Uchaguzi 2020 Kwa mambo haya 10, mimi kama Mtumishi wa Umma (mwalimu), John Pombe Magufuli sikupi kura yangu asilani

Mar 6, 2017
33
135
Pamoja na kujipitisha mashuleni kutuomba kura za huruma, mie nimeamua kura yangu sitampa mgombea wa ccm kama nilivyofanya 2015 hii ni kutokana na mambo 10 niliyoyaona kipindi hiki cha miaka mitano

1. Makato ya bodi ya mikopo toka 8% hadi 15% bila sababu maalum tena kwa ubabe.

2. kutunyima nyongeza ya mshahara (annual increment) kwa miaka takribani mitano wakati ni haki ya msingi ya mtumishi.

3. Kutopandishwa daraja mwaka wa 6 huu unakwenda wa 7. Mie nimeajiriwa mwaka 2014 mwezi Aprili, mpaka leo Oktoba 2020 takribani miaka sita imepita huku nikilipwa mshahara wa TGTS D ambao ndio nilioanza nao mwaka 2014 na hata anayeajiriwa leo naye atalipwa hivyohivyo. Halafu wasanii wa bongo fleva wanatanua na kuchezea hela ya serikali kwenye kampeni zako.

4. Kutolipa hela ya likizo kwa wakati. Mfano mie likizo ya malipo nimeenda juni 2017 na juni 2019 JPM ukiwa madarakini, likizo zote nimesafiri toka Lindi hadi Mwanza bila kulipwa hata senti, mwaka huu ndio nimepewa hela ya likizo ya mwaka 2017 tena nusu tu.

5. Hela ya usimamizi wa mitihani ya Taifa kidato cha 4, 2 na 6 kutolipwa yote ya mwaka 2018 na 2019 huku siku za usimamizi (za malipo) kwa wataalamu wa maabala zikishushwa kuanzia mwaka huu toka siku 6 hadi moja.

6. Sheria mpya ya wastaafu ambayo umejifanya Kuibatilisha hadi 2022 ni geresha tu kupisha uchaguzi mkuu huu ufanyike na baada ya hapo kikokotoo kipya kianze kazi. malipo ya mkupuo kwa wastaafu (Lumpsum) kwa Kikokotoo kipya kinataka mstaafu apewe 25% ya mafao yake yote, na 75% zinazobaki apewe kidogokidogo hadi kufa kwake mfano milioni 100 upewe milioni 25 halafu milioni 75 nilipwe kidogokidogo. Mie kama mtumishi hii kwangu haiingii akilini na ili isiniumize ni kukunyima tu kura yangu

7. Ulituahidi Laptop kila mwalimu 2015 lakini muda wako wa awamu ya kwanza unaenda mwishoni bila dalili yoyote ya kupewa hiyo Laptop.

8. Uzalilishaji unaofanywa na wateule wako kama Ma-RC na ma-DC mbele ya wanafunzi wetu na wewe umekuwa kimya. Mfano kutulazimisha kulala kwenye mwenge tena kwa kuitwa majina kama watoto.

9. Ninachangia bima ya afya (3%) kila mwezi halafu dawa za muhimu zimeondolewa na unapoenda hospitali tunalazimika kujinunulia kwa hela yetu.

10. Sababu za Kutoa kufundisha walimu wa masomo ya sanaa wa sekondari kwenda shule za msingi ni za ajabu sana
 
Siyo mwalimu huyo dalali tu, annual increment kila mwaka imekuwa ikiingia. Madaraja walimu tunaostahili tumepandishwa wale waliostahili kupandishwa halafu hawakupandishwa pasipo sababu walipolalamika maafisa utumishi waliwajibishwa.

Acha kudandia taaluma za watu mimi ni mwalimu niko pamoja na Magufuli.Jikite kwenye siasa zako siyo kuwasemea waalimu.
 
Duh laptop kila mwalimu yaani Serikali hata hii sera imewashinda?

Wangeenda tu kwenye mashirika ya misaada Marekani wakaomba laptop laki 3 wangepewa Tena bure


Wangeandika tu proposal vizuri

Ndio maana nasema tuna Serikali ya ovyo Sana kazi yao kukimbizana na wakosoaji wake miaka 5 Sasa imepita duh yaani ni aibu Sana

Mwaka huu tutawafurahisha.
 
We sio mwalimu no kanjanja flani usie jua unacho kiongea natamani ata nikutafune mzima mzima
Kama ni kutetea ugali wako kiivyo umefeli kabisa afu ukute we ni kula kulala hujui ata adha ya kutafuta mkate wa kila siku
Watu wanaugua mafua kila siku unashindwa at a hela ya maziwa we unaleta porojo zako hapa pumbafu kabisa
Siyo mwalimu huyo dalali tu, annual increment kila mwaka imekuwa ikiingia. Madaraja walimu tunaostahili tumepandishwa wale waliostahili kupandishwa halafu hawakupandishwa pasipo sababu walipolalamika maafisa utumishi waliwajibishwa. Acha kudandia taaluma za watu mimi ni mwalimu niko pamoja na magufuli.
Jikite kwenye siasa zako siyo kuwasemea waalimu.
 
We sio mwalimu no kanjanja flani usie jua unacho kiongea natamani ata nikutafune mzima mzima
Kama ni kutetea ugali wako kiivyo umefeli kabisa afu ukute we ni kula kulala hujui at a aza kutafuta mkate wa kila siku
Watu wanaugua mafua kila siku unashindwa at a hela ya maziwa we unaleta porojo zako hapa pumbafu kabisa
Bila shaka wewe ni mwanafunzi wangu na ulikuwa mbumbumbu ukazungusha.
 
Kila kundi lina hoja zake,wafanyabiashara, vijana wasio na ajira ,huduma duni za afya bora hata JK walitoa tip dawa zikapatikana sasa ni orodha kuanzia gloves,nyuzi,drip nk mbali ya bima za kawaida,Lissu tuokoe.
 
Back
Top Bottom