This is becoming more serious than we expected. Sasa wananchi wa Mtwara kama hawataki hata majadiliano kwa hiyo sasa wanataka nini? Wamejuaje kama alikuwa amekuja kuwashawishi wazee wa Mtwara wakubali na si kwamba alikuja kujadiliana nao juu ya nini kifanyike? Nafikiri ni wakati mzuri kwa wananchi wa Mtwara kutoa nafasi kwa ajili ya majadiliano.
Niliwahi kuuliza siku moja kwamba hivi wakiendelea kufanya haya wanayoyafanya, halafu serikali ikaamua kughairi kabisa mpango wa ama kupeleka gesi Dar au kujenga mtambo pale Mtwara, badala yake wakaelekeza macho kwenye makaa ya mawe kule Ludewa, wananchi wa Mtwara wataifanyia nini hiyo gesi? Watachota kwenye ndoo na kwenda kuuza au wataifanyeje?
Hoja yao ina msingi, lakini waruhusu majadiliano, kama haiwezekani kujenga mtambo kule basi wakubaliane na serikali terms nyingine zinazoweza kuapply ili na wao wanufaike. Lakini ubabe huu hauna maana kabisa, na unaweza usiwafikishe pazuri kabisa.