Mtwara: Gari la 'Afisa Usalama' lapondwa mawe Msimbati

Mtwara: Gari la 'Afisa Usalama' lapondwa mawe Msimbati

Habari za uhakika nilizozipata sasa hivi toka Msimbati zinasema kuwa kuna gari ya afisa usalama wa taifa mmoja toka Dar linapondwa kwa mawe na wananchi wenye hasira.

Afisa usalama huyo inadaiwa ametumwa na viongozi wa juu wa serkali ili aje amshawishi bibi mmoja anaedaiwa kuwa na uwezo wa kuizuia gesi isitoke kwenda Dar kwa njia ya bomba.

Bibi huyo inasemekana ndio mwenye kijiji hicho alishasema wazi kuwa gesi HAITOKI Mtwara kauli iliyowafanya hata viongozi kupata wasiwasi ivo kumtuma mtu huyo ili amshawishi gas itoke.

Wakati akiongea na bibi huyo aliwaita wajukuu zake ili wamsikilize. NDIPO Vurugu kubwa ikaibuka na mwanausalama akatimua mbio na kuliacha gari yake maana watu walikuwa wengi.

Na habari zilizonifikia sasa ni kwamba gari hiyo imechomwa moto.
hiyo ndio faida ya kujipendekeza,akipata nafasi ya kurudi akiwa hai awaeleze kwamba,magamba waende wenyewe mtwara wasiwatume watu
 
Sasa hivi ni usiku sana, polisi wana guts gani kwenda kwenye kijiji gizani namna hii.
Au watu wa Msambati ni waoga sana.
I thought ndo wangewafundisha somo hawa waonevu wa demokrasia.

Hivi polisi huwa hawaoni usiku!
 
Jamani tumesahau umeme uligoma kupita juu ya makaburi pale iringa na Tanesco wakalazimika kupitisha nguzo za umeme upande wa pili wa barabara.USIJE UKAKUTA BIBI ANAJUA KUZUIA SIO BIT HILO.watu wa kutoka mbeya na Iringa wanafahamu hili.
 
Hii Habari kama ni ya kweli basi Kikwete arudishe vijana wake kwenye mafunzo tumeona vijana wa usalama wa taifa wakibamizwa vibao ovyo ovyo tuu pale Muhimbili ilikuwa aibu ,sasa huko Msimbati duh tuna vijana gani wa Usalama wa Taifa wanajiachia kizembezembe tuu mpaka bibi anamzidi kete
au ndio kulewa neno Usalama wa Taifa ndio maana wakiwa baaa unakuta anaweka bastola kaunta wananchi sasa hivi wanapambana na yeyote anayeonekana kudharau utu wao
 
Nashangaa wakurya, wana apolo wa Ar na Wasukuma kimya. Tushikamane iwe tunisia mpya.

Wataongea nini wakati MALI imeishamalizika. Fursa yao ilishapita, tembelea Geita uone kulivyo na vumbi jekundu baada ya dhahabu kushindwa kuweka lami hata mtaa mmoja.
 
Kwa hiyo wanadhani wakimrubuni bibi suala la gesi litaisha. Hii ndiyo ccm kila kitu wanachokitaka kwa maslahi yao lazima watumie rushwa au kutisha na hata kudhuru kimwili.
 
namshukuru Mungu kuwa tumeamka sana, mabomba yatajengwa lakini gesi itakuwa haipiti, chezea makonde wewe kwa ushirikina?
 
Habari hii ni ya kweli kwa mujibu wa mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Msimbati. Pengine nyie mliopo mbali na Mtwara na Msimbambati kwa ujumla hamna habari za kutosha na vyombo vya habari kwa kiasi kikubwa vinapotosha yale yanayojili huku hasa vyombo vya habari vya serikali na ccm, (gezeti la habari leo na uhuru). Bibi yupo na ana umri unaokadiliwa kuwa ni miaka 116 na mtoto wake ambaye anamsaidia kuongea na wageni wote wanaokwenda hapo kwake ana umri wa miaka 70 na wote bado wana nguvu kiakili, hawajapoteza network bado.

Kilichotokea, afisa usalama huyo wa taifa alifika Msimbati jana jioni inayoelekea kuwa usiku kwa nia ya kuonana na bibi ili amchukuwe ampeleke dar, kwa hiyo alikaribishwa hapo nyumbani na mtoto wa huyo bibi lakini afisa usalama alitaka kuongea na bibi huyo kwa faragha hivyo alitaka mtoto wa huyo bibi awapishe, mtoto wa bibi alimwambia afisa usalama kuwa haiwezekani kwani yeye ndiye humsadia bibi kwa mawasiliano yoyote yanayofanywa na wageni wote wanaofika hapo nyumbani, ndipo afisa aliposema amekuja kumchukua bibi anatakiwa dar na viongozi wa serikali, akijibiwa kuwa kutokana na umri wa bibi kuwa mkubwa na hali yake ya kiafya kutokuwa mzuri sana bibi huyo haendi kokote, afisa usalama akasema atwachukuwa wote akaambiwa haiwezekani pia. wakati hayo yakijiri wanakijiji waalianza kujikuasanya hapo nyumbani wengine wakalizinguka gari na wengine wakawa wanafutilia mazungumzo hayo kupitia dirisha la nyumba. afisa akashtuka na kutoka nje kutahamaki akakuta anahojiwa yeye na kila mwanakijiji akawaambia kuwa hawezi kuzungumza na wote alipoona kibano kinazidi na maisha yake yapo hatarini, akatimua mbio, kilichofuata ni wanakijiji kulichoma moto gari lakini afisa usalama amefinikiwa kusepa. Kwa mujibu wa m/kiti wa kijiji anasema afisa huyo ni kijana mzaliwa wa msimbati lakini hajafika hapo msimbati miaka mingi na haishi Mtwara.

Watanzania tunaomba mtambuwe kwamba wakati umefika kuwa wananchi wana haki zote za kunufaika na rasirimali za asili zinazopatikana katika maeneo yao na serikali inawajibu wa kujenga mazingira wezeshi kwa wananchi kunufaika na rasirimali zao, Kama tunavyodai ujenzi wa mtambo wa kufua umeme wa megawatt 300 na kujenga mtambo wa kuchakata gesi hapa Mtwara.

Kujengwa kwa mitambo hiyo kutavutia wajasiriamali wa kimataifa kuja kuwekeza katika viwanda mbalimbali vinavyotumia malighafi (by-product) zinazotokana na gesi asilia, viwanda hivyo ni vya fertilizer, antifreeze, plastics, pharmaceuticals and fabrics. It is also used to manufacture a wide range of chemicals such as ammonia, methanol, butane, ethane, propane and acetic acid. Many manufacturing processes require heat to melt, dry, bake or glaze a product. Natural gas is used as a heat source in making glass, steel, cement, bricks, ceramics, tile, paper, food products and many other commodities. Natural gas is also used at many industrial facilities for incineration.

Viwanda vya uzalishaji wa bidhaa hizo hapo juu vitafanya Mtwara kuwa mji wa viwanda kama mh. rais Dr. Jakaya Kikwete alivyoahidi wakati wa kampeni ya uchaguzi 2010 kama utekelezaji wa ilani ya chama cha ccm. Nchi bado itanufaika kwa makusanyo ya kodi lakini pia serikali zetu za mitaa zitanufaika kwa kodi inayotokana na viwanda hivyo kuwepo katika mikoa yetu ya kusini, kutakuwa na ajira za kutosha kwa watanzania wote na Mtwara itakuwa economic hub of Tanzani miaka 15 had 40 ijayo. inakadiliwa kuwa kuwepo kwa viwanda hivyo kutatengeneza nafasi za ajira za moja kwa moja 1,500,000 na zisizo za moja kwa majo 2,84,7000. Mtwara kuchele mwanzo wa mapinduzi ya kifikra.

Lakini watanzania lazima mjuwe pia kwamba Kilagani ambaye ni mtendaji mkuu wa shirika la maendeleo ya petrol Tanzani ndiye chanzo cha mgogoro huu, huyu ameiambia kamati ya ushauri ya Mkoa wa Mtwara katika warsha iliyofanyika katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mtwara tarehe 20/07/2012 kuwa "mafanikio makubwa iliyoyapata TPDC ni kishawishi na kushauri serikali kuihamisha gesi asilia ya Msimbati Mtwara na Songosongo Kilwa kwa kuisafirisha kwa njia ya bomba hadi Dar" yeye kwake haya ni mafanikio makubwa ambayo sasa ni zahama kwa serikali ambayo haiheshimu kauri na ahadi zake, serikali ambayo imeahidi kuwatumikia wananchi wake kwa uadilifu mkubwa.

WanaJF na watanzania ufisadi wa maliasili sasa basi na Mtwara ndo tumelianzisha, inayezadhani kuwa ni swala la kisiasa na umaarufu wa kisiasa aje sasa Mtwara naye aupati huo umaarufu. mimi ni ccm kwa hili hatuna chetu huku, tujipange tena.
 
Siamini kabisa kama kuna usalama wa taifa, ninachokijua kuna uhasama wa taifa na kazi wanayoijua ni kung'oa watu meno na kucha bila ganzi na kuwatupa mabwepande.
 
gesi kutofika dar ni ushirikina?

ndugu zangu musibishe uyu bibi ndiye mmiliki wa lile eneo lililopatikana ile gesi pia mara ya kwanza ndie aliyekasababisha ata hii gesi tunayopiganisasa ibaki ipatikane pasipo yeye pisinge patikana kitu japo waligundua ila msaada wake ata wazungu walikunywa vikombe vya maji ya dawa baada ya kufanyiwa tambiko na huyu bibi,. Na mpaka sasa wale wazungu walimjengea nyumba kubwa na anaishi mpaka sasaiv ivyo serikali imeshagundua kuwa bb uyu ndie kikwazo kwani nae kaapa kama gesi hii ikitoka kwenda dar basi watatoa maji na si ges, sdo atakama nguvu ya dora itatumika kupeleka gesi dar basi mira na desturi zitachukua mkondo wake.
 
Mkuu Chasoda, hata kama hili tukio ni la kweli, I doubt kama huyo mtu ni wa usalama kweli, kwa sababu "modus oparandi" ya usalama sio hiyo!. Ofisa hawezi kutoka Dar straight kwa kibibi hicho!, Wana usalama huwa kwanza wana "exhaust local remedies" kwa kuwatumia locals na kama hakuna, huwa wana "recruit" ndipo wamuingie huyo bibi.

Nimesema hivi kupitia uzoefu wangu enzi nikiwa "mjeda" pale "Airwing chini ya IO".
Pasco.
mkuu tusishangae pengine ndio hawa wana usalama wa mtoto wa mjomba,ba mdogo,binadamu au watoto wa vigogo.ubishoo mwingi na kupenda kuji-show off.ukiwapeleka front line matokeo yake ndio kama haya.but kwa issue ya mtwara mimi nimeifurahia sana tena sana....nilitamanai wamkamate na achapike kweli kweli.
 
Kumbe Tanzania ndiyo huko inaelekea??? Bibi Mshirikina, Afisa usalama mshirikina, aliyemtuma afisa usalama mshirikina, mleta topic mshirikina mwisho tunachangia ushirikina. Aaaagh!
 
inchi inaendeshwa kwa ramli,maamuzi yanafanywa na watabiri.?
 
Kaskazini mjifunze sio kutwa kucha kwenye maandamano ya kupigania wanasiasa uchwara wakati Tanzanite inasafirishwa tu, Nyie mmekazania kumng'oa Meya!

kubwa zima hata aibu halina, watu wanaongea mambo ya maana lenyewe linakuja na ukaskazini...... pambafu!
 
Kaskazini mjifunze sio kutwa kucha kwenye maandamano ya kupigania wanasiasa uchwara wakati Tanzanite inasafirishwa tu, Nyie mmekazania kumng'oa Meya!

Na wa shinyanga nao dhahabu inachukuliwa yanaachwa mashimo tu
 
Ukiona habari kama hii, (yaani haijafanyikia chumbani), afu inakosa picha, ujue ni ya kutunga.
 
bibi ni nani, sidhani kama kijiji kinamilikiwa na mtu mmoja, kama mambo ya ushirikina sawa, otherwise hii changa la macho
 
Back
Top Bottom