Maboso
JF-Expert Member
- Feb 18, 2013
- 5,164
- 5,762
Kwanza nitoe muongozo kwamba kwa nini hii habari nimeweka huku badala ya jukwaa la celebrities au entertainment. Nimeweka huku kwa sababu ni swala linalohusu utambulisho wa utaifa na si burudani wala umaarufu. Katika pitapita yangu kwenye mitandao ya kijamii nimekutana na hii post ya Mhe Ridhiwan Kikwete. Post ilivyokaa ni kama huyu mheshimiwa hakubaliani na suala la msanii Diamond kukabidhiwa bendera ya taifa. Ninaombeni kujua kutoka kwenu wataalamu wa siasa na utaifa, mwenye haki ya kukabidhiwa bendera ya taifa anapokwenda nje ya nchi ni nani au ni sekta ipi ya michezo au sanaa? Naomba tujadili katika fikra ya utaifa na si katika fikra ya chama fulani au mapenzi kwa mwanamziki fulani.