BASATA: Diamond amestahili kukabidhiwa bendera ya Taifa kwa ajili ya show ya ufunguzi wa AFCON 2017

Maboso

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
5,164
5,762

Kumekuwa na sitofamu katika mitandao ya kijamii kuhusu ni nani anastahili kukabidhiwa bendera ya Taifa ili kuwakilisha nchi, baada ya Diamond Platnumz kukabidhiwa bendera ya Taifa jana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye kwajili ya show yake ya kutumbuiza ufunguzi wa michuano ya Afcon 2017 inayofanyikia nchini Gabon weekend hii.

tmp_22785-1-51271028487.jpg

Mashabiki wengi katika mitandao hiyo wamekuwa wakizozana bila kupata jibu kwamba ni kwanini Daimond alikabidhiwa bendera hiyo kwa ajili ya kuwakilisha Tanzania wakati anaenda kufanya show yake binafsi.

Akiongea na Bongo5 Alhamisi hii kuhusu suala hilo Katibu mkuu wa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) Godfrey Mngereza amesema bendera ya Taifa anaweza kupewa mtu yeyote ambaye anaenda nje ya nchi, na safari yake ina manufaa kwa taifa lake.

“Suala wa Waziri Nape ambaye ndiye Waziri mwenye dhamana ndani ya Wazira wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kumkabidhi Diamond bendera ya Taifa ni jambo zuri kwa sababu ingawa Diamond anakwenda kufanya show yake lakini tukumbuke yule ni mtanzania pekee pale ambaye anakwenda kuliwakilisha Taifa lake kwa show yake mbele ya maelfu ya watu Afrika nzima, jina lake linatambulika pale lakini wao wanamtambua yule kama mtanzania na hata akifanya vizuri sifa zinaenda kwa yeye pamoja na Taifa lake,” alisema Nngereza.

Pia Nngereza alidai mtanzania yeyote anaweza kukabidhiwa bendera ya katifa kama anaenda kufanya tukio lolote ambalo linaweza kuipatia sifa nchi yake kwa namna yoyote.

“Mtu yoyote ambaye anaenda nje ya nchi kwa ajili ya matamasha makubwa au kama kuna namna ambavyo anaenda kufanya kitu ambacho kimpatia yeye faida pamoja na Taifa lake anaweza kukabidhiwa bendera, awe mtanzania tu. Kwa hiyo hata ukiwa mtangazaji, mchezaji, vikundi vya ngoma na sanaa mbalimbali wanaweza kukabidhiwa bendera kama wakihiitaji kwa sababu kuna wengine hawatoi taarifa kuhusu matukio yao lakini kama ukitoa taarifa na mamlaka ikaona kuna umuhimu wa kufanya tunafanya hivyo kwa sababu ni kwa ajili ya taifa letu,”
 
Naona ili jambo limekuzwa na watu ambao kwa makusudi hawakutaka kumuelewa Ridhiwani Kikwete....
Ridhiwani kikwete aliandika vile kuwa challange TFF kuhusu Taifa stars..maana ingependeza kama Taifa stars wangelikuwa nao ni wamoja wanao kabidhiwa bendera ya Taifa kama ilikuwa kwa Diamond jana...

Pia nimesikitishwa jinsi Babu tale na Mkubwa Fella walivyo react kiasi kwamba wamekuwa kama watoto vile yani kama vile Ridhiwani ana muonea wivu Diamond...Ni vyema Mameneja wakawa si wepesi wakudandia na kupost mambo kabla ya kutafakari na si lazima kila jambo lazima Meneja uliongelee.... kwakweli nimekuwa disapointed sana na utoto wa Babu Tale na Fella.... Sioni sababu ya Ridhiwani kumuonea wivu Diamond.
 
Hivi watanzania mna nini cha kujivunia au kitu gani cha kuwatanganza kama taifa??!!! Ukiachana na matusi mnayotukana kwenye pages za watu mitandaoni mna nini kingine cha kuwatangaza kama taifa??!!!! Acheni upumbavu ninyi!!
 
Tatizo sio mameneja. Tatizo liko kwa riziwan. Hakuwa na sababu ya kutoa maoni yale. Hata kama angeyatoa hakutakiwa kuyatoa kwa kujichanganya kiasi cha kutoeleweka kwa jamii.
 
Naona ili jambo limekuzwa na watu ambao kwa makusudi hawakutaka kumuelewa Ridhiwani Kikwete....
Ridhiwani kikwete aliandika vile kuwa challange TFF kuhusu Taifa stars..maana ingependeza kama Taifa stars wangelikuwa nao ni wamoja wanao kabidhiwa bendera ya Taifa kama ilikuwa kwa Diamond jana...

Pia nimesikitishwa jinsi Babu tale na Mkubwa Fella walivyo react kiasi kwamba wamekuwa kama watoto vile yani kama vile Ridhiwani ana muonea wivu Diamond...Ni vyema Mameneja wakawa si wepesi wakudandia na kupost mambo kabla ya kutafakari na si lazima kila jambo lazima Meneja uliongelee.... kwakweli nimekuwa disapointed sana na utoto wa Babu Tale na Fella.... Sioni sababu ya Ridhiwani kumuonea wivu Diamond.

Mkuu wamefanyaje hao? Tumegee kidogo mkuu
 
Mkuu post ya Ridhiwan ni ya kijinga na iliyojaa dharau na kejeli. Alikuwa na namna nyingi nzuri tu za kuwachallenge TFF na si kama alivyofanya.
 
Naona ili jambo limekuzwa na watu ambao kwa makusudi hawakutaka kumuelewa Ridhiwani Kikwete....
Ridhiwani kikwete aliandika vile kuwa challange TFF kuhusu Taifa stars..maana ingependeza kama Taifa stars wangelikuwa nao ni wamoja wanao kabidhiwa bendera ya Taifa kama ilikuwa kwa Diamond jana...

Pia nimesikitishwa jinsi Babu tale na Mkubwa Fella walivyo react kiasi kwamba wamekuwa kama watoto vile yani kama vile Ridhiwani ana muonea wivu Diamond...Ni vyema Mameneja wakawa si wepesi wakudandia na kupost mambo kabla ya kutafakari na si lazima kila jambo lazima Meneja uliongelee.... kwakweli nimekuwa disapointed sana na utoto wa Babu Tale na Fella.... Sioni sababu ya Ridhiwani kumuonea wivu Diamond.
Mi naiona, hambebei kamzigo. Mjeuri sana dogo.
 
hivi watanzania mna nini cha kujivunia au kitu gani cha kuwatanganza kama taifa??!!! ukiachana na matusi mnayotukana kwenye pages za watu mitandaoni mna nini kingine cha kuwatangaza kama taifa??!!!! acheni upumbavu ninyi!!
Faru John

Singeli

Vigodoro

Majungu 10000 tons

Mchiriku

Taarab

Mwendokasi
 
Tatizo sio mameneja. Tatizo liko kwa riziwan. Hakuwa na sababu ya kutoa maoni yale. Hata kama angeyatoa hakutakiwa kuyatoa kwa kujichanganya kiasi cha kutoeleweka kwa jamii.
HAYO MAONI AMEYATOA KWENYE MTANDAO GANI.MKUU!?
 
Naona ili jambo limekuzwa na watu ambao kwa makusudi hawakutaka kumuelewa Ridhiwani Kikwete....
Ridhiwani kikwete aliandika vile kuwa challange TFF kuhusu Taifa stars..maana ingependeza kama Taifa stars wangelikuwa nao ni wamoja wanao kabidhiwa bendera ya Taifa kama ilikuwa kwa Diamond jana...

Pia nimesikitishwa jinsi Babu tale na Mkubwa Fella walivyo react kiasi kwamba wamekuwa kama watoto vile yani kama vile Ridhiwani ana muonea wivu Diamond...Ni vyema Mameneja wakawa si wepesi wakudandia na kupost mambo kabla ya kutafakari na si lazima kila jambo lazima Meneja uliongelee.... kwakweli nimekuwa disapointed sana na utoto wa Babu Tale na Fella.... Sioni sababu ya Ridhiwani kumuonea wivu Diamond.
4130c5ed0198afab099cdc83936e60b9.jpg

Utoto gani sasa hapo kafanya mkubwa fella au nini kibaya kaandike hapo
 
Back
Top Bottom