Wananchi watatu wafariki kwenye Vurugu za 'Kamchape' Kigoma

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,281
Watu watatu wakazi wa Kijiji cha Kazuramimba wilayani Uvinza mkoani Kigoma wamethibitishwa kufariki katika vurugu zilizohusisha vitendo vya kutoa uchawi maarufu kwa jina la ‘Kamchape’.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Filemon Makungu amesema polisi wawili wamejeruhiwa katika vurugu hizo huku sababu za vifo vya wananchi hao bado hazijabainika.

Amesema vurugu zilianza baada ya polisi kufika kwenye Kijiji hicho kutoa elimu kuhusu madhara ya kukaribisha watu wanaotoa uchawi na kupiga marufuku kuendelea na vurugu hizo, lakini wananchi walikaidi agizo hilo na siku iliyofuata waliendelea na viendo vya kutoa uchawi kwenye nyumba za watu kwa kuwanyoa vipara wananchi ambao wanadaiwa uchawi umetolewa kwenye nyumba zao.

Kamanda ameongeza kuwa walifika kijijini hapo kuzuia vurugu hizo na wananchi hao walifunga Barabara Kuu ya Kigoma- Tabora inayopitia kijijini hapo kwa kuweka magogo na kuwasha moto ili kuzuia polisi na vyombo vya usalama wasifike kwenye maeneo wanayofanya matukio hayo, ndipo polisi walitoa vizuizi hivyo na kuanza kukamata watu, ambapo vurugu zilitokea na kupelekea vifo hivyo.

Aidha, amesema magari mawili ya polisi na uhamiaji yalivunjwa vioo na kituo cha polisi cha Kazuramimba kilishambuliwa kwa mawe.
 
Watu wasiosoma ndio wanahamini uchawi, wasomi wangapi kutwa kwenda Bagamoyo kufanya ndumba.
 
Watu watatu wakazi wa Kijiji cha Kazuramimba wilayani Uvinza mkoani Kigoma wamethibitishwa kufariki katika vurugu zilizohusisha vitendo vya kutoa uchawi maarufu kwa jina la ‘Kamchape’...
Kigoma ni ngome kubwa sana ya ya uchawi wa asili uliochanganyika na uchawi wa kitabu.
 
Kama uliwahi kurogwa huwezi kuacha polisi walete mushkeli kwa akina "kamchape"
 
Kamchape wanasumbua sana mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma. Na pia nchi jirani ya Zambia kwenye maeneo yanayopakana na Tanzania. Kule Zambia walitimuliwa na baadhi yao kukamatwa na kufikishwa mahakamani. Kamchape ni wa kupigwa marufuku kwasababu kamwe huwezi kukuta wameenda kutoa uchawi wanapoishi matajiri. Wao ni maeneo ya vijijini ambako huwanyooshea vidole raia wanaoonekana wana unafuu maeneo hayo. Yaani kama una hali nzuri kimaisha ukawa unaishi katikati ya maskini jua Kamchape watakufikia penda usipende. Ni ngumu kukuta Kamchape kaenda kutoa uchawi kwa mtu hohehahe. Ubaya ni kwamba siku Kamchape wakifika hata majirani zako siku hiyo wanakukataa na kukuita mchawi. UKIWA VIZURI KIUCHUMI HAMA... USIKAE MAENEO YALIYOJAA MASKINI KWASABABU HAWAAMINIKI.
 
Watu watatu wakazi wa Kijiji cha Kazuramimba wilayani Uvinza mkoani Kigoma wamethibitishwa kufariki katika vurugu zilizohusisha vitendo vya kutoa uchawi maarufu kwa jina la ‘Kamchape’.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Filemon Makungu amesema polisi wawili wamejeruhiwa katika vurugu hizo huku sababu za vifo vya wananchi hao bado hazijabainika.

Amesema vurugu zilianza baada ya polisi kufika kwenye Kijiji hicho kutoa elimu kuhusu madhara ya kukaribisha watu wanaotoa uchawi na kupiga marufuku kuendelea na vurugu hizo, lakini wananchi walikaidi agizo hilo na siku iliyofuata waliendelea na viendo vya kutoa uchawi kwenye nyumba za watu kwa kuwanyoa vipara wananchi ambao wanadaiwa uchawi umetolewa kwenye nyumba zao.

Kamanda ameongeza kuwa walifika kijijini hapo kuzuia vurugu hizo na wananchi hao walifunga Barabara Kuu ya Kigoma- Tabora inayopitia kijijini hapo kwa kuweka magogo na kuwasha moto ili kuzuia polisi na vyombo vya usalama wasifike kwenye maeneo wanayofanya matukio hayo, ndipo polisi walitoa vizuizi hivyo na kuanza kukamata watu, ambapo vurugu zilitokea na kupelekea vifo hivyo.

Aidha, amesema magari mawili ya polisi na uhamiaji yalivunjwa vioo na kituo cha polisi cha Kazuramimba kilishambuliwa kwa mawe.
Huyu polisi ni mwongo. Hizi habari zipo hapa tangu juzi na zililetwa na member ambaye yuko huko. Alisema hao watoa uchawi walikwenda kijijini na kumtuhumu raia mmoja kuwa ana uchawi. Raia yule akakimbilia kituo cha polisi kutafuta usalama na wananchi wakamfuata kutaka kumtoa kwa nguvu hivyo polisi wakapiga risasi na baadhi wakauawa. Sasa kwenye hii habari inaonyesha polisi wanataka kujitoa kwenye lawama ya kuachia huu ujinga wa ufanyike kwa muda mrefu bila kuchukuwa hatua mpaka maafa yakatokea. Swali liko pale pale na polisi na maafisa wote wa usalama na serikali wanatakiwa kujibu: Kwa nini wameachia huu ujinga wa kutafuta wachawi ufanyike kwa muda mrefu bila kuchukuwa hatua?
 
Adui ujinga
 
Ujinga upi Sasa acheni wachawi washughulikiwe waje na Dar
 
Wachawi Wana nguvu hadi Serikalini wakizidiwa nguvu ni lazima Serikali iingilie kuwasaidia kwa sababu watumishi wengi ni wachanawama wao,ni lazima wawaokoe ndugu zao
 
Maandiko yote yanataka mchawi auwawe we nani unapinga hili.
Mchawi na wezi hawataki kuishi
 
Back
Top Bottom