Mtwara: Gari la 'Afisa Usalama' lapondwa mawe Msimbati

Mtwara: Gari la 'Afisa Usalama' lapondwa mawe Msimbati

kumbe tanzania ndiyo huko inaelekea??? Bibi mshirikina, afisa usalama mshirikina, aliyemtuma afisa usalama mshirikina, mleta topic mshirikina mwisho tunachangia ushirikina. Aaaagh!
ngoma droo!
 
Mawazo yako ya serikali ya ccm kuisusa gesi ni mepesi sana, hata wakiisusa gesi itatoweka ardhni? Na nani kakwambia Kikwete na ccm yake itatawala milele? Au hata CUF,CDM,NCCR wakishika madaraka na wao wataisusa? Tena wakiisusa wamakonde tunatakiwa kufanya sherehe kubwa ya ushind na then tuwashinikize wasuse na kununua korosho kwa mfumo wao wadhuluma. Kwa mawazo yako hayo, ungekuwa bondia basi ni wa uzito wa unyoya.
Ndugu yangu nina uhakika huzijui hujuma za serikali ya CCM. Na hivyo ndivyo ilivyokuwa tangu wakati wa Nyerere, wala siyo kwamba itakuwa ni mara ya kwanza kwa serikali kuususa mkoa au wilaya fulani kutokana na misimamo mikali ya wananchi. Mwisho wa siku wananchi wenyewe wanarudi serikalini kupiga magoti kuiomba serikali iendelee na mpango wake. To my opinion, wanaMtwara wasitumie mabavu sana, badala yake waombe nafasi ya mazungumzo na serikali, na wakubaliane juu ya vipaumbele vyao.
 
CCM inajitengenezea mazingira ya kushindwa 2015.
 
Ndugu yangu nina uhakika huzijui hujuma za serikali ya CCM. Na hivyo ndivyo ilivyokuwa tangu wakati wa Nyerere, wala siyo kwamba itakuwa ni mara ya kwanza kwa serikali kuususa mkoa au wilaya fulani kutokana na misimamo mikali ya wananchi. Mwisho wa siku wananchi wenyewe wanarudi serikalini kupiga magoti kuiomba serikali iendelee na mpango wake. To my opinion, wanaMtwara wasitumie mabavu sana, badala yake waombe nafasi ya mazungumzo na serikali, na wakubaliane juu ya vipaumbele vyao.

Hivi mkuu na huu mwamko wa REPUBLICA DE ........ na waisuse tu kusini. ntapokea kwa mikono miwili ususaji wao.
 
Huyo bibi ndo mwnye kijiji kwan anasadikiwa ana umri wa miaka 116, pia haon. Kukumbuka kwamba mwanzo wanagundua ges wazungu waliingia kiholela bla kubsha hod hatmimae machne zao zlishndwa kutoboa hata punje ya mchanga. Ndo wakaambia kla sehemu kuna mira na destur hivyo kuna mwenye kjij ndo wakapelekwa kwa bb na kuanza kujieleza, hatmay bb akawapa maj wanye na mengne kumwagia kwenye mashne hatmaye kaz ikaanza bla matatzo. Xo serkal inajua hlo ndo maana ina2ma wa2 kumshawsh bb.
 
Huyo bibi hana uwezo wa kuizia hiyo gesi ni wanaMtwara tu kwa umoja wao ndo wanaweza kuizuia huyo bibi sio Mungu hadi aizuie hiyo gesi
 
Huyo bibi ndo mwnye kijiji kwan anasadikiwa ana umri wa miaka 116, pia haon. Kukumbuka kwamba mwanzo wanagundua ges wazungu waliingia kiholela bla kubsha hod hatmimae machne zao zlishndwa kutoboa hata punje ya mchanga. Ndo wakaambia kla sehemu kuna mira na destur hivyo kuna mwenye kjij ndo wakapelekwa kwa bb na kuanza kujieleza, hatmay bb akawapa maj wanye na mengne kumwagia kwenye mashne hatmaye kaz ikaanza bla matatzo. Xo serkal inajua hlo ndo maana ina2ma wa2 kumshawsh bb.

Porojo za vijiweni tu hizo
 
Aisee kwa kweli mambo yanazid kuielemea serikali ya jamuhuri na kwa mising hiyo mi naona wanamtwara kupitia viongoz wake wawashawish vilivyo kamati ya waziri wa nishat na madini kuweza kufikia hitimisho juu ya mali asili hiyo,mi yangu macho tu,lakin pongezi pia kwa bibi huyo.
 
ndugu zangu musibishe uyu bibi ndiye mmiliki wa lile eneo lililopatikana ile gesi pia mara ya kwanza ndie aliyekasababisha ata hii gesi tunayopiganisasa ibaki ipatikane pasipo yeye pisinge patikana kitu japo waligundua ila msaada wake ata wazungu walikunywa vikombe vya maji ya dawa baada ya kufanyiwa tambiko na huyu bibi,. Na mpaka sasa wale wazungu walimjengea nyumba kubwa na anaishi mpaka sasaiv ivyo serikali imeshagundua kuwa bb uyu ndie kikwazo kwani nae kaapa kama gesi hii ikitoka kwenda dar basi watatoa maji na si ges, sdo atakama nguvu ya dora itatumika kupeleka gesi dar basi mira na desturi zitachukua mkondo wake.

Hee,ss yakifika maji ndo watajua chinga noma!
 
This is becoming more serious than we expected. Sasa wananchi wa Mtwara kama hawataki hata majadiliano kwa hiyo sasa wanataka nini? Wamejuaje kama alikuwa amekuja kuwashawishi wazee wa Mtwara wakubali na si kwamba alikuja kujadiliana nao juu ya nini kifanyike?

Mkuu kama ni majadiliano kwa nini yafanyike usiku wa manane tena na wazee fulani tuu?

Kama kweli serikali inataka kufanya majadiliano kwa nini wasifanye mchana kweupe tena na kuwahusisha stakeholders wote?

Kama kweli haya kweli yametokea kwa nini serikali itume watu wa usalama wa taifa kujadiliana na section ya stakeholders?

Kuna usiri gani kwenye hayo majadiliano mpaka yafanyike kisirisiri?

Hapa ni kama serikali ilikuwa inataka kucheza ule mchezo wa "divide and rule" .
 
Mkuu Chasoda, hata kama hili tukio ni la kweli, I doubt kama huyo mtu ni wa usalama kweli, kwa sababu "modus oparandi" ya usalama sio hiyo!. Ofisa hawezi kutoka Dar straight kwa kibibi hicho!, Wana usalama huwa kwanza wana "exhaust local remedies" kwa kuwatumia locals na kama hakuna, huwa wana "recruit" ndipo wamuingie huyo bibi.

Nimesema hivi kupitia uzoefu wangu enzi nikiwa "mjeda" pale "Airwing chini ya IO".

Pasco.

Waliopo kwenye eneo la tukia wanasema hivi. Huyo afisa anaweza akawa ametoka Dar straight kwa sababu kuna allegations kuwa ni mzaliwa wa hapo hapo Msimbati.

Habari hii ni ya kweli kwa mujibu wa mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Msimbati. Pengine nyie mliopo mbali na Mtwara na Msimbambati kwa ujumla hamna habari za kutosha na vyombo vya habari kwa kiasi kikubwa vinapotosha yale yanayojili huku hasa vyombo vya habari vya serikali na ccm, (gezeti la habari leo na uhuru). Bibi yupo na ana umri unaokadiliwa kuwa ni miaka 116 na mtoto wake ambaye anamsaidia kuongea na wageni wote wanaokwenda hapo kwake ana umri wa miaka 70 na wote bado wana nguvu kiakili, hawajapoteza network bado.

Kilichotokea, afisa usalama huyo wa taifa alifika Msimbati jana jioni inayoelekea kuwa usiku kwa nia ya kuonana na bibi ili amchukuwe ampeleke dar, kwa hiyo alikaribishwa hapo nyumbani na mtoto wa huyo bibi lakini afisa usalama alitaka kuongea na bibi huyo kwa faragha hivyo alitaka mtoto wa huyo bibi awapishe, mtoto wa bibi alimwambia afisa usalama kuwa haiwezekani kwani yeye ndiye humsadia bibi kwa mawasiliano yoyote yanayofanywa na wageni wote wanaofika hapo nyumbani, ndipo afisa aliposema amekuja kumchukua bibi anatakiwa dar na viongozi wa serikali, akijibiwa kuwa kutokana na umri wa bibi kuwa mkubwa na hali yake ya kiafya kutokuwa mzuri sana bibi huyo haendi kokote, afisa usalama akasema atwachukuwa wote akaambiwa haiwezekani pia. wakati hayo yakijiri wanakijiji waalianza kujikuasanya hapo nyumbani wengine wakalizinguka gari na wengine wakawa wanafutilia mazungumzo hayo kupitia dirisha la nyumba. afisa akashtuka na kutoka nje kutahamaki akakuta anahojiwa yeye na kila mwanakijiji akawaambia kuwa hawezi kuzungumza na wote alipoona kibano kinazidi na maisha yake yapo hatarini, akatimua mbio, kilichofuata ni wanakijiji kulichoma moto gari lakini afisa usalama amefinikiwa kusepa. Kwa mujibu wa m/kiti wa kijiji anasema afisa huyo ni kijana mzaliwa wa msimbati lakini hajafika hapo msimbati miaka mingi na haishi Mtwara.

Watanzania tunaomba mtambuwe kwamba wakati umefika kuwa wananchi wana haki zote za kunufaika na rasirimali za asili zinazopatikana katika maeneo yao na serikali inawajibu wa kujenga mazingira wezeshi kwa wananchi kunufaika na rasirimali zao, Kama tunavyodai ujenzi wa mtambo wa kufua umeme wa megawatt 300 na kujenga mtambo wa kuchakata gesi hapa Mtwara.

Kujengwa kwa mitambo hiyo kutavutia wajasiriamali wa kimataifa kuja kuwekeza katika viwanda mbalimbali vinavyotumia malighafi (by-product) zinazotokana na gesi asilia, viwanda hivyo ni vya fertilizer, antifreeze, plastics, pharmaceuticals and fabrics. It is also used to manufacture a wide range of chemicals such as ammonia, methanol, butane, ethane, propane and acetic acid. Many manufacturing processes require heat to melt, dry, bake or glaze a product. Natural gas is used as a heat source in making glass, steel, cement, bricks, ceramics, tile, paper, food products and many other commodities. Natural gas is also used at many industrial facilities for incineration.

Viwanda vya uzalishaji wa bidhaa hizo hapo juu vitafanya Mtwara kuwa mji wa viwanda kama mh. rais Dr. Jakaya Kikwete alivyoahidi wakati wa kampeni ya uchaguzi 2010 kama utekelezaji wa ilani ya chama cha ccm. Nchi bado itanufaika kwa makusanyo ya kodi lakini pia serikali zetu za mitaa zitanufaika kwa kodi inayotokana na viwanda hivyo kuwepo katika mikoa yetu ya kusini, kutakuwa na ajira za kutosha kwa watanzania wote na Mtwara itakuwa economic hub of Tanzani miaka 15 had 40 ijayo. inakadiliwa kuwa kuwepo kwa viwanda hivyo kutatengeneza nafasi za ajira za moja kwa moja 1,500,000 na zisizo za moja kwa majo 2,84,7000. Mtwara kuchele mwanzo wa mapinduzi ya kifikra.

Lakini watanzania lazima mjuwe pia kwamba Kilagani ambaye ni mtendaji mkuu wa shirika la maendeleo ya petrol Tanzani ndiye chanzo cha mgogoro huu, huyu ameiambia kamati ya ushauri ya Mkoa wa Mtwara katika warsha iliyofanyika katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mtwara tarehe 20/07/2012 kuwa "mafanikio makubwa iliyoyapata TPDC ni kishawishi na kushauri serikali kuihamisha gesi asilia ya Msimbati Mtwara na Songosongo Kilwa kwa kuisafirisha kwa njia ya bomba hadi Dar" yeye kwake haya ni mafanikio makubwa ambayo sasa ni zahama kwa serikali ambayo haiheshimu kauri na ahadi zake, serikali ambayo imeahidi kuwatumikia wananchi wake kwa uadilifu mkubwa.

WanaJF na watanzania ufisadi wa maliasili sasa basi na Mtwara ndo tumelianzisha, inayezadhani kuwa ni swala la kisiasa na umaarufu wa kisiasa aje sasa Mtwara naye aupati huo umaarufu. mimi ni ccm kwa hili hatuna chetu huku, tujipange tena.
 
This is becoming more serious than we expected. Sasa wananchi wa Mtwara kama hawataki hata majadiliano kwa hiyo sasa wanataka nini? Wamejuaje kama alikuwa amekuja kuwashawishi wazee wa Mtwara wakubali na si kwamba alikuja kujadiliana nao juu ya nini kifanyike? Nafikiri ni wakati mzuri kwa wananchi wa Mtwara kutoa nafasi kwa ajili ya majadiliano.

Niliwahi kuuliza siku moja kwamba hivi wakiendelea kufanya haya wanayoyafanya, halafu serikali ikaamua kughairi kabisa mpango wa ama kupeleka gesi Dar au kujenga mtambo pale Mtwara, badala yake wakaelekeza macho kwenye makaa ya mawe kule Ludewa, wananchi wa Mtwara wataifanyia nini hiyo gesi? Watachota kwenye ndoo na kwenda kuuza au wataifanyeje?

Hoja yao ina msingi, lakini waruhusu majadiliano, kama haiwezekani kujenga mtambo kule basi wakubaliane na serikali terms nyingine zinazoweza kuapply ili na wao wanufaike. Lakini ubabe huu hauna maana kabisa, na unaweza usiwafikishe pazuri kabisa.

acha uoga soma historia vizuri hakuma ukombozi bila damu kumwagika, hapo mtwara lazime damu imwagwe ndo kitaeleweka,,
 
I can't believe this so these our rulers can sink so low mpaka kuanzia kumfuatilia bibi kizee aliyewatisha kuhusu Gesi kugeuka maji,Ndio matokeo yakuongozwa na vichwa vinavyoamini nguvu za majini.......ona sasa wanavyoipeleka inchi pabaya kwa kasi Mimi kwa kweli naogopa,Huko tuendako..........
 
Back
Top Bottom