Mtwara kimenuka: Mabomu ya machozi yarindima!

Mtwara kimenuka: Mabomu ya machozi yarindima!

me ndio natoka saiz nafika nyumbani mda huu sikutembea na laptop yangu,then nilikuwa nasumbuka sana kufanya updates kwa kutumia simu,tulikuwa pamoja na mkuu sizinga,tumechukuwa picha za kutosha sana,atakuja kuzimwaga hapa bila hiyana
hali imekuwa mbaya sana,nitarudi kwa updates za uhakika hapa
 
tupo pamoja watu wa mtwara lindi na ruvuma.kwa hakika haki na riziki za watu hazipotei ila hucheleweshwa tu kwa hakika ipo siku kilio cha wengi kitasika.Lakini siku ingine tujifunze kutokana na makosa yetu kwa kuwakataa wanaotugandamiza kwa kufanya maamuzi sahihi bila kuangalia wanakanga,vitenge,tshit au mchele.2015 si mbali maamuzi yote tunayo mikononi mwetu.
 
Hakika wananchi wanataka maisha Bora na sio Bora maisha,mamlaka zisifanye ajizi katika kusikiliza matakwa yao ndio njia pekee iliyobaki katika kutatua mgogoro huu.
 
Hakuna haja ya kuwapiga wenye nchi mabomu! Mara zote nasema suala la gas na wanamtwara litamalizwa na serikali na wanamtwara wenyewe endapo tu serikali ikikumbuka kuwa kuna kitu kiitwacho meza ya mazungumzo. Hatutegemei kusikia siasa au mabomu tena!!

kwani serikali si ndo inayowatuma hao manjago wawapige wenye nchi mabom?hawawezi kuzungumza bila mabom mpaka waone damu inamwagika ndo waanze kutafuta round table.kama wangelijua hili wasingeanza kutukana watu,bahati mbaya wamechelewa sana kujirudi wakati watu wakusini wameshaamka.hakika majuto ni mjukuu.
 
Jambo hili hakika limefikia hatua mbaya,wenye mamlaka yawapasa kusikiliza madai ya wananchi kuepusha shari.
 
Mwalimu Nyerere in Shivji (2000), "Critical Elements of a New Democratic Consensus in Africa (pp 25-38):

["It is not that peace has come by itself. The source of peace in Tanzania is not that the Arusha Declaration has done away with poverty even a little bit. Isn't there this poverty we are still living with? This poverty is right here with us. It is not the same economy we are grappling with? The fact is not that the Arusha Declaration has banished poverty even by an iota – nor did it promise to do so. The Arusha Declaration offered hope. A promise of Justice, hopes to the many, indeed the majority of Tanzanians continue to live this hope. So long as there is this hope, you will continue to have peace. Here in Tanzania we have poverty but no ‘social cancer'. It is possible it has just begun. But otherwise we don't have a social cancer. There isn't a Volcano in the making, that one day it is bound to erupt. We have not yet reached that stage because the people still have hopes based on the stand taken by the Arusha Declaration. It did not do away with poverty but it has given you all in this hall, capitalists and socialists alike, an opportunity to build a country which holds out a future of hopes to the many.

To be sure, you few Waswahili, do you really expect to rule Tanzanians through coercion, When there is no hope, and then expect that they will sit quiet in peace? Peace is born of hope, when hope is gone, there will be social upheavals. I'd be surprised if these Tanzanians refuse to Rebel, why?

When the majority don't have any hope you are building a volcano. It is bound to erupt one day. Unless these people are fools. Many in these countries are fools, to accept being ruled just like that. To be oppressed just like that when they have the force in numbers, they are fools. So Tanzanians would be fools, ******, if they continued to accept to be oppressed by minority in their own country. Why?"]

May God Rest Him In Peace


 
Rasilimali za taifa ni kwa ajili ya manufaa ya taifa zima. Kusema GESI HAITOKI MTWARA ni ubinafsi uliopitiliza. Hakuna justification yoyote inayoweza kuhalalisha hilo.
We Mnyisanzu mjinga embu fikiria jinsi wananchi wanaozunguka mbuga za wanyama,na wanavyo athirika na Kuaribiwa,mazao na mara zingine kujeruhiwa, hata Kupoteza maisha!!!!Lakini akiingia hata Mbugani kuwinda Digidigi, akikamatwa,adhabu yake ni kuamrishwa kula Nyama mbichi,na hata kupigwa risasi! Ajabu Waarabu na Mafisadi wanawawinda wanyama kuwaua,na kuwasafirisha nje ya nchi wakiwa hai.!!!!!na hawafanywi kitu.sasa wanakusini wamegundua hilo ndio maana wanasema GESI KWANZA UHAI BAADAE.,,,lazima wanufaike wao kwanza,na sio Mafisadi Wa Ccm.,,,,,,Upo hadi hapo?
 
hali mijini hapa ni tete! Mabomu yanarindima mjini hapa kuwatawanya wananchi wanaojiandaa na mkutano mkubwa unaotarajiwa kufanyika mjini hapa kuhusu suala zima la gesi.

Chanzo cha mabomu hayo kupingwa ni baada ya umeme kukatika/kukatwa eneo panapotarajiwa kufanyika mkutano huo uwanja wa mashujaa mjini hapa na baada ya kuona hivyo wananchi wakaamua kuandamana kuelekea tanesco kujua chanzo cha tatizo hilo la umeme na hali hiyo kupelekea polisi kuanza kuvurumisha mabomu ya machozi.

Ifahamike kwamba kumekuwa na mvua kubwa mjini hapa toka usiku wa leo ambayo inaweza ikawa chanzo cha kukatika kwa umeme huo (huu ni mtazamo wangu) ingawa inaweza ikawa hujuma pia.

Eneo nilipo umeme upo hali hii ya sintofahamu imepelekea huduma muhimu za kijamii kama maduka na soko kufungwa.

updates:
wakuu nimetoka kwenye mkutano umefanyika hapo mashiujaa kiukweli sikuweza kuendelea kuwaletea live kutokana na hali ya mvua pale uwanjani. Kifupi mkkutano umehutubiwa na wazungumzaji kadhaa wakiwepo wasanii na wabunge, wasanii walikuwa ni afande sele na kala pina kwa upande wa bunge nimagdalena sakaya, sulemani bungala (bwe.ge) na barwan, wazuinguzaji wengime walikuwa ni katani na mtatiro

wote kwa hakika wamezungumza mengi sana na wote wameungana na wanamtwara katika kuhakikisha rasilimaliya gesi inawanuifaisha watu wa mtwara nakusini kwa ujmla kwa upande wa wasanii hakika afande sele amejitahidi sana kuongea kwa kujenga hoja. Pamoja na kuwa nahali ya mvua wananchi hawakuondoka pale uwanjani kwa kweli serikali isipuuze haya madai ya watu wa mtwara kwa mfano kwa jinsi inavyoonekana vijana wako tayari kwa lolote serikalli iache kiburi. Katika mkutano huo kumekusanywa saini za watu 26,000 na kuwatuma wabunge kupeleka bungeni madai yao na munge wa lindi mjini ameeleza mara baada ya mkutano huo wa bunge kma madi ya wanantwara na kusini yote watakutana lindi kwa maandamano makubwa yatakayo fanyika tarehe 23 februari mwaka huu hadi kieleweke

lakini pia kulikuwa na jambo la kusikisha, kumetokea ajari pale njia panda ya kuelekea eapot ya mtwara gari lililokuwa linatokea tandahimba likiwa na wananchi limepata ajali na watu watatu kuumia nakupelekwa hosptali ya mkoa ligula na mmoja inaelezwa hali yake sinzuri anatakiwa kupelekwa muhimbili kwa matibabu zaidi, jambo ambalo lilimfanya bwana katani kuumba umati mkubwa uliohudhuria kutoa mchango kuwezesha safari hiyo na wananchi kuitikia jambo hilo ni hayo tu wakuu. Picha zitafuata punde.

'ni upepo tu unapita'-jk
 
Issue siyo gesi ibaki
mtwara, ila wananufaikaje na gesi hiyo siyo watu wawe wanachota gesi na
kuwaacha na matatizo yao nyie kama mmeshindwa kupigania pesa zenu zilizo
welwa huko uswiss na kwingineko ni nyie wao wameamua kukaba
mapema...hizi unajua mtwara na lindi kuna watu wana miaka 20 hajawahi
kuzaa kiatu siyo kwamba hapendi ni kwasababu hana uwezo huo sasa leo
wamebahatika tugesi wawalegezee...

Crashwise, mbona kuna watu wamezaliwa Dar wanazeekea Dar na hawajawahi kufaidi mapato ya Bandari? nao waandamane?
 
Last edited by a moderator:
Swala hili si ubaguzi ila CCM ndiyo wanalitengeneza ili ionekane kama ni ubaguzi...
ni kwerli kabisa mkuu jamaa wakibanwa hutafuta sababu na hoja dhaifu katika kupindisha ukweli lakini bahati mbaya safari hii wamekutana na ngangari.wataisoma tu namba.gesi kwanza ukanda,ukabila,udini,uamsho etc baadae!!!!!!!!!!!!!.
 
kuna sredi nimechangia na kuandika hivi...

kama watanywea ktk hili watakua wamekosa the best opportunity ya kuingia katika historia ya nchi hii kama mapioneers wa kutetea rasrimali za nchi zinufaishe wananchi na sio watawala. na kwa msimamo walioonyesha, ninahakika ndugu zangu wa kanda ya ziwa kwenye madini kemkem kuna kitu wamegundua na watakifanyia kazi. just wait and see! its a matter of time! just a matter of time!

naona tunawaza kitu kimoja mkuu!!

nahis watu wa kanda ya ziwa kuna kosa walilifanya na wanapaswa kujisahihisha kupitia wana mtwara,na kusin kwa ujumla
 
TANZANIA KUMEKUCHA, watu
wa Mtwara waungwe mkono na mikoa yote hasa sehemu walizodhulumiwa madini
kama TANZANITE Manyara, Mara - Buhemba na North Mara Gold Barrick,
Mwanza bulyanhulu, kahama, geita na Mwadui.

Mbaya zaidi North Mara wanapigwa risasi, wanatiririsha maji machafu
kwenye mito.

Mererani Wana apolo na watanzania walinyang'anywa Vitalu vyenye madini
wakapewa makaburu

Sasa tuliona Madaktari walikosa uungwaji mkono na wananchi, Hatimae
Dokta Ulimboka akatekwa, akateswa, akasulubiwa.... Mashuka, vifaa tiba
na dawa hospitali hakuna

Waalimu nao wakatishwa wakaogopwa, angalia sasa matokeo ya secondari na
shule za msingi.

wenye hasara ni wananchi, maana hao mafisadi wanatibiwa nje, watoto wao
wanasoma nje.

THIS IS APATHEID HALAFU NI MBAYA KULIKO ILE APATHEID YA MAKABURU SOUTH
BOTHA.

kwa sasa wananchi wa mikoa yote tuungane na Wanamtwara, ili hawa
watawala wakose upenyo na hata ikiwezekana Maandamano yakomae yatapakae
nchi nzima kama Misri, Libya...

We just need coordinator behind scenes ili kuunganisha nguvu, just use
mobile phones, FB and social media to mobilize people.

Hapa ndo mwanzo na safari moja huanzisha nyingine.

Maandamano yakipamba moto nchi nzima hakya nani wanajeshi na polisi
wataunga wananchi mkono.

MPadmire, Ha! we utamsemeaje Ulimboka wakati ye mwenyewe yupo? acha kiherehere subiri atasema mwenyewe!
 
Last edited by a moderator:
.......... do you really expect to rule Tanzanians through coercion, When there is no hope, and then expect that they will sit quiet in peace? .......... Unless these people are fools. ...... Tanzanians would be fools, ******, if they continued to accept to be oppressed by minority in their own country....

Maneno ya Mwalimu Nyerere yana uhai, yanaishi na yanatendeka!
 
:shut-mouth:Geeeeeeeeeeeeeesi jamani hatutaki fujo wana mtwara..serikali sikia maombi yetu mjenge huku hizo plants tufaidike nasi khaaaaaa...barabara yenyewe inasuasua na mkiweka bomba si ndo mtaona hatuna umuhimu kabisa wa kuletewa maendeleo.:target::target:
 
Back
Top Bottom