Mtumishi wa umma atakayekwenda kusomea 'first degree' sasa kuchukua likizo isiyo na malipo

wizara ya Afya si ajabu watasitisha kughalamia masomo kwa watumishi wanaojiendeleza,naona kama vile tamko lipo njiani linakuja
 
Fanya mambo JPM maana nilikuwa nikishangaa sana mtumishi anachukua mshahara na bado hapo hapo anapata mkopo wa board..wacha tuisome number wote..
Mkuu haujaelewa hivi vitu viko kwa mujibu wa sheria na iliyotoa tangazo hilo ni halimashauri mkuu?Usiwe na wivu huu ni utaratibu kwa kuzingatia Kanuni za utumishi wa uma mkuu
 
>Mtumishi atakayekwenda kusomea FIRST DEGREE anatakiwa achukue LIKIZO ISIYO NA MALIPO na hastahili kulipwa chochote na Mwajiri wake ikiwa ni pamoja na kutolipwa Mshahara kwakuwa HAYUPO KAZINI.
>Hakuna malipo yoyote ya UHAMISHO kwa Mtumishi atakayehamishwa umbali usiozidi kilometa 10.
Wenye Mamlaka ya kusema hivi ni Ofisi ya Rais Menejimenti na Utumishi wa umma na kujiendeleza ni haki ya Mtumishi na ipo katika muundo wa utumishi ila sijajua hii Wilaya inatumia vigezo gani?
 
Tanganzo rasmi ni lazima litoke kwa Katibu Mkuu utumishi kitu ambacho sikiono hapa. Au tuseme kuna waraka ambao upo? Angetakiwa katika tangazo lake hilo arejee waraka huo wa utumishi ambao unakataza hivyo.
 
Jf siku hizi inawatu wa ajabu kama facebook..
Ni hivi ukitaka kwenda kusoma bachelor degree ndo unaomba likizo bila malipo....na penyewe uwe umekaa kituo kimoja cha kazi kwa miaka mitatu au zaidi..
Wale ambao wanaenda kusomea masters au zaidi hao ndo watalipwa 90% ya mshahara wao..

Kama hujamliza miaka mitatu kazini na unataka kujiendeleza basi unaruhusiwa kusoma lakini usome chuo kikuu huria huku ukiwa kazini

Huo waraka ni wa wilay moja lakini kitu kama hicho hakiwezi kuwa cha halmashauri moja ila ni maagizo toka utumishi makao makuu na kila halmashauri inajulisha watumishi wake kwa wakati wake
 
Huo waraka ni wa wilay moja lakini kitu kama hicho hakiwezi kuwa cha halmashauri moja ila ni maagizo toka utumishi makao makuu na kila halmashauri inajulisha watumishi wake kwa wakati wake
Hilo ni agizo la Wilaya Mkuu , Utumishi hawajatoa huo waraka na ni easy tu kumchalenge huyo Afisa utumishi kwa kufuata kanuni za utumishi wa uma, standing orders na muundo wa ajira yako
 
Hii barua naona inakasoro kuu tatu

1. Hii ni mahsusi kwa halmashauri moja; hivyo tutahitaji taarifa toka ngazi ya taifa
2. Paragraph ya kwanza na ya pili either hazieleweki au zinataarifa zisizojitosheleza
3. Hata kama ningekuwa mtumishi wa halmashauri hii bado hii barua inakosa sifa ya kuwa official (serious document) coz haina mhuri

Nimawazo Yangu nipo tayari kurekebishwa
 
Habari yenyewe haina muhuri, alafu kama sijaona vizuri ni ya kutoka wilaya moja, hii haiwezi kuwa ya taifa, sidhani kama tunapaswa kuitilia maanani, hadi hapo mamlaka za juu zitakapotoa ukweli wa hii
Sema nembo ya halmashauri husika mhuri kwa tangazo kama hilo silazima
 
Hivi wewe uliendika uliisoma barua ama umekimbilia kupost tu. Maana barua inaonesha atalipwa 90% ya mshahara ww unasema hakuna mshahara,
wewe ndio hauelewi mkuu.Huyo wa 9o% ni yule anayejiendeleza zaidi ya bachelor na anatakiwa awe amemaliza miaka 3 katika kituo cha kazi.
 
Huu waraka haujasainiwa na Tamisemi bali umesainiwa kwa niaba yako Mkurugenzi mtendaji wilaya ya Nsimbo. Hii halmashsur ipo wapi? Hili sio swala la kitaifa, acheni uchonganishi. Oooooohhhhoooo!!
 
Kwahiyo inamaana hata mtu mwenye diploma ya engineering akitaka kujiendeleza atasoma kupitia Open University??
Kweli kila zama na kitabu chake!!
Hapo ndo na mm sielewi mana Chuo Kikuu Huria hakina kozi za kada zote. "Government works on papers", ngoja tusubiri waraka kwanza.
 
D
Kwahiyo inamaana hata mtu mwenye diploma ya engineering akitaka kujiendeleza atasoma kupitia Open University??
Kweli kila zama na kitabu chake!!
E-learning in biomedical engineer ,tellecomunication engineering du sipati picha elimu itakavyokuwa ngumu
 
Back
Top Bottom