Polepole kaumizwa na mwizi aliyemficha yeye mwenyewe

Polepole kaumizwa na mwizi aliyemficha yeye mwenyewe

chief swetu

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2015
Posts
240
Reaction score
246
Kumekucha kumechangamka august-21-2025 tueke kumbukumbu sawa, Bwana HPolepole katuamsha na chupa imejaa chai ya motošŸ”„ balaa.

Binafsi kanifikirisha sana, maana Kuna ile simulizi tulisoma darasa la kwanza/pili miaka ya tisini, kwamba wawindaji walikua wanamtafuta chui mla watu wamuue. Chui alikimbilia kwenye nyumba ya bibi kizee akaomba hifadhi kwa ahadi kwamba kama chui akiepuka kifo Cha wawindaji wale atampa bibi zawadi yoyote atakayo itaka bila kinyongo bibi akakubali kumhifadhi yule chui mla watušŸ™„!

Punde wawindaji wakafika kwa bibi na wakamuuliza bibi yule chui mla watu tumeungana kumsaka tumuue ili sote tuishi kwa amani lakini katupotea ghafla maeneo haya tunaomba ushirikiano wako kama umeona alikoelekea tuelekeze ! Bibi kwa uso mkavu kbs akagoma kutoa ushirikiano na akawa mkali kuwakalipia wawindaji! Wawindaji wakaondoka zao wakamuacha bibi na chui wake ndani.

Ghafla chui akajitokeza sebuleni kwa bibi, akatoa shukrani šŸ™ zake pale. Kisha akamuuliza bibi unataka zawadi gani kama tulivokubaliana? Bibi akajibu hua nina shida sana na ngozi ya chui naomba unipe, yule chui akajawa hasira na akaghadhibika sana akamwambia bibi "wawindaji walitaka kuniua na wewe unataka kuniua " palepale chui alimrarua vibaya yule bibi hakutaka hata kupoteza muda na maisha ya bibi na simulizi ikaishia hapo, lkn hv karibuni nmeona mtandaoni afisa wa polisi akiisimulia na Kuna wachekeshaji wameiigiza mfanano wa simulizi kama hii.

Kwamba afisa wa polisi anamkimbiza muhalifu, muhalifu akaomba hifadhi kwenye gari na mwenye gari kwa chuki zake na wanausalama akampa hifadhi muhalifu, mwanausalama alipofika kwenye gari akaomba ushirikiano kwa mwenye gari ili kujua muhalifu alikoelekea, mwenye gari akamnyima ushirikiano mwanausalama ili kumlinda muhalifu.
Kipindi mwenye gari analumbana na afisa usalama muhalifu akatumia mwanya huo kumuibia Mali mwenye gari zilizokua ndani ya gari alimopewa hifadhi, akatokea upande wa pili na kutokomea kusikojulikanašŸ™„! Afisa wa polisi alivokosa ushirikiano akashika zake njia punde mwenye gari akajuta kwa yaliomkuta.

Sasa ukirejea habari za ndugu HPOLEPOLE na simulizi hizi kwa msomi na kada muandamizi wa kiwango chake kwenye chama/serikali means miaka yote ile kashiriki na kayakumbatia hayo majizi hakutaka tuyajue mpk leo kimemkuta nini akaamua atapike yote ya moyoni? Waliahidiana nini kwenye chama/serikali? Nani kamuomba ngozi mwenzie akaona unataka kuniua bora nikuue ww?

Nawaza kujua kati ya chama/serikali na HPOLEPOLE nani mwenye gari na nani muhalifu kaondoka na Mali baada ya kupewa hifadhi? Siamini kama HPOLEPOLE hajui msemo usemao kisima ulichokunywa maji yake usikitupie mawe! Kisima alichokunywa maji yake(chama/serikali) kimemfanyaje HPOLEPOLE mpk akirushie mawe?

Kuna kilichompata Bw HPOLEPOLE mpk katuamsha na chai ya moto šŸ”„ hivi, vikombe vyenyewe havitoshi anataka tuunguzane bure
 
Samahani ebu weka paragraph, nazingatia alama pia
 
Yeah, yaani watanzania huwa ni bendera fuata upepo, Lowasa alichafiliwa sana na CDM lakini alipotoka CCM walimkumbatia na kumtupilia mbali Dr.Slaa, leo wanamsema Samia lakini angetangaza leo kuhamia kwao atapewa form ya kugombea siku hiyohiyo. Ko tumesahau kabisa uongozi wa Polepole kipindi cha mzee na kumsifu kwa anayoongea leo wakati hayana tija yoyote. Angepewa nafasi aliyokuwa ameandaliwa na mwendazake sidhani kama angethubutu kukesha na press zake za maigizo.
 
Kumekucha kumechangamka august-21-2025 tueke kumbukumbu sawa, Bwana HPolepole katuamsha na chupa imejaa chai ya motošŸ”„ balaa.

Binafsi kanifirisha sana, maana Kuna ile simulizi tulisoma darasa la kwanza/pili miaka ya tisini, kwamba wawindaji walikua wanamtafuta chui mla watu wamuue. Chui alikimbilia kwenye nyumba ya bibi kizee akaomba hifadhi kwa ahadi kwamba kama chui akiepuka kifo Cha wawindaji wale atampa bibi zawadi yoyote atakayo itaka bila kinyongo bibi akakubali kumhifadhi yule chui mla watušŸ™„!

Punde wawindaji wakafika kwa bibi na wakamuuliza bibi yule chui mla watu tumeungana kumsaka tumuue ili sote tuishe kwa amani lakini katupotea ghafla maeneo haya tunaomba ushirkiano wako kama umeona alikoelekea tuelekeze ! Bibi kwa uso mkavu kbs akagoma kutoa ushirkiano na akawa makali kuwakalipia wawindaji! Wawindaji wakaondoka zao wakamuacha bibi na chui wake ndani.

Ghafla chui akajitokeza sebuleni kwa bibi akatia shukrani šŸ™ zake pale Kisha akamuuliza bibi unataka zawadi gani kama tulivokubaliana? Bibi akajibu hua nina shida na ngozi ya chui naomba unipe, yule chui akajaa hasira akamwambia bibi "wawindaji walitaka kuniua na wewe unataka kuniua " palepale chui alimrarua vibaya sana yule hakutaka Wala kupoteza muda na maisha ya bibi na simulizi ikaishia hapo, lkn hv karibuni nmeona mtandaoni afisa wa polisi akiisimulia na Kuna wachekeshaji wameiigiza mfanano wa simulizi kama hii.

Kwamba afisa wa polisi anamkimbiza muhalifu, muhalifu akaomba hifadhi kwenye gari na mwenye gari kwa chuki zake na wanausalama akampa hifadhi muhalifu akamnyima ushirikiano mwanausalama, kipindi mwenye gari analumbana na afisa usalama muhalifu akatumia mwanya huo kumuibia mwenye garišŸ™„! Afisa wa polisi alivokosa ushirikiano akashika zake njia punde mwenye gari akajuta kwa yaliomkuta.

Sasa ukirejea habari za ndugu HPOLEPOLE na simulizi hizi kwa msomi na kada muandamizi wa kiwango chake kwenye chama na serikali means miaka yote ile kashiriki na kayakumbatia hayo machafu hakutaka tuyajue mpk leo kimemkuta nini akaamua atapike yote ya moyoni? Waliahidiana nini kwenye chama/serikali? Nani kamuomba ngozi mwenzie akaona unataka kuniua nakuua ww?

Nawaza kujua kati ya chama/serikali na HPOLEPOLE nani mwenye gari na nani muhalifu? Siamini mtu kama HPOLEPOLE hajui msemo usemao kisima ulichokunywa maji yake usikitupie mawe! Kisima alichokunywa maji yake(chama/serikali) kimemfanyaje HPOLEPOLE mpk akirushie mawe?

Kuna kilichompata Bw HPOLEPOLE mpk katuamsha na chai ya moto šŸ”„ hivi, vikombe vyenyewe havitoshi anataka tuunguzane bure
FB_IMG_1755916364478.jpg
 
Yeah, yaani watanzania huwa ni bendera fuata upepo, Lowasa alichafiliwa sana na CDM lakini alipotoka CCM walimkumbatia na kumtupilia mbali Dr.Slaa, leo wanamsema Samia lakini angetangaza leo kuhamia kwao atapewa form ya kugombea siku hiyohiyo. Ko tumesahau kabisa uongozi wa Polepole kipindi cha mzee na kumsifu kwa anayoongea leo wakati hayana tija yoyote. Angepewa nafasi aliyokuwa ameandaliwa na mwendazake sidhani kama angethubutu kukesha na press zake za maigizo.
Ndio, huyu kuna namna katolewa kwenye meza ya chakula bila kunawa, ss anajaribu kuitigisha na kuwapaka shombo wengine
 
CCM ni majizi yaliyokubuhu ndio maana asilimia kubwa ya miccm inakuaga na mwisho mbaya na familia mbaya

CCM ni majizi yaliyokubuhu ndio maana asilimia kubwa ya miccm inakuaga na mwisho mbaya na familia mbaya
Hawa jamaa cake ya taifa washaifanya ya chama na familia zao, wananchi tumeshikilia mapembe wenyewe wanakamua tu
 
Back
Top Bottom