rmashauri
JF-Expert Member
- Jan 29, 2009
- 3,011
- 454
swali zuri sana,tunataka zile ahadi walizotuambia kua baada ya kugundua gesi,kuwa viwanda vingi vitajengwa,gesi itabaki,na viwanda vya kutengeneza gesi ya matumizi ya majumbani vitajengwa huku,na viwanda mbalimbali,mfano leo kusini ndio umeme haukatiki mikoa mingine ina tatizo la umeme tokea ishu ya Richmond,na mpaka leo umeme dar,arusha aujatulia,kwanini viwanda aviletwi kusini
Jamani watu wa kusini acheni ubinafsi. Kumbukeni kuwa viwanda vyewenye ni vya kutegemea wawekezaji kwahiyo mtakuwa hamwuatendei haki waTZ wenzenu mkigomea gesi isiende DAR. DAR ndo kuna viwanda vingi na pia itatumika kuzalisha umeme wa gridi ya taifa ili kuondoa tatizo la umeme nchi nzima. Nyie sasa hivi mnajinoma na umeme wa Artumas tena kwa bei chee na umeme wenu kama mko Ulaya vile maana haukatiki. Wahurumieni waTZ wenzenu nao wapate nishati ya uhakika. Pia kuna ndugu zenu wengi tu waonaofanyakazi kwenye viwanda huko DAR. Viwanda vitakuja pole pole kwa kadri wawekezaji watakapoona fursa ya kuwekeza huko kwa maana hata mkiikatalia hiyo gesi si kwamba ndo wawekezaji watakuja kesho na kuanza kujenge viwanda kama mnavyodai.