Mtu mmoja anadaiwa kupigwa risasi na kuuawa na polisi huku watatu wakijeruhiwa akiwemo polisi wakati polisi wakikabiliana na wananchi mkoani Kigoma

Msitari wa pambizo

JF-Expert Member
Sep 25, 2014
2,880
4,883
Tukio hilo limetokea leo Siku ya Jumapili katika kijiji cha Malagarasi kilichopo wilayani Uvinza mkoa wa Kigoma.

Ilikuwa hivi

Polisi walipata habari kuwa katika kijiji hicho wamekuja watu wanaowaumbua wachawi maarufu kama KAMCHAPE hivyo polisi walifika katika kijiji hicho ili kuwazuia.

Taarifa zinasema kuwa polisi walitapakaa maeneo ya kijiji hicho huku wakipiga mabomu kuwazuia wananchi wasizagae maeneo ya kijiji. Kwa sababu polisi walivamia maeneo ya sokoni ambayo yana watu wengi kulitiokea taharuki iliyopeleke vurugu kubwa zilizotokana na makabiliano ya polisi na wananchi.

Katika makabaliano hayo polisi walitumia risasi za moto na kuwapiga watu watatu ambao kati yao mmoja amefariki dunia. Wakati huo huo wakati polisi akiwa anaseti bunduki yake naye alijikuta kwa bahati mbaya bunduki ikamfyatukia na kumpiga mguuni hivyo na yeye kujeruhiwa mguuni.

Baada ya tukio hilo wananchi waliuchukua mwili wa aliyefariki na kuupeleka kwa mwenyekiti wa kijiji wakimtuhumu kushirikiana na polisi kuwabugudhi wananchi ambao hata hawahusiki wala hawajui kuhusu mambo hayo huku wanaofanya mambo hayo wako mbali kabisa wanaendelea na shughuli hizo

Mpaka wakati naingia mitamboni naambiwa wananchi wamezingira nyumba ya wageni ambayo inasemekana polisi wako humo.

My take.

Huu mkoa wa Kigoma umekuwa na imani za ushirikina sana nafikiri elimu zaidi inatakiwa. Lkn pia najiuliza kwa nini polisi watumie nguvu kubwa kiasi hicho mpaka kutumia risasi za moto.
 
Wachawi na waganga wa kienyeji ndo mtaji wa watawala kipindi cha uchaguzi maana hupishana Kwa waganga je wakimalizwa na kamchape wanahofu kurudi madarakani hivyo hawatakubari kamchape achezee chanzo Chao cha madaraka
 
Tafuteni petrol hapo pigeni kibiriti hiyo nyumba waliyojificha polisi
 
Tukio hilo limetokea leo Siku ya Jumapili katika kijiji cha Malagarasi kilichopo wilayani Uvinza mkoa wa Kigoma.

Ilikuwa hivi

Polisi walipata habari kuwa katika kijiji hicho wamekuja watu wanaowaumbua wachawi maarufu kama KAMCHAPE hivyo polisi walifika katika kijiji hicho ili kuwazuia.

Taarifa zinasema kuwa polisi walitapakaa maeneo ya kijiji hicho huku wakipiga mabomu kuwazuia wananchi wasizagae maeneo ya kijiji. Kwa sababu polisi walivamia maeneo ya sokoni ambayo yana watu wengi kulitiokea taharuki iliyopeleke vurugu kubwa zilizotokana na makabiliano ya polisi na wananchi.

Katika makabaliano hayo polisi walitumia risasi za moto na kuwapiga watu watatu ambao kati yao mmoja amefariki dunia. Wakati huo huo wakati polisi akiwa anaseti bunduki yake naye alijikuta kwa bahati mbaya bunduki ikamfyatukia na kumpiga mguuni hivyo na yeye kujeruhiwa mguuni.

Baada ya tukio hilo wananchi waliuchukua mwili wa aliyefariki na kuupeleka kwa mwenyekiti wa kijiji wakimtuhumu kushirikiana na polisi kuwabugudhi wananchi ambao hata hawahusiki wala hawajui kuhusu mambo hayo huku wanaofanya mambo hayo wako mbali kabisa wanaendelea na shughuli hizo

Mpaka wakati naingia mitamboni naambiwa wananchi wamezingira nyumba ya wageni ambayo inasemekana polisi wako humo.

My take.

Huu mkoa wa Kigoma umekuwa na imani za ushirikina sana nafikiri elimu zaidi inatakiwa. Lkn pia najiuliza kwa nini polisi watumie nguvu kubwa kiasi hicho mpaka kutumia risasi za moto.
si wawaache tu hao waya na uchawi wao, kama wachawi kwa wachawi wakiwa wanaafichuana uchawi shida ni nini? wakishindwana ndio polisi iingilie kati. waacheni wafu wazikane wao kwa wao.
 
Tukio hilo limetokea leo Siku ya Jumapili katika kijiji cha Malagarasi kilichopo wilayani Uvinza mkoa wa Kigoma.

Ilikuwa hivi

Polisi walipata habari kuwa katika kijiji hicho wamekuja watu wanaowaumbua wachawi maarufu kama KAMCHAPE hivyo polisi walifika katika kijiji hicho ili kuwazuia.

Taarifa zinasema kuwa polisi walitapakaa maeneo ya kijiji hicho huku wakipiga mabomu kuwazuia wananchi wasizagae maeneo ya kijiji. Kwa sababu polisi walivamia maeneo ya sokoni ambayo yana watu wengi kulitiokea taharuki iliyopeleke vurugu kubwa zilizotokana na makabiliano ya polisi na wananchi.

Katika makabaliano hayo polisi walitumia risasi za moto na kuwapiga watu watatu ambao kati yao mmoja amefariki dunia. Wakati huo huo wakati polisi akiwa anaseti bunduki yake naye alijikuta kwa bahati mbaya bunduki ikamfyatukia na kumpiga mguuni hivyo na yeye kujeruhiwa mguuni.

Baada ya tukio hilo wananchi waliuchukua mwili wa aliyefariki na kuupeleka kwa mwenyekiti wa kijiji wakimtuhumu kushirikiana na polisi kuwabugudhi wananchi ambao hata hawahusiki wala hawajui kuhusu mambo hayo huku wanaofanya mambo hayo wako mbali kabisa wanaendelea na shughuli hizo

Mpaka wakati naingia mitamboni naambiwa wananchi wamezingira nyumba ya wageni ambayo inasemekana polisi wako humo.

My take.

Huu mkoa wa Kigoma umekuwa na imani za ushirikina sana nafikiri elimu zaidi inatakiwa. Lkn pia najiuliza kwa nini polisi watumie nguvu kubwa kiasi hicho mpaka kutumia risasi za moto.
Asante kwa taarifa
 
Ujinga mtupu,unamsingizia kua mtu flani ni mchawi,mnamuadhibu na kumuaibisha.Bora wazuiliwe.
 
Back
Top Bottom