Mtumishi wa umma atakayekwenda kusomea 'first degree' sasa kuchukua likizo isiyo na malipo

>Mtumishi atakayekwenda kusomea FIRST DEGREE anatakiwa achukue LIKIZO ISIYO NA MALIPO na hastahili kulipwa chochote na Mwajiri wake ikiwa ni pamoja na kutolipwa Mshahara kwakuwa HAYUPO KAZINI.
>Hakuna malipo yoyote ya UHAMISHO kwa Mtumishi atakayehamishwa umbali usiozidi kilometa 10.

View attachment 361929
Safi sana Aliyetoa huu waraka. Watumishi Wa Umma wamefanya taasisi za Umma vyuo vikuu. Badala ya kupewa training wafanye kazi husika wanaondoka kusoma degree 4 years huku wakilipwa mshahara na stahiki zake na kulipiwa ada. Training Programs za taasisi haziko wazi hasa zile za core functions. Ni kusoma tuu hakuna kufanya kazi. Unakuta taasisi I watumishi zaidi ya 50 wako masomo nje na ndani ya nchi wakilipwa mshahara
 
Watu watakuwa hawasomi watu, ila hii habari hai make sense, kwanza barua yenyewe imekaa kama haijatoka wizarani, chafuchafu haina muhuri unaoeleweka
 
Hii mbona ni kama chai.

Barua haina header wala muhuri.
 
Someni hiyo barua then mtoe maoni yenu ...is it fair serikali kutotoa kipaumbele cha watumishi wake kusoma...??
1467387444830.jpg
 
>Mtumishi atakayekwenda kusomea FIRST DEGREE anatakiwa achukue LIKIZO ISIYO NA MALIPO na hastahili kulipwa chochote na Mwajiri wake ikiwa ni pamoja na kutolipwa Mshahara kwakuwa HAYUPO KAZINI.
>Hakuna malipo yoyote ya UHAMISHO kwa Mtumishi atakayehamishwa umbali usiozidi kilometa 10.

View attachment 361929

Barua ya Halmashauri ya NSIMBO.
Huduma wananchi wanapata kupitia Halmashauri ya MPANDA.
Sijaelewa
 
Kakurupuka tena na wakati huo huo yeye anaendelea kukwepa kulipa kodi na mshahara wake wa milioni 400 kwa mwaka.
Aliyekurupuka ni yule aliyehama toka ccm kwenda chadema kwa malipo ya bill.10 akililia urais
 
Ina maana wengi humu sio watumishi wa umma!?mabadiliko ya Sheria za utumishi wa umma na kanuni zake yamefanyika lini.Vyama vya wafanyakaz vinavyolamba 2℅ ya mshahara kwa watumishi kwanini visitolee maelezo au tamko hili kama lipo?taarifa hii ni ya uongo
 
Hii mbona inaonekana kama sio document halali? hata hivyo, tu-assume ni halali; bado hii si ya kitaifa, ni ya kiwilaya; lakini pia inakanganya, kuna sehem inasema mtu atachukua likizo ya bila malipo, pengine inasema mtu atalipwa 90% ya mshahara
Yule ataelipwa 90% ni anaendakusoma shahada ya pili na kuendelea. Lakini anaenda kusoma shahada yakwanza anaomba likizo ya bila malipo. Hii kitu ilianzia Idara ya afya.
 
Hii barua ina mkanganyiko.Hata hivyo kwenye ma-group ya whatsaap kuna habari kama hii inayoonyesha hakuna kulipwa mshahara ukienda kusoma.Niliona hio habari tangu mchana wa leo ila nikasita kuileta hapa maana nilikuwa sina uhakika nayo.

Haina mkanganyiko wowote kama ni halali inaeleweka vizur. Viroba vikiisha tulia soma tena acha papara. Wewe unaunganisha paragrafu zote as if hiyo barua haina nukta wala mkato
 
HII SERIKALI KWANI WALIOAJIRIWA KWA MISHAHARA YA LAKI MBILI WATAWEZA LIPA MILION 9 MIAKA 3 BILA MIKOPO
 
Back
Top Bottom