Mtumbuizaji kupewa bendera ya Taifa!

Una mawazo mazuri lakini waziri hawezi kuifanya timu ya taifa ikapata uwakilishi kwenye mashindano hayo. Serikali imetengeneza mazingira ya viwanja. Usimamizi wa timu na wachezaji sio wa serikali bali ni wadau wa michezo. Kwa hiyo Serikali imetekeleza majukumu yake kilichobaki ni viongozi wa soka na wadau. Diamond kama msanii anafahamika kuwa anatoka Tanzania na ameing'arisha nchi kuliko wasanii wengine. Kama ameonekana AFCON ni juhudi zake binafsi ndizo zimemfanya aonekane. Kuna wanamuziki wengi sana Tanzania lakini wakishapata umaarufu kidogo wanaanza kuingia kwenye bifu. Wanaanzisha ugomvi ambao hauna maana. Kuna mtu mmoja nilimsikia akisema diamond ni mfanya burudani lakini sio mwanamuziki. Kwa kauli hiyo ni lazima huyu mtu atakuwa anafikiria diamond ashuke ili yeye apande.
 
Umenena
 
Umechemka mkuu.lazima kuwe na tofauti.unampa bendera anayeenda kushindana au kusherehesha?(entertainment)
 
hapana , huwezi kufix kitu kila kumpa onyo mlengwa.
Mimi nadhani diamond akienda kufanya vizuri.
baada ya hapo Watajirekebisha
. hapo ndipo atakapoanza michakato ya kuwaweka saw a!
Mimi nadhani haya tuyafikiriayo Mimi na wewe ,yeye yuko one Step ahead

halafu sio kilaPresident Ana interest ya michezo na burudani.
nadhani baba yetu tunamjua
hataki ujinga ujinga[emoji23][emoji23]
yeye Ana interest na ujenzi tu.
 
Kwa pamoja tumpongeze Mond kwanza kisha tuulizane je ni taifa lililomfikisha hapo au jitihada binafsi. Sisi je tumefanya nini kinachoweza kututangaza? Vinginevyo mkuu nahisi tumechagua kuwa walalamishi tu.hata mpira wakifanya vema tutasema mbona utalii bado,mbona elimu siyo,mbona filamu zetu nk.
 
Kama soka limeshindwa kuitambulisha Taifa, wacha Diamond akaiwakilishe Taifa..
 
kweli hana interest na michezo labda lakini waziri wake angalau ajiongeze ili tupate wawakilishi huko! Baba anataka ndege na kazi tu
 
Umeandika point mkuu!!Labda mleta mada alitaka kibakuli mzee wa tour dunia nzima ndio apewe bendera
 
Bendera anastahili kupewa mtanzania yoyote anafanya vzur kweny tasnia yoyote endapo atapata nafas ya kutuwakilisha. Mtu makin angetoa kwanza sifa za mtu anaestahil kupewa bendera ndipo aanze kukosoa. Kijana anafanya vizuri na ni mtanzania
 
Bendera anastahili kupewa mtanzania yoyote anafanya vzur kweny tasnia yoyote endapo atapata nafas ya kutuwakilisha. Mtu makin angetoa kwanza sifa za mtu anaestahil kupewa bendera ndipo aanze kukosoa. Kijana anafanya vizuri na ni mtanzania
Point mkuu
 
Umeandika point mkuu!!Labda mleta mada alitaka kibakuli mzee wa tour dunia nzima ndio apewe bendera
ili ujue mtu katoa point lazima wewe binafsi uwe na point na ujue maudhui ya mada. RICKY MARTIN MFARANSA Ali perform kwenye fainali za kombe la Dunia na kuachia kibao kinachopendwa mpaka kesho la copa de la vida.lakini hakubeba bendera ya Ufaransa.HAPA KAZI TU. Leta data usiongee tu pumba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…