Mtumishi wa umma atakayekwenda kusomea 'first degree' sasa kuchukua likizo isiyo na malipo

Chinga One

JF-Expert Member
May 7, 2013
11,471
12,373
>Mtumishi atakayekwenda kusomea FIRST DEGREE anatakiwa achukue LIKIZO ISIYO NA MALIPO na hastahili kulipwa chochote na Mwajiri wake ikiwa ni pamoja na kutolipwa Mshahara kwakuwa HAYUPO KAZINI.
>Hakuna malipo yoyote ya UHAMISHO kwa Mtumishi atakayehamishwa umbali usiozidi kilometa 10.

1467384890217.jpg
 
Habari yenyewe haina muhuri, alafu kama sijaona vizuri ni ya kutoka wilaya moja, hii haiwezi kuwa ya taifa, sidhani kama tunapaswa kuitilia maanani, hadi hapo mamlaka za juu zitakapotoa ukweli wa hii
 
Hii haiko sawa....siamini kama ni sahihi sana hasa kama mtu anaenda kujiendeleza kwa faida ya mwajiri na yy binafsi...at least angepewa nusu mshahara basi....unajua kusoma na utu uzima...kuna majukumu mengi sana yanakuhitajia....i am just thinking anyway!
Ni kweli kaka hii kitu wamekurupuka ama hawataki watu wakasome kabisa
 
Hivi wewe uliendika uliisoma barua ama umekimbilia kupost tu. Maana barua inaonesha atalipwa 90% ya mshahara ww unasema hakuna mshahara,
 
Hivi wewe uliendika uliisoma barua ama umekimbilia kupost tu. Maana barua inaonesha atalipwa 90% ya mshahara ww unasema hakuna mshahara,
Hii barua ina mkanganyiko.Hata hivyo kwenye ma-group ya whatsaap kuna habari kama hii inayoonyesha hakuna kulipwa mshahara ukienda kusoma.Niliona hio habari tangu mchana wa leo ila nikasita kuileta hapa maana nilikuwa sina uhakika nayo.
 
Sheria za utumishi wa umma hazijasema hayo.
Halafu kujiendeleza kielimu ni haki ya mumishi wa umma. Pia rikizo bila malipo zimezuiliwa!! Mwisho kabisa haiwezekani vitu kama hivyo kazi bila carrer development ni uongo wa asububi kweupeeee
 
Walimu wa diploma inakuwaje? Diploma za ufundi; FTCs, diplomas mbali mbali zilizoko kwenye ajira inakuwaje? Hawa wamenyumwa kabisa fursa za kujiendeleza? Sijaelewa.
 
Hii mbona inaonekana kama sio document halali? hata hivyo, tu-assume ni halali; bado hii si ya kitaifa, ni ya kiwilaya; lakini pia inakanganya, kuna sehem inasema mtu atachukua likizo ya bila malipo, pengine inasema mtu atalipwa 90% ya mshahara
 
Back
Top Bottom