Msamaha wa Ushuru kwa Watumishi wa Umma

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
1.0 Utangulizi

Kipeperushi hiki kinatoa maelezo kuhusu taratibu muhimu ambazo watumishi wa umma wanatakiwa kuzingatia wanapohitaji msamaha wa ushuru kwenye vyombo vya usafiri (Magari na pikipiki). Maelezo haya yanazingatia sheria husika za kodi pamoja na Matangazo ya Serikali yaani GN. Na. 520 na 522 za mwaka 1995.

2.0 Lengo la msamaha wa ushuru kwa watumishi wa umma

Lengo la msamaha wa ushuru kwenye vyombo vya usafiri kwa watumishi wa umma ni hatua za makusudi zilizochukuliwa na Serikali katika kuboresha ufanisi katika utendaji kazi kwa kuwasaidia usafiri hususani kwenda kazini na kurudi nyumbani kwao.

3.0 Maana ya Mtumishi wa Umma.

Mtumishi wa umma ni mtu ambaye anashika ofisi ya umma kwa kuteuliwa, kuchaguliwa au yuko kwenye mkataba wa ajira katika Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, Taasisi na wakala za Serikali ikiwa ni pamoja na Mashirika ya Umma. Shirika la umma ni lile ambalo asilimia 50% au zaidi ya matumizi yake yanatokana na ruzuku ya Serikali. Asasi na taasisi zingine zisizo za kiserikali hazihusiki na utaratibu huu kwa mujibu wa sheria.

Mtumishi wa umma ambaye kwa mujibu wa sheria anafaidika na msamaha wa ushuru katika vyombo vya usafiri ni yule mwenye ngazi ya mshahara ya TGS D au zaidi kwa upande wa Serikali au inayolingana na hiyo kwa upande wa Taasisi zingine za Serikali na mashirika ya umma.

4.0 Aina ya vyombo vya usafiri vinavyohusika na msamaha

Kwa mujibu wa sheria, vyombo vya usafiri vinavyohusika na msamaha huu bila kujali kama chombo kimenunuliwa hapa nchini au nje ni hivi vifuatavyo:-

(a) Magari

• Magari madogo aina ya saloon.
MISAMAHA YA MAGARI WATUMISHI WA UMMA.indd 2
• Magari aina ya pick – up yenye uwezo wa kubeba mzigo usiozidi uzito wa tani mbili.
• Magari mengine ambayo hayabebi zaidi ya abiria tisa.
• Gari lenye ujazo wa injini usiozidi 3,000.
• Gari lenye umri chini ya miaka kumi tangu lilipotengenezwa bila kujali miezi.

(b) Pikipiki za aina zote.

5.0 Ushuru unaosamehewa
Mtumishi wa umma ambaye ametimiza masharti yote yanayotakiwa kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa anasamehewa kulipa ushuru wa forodha (import duty) tu. Kodi na ada zingine kama Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), ushuru wa bidhaa (Excise duty) na ada za usajili atatakiwa kulipa.

Zingatia: Mtumishi wa umma akinunua gari lenye umri wa miaka kumi au zaidi toka kutengenezwa hatapata msamaha kabisa.

6.0 Masharti ya kuzingatia kwa mtumishi wa umma.

Ikumbukwe kuwa Serikali ina nia njema kwa watumishi wake kutoa upendeleo kwao kwa njia ya msamaha wa ushuru wa forodha kwenye vyombo vya usafiri. Hivyo ni vema masharti yafuatayo yakazingatiwa: -

(a) Kibali cha msamaha kinachotolewa ni kwa ajili ya mtumishi wa umma anayehusika na sio mtu mwingine yoyote. Ni kosa kisheria kwa mtu yeyote asiye husika kufaidika na msamaha huu, na wala chombo cha usafiri chenye msamaha wa ushuru hakiruhusiwi kutumika kwa shughuli za biashara.

(b) Msamaha utasitishwa na ushuru uliosamehewa utatakiwa kulipwa mara moja iwapo mtumishi wa umma ataacha kuwa mtumishi wa umma kabla ya miaka minne kupita tangu tarehe ya kupewa msamaha, au iwapo atahamisha umiliki au kuuza chombo hicho cha usafiri kwa mtu mwingine.

(c) Msamaha utatatolewa kwa chombo kimoja tu cha usafiri katika kipindi cha miaka minne. Baada ya muda huo kupita, mtumishi wa umma anaruhusiwa kuomba msamaha mwingine, lakini ni lazima ushuru ulipwe kwa chombo cha usafiri cha zamani kwa kiwango cha uthaminishaji kama ilivyoainishwa na Idara ya Forodha. Thamani itakayotumika kukokotoa kodi husika ni thamani ya chombo hicho wakati kilipoingia nchini; mmiliki anapaswa kutunza nyaraka zote za chombo hicho cha usafiri vizuri.

Hivyo basi, ili mtumishi wa umma astahili kupewa msamaha mwingine baada ya miaka minne kupita ni lazima aambatanishe maombi yake na stakabadhi ya malipo ya ushuru kwa ajili ya chombo cha usafiri cha zamani toka TRA

7.0 Watumishi wa umma ambao wako masomoni

Mtumishi wa umma ambaye anaendelea na masomo yake hapa nchini au nje ya nchi haruhusiwi kupewa msamaha wa ushuru hadi pale atakapomaliza masomo yake na akaendelea na utumishi wa umma.
Isipokuwa mtumishi wa umma anayesoma nje ya nchi anaweza kutumia msamaha wa mkazi anayerejea nchini(returning resident) iwapo ameishi nje ya nchi miezi kumi na mbili au zaidi na chombo hicho cha usafiri amekimiliki kwa miezi kumi na mbili au zaidi.

8.0 Taratibu muhimu za kufuata
Kujaza fomu ya maombi (Nakala nne) ambayo ni lazima iwe na viambatanisho vifuatavyo:-

(a) Magari yanayoagizwa toka nje ya Nchi
i. Barua ya utambulisho toka kwa mwajiri, ii. Salary Slip ya mwezi wa karibu,
iii. Barua ya kuajiriwa kazini/Barua ya kupandishwa
Cheo, iv. Nakala ya kitambulisho cha kazi,
v. Anatakiwa pia kuambatanisha picha nne (4) za
“passport size “kwenye fomu ya maombi,

vi. Kuambatanisha namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN), vii. Kumbukumbu za ununuzi au uingizaji wa chombo husika cha usafiri hapa nchini.

4/15/2013 4:33:27 PM
 

Attachments

  • Msamaha wa ushuru kwa vyombo vya usafiri kwa watumishi wa umma.pdf
    463.1 KB · Views: 100
Wazee wa vi8 orijino, wanaingia Tu pale Toyota wanaondoka na gari, huku wakiwaachia vijakazi wakikimbizana na milolongo ya makaratasi?
 
Back
Top Bottom