Mbunge wa Nanyamba Abdallah Chikota Ametaka Watu wa Mikoa ya Lindi na Mtwara Kuendelea Kushirikishwa Katika Mradi wa Gesi Asilia Iliyosindikwa (LNG)

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
945

MBUNGE ABDALLAH CHIKOTA ATAKA USHIRIKISHWAJI MRADI WA GESI ASILIA WA LNG​

Mbunge wa Nanyamba (CCM) Abdallah Chikota ametaka watu wa mikoa ya Lindi na Mtwara kuendelea kushirikishwa katika mradi wa Gesi asilia iliyosindikwa (LNG) kwasababu yapo mambo mengi yanayohitaji ushirikishwaji.

Chikota aliungana na Wabunge wengine wa mikoa ya Lindi na Mtwara ambao walipongeza hatua ya kufufuliwa kwa mradi huo uliosimama kwa miaka saba.

Akichangia mjadala wa makadirio ya Wizara ya Nishati kwa 2023/24 Jumatano Mei 31, 2023, Chikota amesema awali ziliundwa kamati mbili za upatikanaji wa ardhi na kuijumuisha jamii kwenye mradi.

Amesema kamati hizo zilizoundwa na Serikali na wawekezaji zilifanya kazi zake kwa kushirikiana na wananchi wa Lindi.

“Vijana, wanawake, wazee, makundi ya kijamii lazima yajulishwe hatua inayoendelea katika mradi huu, waelezwe fursa zilizopo, jinsi watakavyonufaika na mradi huu,” amesema.

Mbunge huyo amepongeza kauli ya Waziri wa Nishati January Makamba pale alipowaeleza juu ya mpango wa ujenzi wa chuo kikubwa, ambapo wananchi watanufaika maana awali walikuwa wanawapeleka vijana kupata elimu ya kati katika vyuo vya Veta Mtwara na Lindi.

Amesema malengo ni vijana wapate ujuzi wakati mradi ukianza na wataweza kuajiriwa na hivyo kuomba kamati hizo kuelimisha wananchi jinsi ya kuishi na mradi huo.

Ameitaka jamii ijifunze kwa yanayotokea nchini Nigeria na Msumbiji na kwamba hayo yawatayarishe kuishi na mradi pale utakapoanza.

Kwa upande mwingine, Chikoka ametaka kujengwa kwa uwanja wa Ndege wa Lindi, barabara za mikoa ya Lindi na Mtwara na kuboresha huduma nyingine katika mikoa hiyo.

WhatsApp Image 2023-05-13 at 10.02.03 AM.jpeg
 
Back
Top Bottom