimejaa kwanini wanajenga kingine ndani ya Dar? Kwanini Mzumbe imefungua tawi dar na lina wanafunzi wengi kuliko la Morgorogo?. Ukipata majibu ya hayo utajua kwanini ni muhimu kuwa na utawala wa serikali za mtaa

mkuu ukigusia vyuo hasa vya elimu ya juu ndio upendeleo wa wazi. Dar viko zaidi ya 30 wakati Mwanza hata vitano havifiki. Na bado kuna chuo kikuu cha anga kinajengwa, Kigamboni kipo cha Wakorea kinajengwa. Huu ni upuuzi!
 
TUNAOMBA WATU WA KUSINI, KESHO MTUME WAWAKILISHI WENU WAJE WACHUKUE TAARIFA KATIKA MAANDAMANO YA WATU WA KUSINI KUGOMEA BOMBA KWENDA DARESALAAM,wale wote wasiojua kwanini ili swala naomba watege sikio,tutawajuza kesho dunia mzima
 
TUNAOMBA WATU WA KUSINI, KESHO MTUME WAWAKILISHI WENU WAJE WACHUKUE TAARIFA KATIKA MAANDAMANO YA WATU WA KUSINI KUGOMEA BOMBA KWENDA DARESALAAM,wale wote wasiojua kwanini ili swala naomba watege sikio,tutawajuza kesho dunia mzima

kama wananchi hiyo gesi wanaitaka kwa ajili ya matumizi gani hasa.
 
kama wananchi hiyo gesi wanaitaka kwa ajili ya matumizi gani hasa.

swali zuri sana,tunataka zile ahadi walizotuambia kua baada ya kugundua gesi,kuwa viwanda vingi vitajengwa,gesi itabaki,na viwanda vya kutengeneza gesi ya matumizi ya majumbani vitajengwa huku,na viwanda mbalimbali,mfano leo kusini ndio umeme haukatiki mikoa mingine ina tatizo la umeme tokea ishu ya Richmond,na mpaka leo umeme dar,arusha aujatulia,kwanini viwanda aviletwi kusini
 
huna hoja
viwanda vitaota kama majani na sio kujengwa na mwekezaji?,
mtabaki mnalia lia bomba litajengwa kwa lazima kuja dar
 
TUNAOMBA WATU WA KUSINI,
KESHO MTUME WAWAKILISHI WENU WAJE WACHUKUE TAARIFA KATIKA MAANDAMANO YA
WATU WA KUSINI KUGOMEA BOMBA KWENDA DARESALAAM,wale wote wasiojua
kwanini ili swala naomba watege sikio,tutawajuza kesho dunia
mzima

Wewe na CDM wenzako ni wachochezi! nyie mnadhani kuwa itakopoanza vurugu na umwagaji damu kama mlivyosema eti mtaingia msituni! wewe kilaza unajua madhara ya vita? au ukisha kula ugali wako na samaki wa kukaangwa akili zinakuruka na unatamani damu sio! Hujui madhara ya hicho unachoshabikia:!
 
TUNAOMBA WATU WA KUSINI, KESHO MTUME WAWAKILISHI WENU WAJE WACHUKUE TAARIFA KATIKA MAANDAMANO YA WATU WA KUSINI KUGOMEA BOMBA KWENDA DARESALAAM,wale wote wasiojua kwanini ili swala naomba watege sikio,tutawajuza kesho dunia mzima
Kazeni sana wadau! Huku mwadui tumeachiwa mashimo tu! Solidarity forever.
 
Wewe na CDM wenzako ni wachochezi! nyie mnadhani kuwa itakopoanza vurugu na umwagaji damu kama mlivyosema eti mtaingia msituni! wewe kilaza unajua madhara ya vita? au ukisha kula ugali wako na samaki wa kukaangwa akili zinakuruka na unatamani damu sio! Hujui madhara ya hicho unachoshabikia:!
chadema imeingiaje hapa?mbona mna hofu sana?
 
Haya mambo ya ubishi njaa, bomba litajengwa na hakuna kitu mtafanya, kazi hamtaki kufanya mnataka kuleta njaa njaa zenu yaani nyie watu sijui nani anawadanganya
 
Hawa Watu wa Kusini wacha watie adabu sasa, maana wao hujiona ndio CCM hata kumzidi Rizione. Hapa ndipo watakapojua kwamba ujinga si sifa nzuri.
 
Status
Not open for further replies.
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom